Mufindi: Mwandishi wa habari Sebastian Emmanuel Atilio, afikishwa mahakamani, anyimwa dhamana...

Jollie

Member
Jul 26, 2019
35
64
Mwandishi wa habari wa kujitegemea ndugu. Sebastian Emmanuel Atilio ameshikiliwa na Polisi Wilayani Mufindi mkoani Iringa kwa siku tatu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za kinachoitwa mgogoro wa ardhi kati ya kijiji cha Ifupila na kampuni ya Unilever inayolima zao la chai Wilayani humo.

Mwandishi huyo leo amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mufindi na kusomewa makosa mawili likiwemo na kufanya kazi bila kusajiliwa na bodi na kosa la pili kuandika habari za uongo juu ya mgogoro wa wananchi Ifupila.

Dhamana imezuiliwa hadi Septemba18

Hapa chini ni habari inayodaiwa ni ya Uongo

Sebastian Emmanuel Atilio said:
Taarifu zilizo nifikia asubuhi hii ni kuwa huenda nusu ya kijiji cha Ifupira, kilichopo kata ya Ifwagi, wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa, kitafutwa kwa sharia ya ardhi ya mwaka 1932.

Taarifu zinasema kuwa eneo lote la mitaa ya Godown na Luhanga ambako ndiko kuliko jengwa ofisi za kijiji, ofisi za chama cha Mapinduzi, Zahanati ya kijiji pamoja na makazi ya watu kumewekwa Alama za umiriki (beckons) wa ardhi na maofisa wa kampuni ya Unilever Tea Tanzania Ltd, maofisa hao wanadai kuwa eneo hilo linamirikiwa na Kampuni hiyo ya kibepari tangu mwaka 1932.

Ikumbukwe kuwa kijiji hicho cha Ifupira kimezungukwa na makampuni mawili ya kibepari ya UNILEVER TEA TANZANIA LTD NA MUFINDI TEA TANZANIA LTD AU RIFT VALEY HOLDINGS LTD, yanayo lima zao la kibiashara la chai.

Kwa mjibu wa taarifu nilizo nazo ni kuwa 1974 Mzee wetu Mwamtengelea (marehemu) wakati huo akiwa diwani wa kata ya Ikonongo aliiomba Serikali kupitia kampuni hiyo ikiongezee kijiji hicho eneo zaidi kwakuwa kijiji kilikuwa na eneo dogo sana na Kampuni iliridhia kutoa eneo hilo, lakini wananchi wanashangaa kuwa hapo jana kampuni hiyo imekuja na kuingia kijijini hapo na kuweka alama tofauti na makubaliano ya awali.

Tunaendelea na kutafuta ukweli zaidi...

Wananchi wote (HASA VIJANA WASOMI) walio zaliwa Ifupira, ama kusoma ama kuishi hapo nawashauri turudi kwetu mara moja.

Mwenyekiti wa kijiji cha Ifupira Mh. Ngunda amezungumza nami mda mfupi ulio pita kuwa, Nyaraka mhimu za ugawaji wa ardhi ya kijiji hicho zimepatikana hivyo wale walio tumwa na kampuni ya Unilever wazitoe zile alama za mipaka ya ardhi walizo ziweka.

Amesema kuwa kijiji hicho hakikuwa na nyaraka hizo hivyo walilazimika kuzitafuta popote na kwa bahati nzuri zimepatikana. Mwenyekiti ameeleza kuwa nyaraka hizo zimepatikana ofisi ndogo ya Unilever division ya Ifupira.
dd91775e-708d-4448-8764-47a937e44c30.jpg

Amewaomba wananchi wawe watulivu wakati utaratibu wa kuwafikishia taarifu rasmi unaandaliwa
 
Haya media council, media organisation na wale watetezi nendeni fasta huko mufindi mkaokoe jahazi, hiki siyo kipindi kile cha utoaji ovyo wa habari, now hata katibu kata awe mhariri ili mwandishi usiharibu.
 
Lakini mwandishi ameandika kishabiki sana na kuelekea upande mmoja bila kuweka facts... katika andiko lake hilo kuna maneno yanajirudia rudia kama "kampuni ya kibepari" kuonesha bias kabisa kukosekana kwa weledi katika uandishi... pia wito wake wa kuwaita vijana warudi home umekaa kichochezi.. kiufupi haieleweki huyu mwandishi karipoti habari au ni maoni yake ... asamehewe tu na apelekwe shule ya uandishi
 
Sio hivyo tu, huyu kijana inaelekea wala si mwenyeji wa Ifupila. Inawezekana yeye binafsi au kuna tapeli moja la ardhi alitaka kumtumia kuchafua wawekezaji ("Anaowaita Mabepari") kwa maslahi yake. Ifupila hakuna kampuni ya Rift Valley, bali kuna Stone Valley. Hakuna ukoo wa Mtengelea bali kuna Mtengela. Na huyo marehemu Mwamtengela amefariki akiwa Mwenyikiti wa CCM wilaya ya Mufindi hajawahi kuwa Diwani. Aliyewahi kuwa diwani ni mwanaye Zarafi Mtengela, aliyeamua 2010 kutogombea sababu ya majungu ya vijana kama huyu.
Hata hajui ushirika wa karibu sana wa wakulima wadogo ktk kata za Ifwagi na Mdabulo na kampuni ya Unilever unavyowawezesha wakulima hao kwa miche na utaalamu wa kuanzisha mashamba yao ya chai na kisha kukiuzia kiwanda hicho. Ushirikiano ambao hakuwapo kwa kampuni kongwe toka ukoloni ya Stone Valley.
 
