PostGE2025 Muda wa Samia kukaa Ikulu ulikwisha siku aliposema, ‘Kama hamkutaka Serikali tuwaue kwanini mliwaruhusu waingie barabarani?'

PostGE2025 Muda wa Samia kukaa Ikulu ulikwisha siku aliposema, ‘Kama hamkutaka Serikali tuwaue kwanini mliwaruhusu waingie barabarani?'

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Doctor Mama Amon

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,311
Reaction score
3,490
1766844324184.png

SAMIA NA ANGUKO LA KATIBA: KAMA HAMKUTAKA NIWAUE WATOTO WENU KWANINI MLIWARUHUSU WAINGIE BARABARANI KUFANYA MAANDAMANO YA KUNIPINDUA?

I. USULI

“Ukiona serikali ambayo haitaki kukosolewa, tambua kuwa hiyo si serikali nzuri. Serikali inayokataa kusikia sauti za watu wake inaelekea kwenye udikteta, maana demokrasia ni sauti ya wananchi, si amri ya viongozi.” — Julius K. Nyerere (Hotuba ya 1995)

Kwa kuzingatia uzito wa nukuu hii kutoka kwa Baba wa Taifa; naandika barua ya Kijasiriadola kwa Wadogo zangu wa GenZ; Wanarika wenzagu, Wakubwa zangu, na Wakuu wa Vyombo vya Usalama, pamoja na Maofisa wote walioko chini yao; bila kujali kama msomaji yuko ndani au nje ya chama tawala, ndani au nje ya utumishi wa umma.

Kwa ujumla, nawandikia Watanzani wote wanaoamini katika haki ya uhuru wa kufikiri na kujieleza kimantiki, bila matusi, kama njia mojawapo ya “kuwaongoza viongozi” na “kutakatifuza malimwengu” ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kijeshi, kwa kutumia hoja sanifu.

Natumia barua hii kutoa Pole, Salamu za Krismasi na Heri ya Mwaka Mpya kwa kuzingatia sababu na madhara ya maafa makubwa yaliyolikumba Taifa letu katika wiki ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, ambapo, pamoja na mauaji ya kupangwa ya raia zaidi ya 1,500 yaliyotekelezwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania, hakuna mtu aliyewajibika wala kuwajibishwa hadi sasa.

Hivyo, napendekeza kwamba, muda wa Samia kukaa Ikulu ulikwisha siku alipojitenga na Watanzania na kisha kuwauliza hivi, ‘Kama hamkutaka niwaue watoto wenu kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani kufanya maandamano ya kunipindua?

Najenga hoja kwamba, swali hili ni kielelezo thabiti cha dhamira yake ya kuendelea kutekeleza sera haramu 17 zenye sura ya ukoloni mamboleo na utumwa mambosasa nchini Tanzania, wakati sera hizi zinapingana na Katiba ya nchi, na ndio kiini cha matukio ya wiki ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Hatimaye natoa wito kwa Samia kujiwajibisha mwenyewe au kuwajibishwa na wadau baki, bila kuvunja katiba ya nchi, kama ilivyotokea huko Zimbabwe mwaka 2017 dhidi ya Robert Mugabe.

Kwa ajili ya kutetea msimamo huu hatua kwa hatua, andiko hili limegawanyika kwenye sehemu zifuatazo:

  1. Usuli
  2. Utangulizi
  3. Kanuni ya Utanzania na matarajio ya Watanzania
  4. Sera haramu 17 zinazokiuka Kanuni ya Utanzania
  5. Samia kiini cha anguko la Katiba
  6. Hitimisho na mapendekezo
II. UTANGULIZI

Miaka 64 iliyopita, yaani mwaka 1961, kijana Mtanganyika aitwaye Julius Nyerere alitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Tanganyika” kutoka kwa wakoloni wa Kizungu.

Miaka mitatu baadaye, kijana Mzanzibari aitwaye Abedi Karume, alitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Zanzibar” kutoka kwenye ukoloni wa miaka ipatayo 200 chini ya Waarabu wa Omani, waliokuwa wameikalia Zanzibar tangu 1698.

Hatimaye, vijana Julius Nyerere na Abedi Karume walitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Tanzania” iliyopaswa kuendelea kuwa huru dhidi ya ukoloni mamboleo na utumwa mambosasa.

Vijana Julius Nyerere na Abedi Karume walifanikiwa kuzika kabisa ukoloni mkongwe wa Kizungu uliofanyika kwa miaka 77 na kutokomeza utumwa mambokale wa Kiarabu uliofanyika kwa miaka 1000.

Hivyo, tangu 1964 mpaka Machi 2021, Watanzania waliendelea kuwa huru dhidi ya ukoloni wa Kizungu na utumwa wa Kiarabu, wakiwa wanaongozwa na kanuni ya kuheshimu utu wa kibinadamu unaounganishwa na Katiba moja ya kisiasa.

Vijana wawili Julius Nyerere na Abedi Karume waliwafundisha Watanzania, na Watanzania wakakubali, mafundisho mahsusi kuhusu misingi ya utu wa kibinadamu, ambayo hapa nairejea kama Kanuni ya Utanzania.

Kanuni ya Utanzania ndio msingi wa ndoto ya Mtanzania, maana inabeba ahadi za urithi wa watoto wa Tanzania kutoka kwa waasisi wa Taifa hili. Ni chimbuko la ndoto ya kitaifa.

Ndoto ya kitaifa ni maono au maadili ya pamoja ambayo hufafanua utambulisho wa pamoja na kuweka mwelekeo wa maadili na matarajio ya taifa.

Inatumika kuwaunganisha watu, kuhamasisha maendeleo, na kuelezea seti ya maadili na malengo ya pamoja. Majukumu muhimu ya ndoto ya kitaifa ni pamoja na haya:

Mosi, kuunda Utambulisho wa Pamoja: Ndoto ya kitaifa husaidia kuunganisha mahusiano ya kijamii yasiyotulia na idadi tofauti ya watu kwa kuunda hisia ya pamoja ya kusudi na umiliki ambayo hupita tofauti za kikanda, kikabila, au kitabaka.

Pili, kuongoza Mwelekeo na Sera ya Kitaifa: Inatoa "mchoro wa njia" ambayo taifa litafuata, ikishawishi mijadala ya kisiasa na maadili, pamoja na mipango mikubwa ya kitaifa na miradi ya miundombinu.

Tatu, kuhamasisha Hatua na Maendeleo: Kwa kutoa maono chanya ya mustakabali bora, inawahamasisha raia kufanya kazi kuelekea malengo ya pamoja, kuhimiza juhudi za pamoja na mafanikio ya mtu binafsi katika kutumikia matarajio mapana ya kitaifa.

Nne, kufafanua Maadili ya Msingi: Ndoto za kitaifa mara nyingi hutokana na maadili ya msingi kama demokrasia, uhuru, usawa, na fursa, ikitumika kama himizo kwa raia kujitahidi kwa utaratibu wa kijamii unaofafanuliwa na kanuni hizi.

Na tano, kukuza Ujamaa wa Mawazo: Husaidia katika kusambaza maadili ya kitamaduni ya msingi kwa vizazi na zaidi ya mipaka ya kitaifa, wakati mwingine hata kuwa na wapiga kura wa kimataifa.

KUna mifano ya Ndoto za Kitaifa katika nchi nyingi duniani. Mfano, kuna Ndoto ya Taifa la Marekani, Ndoto ya Taifa la Kanada, na Ndoto ya Taifa la China. Hata Tanzania tunayo Ndoto ya KItaifa, iliyosimikwa na waasisi wa Taifa letu katika Katiba ya nchi yetu (1977).

1766919798172.png

II. KANUNI YA UTANZANIA NA MATARAJIO YA WATANZANIA

Kulingana na mafundisho ya Vijana wawili Julius Nyerere na Abedi Karume, Kanuni ya Utanzania inaweza kufupishwa kwenye aya 16 zinazosema:

  1. Kwamba, wakati mizimu, majini, malaika, miungu na Mungu ni watu wasio na miili, kila binadamu ni mtu mwenye mwili unaoonekana na kushikika, na ambao ni kitovu cha hazina ya uhai, akili, hisia na utashi huru.
  2. Kwamba, kikundi cha binadamu wanaomiliki na kukalia kipande cha nchi chenye mipaka rasmi ya kijiografia, wakiwa na katiba rasmi yenye kutaja misingi mahsusi ya kiutawala, ukiwemo muundo wa mamlaka ya kitawala ndani ya mipaka hiyo, ambapo mamlaka hiyo iko huru dhidi ya udhibiti wa wadau baki katika jumuiya ya kimataifa na inao uwezo wa kuingia mikataba ya kimataifa na chi zingine zenye hadhi sawa, huitwa dola.
  3. Kwamba, muundo wa mamlaka ya kitawala ndani ya mipaka ya nchi unaweza kuwa wa kifalme au kijamhuri, kidemokrasia au kiimla, kishirikisho au kiyunitariani, ambapo mseto wa jozi hizi tatu unazalisha aina nane tofauti za miundo ya serikali, muundo mmojawapo ukiwa ni Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia.
  4. Kwamba, Katiba ya nchi inayotambua muundo wa mamlaka ya kitawala unaojulikana kama Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia, ndio njia pekee ya kujenga Taifa jipya la binadamu wanaojitawala kwa uhuru pasipo hofu ya kukwekwa tena chini ya utumwa au ukoloni na Taifa jingine lolote.
  5. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea heshima ya binadamu, binadamu wote ni sawa katika mizania ya vinasaba vya kiutu, na heshima yao inapaswa kuhifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu.
  6. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea usawa wa binadamu wote katika mizania ya haki, binadamu wote huzaliwa wakiwa na haki za msingi zilizo sawa, haki hizo zikijumuisha haki ya uhai; haki ya uhuru wa kufikiri, kuhukumu na kutenda; na haki ya kustawi, kwa maana ya haki ya kila mtu kuishi maisha kamili, yenye furaha, na mafanikio, akiendeleza hazina ya vipaji vyake alizvyozaliwa navyo, kwa ajili ya kufukuzia ustawi wa kimwili, kiakili, na upatikanaji wa fursa za kisiasa, kiuchumi na kijamii, na kiutamaduni.
  7. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea uhuru wa dhamiri, kila binadamu anayo haki ya kukubali au kukataa imani ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kidini, kifalsafa, na kuunda maoni yake mwenyewe bila kulazimishwa na serikali au mtu yeyote baki, na hatimaye kueleza imani yake hadharani au faraghani, ilimradi asidhuru watu wengine katika kufanya hivyo.
  8. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea ukuu wa mamlaka ya watu juu ya serikali yao, kwa ajili ya kukuza na kuhami haki, watu makini lazima wakubaliane kuunda Jamhuri ya Kidemokrasia, yenye kutawaliwa na serikali iliyopata madaraka ya kiutawala kutokana na kibali cha kura za watawaliwa, ambapo kura hizo zinazopigwa kwa kufuata utaratibu unaokubalika kikatiba.
  9. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea utawala wa sheria, binadamu wote ni sawa mbale ya Katiba, sheria na kanuni husika, ambapo, vifungu vya kikatiba vinayo nguvu ya kuvipiku vifungu vya kisheria na vifungu vya kisheria vinayo nguvu ya kuvipiku vifungu vya kikanuni.
  10. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea chimbuko la sheria za nchi, sheria za kibunge, kidini na kimila zinazopingana na misingi ya maadili asilia, kama inavyotamkwa kwenye Tangazo la Dunia Kuhusu Haki za Binadamu, huwa ni batili.
  11. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mgawanyo wa madaraka, mamlaka ya nchi lazima yagawanywe katika mihimili mitatu, yaani mhimili wenye madaraka ya utawala (serikali), mhimili wenye madaraka ya kutunga sheria (Bunge), na mhimili wenye madaraka ya utoaji haki (mahakama), itakayofanya kazi kwa kushauriana na kukosoana.
  12. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea uwajibikaji wa kimamlaka, mamlaka ya nchi lazima iwajibike kwa wananchi walioiweka madarakani.
  13. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea ustawi wa watu, lengo kuu la serikali ni ustawi wa wananchi walioiweka madarakani.
  14. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea njia kuu za uchumi, shughuli za Serikali zinapaswa kutekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na kwa kuzuia mtu mmoja kumyonya mtu mwingine.
  15. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mamlaka ya umma kufukuza serikali, watu wanayo haki ya kutumia mchakato stahiki kufukuza serikali inayohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kuajiri serikali mpya, ambayo, kwa maoni yao, itakuwa na weledi wa kukuza na kuhami haki zao.
  16. Na kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mamlaka ya kubadilisha katiba kwa lengo la kubadilisha muundo wa serikali, watu wanayo haki ya kufuta muundo wa kiserikali unaohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kubuni na kuweka muundo mpya wa serikali, ambao kwa maoni yao utakuwa na yamkini ya kukuza na kuhami haki zao.
Katika muda wote wa utawala wa waasisi wa Taifa letu, hizi kanuni za kikatiba ziliheshimiwa sana kiasi kwamba, Raisi alichukuliwa kuwa ni "Baba wa Taifa" asiyeweza kunyanyua mkono na kumwaga damu ya watoto wake, mara zote akisimama kama alama ya umoja wa kitaifa, chimbuko la matumaini kwa raia wenye hofu, mlinzi mkuu wa uhai wa raia wote, na msimamizi mkuu wa usalama wa Taifa lote.

Hata siku moja, Watanzania hawakuwahi kufikiri kwamba wangempata Rais atakayejitenga nao na kisha kuwakejeli kwa kuwauliza swali tata, kama ilivyotokea tarehe 02 Desemba 2025, pale Samia alipowauliza Watanzania kwamba: “Nyie Watanzania, kama hamkutaka niiwaue watoto wenu kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani kufanya maandamano ya kunipindua?

Kwa hakika, Matukio tuliyoyashuhudia kabla, wakati na baada ya wiki ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 yalikuwa, kwa pamoja, yanamaanisha kwamba muundo wa kikatiba haukuwa na uwezo tena wa kuzizuia mamlaka ya serikali kufanya utovu wa nidhamu ya kiutawala.

Athari ya jumla ilikuwa kwamba haki na michakato ya kikatiba ipo kwenye karatasi pekee huku kivitendo ikiwa haifanyi kazi kabisa. Hii ndiyo fasili ya tukio linaloitwa anguko kamili la katiba.

Ni anguko la katiba, badala ya tukio la kujikwaa kikatiba, kwa sababu tukio la kujikwaa kikatiba linaashiriwa na mmomonyoko wa nidhamu ya kiutawala ambao ni wa mpito na ulioenea katika ofisi chache za utawala.

