Jollie
Member
- Jul 26, 2019
- 35
- 64
Mwandishi wa habari wa kujitegemea ndugu. Sebastian Emmanuel Atilio ameshikiliwa na Polisi Wilayani Mufindi mkoani Iringa kwa siku tatu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za kinachoitwa mgogoro wa ardhi kati ya kijiji cha Ifupila na kampuni ya Unilever inayolima zao la chai Wilayani humo.
Mwandishi huyo leo amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mufindi na kusomewa makosa mawili likiwemo na kufanya kazi bila kusajiliwa na bodi na kosa la pili kuandika habari za uongo juu ya mgogoro wa wananchi Ifupila.
Dhamana imezuiliwa hadi Septemba18
Hapa chini ni habari inayodaiwa ni ya Uongo
Mwandishi huyo leo amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mufindi na kusomewa makosa mawili likiwemo na kufanya kazi bila kusajiliwa na bodi na kosa la pili kuandika habari za uongo juu ya mgogoro wa wananchi Ifupila.
Dhamana imezuiliwa hadi Septemba18
Hapa chini ni habari inayodaiwa ni ya Uongo
Sebastian Emmanuel Atilio said:Taarifu zilizo nifikia asubuhi hii ni kuwa huenda nusu ya kijiji cha Ifupira, kilichopo kata ya Ifwagi, wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa, kitafutwa kwa sharia ya ardhi ya mwaka 1932.
Taarifu zinasema kuwa eneo lote la mitaa ya Godown na Luhanga ambako ndiko kuliko jengwa ofisi za kijiji, ofisi za chama cha Mapinduzi, Zahanati ya kijiji pamoja na makazi ya watu kumewekwa Alama za umiriki (beckons) wa ardhi na maofisa wa kampuni ya Unilever Tea Tanzania Ltd, maofisa hao wanadai kuwa eneo hilo linamirikiwa na Kampuni hiyo ya kibepari tangu mwaka 1932.
Ikumbukwe kuwa kijiji hicho cha Ifupira kimezungukwa na makampuni mawili ya kibepari ya UNILEVER TEA TANZANIA LTD NA MUFINDI TEA TANZANIA LTD AU RIFT VALEY HOLDINGS LTD, yanayo lima zao la kibiashara la chai.
Kwa mjibu wa taarifu nilizo nazo ni kuwa 1974 Mzee wetu Mwamtengelea (marehemu) wakati huo akiwa diwani wa kata ya Ikonongo aliiomba Serikali kupitia kampuni hiyo ikiongezee kijiji hicho eneo zaidi kwakuwa kijiji kilikuwa na eneo dogo sana na Kampuni iliridhia kutoa eneo hilo, lakini wananchi wanashangaa kuwa hapo jana kampuni hiyo imekuja na kuingia kijijini hapo na kuweka alama tofauti na makubaliano ya awali.
Tunaendelea na kutafuta ukweli zaidi...
Wananchi wote (HASA VIJANA WASOMI) walio zaliwa Ifupira, ama kusoma ama kuishi hapo nawashauri turudi kwetu mara moja.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ifupira Mh. Ngunda amezungumza nami mda mfupi ulio pita kuwa, Nyaraka mhimu za ugawaji wa ardhi ya kijiji hicho zimepatikana hivyo wale walio tumwa na kampuni ya Unilever wazitoe zile alama za mipaka ya ardhi walizo ziweka.
Amesema kuwa kijiji hicho hakikuwa na nyaraka hizo hivyo walilazimika kuzitafuta popote na kwa bahati nzuri zimepatikana. Mwenyekiti ameeleza kuwa nyaraka hizo zimepatikana ofisi ndogo ya Unilever division ya Ifupira.
Amewaomba wananchi wawe watulivu wakati utaratibu wa kuwafikishia taarifu rasmi unaandaliwa