Asante kutupatia taarifa hii ya madhila yanayomkuta mwandishi mwenzetu wa habari huko Iringa na huyu ni wa pili.

As a matter of interest, naomba utueleze zaidi kuhusu mwandishi huyo wa kujitegemea anaandikia media gani, na hiyo story ilichapishwa wapi, ili tuu nijue ni editor gani anaweza ku publish unbalanced story ya kiwango hicho.

Ila kukweli kabisa hiki tunachofanyiwa sisi waandishi, na haswa sisi wa kujitegemea, sicho kabisa!.

Nimeisoma hiyo habari japo ni one sided, imeegemea upande mmoja kwa kukosa balance na upande wa pili, pia Ilihitaji authoritative imput kutoka kwenye authorities kwa sababu ni kweli Unilever anamiliki ardhi iliyokuwa ya kampuni ya Brooke Bond ya Uingereza toka mwaka huo wa 1938, lakini Sheria ya Ardhi Namba 8 ya 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 9 ya mwaka 1999 zinatambua subsisting titles zote zilizokuwepo prior to sheria hizo, na kama ni kweli eneo hilo lilitolewa kwa vijiji then lazima kuna documentation, kwa sababu in Tanzania mikataba mingine yote ya jambo lolote inaweza kuwa ya mdomo lakini mkataba wowote wa ardhi lazima uwe ni wa maandishi.

Pamoja na madhaifu hayo, hilo sio kisa la kumshitaki mwandishi huyo na kosa hilo ni bailable, sio la kumyima dhamana.

Kiukweli sisi waandishi wa habari kwa mwaka huu...sijui!.
P
 
Huyu mwandishi wa blog siyo habari. Ili kubalance story yake ilibidi aongee na mamlaka za ardhi wilayani au hata mkoani... Aende shule
 
Huenda hakimu kaagizwa Na Mkuu wa wilaya ahakikishe dhamana haipo, maana kwa wilaya Mkuu wa wilaya ndo Mkuu wa maswala ya kinidhamu kwa mahakimu, mhimili wa mahakama bado hauko Huru.
 
Mmmmmmh huyu anayeitwa wandishi alisomea wapi taaluma hiyo?

'Ifupira'!!!??? Ninavyofahamu mimi vijiji vya Iringa havina 'r'....Hata Iringa yenyewe naamini pengine ni ilinga...tehtehteh
 
Mimi nampa tu pole kwa kupelekwa kupumzishwa kwenye hilo gereza la wilaya Mufindi (gereza la Isupiro) ambalo ni la kilimo na linasadikiwa kuwa na miundombinu migumu sana hasa ile ya maji.

Harakati za kuwapigania hao 'wanakijiji wenzake' akiwa kama mmoja wa wasomi wa hicho kijiji kwa njia ya mkato, sasa zinamtokea puani.
 
Asante kutupatia taarifa hii ya madhila yanayomkuta mwandishi mwenzetu wa habari huko Iringa na huyu ni wa pili.
As a matter of interest, naomba utueleze zaidi kuhusu mwandishi huyo wa kujitegemea anaandikia media gani, na hiyo story ilichapishwa wapi, ili tuu nijue ni editor gani anaweza ku publish unbalanced story ya kiwango hicho.
Ila kukweli kabisa hiki tunachofanyiwa sisi waandishi, na haswa sisi wa kujitegemea, sicho kabisa!.
Nimeisoma hiyo habari japo ni one sided, imeegemea upande mmoja kwa kukosa balance na upande wa pili, pia Ilihitaji authoritative imput kutoka kwenye authorities kwa sababu ni kweli Unilever anamiliki ardhi iliyokuwa ya kampuni ya Brooke Bond ya Uingereza toka mwaka huo wa 1938, lakini Sheria ya Ardhi Namba 8 ya 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 9 ya mwaka 1999 zinatambua subsisting titles zote zilizokuwepo prior to sheria hizo, na kama ni kweli eneo hilo lilitolewa kwa vijiji then lazima kuna documentation, kwa sababu in Tanzania mikataba mingine yote ya jambo lolote inaweza kuwa ya mdomo lakini mkataba wowote wa ardhi lazima uwe ni wa maandishi.
Pamoja na madhaifu hayo, hilo sio kisa la kumshitaki mwandishi huyo na kosa hilo ni bailable, sio la kumyima dhamana.
Kiukweli sisi waandishi wa habari kwa mwaka huu...sijui!.
P
Inasemekana aliandika habari ya kudhania ambayo yeye hakuwa na uhakika nayo, ni tatizo tunapokuwa na taifa ambalo linataka kila kitu kisemwacho kiwe na ukweli wa asilimia mia! Licha ya wao kutokuwa hivyo. Kisa, alisema huenda kijiji cha.......kikafutwa, hapa ni tofauti na kusema kijiji cha........kitafutwa, sijui uchochezi uko wapi, wataalamu wa lugha ya kiswahili watufafanulie, Mimi sioni kudhani kuwa ni kosa kwani kudhani hakuthibitishi jambo.
Karibu.
 
Back
Top Bottom