Lakini, tukio la anguko kamili la katiba linaashiriwa na mmomonyoko endelevu wa nidhamu ya kiutawala na ulioenea katika ofisi zote za utawala.

Kwa hakika, uchaguzi mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 2025 ulikuwa tukio lililovuka mstari unaotenganisha tukio la kujikwaa kikatiba na tukio la anguko kamili la katiba kwa sababu nyingi.

Kwa mfano, usimamizi huru wa maamuzi ya uchaguzi na utovu wa nidhamui katika mwenendo wa watendaji wa serikali ulikoma; usimamizi wa maana kutoka kwenye bunge huru haukutokea kabisa; vyombo vya usalama vilifanya kazi kama maafisa wa chama tawala bila uwezkano wa ofisa yeyote kuadhibiwa kwa utovu wa nidhamu; na mifumo ya kisheria ilitumiwa kama silaha ya kuzuia ushindani huru wa kiraia na kisiasa.

Ni katika wakati huu ambapo Samia alijisifu kuwa ni Dikteta Mkuu anayeweza kuua mtu yeyote kwa hiari yake mwenyewe, na hakuna mtu wa kumfanya lolote.

III. SERA HARAMU 17 ZINAZOKIUKA KANUNI YA UTANZANIA

Napendekeza kwamba, swali hili ni kielelezo cha ujasiri alio nao Samia katika azima yake ya kutekeleza program ya sera haramu, ambayo sasa inafahamika kwa jina la “NEW DECIDED MOPPERS.”

Hii ni programu inayoongelea sera haramu 17, kila sera ikiwakilishwa na herufi moja katika kifungu cha maneno yafuatayo “NEW DECIDED MOPPERS,” kwa maana ya sera zifuatazo:

(1) Nepotic autocracy and cleptocracy in state administration; (2) Elevation of Shariah Law over the Constitution and the Natural Moral Law; (3) War on Indigenous Africans in favor of Foreign Direct Investors; (4) Detentive abductions and tortures; (5) Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity from criminal charges; (6) Court authority perversion and litigation dramas; (7) Inquiry commission dramas; (8) Deregistration of critical associations; (9) Election rigging in the name of INEC’s constitutional immunity from criminal charges; (10) Disinformation, media capture and mind capture; (11) Military integrity perversion, politicization and paralysis; (12) Organized violence against republican principles; (13) Parliamentary incapacitation and legislative dramas; (14) Police and paramilitary forces brutality; (15) Embezzlement of financial and natural resources; (16) Religious oppressions; and (17) Security forces outsourcing for domestic oppressions.

Katika aya zifuatazo nitaeleza kila sera kwa ufupi.

1. Nepotic autocracy and cleptocracy in state administration:

Samia anatekeleza sera ya kugawa vyeo vya kisiasa kwa kuangalia undugu, urafiki, uswahiba, ukanda na udini, yaani “nepotism”.

Binti yake na mumewe ni Mawaziri; Mtalaka wa bintiye ni DC; Mshenga katika ndoa ya binti yake ni Waziri; na orodha inaendelea.

Maamuzi yote haya anayafanya Samia yeye mwenyewe kinyume cha ushauri thabiti anaopewa na wasaidizi wake makini.

Hii ni tabia ya udikteta wa mtu mmoja, yaani “autocary,” na hivyo kifungu cha maneno “nepotic autocracy.”

Madhara ya kusimika mfumo wa udekteta wa kifamilia ni kuigeuza ikulu ya Tanzania kuwa pango la walanguzi wa rasilimali za nchi, na hivyo kuunda serikali ya wezi, yaani "cleptocracy."

Ushahidi uko wazi. Huku upinzani ukivunjwa, ukosoaji wa serikali ukifanywa kuwa uhalifu, na mchakato wa uchaguzi ukikataliwa, Samia alichukua hatua haraka kuimarisha mamlaka yake kupitia mpangilio wa uteuzi ambao ulifuta mpaka kati ya ofisi ya umma na maslahi ya familia binafsi.

Tangazo la televisheni la baraza jipya la mawaziri kutoka Ikulu ya Chamwino lilithibitisha kile ambacho wachambuzi wengi walikuwa wamekitabiri
wakati wa kampeni.

Kwamba uchaguzi haukuwa tu kuhusu kupata mamlaka bali kuhusu kusimika utawala wa kinasaba.

Kwa kuwatupa nje maafisa wakuu na kusimika wanachama wa familia yake ya karibu katika nafasi zao, Samia alibadilisha baraza la mawaziri kutoka kuwa chombo cha utawala wa pamoja kikatiba kuwa chombo cha kifamilia na cha kimakundi ambacho kazi yake kuu ni kuimarisha uaminifu, kudhibiti bajeti za kimkakati, na kuilinda urais dhidi ya ushindani wa ndani.

Katika kutekeleza azima yake hii Samia alimteua bintiye, Wanu Hafidh Ameir, kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia.

Uteuzi wa Wanu sio kwa sababu ya umri wake au hadhi yake ya ubunge, bali ni kwa sababu ya umuhimu wa wizara anayoiongoza kwa Samia.

Elimu inasalia kuwa moja ya sekta kubwa na muhimu zaidi kimkakati katika Tanzania. Ushawishi wake unakwenda mbali zaidi ya muundo wa mtaala hadi kwenye malezi ya kiitikadi ya vijana, usimamizi wa ajira za walimu, mzunguko wa fedha za umma katika miradi ya miundombinu, na uundaji wa utambulisho wa taifa.

Kwamba wizara hii ilikabidhiwa kwa jamaa wa karibu wa Samia mara tu baada ya uchaguzi wenye utata ambapo wapiga kura vijana waliunga mkono upinzani kwa nguvu zote inaonyesha uwepo wa hatua ya makusudi ya kuwaondoa watu walio tishio dhidi ya utawala.

Ni mkakati wa kujenga ushawishi wa kiitikadi kwa faida ya serikali kwa kupandikiza itikadi chanya kuanzia darasani moja kwa moja.

Vile vile uteuzi wa mkwe wake Samia, Mohamed Mchengerwa, kama Waziri wa Afya ni utekelezaji wa mkakati mahsusi.

Wizara ya Afya inaongoza baadhi ya matumizi ya juu zaidi katika bajeti ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa dawa, miundombinu ya hospitali, na fedha kubwa za wafadhili kutoka taasisi kama vile Mfuko wa Dunia na UNAID.

Uteuzi huu unaweka udhibiti wa mtiririko huu mkubwa wa kifedha ndani ya kaya ya Samia.

Katika mazingira ya kisiasa ambapo taasisi za usimamizi zimedhoofishwa na asasi za kiraia zimekandamizwa, mkusanyiko huu wa mamlaka huunda mazingira mazuri ya familia kukamata serikali.

Tanzania tayari imepitia kashfa, kama vile masuala ya EPA na Tegeta Escrow, ambapo fedha za umma zilichukuliwa kupitia mitandao ya madalali waliounganishwa kisiasa.

Kwa kumweka mkwewe kama mkuu wa wizara hii, Samia ameondoa kwa ufanisi ulinzi wa kimfumo ambao kihistoria ulizuia ufisadi mkubwa. Sasa, angalau fedha hiyo itaingia moja kwa moja katika sebule ya familia ya Samia.

Aidha, Samia ameimarisha mamlaka yake familia tawala kwa kuiunganisha kimkakati na mtandao wa kisiasa wa Kikwete kupitia uteuzi wa Ridhiwani Kikwete, mwana wa Rais wa zamani Jakaya Kikwete.

Ridhiowani ameteuliwa kuwa Waziri wa Usimamizi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya kupatanisha pande zote mbili kati ya utawala wa sasa na mitandao ya kisiasa iliyotawala CCM mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Kinadharia, wizara hii inasimamia uwajibikaji wa kiserikali kwa kufuata ngazi za kiutawala. Kiuhalisia, sasa ni Wizara ya "Zimwi Likujualo", ambapo kupandishwa vyeo, nyongeza za mishahara, na marupurupu hutolewa kulingana na pointi za uaminifu wa kifamilia.

Athari ya jumla ya uteuzi huu ni mabadiliko ya Tanzania kutoka kuwa dola ya kijamhuri na kugeuka "dola ya kifamle," ambayo hutawaliwa na wanaukoo.

Katika hali hii Tanzania inaendelea kuitwa Jamhuri kwa jina tu, lakini sifa zake za utendaji kazi zinadhibitiwa na maslahi binafsi ya kaya tawala.

Kwa kifupi, Jamhuri ya Tanzania iliyofikiriwa na Julius Nyerere imestaafu kwa heshima. Azimio la Arusha limebadilishwa na Sheria za Familia Samia, ambapo mamlaka ya kisiasa yanarithiwa, uaminifu ni sarafu, na ridhaa ya umma ni tanbihi ya hiari.

Kama hali hii isipobadilishwa kimkakati, Tanzania iko kwenye njia ya kuwa tamthilia ya hivi karibuni ya kiserikali ya Afrika Mashariki: mahali ambapo utawala ni burudani ya familia, bajeti ni zawadi za siku ya kuzaliwa, na demokrasia ni kitu ambacho kinasomwa kwenye vitabu vya kiada tu.

2. Elevation of Shariah Law over the Constitution and the Natural Moral Law:

Samia anatekeleza sera ya kuendesha nchi kwa kutumia mfumo wa sheria za kiislamu uitwao “Islamic shariah law.”

Huu ni mfumo rasmi wa sheria za kuendesha nchi katika mataifa ambayo ni wanachama wa Jumuiya ya Waislamu iitwayo “OIC”.

Wakati Tanzania sio, na haipaswi, kuwa mwanachama rasmi wa OIC (de-jure OIC member), sasa ukweli mchungu ni kwamba tayari Tanzania ni mwanachama asiye rasmi wa OIC (de-facto OIC member).

Hali halisi iko hivi: Katiba ya Tanzania (1977) inakataza uhalifu wa kijinai kama vile utekaji, utesaji wa raia, mauaji holela ya raia wasio na hatia, na ubadhirifu wa fedha, na utoroshaji wa mali za umma, isipokuwa kama uhalifu huu utafanywa na Rais mwenyewe wakati akiwa madarakani.

Ruhusa hii ya kikatiba, japo haiingii akilini, ipo kwenye ibara ya 46 ya Katiba yetu. Ibara hii inampatia Rais kinga dhidi ya mshtaka yoyote ya uhalifu wa kijinai atakaoufanya wakati akiwa Rais.

Hivyo, Rais wa Tanzania anaweza kujizuia kufanya uhalifu huu kwa mujibu wa sababu za kimaadili tu, kama zipo na anazikubali katika nafsi yake.

Tunazo dini kubwa mbili, yaani Ukristo na Uislamu. Kwa upande mmoja, basi, kama Rais ni Mkristo, atakuwa na machaguo mawili.

Ama atachagua mfumo wa Sheria ya Torati" yenye Amri 613 zikijumuisha "Amri Kumi za Musa,” zote zikiwa zinapatikana katika Biblia au atachagua mfumo wa Kanuni za Maadili Asilia zinazodokezwa kwenye Katiba ya nchi, ibara ya 3 kama ikisomwa pamoja na ibra ya 9(f).

Kwenye Katiba ya nchi yetu, nakala ya Kiingereza, kama inavyopatikana kwenye tovuti ya ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (National Audit Office), ibara ya 3(1) inasomeka, bila kuchakachuliwa, kama ivuatavyo:

"3(1) The United Republic is a democratic, secular and socialist state which adheres to multi-party democracy."
Lakini, mtu aliyeandaa nakala ya Kiswahili ya Katiba (1977) alichakachua ibara ya 3(1) kwa kuruka tafsiri ya neno "secular," ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya au kwa kuagizwa na watu wenye hulka ya udini, na hivyo kuifanya isomeke kimakosa hivi:

"3(1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia naya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa."

Lakini, ibara ya 9(f) kwenye katiba ya Kiswahili haina tatizo na inasomeka kama ifuatavyo:

"(9)(f) ... Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha ... kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa nakudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu."

Na kama Rais hajui ukuu wa misingi ya maadili asilia ndani ya dola ya kisekulari au anaujua lakini haikubali, basi, atatumia sheria ya Kibiblia iitwayo “Sheria ya Torati."

Kwa sababu hii Watanzania wasio Wakristo watageuka watumwa wa kiidini ndani ya nchi yao, maana Sheria ya Torati" ni "Sheria za Musa katika Biblia" ambazo ni kwa ajili ya Wayahudi na Wakristo pekee, na sio vijnginevyo.

Na kwa upande mwingine, kama Rais ni Muislamu, atakuwa na machaguo mawili pia.

Ama atachagua maadili ya Kurani yaitwayo “Islamic Shariah Lawau atachagua Kanuni za Maadili Asilia zinazodokezwa kwenye Katiba ya nchi, ibara ya 3 kama ikisomwa pamoja na ibara ya 9(f).

Na kama Rais hajui ukuu wa misingi ya maadili asilia ndani ya dola ya kisekulari au anaujua lakini haikubali, basi, atatumia mfumo wa maadili ya Kurani yaitwayo “Islamic Shariah Law,” ambao kwa sasa unatumika katika nchi 46 duniani kote.

1767076422752.png

Kwa sababu hii Watanzania wasio Waislamu watageuka watumwa wa kidini ndani ya nchi yao, maana Islamic Shariah Law” ni "Sheria za Mohamed katika Kurani" ambazo ni kwa ajili ya Waislamu pekee na sio vijnginevyo.

Mti hujulikana kwa matunda yake. Na kwa sababu hii kuna ushahidi wa kimazingira usiokanushika wenye kuonyesha kwamba Samia amechagua kutumia maadili ya Kurani yaitwayo “Islamic Shariah Law” katika kuendesha nchi.

Bahati mbaya tuliyo nayo Watanzania ni kwamba, mfumo wa "Sheria za Musa katika Biblia" na mfumo wa "Sheria za Mohamed katika Kurani" ni kama shilingi zenye pande mbili. Kila mfumo una "upande wa sifa nzuri" na "upande wa sifa mbaya."

Upande mbaya wa mifumo hii hausikilizani na ustaarabu wa haki za binadamu, kama zinavyofahamika katika milenia ya tatu, hasa tangu mwaka 1948 lilipotamkwa Tangazo la Dunia Kuhusu Haki za Binadamu.

Kwa upande mmoja, ubaya wa mfumo wa "Sheria za Musa katika Biblia" unatokana na sababu kadhaa. Lakini kubwa ni kwa sababu ya kuruhusu adhabu ya kifo kwa makosa madogo madogo kama vile kuabudu sanamu, kufuru, kumpiga mzazi, kudharau amri ya mahakama, na uzinzi.

Adhabu hizi zinapingana na fundisho kwamba kila binadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Hivyo, Agano Jipya ni kama "contract addendum" kwenye Agano la kale, ambapo, hii "contract addendum" inasemekana kubatilisha adhabu hizi, kulingana na skuli mojawapo ya wanateolojia wa Biblia wanaopenda kuwianisha Mfumo wa Maadili ya Biblia na Mfumo wa Maadili Asilia. Kanisa Katoliki na TEC yao liko katika kundi hili.

Kwa upande mwingine, ubaya wa mfumo wa "Sheria za Mohamed katika Kurani" unatokana na sababu kadhaa.

Lakini kubwa ni ukali wa adhabu kwa baadhi ya makosa ya kijinai kama vile wizi, uzinzi, uasherati, mavazi, unywaji wa pombe, kusikiliza muziki ya kisasa, kukataa mafundisho ya dini ya Kiislamu na kujitoa kwenye Uislamu, na kukosoa itikadi na sera zinazotekelezwa na serikali ya chama tawala kama walivyokuwa wanafanya Humphrey Polepole, Deusdedit Soka na Mdude Nyagali.

Adhabu dhidi ya makosa haya zinaweza kujumuisha kupigwa viboko, kupigwa mawe hadi kufa, kuuwawa kwa kuchinjwa kwa jambia hadharani, kukatwa mikono kwa panga, kutekwa na kuwekwa kizuizini mahali kusikojulikana, au mhusika kutekwa na kutelekezwa msituni ili afe kwa kuliwa na wanyama wakali.

Hizi ni adhabu ambazo watu wengi huziona kuwa haziendani na viwango vya kisasa vya haki za binadamu.

1766916971413.png

Jambiah: A Tool for public beheading as per Shariah Law

Kwa ujumla, “Shariah Law” ni mfumo unaongozwa na itikadi ya jino kwa jino, jicho kwa jicho, mkono kwa mkono, damu kwa damu, na matumizi ya "jambia" dhidi ya mtu asiyekubaliana na hoja hata bila kumpa haki ya kusikilizwa kwa ukamilifu.

Kwa sababu hizi zote, ni wazi kuwa “Shariah Law” ni mfumo ambao hautambui "ukuu" wa tunu ya uhai dhidi ya tunu baki.

Kimantiki basi, “Shariah Law” ni mfumo unaoruhusu utekaji, utesaji, na mauaji ya kupangwa na serikali. Na mwenye macho haambiwi tazama. Yote haya yanatokea katika Tanzania ya leo.

Na hakuna ubishi kwamba yanatokea kwa sababu Samia amechagua kuendesha nchi kwa kutumia "Sharia Law." Mti hujulikana kwa matunda yake na sio vinginevyo.

1766916138747.png

Lakini, kwa mujibu wa ibara ya 3 kama ikisomwa pamoja na ibara ya 12-32, ya Katiba ya nchi (1977), Tanzania ni dola isiyofungamana na upande wowote wa kidini.

Hivyo, inayopaswa kuongozwa kwa kufuata misingi ya maadili asilia, kama inavyotafsiriwa na sisi Watanzania wenyewe.

Tayari mara kadhaa Samia amemfahamishwa kwa udadavuzi wa maandishi laini kuhusu msingi wa ukweli wanaopigania GenZ.

Ameelezwa kwamba anapaswa kuendesha nchi kwa kufuata, sio matakwa binafsi wala misahafu, bali kwa kufuata misingi ya maadili asilia inayotajwa katika katiba ya nchi.

Mfano, amewahi kupewa ushauri Ufuatao kuhusu "MISINGI YA MAADILI ASILIA," yaani "NATURAL LAW POLICY FRAMEWORK," anayopaswa kuifuata:

“Specifically, in every human person’s nature there are natural inclinations that are the origin of our moral choices and actions, as opposed to our immoral choices and actions, namely: (1) Natural inclination to the good as opposed to an aversion to the evil; (2) Natural inclination to preserve life as opposed to an aversion to intentionally causing death of an innocent person; (3) Natural inclination to preserve health as opposed to an aversion to sickness; (4) Natural inclination to copulation as opposed to an aversion to pedication; (5) Natural inclination to marriage as opposed to an aversion to celibacy; (6) Natural inclination to knowledge of truth as opposed to an aversion to ignorance; (7) Natural inclination to live in society as opposed to an aversion to solitude; (8) Natural inclination to self-integration as opposed to an aversion to self-disintegration; (9) Natural inclination to ownership as opposed to an aversion to material poverty; (10) Natural inclination to technology as opposed to an aversion to technological aversion; (11) Natural inclination to personal self-determination as opposed to an aversion to subjugation; (12) Natural inclination to order as opposed to an aversion to chaos; (13) Natural inclination to peace as opposed to an aversion to violence; (14) Natural inclination to coherence as opposed to an aversion to incoherence; (15) Natural inclination to culture; (16) Natural inclination to the common good as opposed to an aversion to the common evil; and (17) Natural inclination to knowledge of religious truth as opposed to an aversion to religious ignorance.

Wanasiasa na viongozi wa dini wenye umakini wa kutosha, hufundisha juu ya umoja wa kitaifa kwa kusisitiza hii misingi ya maadili asilia, huku wakiwa wanazingatia ukweli kwamba, misingi hii inao ukuu juu ya sheria za misahafu ya kisekta, ukuu juu ya sheria za kimila na ukuu juu ya sheria zinazotungwa na bunge.

Samia na timu yake hawanekani kuwa na umakini wa kutofautisha ukuu wa misingi ya maadili asilia dhidi ya sheria za misahafu ya kisekta, sheria za kimila na sheria zinazotungwa na bunge.

Bila aibu, wameamua kujinasibisha na Tangazo la Haki za Binadamu la OIC lenye kupingana wazi wazi na Tangazo la Dunia Kuhusu Haki za Binadamu linalotambuliwa na Katiba ya Tanzania (1977) katika ibara ya 9(f).

Naongelea tamko liitwalo "The Cairo Declaration on Human Rights in Islam (1990)," linalomomonyoa haki za binadamu kwa kutumnia "Islamic shariah" kama ifuatavyo:

"2(a) It is the duty of individuals, societies and states to safeguard this right [to life] against any violation, and it is prohibited to take away life except for a shariah prescribed reason... 2(d) Safety from bodily harm is a guaranteed right. It is the duty of the state to safeguard it, and it is prohibited to breach it without a Shariah-prescribed reason... 12. Every man shall have the right, within the framework of the Shari'ah, to free movement... 19(d) There shall be no crime or punishment except as provided for in the Shari'ah... 22 (a) Everyone shall have the right to express his opinion freely in such manner as would not be contrary to the principles of the Shari'ah. (b) Everyone shall have the right to advocate what is right, and propagate what is good, and warn against what is wrong and evil according to the norms of Islamic Shari'ah. 23(b) Everyone shall have the right to ... assume public office in accordance with the provisions of Shari'ah. 24. All the rights and freedoms stipulated in this Declaration are subject to the Islamic Shari'ah. 25. [Islamic principles under] the Islamic Shariah is the only source of reference for the explanation or clarification of any of the articles of this Declaration."

Azimio la Cairo lilirekebishwa mwaka wa 2020, na kurithiwa na Azimio jipya la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) kuhusu Haki za Binadamu. Yaani, "The Cairo Declaration of the Organization of Islamic Cooperation on Human Rights (2020)," pasipo mabadiliko yoyote ya maana.

Kilichofanyika katika Azimio la OIC ni kuondoa maneno "Islamic Sharia Law" na kuingiza "Islamic Values and Principles [under shariah law]."

Haya ni mabadiliko hewa. Na kwa viwango vya kirazini, ni wazi kuwa Tamko la Cairo na lile la OIC yanakinzana sana na misingi ya Maadili Asilia.

1766982783613.png

3. War on Indigenous People in favor of Foreign Direct Investors:

Samia amefunga mikataba ya uwekezaji wa kigeni inayowasukuma watanzania wazawa nje ya njia kuu za uchumi. Mfano ni mkataba wa DP World katika bandari ya Dar Es Salaam, mkataba wa makaa yam awe huko Tanzania Kusini, Mkataba wa kuuza madini huko Mwadui, Mkataba wa Mwendokasi Dar, na mikataba kama hiyo.

Pia kuna mkataba wa kuwahamisha Wamsai wa Ngorongoro na kuwapeleka Tanga kinyemela ili kupisha wawekezaji wa Kiarabu katika biashara ya uwindaji na biashara ya kaboni kwenye bonde la Ngorongoro.

Hii ni biashara ya “trophy hunting and carbon trade” inayoendeshwa na Waarabu wa Dubai.

Kwa ujumla, Samia anatekeleza sera ya kuwageuza Watanzania watumwa ndani ya nchi yao. Jambo hili halikubaliki kwa kuwa ni aina mpya ya ukoloni mkongwe.

4. Detentive abductions, tortures and enforced dissappearances:

Samia anatekeleza sera ya kuwateka na kuwaweka katika kambi za watumwa waafrika wengi wanaomkosoa.

Kuna watu wengine wanapotea bila maelezo yoyote kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kulinda raia na mali zao.

Kwa mujibu wa ripoti ya chama cha wanasheria wa Tanganyika na UN tangu 2016, alipopotea Ben Saanane, tayari wamepotea Watanzania zaidi ya 200. Hii maana yake ni kwamba, Rais aliyekula kiapo cha kulinda usalama wan chi, raia na mali zao ameshindwa kazi hiyo.

5. Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity from criminal charges:

Samia anatekeleza sera ya kuua wakosoaji wake wazi wazi kama mbinu ya kubaki madarakani.

Kifo cha Mohammed Ali Kibao ni tukio muhimu sana kueleza ukweli huu. Tangu KIbao auwawe serikali haijawahi kutwambia lolote.

Ukimya huo maana yake ni kwamba ama serikali inahusika moja kwa moja au inahusika kwa njia ya mzunguko.

Lakini sio hivyo tu. Mauaji ya waandamanaji wakati wa wiki ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 ni mauaji ya kupanga.

Waandamanani walibatizwa jina la "vibaka wenye silaha" na kumiminiwa risasi za moto kama vile ni nyani. Takwimu rasmi hazijatangazwa na serikali.

Lakini sasa tunafahamu kuwa mauaji ya raia katika wiki ya uchaguzi ni makubwa kuliko mauaji ya raia yaliyofanywa na Idd Amin wakati wa vita ya Kagera, mwaka 1978-79.

Katika vita hiyo, waliuwawa raia wapatao 1,500. Kwa hiyo, mauaji ya Oktoba mwaka huu ni zaidi ya vijana 1,500. Yote haya ni mauaji holela yaliyo haramu kisheria.

Tunayaita "extra-judicial killings" na yanafanyika kwa sababu ya uwepo wa kinga ya kikatiba dhidi ya mashitaka ya jinai yanayomlenga Rais aliye madarakani.

Tunayo katiba ya hovyo sana, lakini Samia anaipenda sana katiba hii kwa sababu ya uhovyo huo.

6. Court authority perversion and litigation dramas:

Samia anatekeleza sera ya kuziteka mahakama na kuzitumia kuendesha kesi za kubumba na hatimaye kutoa humu za kisiasa, na hivyo kuunajisi mfumo wa utoaji wa haki.

Kesi ya uhaini inayoendelea dhidi ya Tundu Lissu na Kesi dhidi ya Bodi ya wadhamini wa chadema iliyosababisha Chadema kuzuiwa kutekeleza shughuli zake za kisiasa ni mifano hai.

Kwa ujumla, vyombo vya kisheria vilibadilishwa kuwa vyombo vya ukandamizaji. Vifungu vya kisheria ambavyo vinaweza kutumika kihalali kulinda utulivu vilitumika badala yake
kwa hiari kukandamiza upinzani.

Sheria ya Makosa ya Mtandaoni (2015) imetafsiriwa na kutekelezwa kwa njia ambazo zinaharamisha ukosoaji mtandaoni na ufichuzi wa taarifa.

Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari (2016) iliunda mifumo ya leseni za kiutawala na vibali ambavyo viliruhusu kusimamishwa na kufutwa kwa usajili wa vyombo vya habari.

Vifungu vya uchaguzi na udhibiti wa vyama vya siasa vilimpa mamlaka Msajili wa Vyama vya Siasa kuwaadhibu na kuwafuta usajili wapinzani.

Sheria hizi, pamoja na kanuni za kiutawala, kwa mfano, kanuni za maudhui mtandaoni na sheria za utulivu wa umma, zilitumika kama kifaa cha kisheria cha ukandamizaji huku, kwa nje, zikionekana kudumisha mwonekano wa uadilifu katika ngazi ya utaratibu.

7. Inquiry commissions dramas:

Samia anatekeleza sera ya kutumia Tume ya Uchunguzi kuwazunga wananchi kwa kuipangia ratiba ya miezi mitatu wakati kazi hiyo inaweza kufanyika kwa siku tatu na kukamilika.

Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 2025 wakati wa uchaguzi mkuu imepewa kazi ya kutafuta taarifa ambazo tayari rais anazo mezani kwake. Ukweli uko hivi:

  • MKurugenzi wa uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi wapo na wanajua kilichotokea vituoni nchi nzila,
  • Waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na Ma-RPC wapo na wanajua kilichotokea barabarani chini ya usimamizi wa Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Hajj,
  • Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Wizi wa Kutumia Silaha (Special Anti-Armed Robbery Unit-SARU) yupo na anajua kikosi chake kilifanya nini mitaani katika wiki ya uchaguzi na kwa maagizo ya nani,
  • DGIS, ZSOs, RSOs, DSOs, na field officers wa TISS wapo na wamekusanya taarifa za kilichotokea kwenye makaburi ya halaiki wakati intaneti na umeme vimekatwa,
  • Waziri wa Ulinzi, CDF, Wakuu wa Komandi za JWTZ wapo na wanajua kilichotokea mitaani nchi nzima,
  • Waziri wa TAMISEMI, ma-RCs, ma-DCs, ma-DEOs na wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa na wilaya wapo na wanajua kilichotokea kwenye mikoa, wilaya na tarafa zao katika wiki ya uchaguzi, na
  • Mkurugenzi wa Jukwaa la Wahariri, Wahariri na Waandishi wa habari wapo na wanajua matukio yote muhimu japo walikatazwa kuyachapisha magazetini.
Hivyo, taarifa za kawaida za kiutawala zinatosheleza mahitahi ya taarifa anazozihitaji Rais ili aweze kutekeleza majukumu yake.

Kwa sababu hizi zote hakuna sababu nzuri ya kuunda Tume inayopewa miezi mitatu kufanya kazi ya kutafuta ukweli unaojulikana, kama sio mkakati wa kuendesha nchi kiujanjaujanja.

8. Deregistration of critical associations:

Samia anatekeleza sera ya kufuta au kudhoofisha vyama vya kijamii, taasisi za dini, vyama vya siasa, na vyombo vya habari ili kudhoofisha sekta ua asasi za kiraia, na hivyo kupata unafuu wa kutawala bila kukosolewa.

Amesitisha au kudhoofisha shughuli za Kanisa la ufufuo na uzima, Chadema, Jamiiforums, JamboTV, Twitter(X), Telegram, Clubhouse, na tovuti 80,000 kwa mdai kwamba zina maudhi yasiyo adilifu, gazeti la The Chanzo.

9. Election rigging in the name of INEC’s constitutional immunity from criminal charges:

Samia kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi anatekeleza sera ya kuiba uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani tangi 2024. Mwitiko wa wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2025 haukuzidi 20% ya wapiga kura wote waliojiandikisha.

Hata hivyo, Tume ilitangaza matokeo yanayoonesha ushindi wa asilimia zaidi ya 80% kwa wagombea wote. Huu ni ulaghai usiofichika na wenye kuondoa uhalali kwa serikali ya sasa.

Mara tatu, kupitia hotuba zake, Samia amejaribu kutetea ushindi wake pasipo mafanikio. Kila anapojaribu kufafanua ndivyo anavyoongeza mashaka kuhusu uhalali wake.

Ujasiri huu wa kuiba uchaguzi, hasa kura za Rais, unatokana na kinga ya kikatiba iliyo nayo Tume, pale inapokuwa imetangaza mshindi wa kiti cha Urais.

Ibara ya 41(7) inazuia mahakama za Tanzania kusikiliza kesi yoyote ya kupinga tangazo la ushindi huo.

Lakini, ibara hii inapingana na ibara ya 5(1) na ibara ya 8(1) zinazosema madaraka ya serikali yatatoka kwa watu kwa njia ya kuopiga kura.

Pasipo fursa ya kuomba mahakama ihakiki usahihi wa kura zilizotangawa, wanancho wanaweza kuporwa “ukuu” wao kama “wenye nchi” bila kuwa namna ya kujitetea.

Sasa Samia anatumia mwanya huu kufanya uhalifu wa kisasa wazi wazi halafu anasema kuwa yeye ni Rais halali. Hapana. Ushahidi ulioko mitaani kutoka kwenye vituo vya kupigia kura haukubaliani na utapeli huo.

Ukweli ni kwamba, Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 2025 haukuwa zoezi la kidemokrasia la kweli bali ulikuwa igizo lililopangwa kufanyika kwa kutumia taratibu za uchaguzi baada ya serikali kuvunja masharti muhimu ya ushindani wa kisiasa wenye maana.

Kufikia siku raia walipokwenda kwenye vituo vya kupigia kura, matokeo yalikuwa tayari yamepangwa mapema kwa kuwaweka kizuizini na kuwaengua kimkakati viongozi wakuu wa upinzani, kuvizuia vyama vikuu vya upinzani kufanya siasa, kupiga marufuku mikutano ya hadhara, na kufanya vitisho dhidi ya wapiga kura.

Kipindi cha uchaguzi kilionyesha zaidi ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kutorosha watu na kuwapeleka kusiko julikana kwa lazima, mauaji ya kiholela yaliyo kinyume cha sheria, mateso, na kuzimwa kwa intaneti nchi nzima kwa kiasi ambacho kilizuia uwazi katika mchakato wa uchaguzi.

Aidha, matukio haya yanaashiria uvunjifu mkubwa wa katiba ya nchi ambapo taasisi kama vile mahakama, bunge, na tume ya uchaguzi zilishindwa kabisa kufanya usimamizi wa michakato ya kiserikali wenye maana.

Mifumo ya kisheria ilitumiwa ili kutoa uhalali kwa wakandamizaji, huku uteuzi wa wanafamilia na marafiki baada ya uchaguzi ukifichua uimarishaji wa mfumo wa utawala uliobinafsishwa na usiowajibika.

Kwa ujumla, mgogoro wa Tanzania katika wiki ya uchaguzi mkuu unaleta hatari kubwa kwa utulivu wa kikanda, kwa kuongeza uwezekano wa kuingilia siasa kijeshi, na kudhoofisha kanuni za kidemokrasia za Afrika.

Ukimya na kutochukua hatua kwa vyombo vya kikanda, hasa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki, sio tu kwamba vinawezesha mkondo huu wa kimabavu lakini pia vinaweka mfano hatari kwamba uchaguzi unaweza kuibwa na haki kukiukwa kwa kiwango kikubwa bila wahusika kuchukuliwa hatua yoyote.

10. Disinformation, media adoption and mind capture:

Samia anatekeleza sera ya kuteka akili za umma kwa kuwanyima habari sasa na kuwalisha habari zilizochujwa.

Samia amelazimisha vyombo vyote vya habari kufanya kazi kama idara ya serikali inayosimamia mahusiano kwa umma. Kwa sasa zinaandikwa habari zisizo na ukosoaji wa aina yoyote dhidi ya serikali.

Hata Jukwaa la wahariri (TEF) limefyata mkia kabisa. Kimapokeo, sekta ya habari inayo majukumu matatu.

Kuna majukumu sita yanayoifanya sekta ya habari kuwa mhimili wa nne wa dola.

Mosi, ni kuandika habari za udukuzi (watchdog), yaani kutafiti na kuchapisha habari za rushwa, kashfa, uzembe, na kuwakosoa wakubwa kwa lengo la kuimarisha utawala bora.

Pili, ni kuchuja, kuhariri na kuandika habari zenye maslahi kwa umma (gatekeeping), katika namna ambayo ni salama na yenye faida kwa umma.

Tatu, ni kuandika habari zenye kuibua matatizo ya kijamii na kupendekeza majibu yake kwa watawala (agenda setting), yaani kuifanya jamii ione matatizo yake na kuyapa vipaumbele sahihi katika kuyatatua.

Nne, ni kutunza kumbukumbu za maisha ya jamii (scorekeeping), yaani kufuatilia siku hadi siku matukio muhimu na kutunza shajara maalum kwa ajili ya matumizi ya baadaye, kwa lengo la kuonyesha nano anafanikiwa, nani anashidwa, na kusaidia kuionyesha jamii wapi inapaswa kwenda kwa kuzingatia ilikotoka.

Tano, ni kueneza utamaduni wa jamii (cultural Transmission), yaani kuandika, kueneza imani, tunu na maadili ya jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Na sita, ni kuwa jukwaa la majadiliano huru ya umma (public forum/agora), yaani kuisadia jamii kupata jukwaa linaloweza kutumiwa na jamii kama soko la mawazo mseto, majadiliano na hatimaye kama njia ya kusukuma mawazo ya pamoja ili yafike serikalini na kufanyiwa kazi.

Lakini sasa, Samia amevipiga marufuku vyombo vya habari kutekeleza majukumu yote haya.

Anachokisema yeye ndio kinapaswa kuchukuliwa kama ukweli, na wengine wote ni waongo. Huu ni uvunjaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania (1977).

11. Military integrity perversion, politicization and paralysis:

Katika uendeshaji wa nchi, utaratibu wa kikatiba unaofanya kazi vizuri unategemea uwepo wa vyombo vya usalama ambavyo havina upande wowote, vinawajibika
na vinavyohesnimu utawala wa kiraia.

Lakini, katika kipindi cha matukio ya baada ya uchaguzi mkuu, vyombo vya usalama, hasa polisi na jeshi, vilionekana kutumika kama vyombo vya udhibiti wa kisiasa kwa ajili ya kukandamiza maandamano, kuwakamata viongozi wa upinzani, na kulinda matokeo ya uchaguzi yenye utata wa kisiasa.

Mbinu kali za kijeshi, kutorosha watu kwa lazima, na matumizi ya nguvu kali dhidi ya waandamanaji zilionyesha kwamba vyombo vya usalama vilifanya kazi kama watendaji wa chama tawala badala ya kuwa walinzi wa utulivu wa umma wasio na upande wowote.

Pale ambapo mnyororo wa amri unaofuata muundo wa kiutawala inapowekwa chini ya maelekezo ya kisiasa na mashtaka dhidi ya watu wanaokiuka sheria kufanyika kwa upendeleo au kutokuwepo kabisa, basi, milango kwa ajili ya watu kuwekwa kizuizini na kuteswa kiholela huwa imefunguliwa, na hili lilitokea.

Na kwa ujumla, kubadilisha matumizi ya vyombo vya usalama kuwa watendaji wa chama tawala ni ishara ya tukio la anguka la kikatiba, na hili limetokea katika wiki ya uchaguzi.

Lakini, mpaka leo, swali kubwa zaidi linalowaumiza vichwa wajasiriadola kuhusu utendaji kazi wa JWTZ ni hili hapa:

Kwa nini
, wakati wa wiki ya uchaguzi mkuu wa 2025, raia wasio na hatia zaidi ya 1,500 waliuwawa kama kuku kwa risasi za moto bila JWTZ, ambalo ni "jeshi la wananchi," kuchukua hatua stahiki za kuzuia maafa haya?

Jawabu linalotokana na utafiti wangu ni kwamba, ni kwa sababu Samia anatekeleza sera ya uteuzi wa viongozi wakuu wa komandi za JWTZ katika namna ambayo inawalazimisha viongozi wakuu wa JWTZ kuingia katika siasa za kulinda uhalifu wa kimtandao serikalini badala ya kulinda raia.

Uhalifu wa kimtandao unaoudhoofisha uongozi wa JWTZ unaonekana kuanzia kwenye mradi wa ununuzi wa vifaa vya kijeshi kutoka huko UAE na Uturuki. Kiungo muhimu katika miradi hii kati ya viongozi wa JWTZ na Samia ni Angela Kizigha (pichani).

1767029621348.png

Uwezekano mkubwa ni kwamba mikataba ya ununuzi wa vifaa vya kijeshi kutoka UAE na Uturuki intatumika kama mkakati wa kutakatishaji matrilioni ya fedha kutoka Tanzania kwenda Uturuki na UAE kwenye biashara za Familia ya Samia zinazohusiana na majumba ya kupangisha, yaani "real estate business."

Matrilioni haya ni sehemu ya mikopo inayochukuliwa na Tanzania kutoka vyanzo mbalimbali.

Sehemu ya mikopo hiyo inaonekana kumegwa na kuhamishiwa ughaibuni kwa msaada wa Utatu Mtakattifu kati ya viongozi wa JWTZ, Familia ya Samia na Angela Kiziga, anayesemakana kusimamia biashara za familia ya Samia huko Uturuki na UAE.

Kwa sababu vifaa vya kijeshi vinagawiwa kwenye komandi zote za JWTZ, mradi huu, pamoja na makandokando yake, vinawagusa wakuu wa komandi husika.

Hawa ndio wanaongoza JWTZ. Hivyo, wakubwa hawa wanajikuta njiapanda ya ama kumtumikia Kaizari au kumtumikia Mungu wa Katiba. Matukio ya wiki ya uchaguzi mkuu ni ushahidi tosha kwamba wakuu wa komandi za JWTZ wamelazimika kumtumikia Kaizari.

Waturuki na Waarabu ni sehemu muhimu ya mmomonyoko wa nidhamu ya wakubwa hawa ndani ya JWTZ na ndani ya Jeshi la Polisi, maana hata huko kuna mikataba ya kununua vifaa vya kijeshi na kipolisi inayosimamiwa na Angela Kizigha.

Kwa ajili ya kufanikisha "mchongo" huu unaohusisha nchi za Kiislamu, inaonekana kuwa, Samia aliamua kuteua wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao ni Waislamu zaidi, ukiondoa CDF na IGP ambao ni Wakristo. Ni mkakati uliosukwa kisayansi na kwa siri kubwa.

Ni sahihi kuhitimisha kuwa, ni kwa sababu hizi, maamuzi ya Samia yamedumaza utayari na weledi wa uongozi wa kijeshi kwa sababu ya kutumia ukanda na udini kama vigezo vya uteuzi, na hatimaye kutumia kanuni ya "zawadi kwa wakubwa wanaofanikisha mchongo," kanuni ambayo hatimaye imeifanya JWTZ na Jeshi la Polisi kushindwa kutekeleza jukumu yao ya kikatiba ya kulinda uhai wa Taifa, raia na mali zao dhidi ya maadui wa ndani na nje.

Lakini sio hivyo tu. Samia amekuwa akitoa kauli na maagizo yanayomomonyoa nidhamu ya JWTZ na Jeshi la Polisi.

Mfano, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania, siku moja, aliliagiza jeshi kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Agizo hili lilitolewa mnamo 22 Januari 2024, wakati wa Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama (CDF) na Makamanda jijini Dar es Salaam. Malengo makuu ya agizo hilo yalionekana kuwa ni mawili.

Mosi, kuhakikisha usalama wa nchi unakuwa wa kutosha wakati wa mchakato wa uchaguzi, kwani chaguzi zinahusisha vyama vingi na mitazamo tofauti, na hivyo kuna uwezekano wa kutokea changamoto zisizotarajiwa.

Na pili, Kutoa tahadhari viongozi wa jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama ili wawe tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.

Rais alisisitiza kuwa maandalizi hayo hayamaanishi matumizi ya nguvu, bali ni kuhakikisha taratibu, sheria na miongozo ya uchaguzi inafuatwa huku jeshi likiwa limekaa tayari kudhibiti uvunjifu wa amani.

Kwa sababu hii, tamko la CDF, saa mbili usiku, tarehe 30 Oktoba 2025, lilionyesha wazi kwamba alikuwa tayari kuliingiza jeshi barabarani ili kukabiliana na waandamanaji, ambapo yeye alishauriwa na wasaidizi wake, ambao ni wakuu wa komandi za JWTZ, awatambulishe waandamanaji kama “vibaka wenye silaha.”

Lakini makapteni wa JWTZ hawakukubaliana na mtazamo wa Afande CDF na wasaidizi wake. Walimgomea wakimtaka atoe tamko la kuchukua nchi.

Kilichofuata ni Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Vibaka wenye Silaha (Special Anti-Armed Robbery Unit-SARU) kuingizwa mitaani wakiongozwa na kaulimbiu hiyo hiyo ya “vibaka wenye silaha wauwawe.”

Waandamanaji wakavalishwa “joho la vibaka wenye silaha” na wakauwawa kama kuku bila kutofautisha kati ya kibaka na mwandamanaji.

CP Awadhi Hajj anapaswa kujua vizuri zaidi walichofanya hawa vijana wa SARU kwa kuwa wako chini ya ofisi ya Mkuu wa Operesheni za Polisi anayoiongoza yeye.

Wakati SARU wanaendelea kukabiliana na kilichoitwa “vibaka wenye silaha” JWTZ wachache waliokuwa barabarani wakajikuta wanakabiliana na SARU kwa upande mmoja na majeshi ya kukodi kutoka nje kwa upande wa pili.

JWTZ waliwaua baadhi ya wanajeshi wa kigeni na wengine kuwaweka mateka. Lakini JWTZ wakaambiwa na wakubwa kwamba hao mateka waachiwe kwa kuwa ni kikosi cha “kazi maalum.”

Jeshi la polisi liliwakabili waandamanaji kwa kutumia taarifa za kiintelijensia zilizokuwa zinakusanywa kwa kutumia magari ya kivita tuliyouziwa na kampuni ya Uarabuni inayoitwa STREIT, mradi ambao ulisimamiwa na Swahiba wa Samia aitwaye Angela Kiziga. Mfano wa magari hayo huu hapa:

1767009196460.png

Mfano wa magari ya kijeshi na kipolisi yanayonunuliwa na serikali ya Tanzania kupitia udalali wa Angela Kizigha kutoka Uturuki na Uarabuni.

Magari haya huwa yanapaki kandoni mwa barabara, hasa katika sehemu za makutano, yakiwa na kamera na antenna za kurusha mawimbi mbashara kwenda kwenye kituo cha taarifa jumuishi (control center).

Kwa upande wa Dar Es Salaam mara nyingi magari haya utayakuta Ubungo mtaa, Magomeni, Ocen Road, Faya, Posta Mpya na Kariakoo.

Baadhi ya magari haya yanamilikiwa na JWTZ wakati mengine yanamilikiwa na polisi. Lakini pia, JWTZ walionekana wakifanya doria kwa kutumia magari ya kivita tuliyoyanunua kutoka Uturuki, aina ya "Nurol Makina".

Kwa hiyo, JWTZ walikuwa na nafasi ya kukusanya taarifa haraka na kubaini ukweli kwamba dhana ya “wale sio waandamanaji bali ni vibaka wenye silaha” haina ukweli mwingi.

Hivyo wangegundua kwamba mauaji holela ya waandamanaji ni haramu na hatimaye kuingilia kati kwa mujibu wa dhaman yao ya kikatiba.

Lakini, JWTZ hawakufanya hivyo, kwa kuwa CDF alikuwa tayari amemezeshwa msimamo kwamba “wale sio waandamanaji bali ni vibaka wenye silaha.”

Adande CDF aliendelea na msimamo huu hata baada ya makapteni wake waliokuwa “field” kumpa taarifa mbadala, na kumtaka atoe tangazo la “kuchukua nchi” ili kutuliza “upepo mbaya.”

Hata hivyo, afande CDF alikatazwa na washauri wake wakuu ambao ni wakuu wa komandi za kijeshi, mkurugenzi wa intelijensia jeshini na mkuu wa utumishi jeshini.

Wakubwa hawa wote walikubaliana na kaulimbiu kwamba “wale sio waandamanaji bali ni vibaka wenye silaha.”

Kwa hiyo, ni sahihi kuhitimisha kwamba, tekinolojia ya kijeshi kutoka UAE imechangia katika kufanikisha vifo vya Watanzania katika wiki ya uchaguzi kwa njia ifuatayo:

Jeshi la polisi wameitumia kukusanya taarifa za watu walioitwa “vibaka” na wakafanikiwa kuwashughulikia kwa kutumia risasi za moto.

Lakini, hata JWTZ walitumia tekinolojia hii kukusanya taarifa za “waandamaji” ili waweze kuwapa ulinzi stahiki ili wafanikishe azima yao ya kupigania Tanzania mpya kwa njia ya maandamano ya kufa na kupona.

Hata hivyo, taarifa hizi hazikuwa na msaada maada wakubwa walishaweka msimamo unaowashangaza watu wengi hadi leo.

Kwa sababu hii, tangu siku hiyo ya tarehe 30 Oktoba, makapteni wengi hawana imani na afande CDF, hawana amani na wakuu wa Komandi za JWTZ, hawamwamini Mkuu wa Intelijensia wa JWTZ, na wanamtazama Mkuu wa Utumishi Jeshini kwa kumshangaa hadi wanashindwa kumshangaa.

Kwa ujumla, ukweli kwamba JWTZ walishindwa kuzuia mauaji ya Watanzania zaidi ya 1,500 yaliyofanyika kwa kupangwa ndani ya siku tatu mfululizo, ni ushahidi tosha kwamba, jeshi letu limetekwa na viongozi wasiojua dhima asilia ya JWTZ kiasi kwamba kwa sasa ni sahihi kusema kuwa "uongozi wa sasa wa JWTZ unmefanya JWTZ kuonekana kama sio jeshi la wananchi.”

Hili ni tatizo kubwa la kiusalama, na lazima litatuliwe kwa kushughulikia chanzo chake.

12. Organized violence against republican principles:

Samia anatekeleza sera ya ama kudhoofisha au kufuka mfumo wa kijamhuri nchini Tanzania.

Ndani ya chama chake CCM alizuia ushindani ili apite kama mgombea pekee asite na mpizani. Nje ya CCM, akafanya vivyo hivyo. Kwanza alimfunga mpizani wake mkuu Tundu Lissu.

Kisha akatumia mbinu za ubaguzi wa kitaasisi kumwondoa mpinzani wake wa pili, Luhaga Mpina, kwenye uchaguzi.

Badala yake akatengeneza wagombea dhaifu kupitia vyama vya upinzani vyenye “kazi maalum.”

Akashindana nao na hatimaye akatangazwa mshindi kwa 98%, wakati wapiga kura waliojitokeza vituoni hawazidi 10%.

Hapa hakuna demokrasia. Kanuni ya Jamhuri kwamba madaraka hutoka kwa watu kupitia ushindani wa kidemokrasia imekiukwa. Matendo haya yanakiuka Katiba ya ncho ambayo Samia aliapa kuilinda.

13. Parliamentary incapacitation and legislative dramas:

Rais Samia anatekeleza sera ya kuendesha nchi kwa kuliteka Bunge. Alianza kwa kulilazimisha lipitishe mkataba wa kimataifa wa DP World, kisha mikataba ya bandari ya Bagamoyo na makaa ya mawe ya Kiwira.

Baadaye Samia akalilazimisha lipitishe marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa iliyompa madaraka ya Kimungu.

Na hivi karibuni amekuwa na maamuzi ya veto kuhusu nani awe mgombea ubunge na yupi asiwe.

Lengo ni kuwa na wabunge walio upande wake, wasiohoji lolote. Uhuru wa Bunge umeingiliwa, kiasi kwamba kanuni ya kikatiba kuhusu mgawanyo wa madaraka haina nafasi. Uvunjwaji wa katiba wa kiwango hiki haukubaliki.

Kwa ujumla, Bunge, mfumo wa kamati ya bunge, na mifumo ya usimamizi wa bajeti ni ukaguzi wa kawaida wa mstari wa kwanza kuhusu kudhibiti nidhamu ya serikali.

Katika wakati wa baada ya uchaguzi, jukumu la utendaji la Bunge lilipunguzwa kupitia mchanganyiko wa mambo yafuatayo: idadi kubwa ya wabunge wa chama kimoja waliotokana na matokeo ya uchaguzi; uteuzi wa wafuasi katika nafasi za mawaziri na viti vya kamati, ikiwa ni pamoja na watu wenye uhusiano wa kifamilia au uswahiba na serikali; na uharakishwaji wa utunzi wa sheria unaoambatana na utii wa kamati za bunge kwa chama tawala.

Hatimaye, mapitio ya kibunge ya uteuzi wa watendaji wa serikali, usimamizi wa matumizi ya umma, na hatua za kiusalama zinazoweza kuchukuliwa na bunge dhidi ya serikali zilikoma.

Hivyo, kulibadilisha bunge kutoka chombo kinachosimamia uwajinikaji hadi kuwa chombo cha kugonga mhuri na kuidhinisha maamuzi ya serikali bila kuyachuja.

14. Police and paramilitary forces brutality:

Samia anatekeleza sera ya kulitumia jeshi la polisi kama idara ya CCM. Ni jeshi ambalo limejenga chuki kuu dhidi ya raia wasio wana CCM.

Jeshi linatii maagizo ya viongozi wa CCM hata pale ambapo sheria zinakataza utii wa aina hiyo.

Wahalifu waliovaa nguo za kijani ni raia wema kwa mujibu wa polisi, lakini wasiovaa nguo za kijanii ndio wanavunja sheria. Polisi wanakamata watuhumiwa kininja, usiku wa manane, mbele ya wanafamilia.

Badala ya kuwa walinzi wa raia wema na mali zao, sasa wamegeuka kuwa walinzi wa wana CCM na mali zao. Huu ni utovu wa nidhamu usiokubalika.

15. Embezzlement of financial and natural resources:

Samia anatekeleza sera ya ubadhirifu wa fedha na mali za umma kwa kasi kana kwamba baada ya kundoka ofisini ataondoka nchini na kuhamia Uturuki au Uarabuni.

Mara tu alipoingia madarakani alipandisha mshahara wake kutoka milioni 10 kwa mwezi alizokuwa anapokea hayati Magufuli hadi milioni 30 kwa mwezi. Hili ni ongezeko la 300%.

Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1999, ambayo ilirekebishwa mwaka 2005, inaeleza kuwa Rais Mstaafu anapomaliza kipindi chake cha uongozi, atalipwa posho ya kila mwezi kiasi cha asilimia 80 ya mshahara wa rais aliyeko madarakani.

Mafao hayo ya viongozi wa umma yanampa nafasi Waziri Mkuu mstaafu na makamu wa rais fursa kama anazopata Rais.

Aidha, Rais mstaafu, Makamu wa Rais Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu akifariki dunia, mke au mume wake hupewa posho kiasi cha asilimia 40 ya mshahara wa rais aliye madarakani.

Hivyo, kwa uamuzi wa Samia, kila kiongozi mstaafu anayepaswa kupata 80% ya mshahara wa kiongozi anayekalia ofisi aliyokuwa anaikalia mstaafu, alipata na anaendelea kupata ongezeko la 300% kila mwezi.

Samia ameuza hisa za mgodi wa almasi wa Mwadi kwa bei ya kutupa; ameuza mgodi wa makaa yam awe kiwira kwa bei ya nyanya; ameuza misitu yetu kwa waarabu wanaofanya biashara ya hewa ya ukaa; ameuza wanyama wetu walioko kwenye mbunga za wanyama kwa wanaofanya biashara kuwinda.

Lakini sio hivyo tu. Samia amekopa matrilioni ya fedha na kupanua deni la Taifa hadi kufikia TZS 125 trillion, kama jedwali hapa chini linavyoonyesha.

1767017417152.png

Source: Tanzania Investment and Consultant Group Ltd (TICGL)

Kwa ujumla, katika miongo sita ya uhuru, tangu 1961 mpaka 2025, deni la Taifa limekua kutoka $0.2 billion mwaka 1961 mpaka $53.5 billion mwaka 2025, ambayo ni sawa na ongezeko la 26,650%.

Tangu 2021, wakati wa Rais Samia deni hili limekuwa likikua kwa $6.25 billion kwa kila mwaka. Kwa njia ya ulinganisho wa ukuaji wa deni toka awamu moja hadi nyingine, takwimu ziko hivi:

1767017608845.png

Kwa ujumla, kasi ya ukuaji wa deni hili wakati wa Samia inazua swali moja kubwa kuhusu mantiki ya uamuzi wa kukopa.

Kwa kawaida tunapaswa kukopa kwa sasabu tunao upungufu katika makusanyo ya kodi ya ndani ya nchi. Hii maana yake ni kwamba, kadiri makusanyo ya ndani yanavyopanda, kiasi cha mikopo ya serikali kinapaswa kushuka. Lakini, takwimu zinaonyesha ukweli kinyume chake.

Yaani, kadiri makusanyo ya kodi ya ndani yanavyopanda chini ya serikali ya Samia, kiasi cha mikopo ya serikali ya Samia inapanda pia, badala ya kushika.

Takwimu zitasaidia kuonyesha ukweli huu vizuri, kwa kujaribu kujibu swali lifuatalo kimahesabu: "What is the impact of the size of domestic tax revenues on the magnitude of national public debt?"

Yaani, "Je, mabadiliko katika ukubwa wa deni la Taifa yanatokana na mabadiliko katika makusanyo ya kodi ya ndani ya nchi?

Kinadharia, kuongezeka au kupungua kwa mikopo ya serikali (M) kunaweza kutokana na sababu zifuatazo: nakishi ya kibajeti inayotokana na kupungua kwa makusanyo ya kodi ya ndani ya nchi (N), maamuzi mengine ya kisera serikalini kaka vile gharama za vita(S), na hekaheka za kiuchumi kutoka nje ya nchi (H).

Yaani, "M is a function of N, S and H." Na kimahesabu tunaweza kuandika hivi: M=F(N,S,H).

Na kama tukikadiria uhusiano wenye sura ya mstari mnyoofu katika vibadilika vilivyotajwa, basi, tutakuwa na uhusiano wenye sura ya mlinganyo ufuatao: M=aN + bS +cH + d.

Katika mlinganyo huu, herufi tatu za "M, N, H" ni vibadilika (variables), herufi "M" ni kibadilika tegemezi (dependent variable); herufi "N" na herufi "H" ni vibadilika huru (independent variables); na herufi tatu za "a, b, c, d" ni parameta (constants).

Kisha, parameta "a" inaeleza ukubwa wa mchango wa kibadilika "N" kwenye ukubwa wa kibadilika "M"; parameta "b" inaeleza ukubwa wa mchango wa kibadilika "S" kwenye ukubwa wa kibadilika "M"; na parameta "c" inaeleza ukubwa wa mchango wa kibadilika H kwenye ukubwa wa kibadilika "M."

Sasa tunaweza kupima mchango wa kibadilika tegemezi kwenye ukubwa wa kibadilika huru katika mlinganyo huo hapo juu kwa kutumia ushahidi wa kitakwimu halisi.

Tutatumia ushahidi wa takwimu halisi za mikopo na nakishi katika makusanyo ya kodi katika kipindi cha mwaka 2020-2024 pamoja na takwimu za mwaka 2025 kwa kipindi cha Januari-Septemba, ambapo takwimu za Januari-Septemba 2025 zimetumika kukadiria takwimu za mwaka mzima.

1767015914228.png

Sources: Tanzania Investment and Consultant Group Ltd and Tanzania Investment and Consultant Group Ltd

Uchambuzi wa sababu na matokeo (correlation analysis) kati ya nakishi kwenye makusanyo ya kodi ya ndani na deni la Taifa, kwa kutumia programu ya "Correlation Analysis" kwenye Tekinolojia ya Microsoft Excel, unaonyesha kuwa thamani ya parameta ya "a" ni "+0.63."

Hii maana yake ni kwamba, kuna uhusiano chanya (positive correlation relationship) kati ya mikopo na nakishi katika ukusanyaji wa kodi.

Uhusiano huu unaonyesha kuwa, kadiri nakishi katika makusanyo ya kodi ya ndani inavyopungua kwa Shillingi 100, mikopo ya serikali inaongezeka kwa shilingi 63 tu, badala ya kupungua.

Yaani, tangu 2020 kadiri nakishi katika makusanyo ya kodi ya ndani inavyopungua, ukubwa wa deni la Taifa linaongezeka, badala ya kushuka.

Ndio kusema kuwa, kuna "positive correlation coefficient" ya 0.63, sawa na 63%. Yaani, kushuka kwa nakishi katika makusanyo ya kodi kunachangia ongezeko la deni la Taifa kwa 63%. Hiki ni kitendawili.

Yaani, swali la "Kwa nini ongezeko la makusanyo ya kodi linaongeza deni la taifa badala ya kulipunguza?" halina jawabu kutokana na uchambuzi huu.

Hiki ni kitendawili kinachohitaji majibu kutoka kwa wachumi kama vile Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa muda mrefu, na wataalam kutoka ofisi ya CAG, ofisi za FIU, ofisi za TAKUKURI, na ofisi za DGIS.

Lakini, taarifa nilizonazo zinataja sababu mojawapo ya ukopaji huu ni dhamira ya utakatishaji wa fedha za kiwango cha matrilioni kwenda Uturuki na Uarabuni kwenye miradi binafsi ya Samia.

Nitaeleza kidogo. Kwa mujibu wa Tanzania Investment and Consultation Group Ltd, hadi Septemba 2025, mchanganuo wa deni la taifa ulikuwa hivi:

Deni la taifa la Tanzania lilifikia TZS trilioni 127.47, ambapo, deni la nje lilichangia TZS 90,015.4 trillion (70.6%), na deni la ndani lilikuwa TZS TZS 37,459.1 trillion (29.4%).

Bila kuongelea mgawanyo wa kisekta wa mapato ya serikali kutoka TRA, mgao wa Mapato yanayotokana na Deni la Nje kwa kila Sekta hadi Septemba 2025 uko hivi:

1767005407834.png

Source: Tanzania Investment and Consultant Group Ltd (TICGL)

Hakuna takwimu za kuonyesha Muundo wa Deni la Ndani, ambalo ni sawa na 29.4%, kwa kuzingatia Mgawanyo kwa kila sekta.

Hivyo, kwa ujumla, mpaka sasa, matrilioni ya deni la Taifa hayajulikani inakwenda wapi. Wakubwa zetu walioko ofisi ya CAG, TAKUKURU na FIU wanapaswa kujipanga vizuri ili kulisaidia Taifa katika eneo hili.

Nadharia iliyopo na yenye kuaminika ni hii: Mikataba ya kununua vifaa vya kijeshi kutoka kampuni ya STREIT ya huko UAE na kutoka Uturuki, inayoratiniwa na Angela Kiziga, ndio mkakati wa kufanikisha utakatishaji wa matrilioni kutoka Tanzania kwenda Uarabuni na Uturuki. Kazi kwenu nusanusa wa CAG, TAKUKURU na FIU.

Na kwa ujumla, wadadisi wa mambo sasa wanapendekeza kuwa, huenda theluthi moja tu ya mikopo inayozalisha deni la Taifa tangu 2021 ndio imeingizwa nchini kwenye miradi.

Wanapendekeza kuwa theluthi ya pili imeingizwa nchini na kisha ikahamishiwa Uturuki kwenye biashara za majumba (real estates) ya Samia.

Huu utakuwa ni utakatishaji wa matrilioni ya fedha kwa kutumia mikataba ya kununulia vifaa vya kijeshi na kipolisi tunavyonunua kutoka huko Uturuki.

Na kwamba, theluthi ya tatu imeingizwa nchini na kisha ikahamishiwa UAE kwenye biashara za majumba (real estates) ya Samia.

Pia, huu utakuwa ni utakatishaji wa matrilioni ya fedha kwa kutumia mikataba ya kununulia vifaa vya kijeshi na kipolisi tunavyonunua kutoka huko UAE kwenye kampuni ya STREIT.

Na kwa ujumlam, huu ni uporaji wa rasilimali za nchi ambao unavipa vyombo vya ulinzi na usalama sababu tosha ya kumwondoa Samia ofisini na kuanza mkakati wa kurejesha fedga hizo zilizoporwa.

Ni katika mazingira haya swali moja kuu linazuka. Kuna haja ya TAKUKURU, FIU na Polisi kuhangaika na rushwa, money laundering, na makosa kama hayo yenye kuhusisha “pesa ya mboga” wakati Rais anatakatisha na kuhamisha matrilioni kinyemelea namna hii?

Jawabu langu ni ndio, ikiwa TAKUKURU, FIU na Polisi watatusaidia kurudisha hayo matrilioni yaliyototoshewa Uturuki na Uarabuni.

Uamuzi wetu wa kununia magari na vifaa vya kijeshi haupaswi kuwa mkakati wa Ikulu ya Tanzania kuhujumu uchumi wa Taifa kwa kiwango hiki.

Vinginevyo TAKUKURU, FIU na Polisi waachanane na kazi ya kufuatilia utakatishaji wa fedha na rushwa zinazohusisha “mafisadi vidagaa” wakati “mafisadi papa” wanaikausha nchi.

16. Religious institutions oppression:

Samia anatekeleza sera ya ukandamizaji wa kidini, akiwa anazilenga dini za Kikristo zinazomkosoa kwa hoja. Ametangaza vita na TEC wa Kanisa Katoliki akidai kwamba “wana-override nchi” kwa kufundisha juu ya misingi ya maadili asilia.

Na amefunga Kanisa la Ufufuo na Uzima, na hivyo kuwaondolea maelfu ya Watanzanoa fursa ya kuabudu, kulea watoto wao kidini, na kuwadhoofisha kiuchumi wachungaji na maaskofu wa Kanisa hilo. Kwa hiyo, Samia anatekeleza sera ya kuua familia za Kikristo kwa njia ya mzunguko. Huu ni ukiukwaji wa Katika ya nchi.

17. Security forces outsourcing for domestic oppressions:

Samia anatekeleza sera ya kuhemea majeshi ya kigeni na kuyaingiza nchi kinyume cha taratibu zinazofahamika kisheria. Kuna ushahidi usiokanushika kwamba wakati wa wiki ya uchaguzi Samia aliingiza majeshi kutoka Uganda, DRC, na Zambia.

Wanajeshi hawa walikuwa hawaguswi na mapolisi wa usalama barabarani mara tu baada ya kuonyesha vitambulishi vyao vya kijeshi vilivyotolewa na nchi zao.

Walipofika nchini mwetu kazi yao ilikuwa ni moja tu. Kufanya “spree shooting.” Walikuwa ni wauaji wa kukodi.

Kwa hiyo, haya yalikuwa na mauaji ya kupanga yakiwa yanajumuisha idara nyingi za serikali. Hata hivyo, majeshi yote ya kukodi hayakuwa yanawajibika kwa CDF. Badala yake, yalikuwa yanaratibiwa na Mtoto wa Samia aitwaye Andul.

Huu ni uvunjifu mkubwa wa Katiba ya nchi inayoweka jukumu la kulinda uhai wa Taifa mikononi mwa JWTZ. Samia anayo kesi ya kujibu mbele ya makapteni.

IV. SAMIA KIINI CHA ANGUKO LA KATIBA

Ufafanuzi katika sehemu ya I na sehemu ya II hapo juu unaeleza ukweli kwamba kuna mpasuko kati ya matarajio ya watu kuhusu uendeshaji wa nchi kwa mujibu wa katiba na na mang’amuzi yao kuhusu hali halisi ilivyo.

Mpasuko huu ndio ilikuwa sababu ya maandamano ya GenZ wakati wa wiki ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

GenZ waliingia barabarani kupigania "Kanuni ya Utanzania" kama ilivyofunbdishwa na vijana Julius Nyerere na Abed Karume, na kama inavyoonekana kwenye katiba ya Tanzania ya leo.

GenZ waliingia barabarani kupinga uvunjwaji wa Katiba ya nchi unaofanywa na serikali ya Samia.

Waliamua kufanya maandamano ya kufa na kupona ili kutetea ukweli huu, wakiwa tayari kutoa uhai wao kwa ajili ya ukombozi wetu tuliobaki hai. Walikufa kifo cha kishujaa. Tulioko hai lazima tuendelee kuwakumbuka na kuenzi ajenda yao.

Tayari mara kadhaa Samia amemfahamishwa kwa udadavuzi wa maandishi laini kuhusu msingi wa ukweli wanaopigania GenZ.

Ameelezwa kwamba anapaswa kuendesha nchi kwa kufuata, sio matakwa binafsi wala misahafu, bali kwa kufuata misingi ya maadili asilia inayotajwa katika katiba ya nchi.

Hata hivyo, Samia haonekani kusikiliza ushauri wowote wakati hii ni misingi ya madili asilia iliyotajawa kwenye Katiba ya nchi ambayo Samia aliapa kuilinda.

Yeye anaendelea na programu y sera haramu 17, nilizoziiita “NEW DECIDED MOPPERS POLICY FRAMEWORK,” kwa maana ya sera zifuatazo:

(1) Nepotic autocracy and cleptocracy in state administration; (2) Emigration of Indigenous Africans; (3) War on the Natural Moral Law as opposed to Shariah Law; (4) Detentive abductions and tortures; (5) Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity from criminal charges; (6) Court authority perversion and litigation dramas; (7) Inquiry commission dramas; (8) Deregistration of critical associations; (9) Election rigging in the name of INEC’s constitutional immunity from criminal charges; (10) Disinformation, media capture and mind capture; (11) Military integrity perversion, politicization and paralysis; (12) Organised violence against republican principles; (13) Parliamentary incapacitation and legislative dramas; (14) Police and paramilitary forces brutality; (15) Embezzlement of financial and natural resources; (16) Religious oppressions; and (17) Security forces outsourcing for domestic oppressions.

kuna mpasuko usioweza kusuluhishika kati ya fikra za Samia kama zinavyojieleza kupitia NEW DECIDED MOPPERS policy framreork,” kwa upande mmoja, na fikra za umma wa Watanzania, kwa upande mwingine, kama zinavyojieleza kupitia ""NATURAL LAW POLICY FRAMEWORK".

Hivyo, napendekeza kwamba, ni sahihi kuhitimisha kwamba, Samia amepoteza uhalali wa kukaa ikulu, japo huenda rafiki yangu MALCOM LUMUMBA asipende wazo hili.

V. HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

Hivyo basi, kwa kuwa watu huunda serikali kwa ajili ya kuitumia kama nyenzo ya kulinda uhai wao na haki zinazoambatana na uhai;

Kwa kuwa watu wanayo haki ya kubadili serikali inayohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kusimika serikali mpya, ambayo, kwa maoni yao, itaweza kukuza na kuhami haki zao;

Kwa kuwa watu wanayo haki ya kufuta muundo wa kiserikali unaohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kubuni na kuweka muundo mpya wa serikali mpya, ambao kwa maoni yao utaweza kukuza na kuhami haki zao;

Na kwa kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya Samia na muundo wa serikali mbili vimethibitika kuhahatarisha haki za watu kwa utaratibu endelevu, tangu 2015;

Hivyo basi, natoa mapendekezo yafuatayo, kwa ajili ya utekelezaji kabla ya tarehe 01 Januari 2026:

  1. Mosi, Samia aitishe kikao cha Baraza la Mawaziri ili limpe taarifa sahihi kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Afya, Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Tamisemi.
  2. Pili, Samia aitishe kikao cha Baraza la Usalama la Taifa ili limpatie taarifa sahihi kuhusu matukio ya wiki ya uchaguzi.
  3. Tatu, Samia apitie ushahidi atakaopewa na hatimaye kukubali kwa hiari yake kwamba serikali yake ilifanya makosa makubwa, na hatimaye kuvunja serikali na Bunge ili kutengenza mazingira rafiki kwa mchakato wa maridhiano ya kitaifa.
  4. Nne, Samia akubali kuunda serikali ya mpito itakayosimamia mchakato wa maridhiano ya kitaifa.
  5. Tano, Samia akubali kujiuzulu na kuipa nafasi serikali ya mpito kusimamia mchakato wa maridhiano ya kitaifa, kuundwa kwa katiba mpya na kusimamia uchaguzi mtakatifu chini ya Katiba Mpya.
  6. Na sita, kama Samia hakubaliani na mapendekezo haya, wakati ushahidi wote uliowasilishwa unaonyesha bayana kuwa ameshindwa kuendesha nchi kwa mujibu wa Katiba, basi, bila kuvunja Katiba ya nchi, JWTZ wasimamie mchaka wa mapinduzi ya kidemokrasia kama ilivyofanyika huko Zimbabwe mwaka 2017.
Nawasilisha.
 
Attachments

  • 1767010483810.png
    1767010483810.png
    35.9 KB · Views: 14
  • 1767015851151.png
    1767015851151.png
    50.9 KB · Views: 13
  • 1767017344446.png
    1767017344446.png
    56.9 KB · Views: 10
  • 1767017417152.png
    1767017417152.png
    55.5 KB · Views: 13
View attachment 3521456

Barua ya Kijasiriadola kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama: Muda wa Samia Kukaa Ikulu Ulikwisha Siku Alipouliza Hivi, ‘Kama hamkutaka serikali iwaue watoto wenu kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani?’

I. UTANGULIZI

Katika aya zifuatazi napenda kutoa salamu zangu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa Watanzani wote wanaoamini kati uhuru wa kufikiri na kueleza fikra binafsi kama njia mojawapo ya “kuwaongoza viongozi” kwa njia ya kusanifu hoja thabiti, na hatimaye “kutakatifuza malimwengu” kwa njia hiyo.

Miaka 64 iliyopita, yaani mwaka 1961, kijana Mtanganyika aitwaye Julius Nyerere alitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Tanganyika” kutoka kwa wakoloni wa Kizungu.

Miaka mitatu baadaye, kijana Mzanzibari aitwaye Abedi Karume, alitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Zanzibar” kutoka kwenye ukoloni wa miaka ipatayo 200 chini ya Waarabu wa Omani, waliokuwa wameikalia Zanzibar tangu 1698.

Hatimaye, vijana Julius Nyerere na Abedi Karume walitangaza “Tamko la Uhuru Kamili wa Tanzania” iliyopaswa kuendelea kuwa huru dhidi ya ukoloni mamboleo na utumwa mambosasa.

Vijana Julius Nyerere na Abedi Karume walifanikiwa kuzika kabisa ukoloni mkongwe wa Kizungu uliofanyika kwa miaka 77 na kutokomeza utumwa mambokale wa Kiarabu uliofanyika kwa miaka 1000.

Hivyo, tangu 1964 mpaka Machi 2021, Watanzania waliendelea kuwa huru dhidi ya ukoloni wa Kizungu na utumwa wa Kiarabu, wakiwa wanaongozwa na kanuni ya kuheshimu utu wa kibinadamu unaounganishwa na Katiba moja ya kisiasa.

II. KANUNI YA UTU NA MATARAJIO YA WATU

Vijana Julius Nyerere na Abedi Karume waliwafundisha Watanzania, na Watanzania wakakubali mafundisho mahsusi kuhusu misingi ya utu wa kibinadamu.
  1. Kwamba, wakati majini, malaika, miungu na Mungu ni watu wasio na miili, kila binadamu ni mtu mwenye mwili ambao ni kitovu cha hazina ya uhai, akili na utashi huru.
  2. Kwamba, Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia, inayotamka misingi mahsusi ya kiutawala, ndio njia pekee ya kujenga Taifa jipya linalojitawala pasipo hofu ya kukwekwa chini ya utumwa au ukoloni na Taifa jingine.
  3. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea heshima ya binadamu, binadamu wote ni sawa katika mizania ya utu, na heshima yao inapaswa kuhifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu.
  4. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea uswa wa haki, binadamu wote huzaliwa wakiwa na haki za msingi sawa, zikijumuisha uhai, uhuru na ustawi.
  5. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea ukuu wa mamlaka ya watu juu ya serikali yao, kwa ajili ya kukuza na kuhami haki, watu makini lazima wakubaliane kuunda Jamhuri ya Kidemokrasia, yenye kutawaliwa na serikali iliyopata madaraka ya kiutawala kutokana na kibali cha kura za watawaliwa, ambapo kura hizo zinazopigwa kwa kufuata utaratibu unaokubalika kikatiba.
  6. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea utawala wa sheria, binadamu wote ni sawa mbale ya Katiba, sheria na kanuni husika, ambapo, vifungu vya kikatiba vinayo nguvu ya kuvipiku vifungu vya kisheria na vifungu vya kisheria vinayo nguvu ya kuvipiku vifungu vya kikanuni.
  7. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mgawanyo wa madaraka, mamlaka ya nchi lazima yagawanywe katika mihimili mitatu, yaani mhimili wenye madaraka ya utawala (serikali), mihimili wenye madaraka ya kutunga sheria (Bunge), na mihimili wenye madaraka ya utoaji haki (mahakama), itakayofanya kazi kwa kushauriana na kukosoana.
  8. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea uwajibikaji wa kimamlaka, mamlaka ya nchi lazima iwajibike kwa wananchi walioiweka madarakani.
  9. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea ustawi wa watu, lengo kuu la serikali ni ustawi wa wananchi walioiweka madarakani.
  10. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea njia kuu za uchumi, shughuli za Serikali zinapaswa kutekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na kwa kuzuia mtu mmoja kumyonya mtu mwingine.
  11. Kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mamlaka ya kufukuza serikali, watu wanayo haki ya kutumia mchakato stahiki kufukuza serikali inayohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kuajiri serikali mpya, ambayo, kwa maoni yao, itakuwa na weledi wa kukuza na kuhami haki zao.
  12. Na kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya kikatiba inayoongelea mamlaka ya kubadilisha katiba kwa lengo la kubadilisha muundo wa serikali, watu wanayo haki ya kufuta muundo wa kiserikali unaohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kubuni na kuweka muundo mpya wa serikali, ambao kwa maoni yao utakuwa na yamkini ya kukuza na kuhami haki zao.
Katika muda wote wa utawala wa waasisi wa Taifa letu, hizi kanuni za kikatiba ziliheshimiwa sana kiasi kwamba, kiti cha Uraisi kiligeuka kitako cha mwamba thabiti ulio chimbuko la uimara wa himaya ya Tanzania.

Siku zote hizo Watanzania waliaminishwa na kuamini kihalali kwamba Raisi ni mjuaji wa mambo yote nchini, Raisi ni mweza wa mambo yote nchini, Raisi ni mkazi wa sehemu zote nchini, Raisi ni mpenda watu wote nchini, Raisi ni “mhunzi” wa vitu vyote vinavyoonekana nchini.

Kwa sababu hizi Raisi alichukuliwa kuwa ni Baba au Mfalme aliye alama ya umoja wa kitaifa, nguzo ya matumaini, mlinzi mkuu wa uhai wa raia wote, na msimamizi mkuu wa usalama wa Taifa lote.

II. SERA 17 ZA UKOLONI MAMBOLEO, UTUMWA MAMBOSASA NA UHALISIA WA MAMBO

Hata siku moja, Watanzania hawakuwahi kufikiri kwamba wangempata Rais atakayejitenga nao na kisha kuwakejeli kwa kuwauliza swali tata, kama ilivyotokea tarehe 02 Desemba 2025, pale Samia alipowauliza Watanzania kwamba: “Nyie Watanzania, kama hamkutaka serikali iwaue watoto wenu kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani?”

Napendekeza kwamba, swali hili ni kielelezo cha ujasiri alio nao Samia katika azima yake ya kutekeleza program ya kisera, ambayo sasa inafahamika kwa jina la “NEW DECIDED MOPPERS.”

Hii ni program ya kisera inayoongelea sera 17, kila sera ikiwakilishwa na herufi moja katika kifungu cha maneno yafuatayo “NEW DECIDED MOPPERS.” Sera hizo ni:

(1) Nepotic autocracy in state administration; (2) Emigration of Indigenous Africans; (3) War on the Natural Moral Law as opposed to Shariah Law; (4) Detentive abductions and tortures; (5) Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity from criminal charges; (6) Court capture and litigation dramas; (7) Inquiry commission dramas; (8) Deregistration of critical associations; (9) Election rigging in the name of INEC’s constitutional immunity from criminal charges; (10) Disinformation, media capture and mind capture; (11) Military politicisation, capture and intimidation; (12) Organised violence against republican principles; (13) Parliamentary capture and legislative dramas; (14) Police and paramilitary forces brutality; (15) Embezzlement of financial and natural resources; (16) Religious oppressions; and (17) Security forces outsourcing for domestic oppressions.

Katika aya zifuatazo nitaeleza kila sera kwa ufupi.

1. Nepotic autocracy in state administration:

Samia anatekeleza sera ya kugawa vyeo kwa kuangalia undugu, urafiki na uswahiba, yaani “nepotism”.

Binti yake na mumewe ni Mawaziri; Mtalaka wa bintiye ni DC; Mshenga katika ndoa ya binti yake ni Waziri; na orodha inaendelea.

Maamuzi yote haya anayafanya Samia yeye mwenyewe kinyume cha ushauri thabiti anaopewa na wasaidizi wake makini.

Hii ni tabia ya udikteta wa mtu mmoja, yaani “autocary,” na hovyo kifungu cha maneno “nepotic autocracy.”

2. Elevation of Shariah Law over the Natural Moral Law:

Samia anatekeleza sera ya kuendesha nchi kwa kutumia mfumo wa sheria za kiislamu uitwao “shariah law,” ambao ni mfumo rasmi wa sheria za kuendesha nchi katika mataifa ambayo ni wanachama wa Jumuiya ya Waislamu iitwayo “OIC”.

Ukweli uko hivi: Katiba ya nchi (1977) inakataza uhalifu wa kijinai kama vile utekaji, mauaji holela, na ubadhirifu wa fedha na mali za umma, isipokuwa kama uhalifu huu ukifanywa na Rais mwenyewe.

Ruhusa hii ya kikatiba inapatikana kwenye ibara ya 46 ya Katiba inayompatia Rais kinga dhidi ya mshtaka yoyote ya kijinai. Rais anaweza kujizuia kufanya uhalifu huu kwa sababu za kimaadili tu.

Kama Rais ni Mkristo atatumia maadili ya Kibiblia yaitwayo “Amri Kumi za Mungu”.

Na kama Rais ni Muislamu atatumia maadili ya Kikurani yaitwayo “Shariah Law.”

Bahati mbaya mfumo wa “Shariah Law” inaruhusu mauaji holela, kwa kuwapiga mawe watuhumiwa hadi wafe, hata bila kufuata mfumo wa kimahakama, inahalalisha utekaji na utesaji wa watuhumiwa kwa kuwachapa viboko hadi 100, na kadhalika. Kwa ufupi mfumo wa “Shariah Law” hautambui ukuu wa tunu ya uhai.

Utekaji, mauaji na utesaji wa raia unaoendelea nchini ni ushahidi kuwa sasa mfumo wa “Shariah Law” umerasimishwa kinyemelea nchini Tanzania.

Lakini, kwa mujibu wa ibara ya 3 ya katiba ya Tanzania (1977), Tanzania ni dola isiyofungamana na upande wowote wa kidini, na unayopaswa kuongozwa kwa kufuata misingi ya maadili asilia, kama inavyotafsiriwa na sisi Watanzania wenyewe.

3. War on Indigenous Africans in favor of Foreign Direct Investors:

Samia amefunga mikataba ya uwekezaji wa kigeni inayowasukuma watanzania wazawa nje ya njia kuu za uchumi. Mfano ni mkataba wa DP World katika bandari ya Dar Es Salaam, mkataba wa makaa yam awe huko Tanzania Kusini, Mkataba wa kuuza madini huko Mwadui, Mkataba wa Mwendokasi Dar, na mikataba kama hiyo.

Pia kuna mkataba wa kuwahamisha Wamsai wa Ngorongoro na kuwapeleka Tanga kinyemela ili kupisha wawekezaji wa Kiarabu katika biashara ya uwindaji na biashara ya kaboni kwenye bonde la Ngorongoro.

Hii ni biashara ya “trophy hunting and carbon trade” inayoendeshwa na Waarabu wa Dubai.

Kwa ujumla, Samia anatekeleza sera ya kuwageuza Watanzania watumwa ndani ya nchi yao. Jambo hili halikubaliki kwa kuwa ni aina mpya ya ukoloni mkongwe.

4. Detentive abductions, tortures and enforced dissappearances:

Samia anatekeleza sera ya kuwateka na kuwaweka katika kambi za watumwa waafrika wengi wanaomkosoa.

Kuna watu wengine wanapotea bila maelezo yoyote kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama vyenye jukumu la kulinda raia na mali zao.

Kwa mujibu wa ripoti ya chama cha wanasheria wa Tanganyika na UN tangu 2016, alipopotea Ben Saanane, tayari wamepotea Watanzania zaidi ya 200. Hii maana yake ni kwamba, Rais aliyekula kiapo cha kulinda usalama wan chi, raia na mali zao ameshindwa kazi hiyo.

5. Extrajudicial killings and extralegal operations in the name of presidential constitutional immunity from criminal charges:

Samia anatekeleza sera ya kuua wakosoaji wake wazi wazi kama mbinu ya kubaki madarakani.

Kifo cha Mohammed Ali Kibao ni tukio muhimu sana kueleza ukweli huu. Tangu KIbao auwawe serikali haijawahi kutwambia lolote.

Ukimya huo maana yake ni kwamba ama serikali inahusika moja kwa moja au inahusika kwa njia ya mzunguko. Kuna

6. Court capture and litigation dramas:

Samia anatekeleza sera ya kuziteka mahakama na kuzitumia kuendesha kesi za kubumba na hatimaye kutoa humu za kisiasa, na hivyo kuunajisi mfumo wa utoaji wa haki.

Kesi ya uhaini inayoendelea dhidi ya Tundu Lissu na Kesi dhidi ya Bodi ya wadhamini wa chadema iliyosababisha Chadema kuzuiwa kutekeleza shughuli zake za kisiasa ni mifano hai.

7. Inquiry commissions dramas:

Samia anatekeleza sera ya kutumia Tume za Uchgunguzi kuwazunga wananchi. Mfano mzuri ni Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 2025 wakati wa uchaguzi mkuu.
  • MKurugenzi wa uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi wapo na wanajua kilichotokea vituoni nchi nzila,
  • Mkuu wa Jeshi la Polisi na Ma-RPC wapo na wanajua kilichotokea barabarani chini ya usimamizi wa Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Hajj,
  • Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Uporaji Mkubwa (Special Anti-Robber Unit-SARU) yupo na anajua kikosi chake kilifanya nini mitaani katika wiki ya uchaguzi na kwa maagizo ya nani,
  • Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa yupo na amekusanya taarifa za kilichotokea kwenye makaburi ya halaiki wakati intaneti na umeme vimekatwa,
  • Mkuu wa JWTZ yupo na anajua kilichotokea mitaani nchi nzima,
  • Wakuu wa Wilaya na Kamati za Ulinzi na Usalama wanazoziongoza wapo na wanajua kilichotokea kwenye wilaya zao katika wiki ya uchaguzi, na
  • Mkurugenzi wa JUkwaa la Wahariri na Waandishi wa habari wapo na wanajua matukio yote muhimu japo hayajachapishwa magazetini.
Hivyo, taarifa za kawaida za kiutawala zinatosheleza mahitahi ya taarifa anazozihitaji Rais ili aweze kutekeleza majukumu yake.

Kwa sababu hizi zote hakuna sababu nzuri ya kuunda Tume inayopewa miezi mitatu kufanya kazi ya kutafuta ukweli unaojulikana, kama sio mkakati wa kuendesha nchi kiujanjaujanja.

8. Deregistration of critical associations:

Samia anatekeleza sera ya kufuta au kudhoofisha vyama vya kijamii, taasisi za dini, vyama vya siasa, na vyombo vya habari ili kudhoofisha sekta ua asasi za kiraia, na hivyo kupata unafuu wa kutawala bila kukosolewa.

Amesitisha au kudhoofisha shughuli za Kanisa la ufufuo na uzima, Chadema, Jamiiforums, JamboTV, Twitter(X), Telegram, Clubhouse, na tovuti 80,000 kwa mdai kwamba zina maudhi yasiyo adilifu, gazeti la The Chanzo.

9. Election rigging in the name of INEC’s constitutional immunity from criminal charges:

Samia kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi anatekeleza sera ya kuiba uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani tangi 2024. Mwitiko wa wapiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2025 haukuzidi 20% ya wapiga kura wote waliojinadikisha.

Hata hivyo, Tume ilitangaza matokeo yanayoonesha ushindi wa asilimia zaidi ya 80% kwa wagombea wote. Huu ni ulaghai usiofichika na wenye kuondoa uhalali kwa serikali ya sasa.

Mara tatu, kupitia hotuba zake, Samia amejaribu kutetea ushindi wake pasipo mafanikio. Kila anapojaribu kufafanua ndivyo anavyoongeza mashaka kuhusu uhalali wake.

Ujasiri huu wa kuiba uchaguzi, hasa kura za Rais, unatokana na kinga ya kikatiba iliyo nayo Tume, pale inapokuwa imetangaza mshindi wa kiti cha Urais.

Ibara ya 47(1) inazuia mahakama za Tanzania kusikiliza kesi yoyote ya kupinga tangazo la ushindi huo.

Lakini, ibara hii inapingana na ibara ya 5(1) na ibara ya 8(1) zinazosema madaraka ya serikali yatatoka kwa watu kwa njia ya kuopiga kura.

Pasipo fursa ya kuomba mahakama ihakiki usahihi wa kura zilizotangawa, wanancho wanaweza kuporwa “ukuu” wao kama “wenye nchi” bila kuwa namna ya kujitetea.

Sasa Samia anatumia mwanya huu kufanya uhalifu wa kisasa wazi wazi halafu anasema kuwa yeye ni Rais halali. Hapana. Ushahidi ulioko mitaani kutoka kwenye vituo vya kupigia kura haukubaliani na utapeli huo.

10. Disinformation, media adoption and mind capture:

Samia anatekeleza sera ya kuteka akili za umma kwa kuwanyima habari sasa na kuwalisha habari zilizochujwa.

Samia amelazimisha vyombo vyote vya habari kufanya kazi kama idara ya serikali inayosimamia mahusiano kwa umma. Kwa sasa zinaandikwa habari zisizo na ukosoaji wa aina yoyote dhidi ya serikali.

Hata Jukwaa la wahariri (TEF) limefyata mkia kabisa. Kimapokeo, sekta ya habari inayo majukumu matatu.

Kuna majukumu sita yanayoifanya sekta ya habari kuwa mhimili wa nne wa dola.

Mosi, ni kuandika habari za udukuzi (watchdog), yaani kutafiti na kuchapisha habari za rushwa, kashfa, uzembe, na kuwakosoa wakubwa kwa lengo la kuimarisha utawala bora.

Pili, ni kuchuja, kuhariri na kuandika habari zenye maslahi kwa umma (gatekeeping), katika namna ambayo ni salama na yenye faida kwa umma.

Tatu, ni kuandika habari zenye kuibua matatizo ya kijamii na kupendekeza majibu yake kwa watawala (agenda setting), yaani kuifanya jamii ione matatizo yake na kuyapa vipaumbele sahihi katika kuyatatua.

Nne, ni kutunza kumbukumbu za maisha ya jamii (scorekeeping), yaani kufuatilia siku hadi siku matukio muhimu na kutunza shajara maalum kwa ajili ya matumizi ya baadaye, kwa lengo la kuonyesha nano anafanikiwa, nani anashidwa, na kusaidia kuionyesha jamii wapi inapaswa kwenda kwa kuzingatia ilikotoka.

Tano, ni kueneza utamaduni wa jamii (cultural Transmission), yaani kuandika, kueneza imani, tunu na maadili ya jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

Na sita, ni kuwa jukwaa la umma (public forum/agora), yaani kuisadia jamii kupata jukwaa linaloweza kutumiwa na jamii kama soko la mawazo mseto, majadiliano na hatimaye kama njia ya kusukuma mawazo ya pamoja ili yafike serikalini na kufanyiwa kazi.

Lakini sasa, Samia amevipiga marufuku vyombo vya habari kutekeleza majukumu yote haya.

Anachokisema yeye ndio kinapaswa kuchukuliwa kama ukweli, na wengine wote ni waongo. Huu ni uvunjaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Tanzania (1977).

11. Military politicization, capture and intimidation:

Samia anatekeleza sera ya kuliingiza jeshi katika siasa, kulidumaza kiweledi kwa kutumia ukanda na udini, na hatimaye kulifanya lishindwe kutekeleza jukumu lake la msingi la kulinda uhai wa Taifa dhidi ya maadui wa ndani na nje.

Rais Samia Suluhu Hassan, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania, aliliagiza jeshi kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Agizo hili lilitolewa mnamo Januari 22, 2024, wakati wa Mkutano wa Saba wa Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama (CDF) na Makamanda jijini Dar es Salaam. Malengo makuu ya agizo hilo yalionekana kuwa ni mawili.

Mosi, kuhakikisha usalama wa nchi unakuwa wa kutosha wakati wa mchakato wa uchaguzi, kwani chaguzi zinahusisha vyama vingi na mitazamo tofauti, na hivyo kuna uwezekano wa kutokea changamoto zisizotarajiwa.

Na pili, Kutoa tahadhari viongozi wa jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama ili wawe tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.

Rais alisisitiza kuwa maandalizi hayo hayamaanishi matumizi ya nguvu, bali ni kuhakikisha taratibu, sheria na miongozo ya uchaguzi inafuatwa huku jeshi likiwa limekaa tayari kudhibiti uvunjifu wa amani.

Hata hivyo, tamko la CDF tarehe 30 Oktoba 2025 lilionyesha wazi kwamba alikuwa tayari kuliingiza jeshi barabarani ili kukabiliana na waandamanaji, ambayo yeye aliwaita “vibaka.”

Kikosi Maalum cha Kukabiliana na Vibaka (Special Anti-Robbert Unit-SARU) kiliingia mitaani 29 Oktoba 2025 wakiongozwa na kaulimbiu ya “vibaka wauwawe.” Waandamanaji wakavalishwa “joho la vibaka” na wakauwawa kama kuku bila kutofautisha kati ya kibaka na mwandamanaji. CP Awadhi Hajj anajua vizuri zaidi walichofanya hawa vijana wa SARU.

Wakati SARU wanaendelea kukabiliana na “vibaka” JWTZ wachache waliokuwa barabarani wakajikuta wanakaniliana na majeshi ya kukodi pia.

Baadhi ya wanajeshi wa kigeni waliwaua na wengine kuwaweka mateka, lakini JWTZ wakaambiwa na wakubwa kwamba hao mateka waachiwe kwa kuwa ni kikosi cha “kazi maalum.”

Jeshi la polisi lilishirikiana kuwakabili waandamanaji kwa msaada wa taarifa za kiintelijensia zilizokuwa zinakusanywa kwa kutumia magari ya kivita tuliyouziwa na kampuni ya Uarabuni inayoitwa STREIT, mradi ambao ulisimamiwa na Angela Kiziga.

Magari haya huwa yanapaki kandoni mwa barabara, hasa katika sehemu za makutano, yakiwa na kamera na antenna za kurusha mawimbi papo kwa papo kwenye kituo cha taarifa jumuishi (control center).

Kwa upande wa Dar Es Salaam mara nyingi magari haya utayakuta Ubungo mtaa, Magomeni, Ocen Road, Faya, na Kariakoo.

Baadhi ya magari haya yanamilikiwa na JWTZ wakati mengine yanamilikiwa na polisi. Kwa hiyo, JWTZ walikuwa na nafasi ya kukusanya taarifa haraka na kubaini mauaji holela ya raia na hatimaye kuingilia kati kwa mujibu wa dhaman yao ya kikatiba.

Lakini, JWTZ hawakufanya hivyo, kwa kuwa CDF alikuwa tayari ameweka msimamo kwamba “wale sio waandamanaji bali ni vibaka.”

Adande CDF aliendelea na msimamo huu hata baada ya makapteni wake waliokuwa “filed” kumpa taarifa mbadala, na kumtaka atoe tangazo la “kuchukua nchi” ili kutuliza “upepo mbaya.”

Hata hivyo, afande CDF alikatazwa na washauri wake wakuu ambao ni wakuu wa komandi za kijeshi, mkurugenzi wa intelijensia jeshini na mkuu wa utumishi jeshini. Wakubwa hawa wote walikubaliana na kaulimbiu kwamba “wale sio waandamanaji bali ni vibaka.”

Kwa hiyo, ni sahihi kuhitimisha kwamba, tekinolojia ya kijeshi kutoka UAE imechangia katika kufanikisha vifo vya Watanzania katika wiki ya uchaguzi kwa njia ifuatayo:

Jeshi la polisi wameitumia kukusanya taarifa za watu walioitwa “vibaka” na wakafanikiwa kuwashughulikia kwa kutumia risasi za moto.

Lakini, hata JWTZ walitumia tekinolojia hii kukusanya taarifa za “waandamaji” ili waweze kuwapa ulinzi stahiki ili wafanikishe azima yao ya kupigania Tanzania mpya kwa njia ya maandamano ya kufa na kupona.

Hata hivyo, taarifa hizi hazikuwa na msaada maada wakubwa walishaweka msimamo unaowashangaza watu wengi hadi leo.

Kwa sababu hii, tangu siku hiyo ya tarehe 30 Oktoba, makapteni wengi hawana imani na afande CDF, hawana amani na wakuu wa Komandi za JWTZ, hawamwamini Mkuu wa Intelijensia wa JWTZ, na wanamtazama Mkuu wa Utumishi Jeshini kwa kumshangaa hadi wanashindwa kushangaa.

Kwa ujumla, ukweli kwamba JWTZ walishindwa kuzuia mauaji ya Watanzania zaidi ya 1,500 yaliyofanya kwa kupangwa ndani ya siku tatu mfululizo, ni ushahidi tosha kwamba, jeshi letu limetekwa kiasi kwamba kwa sasa ni sahihi kusema kuwa “JWTZ sio jeshi la wananchi.” Hili ni tatizo kubwa la kiusalama, na lazima litatuliwe kwa kushughulikia chanzo chake.

12. Organized violence against republican principles:

Samia anatekeleza sera ya ama kudhoofisha au kufuka mfumo wa kijamhuri nchini Tanzania.

Ndani ya chama chake CCM alizuia ushindani ili apite kama mgombea pekee asite na mpizani. Nje ya CCM, akafanya vivyo hivyo. Kwanza alimfunga mpizani wake mkuu Tundu Lissu.

Kisha akatumia mbinu za ubaguzi wa kitaasisi kumwondoa mpinzani wake wa pili, Luhaga Mpina, kwenye uchaguzi.

Badala yake akatengeneza wagombea dhaifu kupitia vyama vya upinzani vyenye “kazi maalum.” Akashindana nao na hatimaye akatangazwa mshindi kwa 98%, wakati wapiga kura waliojitokeza vituoni hawazidi 10%.

Hapa hakuna demokrasia. Kanuni ya Jamhuri kwamba madaraka hutoka kwa watu kupitia ushindani wa kidemokrasia imekiukwa. Matendo haya yanakiuka Katiba ya ncho ambayo Samia aliapa kuilinda.

13. Parliamentary capture and legislative dramas:

Rais Samia anatekeleza sera ya kuendesha nchi kwa kuliteka Bunge. Alianza kwa kulilazimisha lipitishe mkataba wa kimataifa wa DP World, kisha mikataba ya bandari ya Bagamoyo na makaa ya mawe ya Kiwira.

Baadaye Samia akalilazimisha lipitishe marekebisho ya sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa iliyompa madaraka ya Kimungu. Na hivi karibuni amekuwa na maamuzi ya veto kuhusu nani awe mgombea ubunge na yupi asiwe.

Lengo ni kuwa na wabunge walio upande wake, wasiohoji lolote. Uhuru wa Bunge umeingiliwa, kiasi kwamba kanuni ya kikatiba kuhusu mgawanyo wa madaraka haina nafasi. Uvunjwaji wa katiba wa kiwango hiki haukubaliki.

14. Police and paramilitary forces brutality:

Samia anatekeleza sera ya kulitumia jeshi la polisi kama idara ya CCM. Ni jeshi ambalo limejenga chuki kuu dhidi ya raia wasio wana CCM.

Jeshi linatii maagizo ya viongozi wa CCM hata pale ambapo sheria zinakataza utii wa aina hiyo.

Wahalifu waliovaa nguo za kijani ni raia wema kwa mujibu wa polisi, lakini wasiovaa nguo za kijanii ndio wanavunja sheria. Polisi wanakamata watuhumiwa kininja, usiku wa manane, mbele ya wanafamilia.

Badala ya kuwa walinzi wa raia wema na mali zao, sasa wamegeuka kuwa walinzi wa wana CCM na mali zao. Huu ni utovu wa nidhamu usiokubalika.

15. Embezzlement of financial and natural resources:

Samia anatekeleza sera ya ubadhirifu wa fedha na mali za umma kwa kasi kana kwamba baada ya kuindoka ofisini atahama nchi.

Mara tu alipoingia madarakani alipandisha mshahara wake kutoka milioni 10 kwa mwezi alizokuwa anapokea hayati Magufuli hadi milioni 30 kwa mwezi. Hili ni ongezeko la 300%.

Kwa kuamuzi huu viongozi wastaafu wanaopata 80% ya mshahara wa kiongozi anayekalia ofisi aliyokuwa anaokalia mstaafu, walipata ongezeko la 300% pia.

Ameuza hisa za mgodi wa almasi wa Mwadi kwa bei ya kutupa; ameuza mgodi wa makaa yam awe kiwira kwa bei ya nyanya; ameuza misitu yetu kwa waarabu wanaofanya biashara ya hewa ya ukaa; ameuza wanyama wetu walioko kwenye mbunga za wanyama kwa wanaofanya biashara kuwinda.

Lakini sio hivyo tu. Amekopa matrilioni ya fedha na kuyagawanya mara tatu. Theluthi moja imeingia nchini. Theluthi ya pili ikahamishiwa Uturuki kwenye biashara zake za majumba (real estates). Na theluthi ya tatu ikahamishiwa UAE kwenye biashara zake za majumba (real estates).

Katika mazingira haya swali moja linazuka. Kuna haja ya TAKUKURU, FIU na Polisi kuhangaika na rushwa, money laundering, na makosa kama hayo yenye kuhusisha “pesa ya mboga” wakati matrilioni yanatakatishwa na kuhamishwa kinyemelea namna hii?

Jawabu langu ni ndio, ikiwa watatusaidia kurudisha haya matrilioni. Vinginevyo waachana ne utakatishaji wa fedha na rushwa zinazohusisha “mafisadi vidagaa” wakati “mafisadi papa” wanaikausha nchi.

16. Religious oppressions:

Samia anatekeleza sera ya ukandamizaji wa kidini, akiwa anazilenga dini za Kikristo zinazomkosoa kwa hoja. Ametangaza vita na TEC wa Kanisa Katoliki akidai kwamba “wana-override nchi” kwa kufundisha juu ya misingi ya maadili asilia.

Na amefunga Kanisa la Ufufuo na Uzima, na hivyo kuwaondolea maelfu ya Watanzanoa fursa ya kuabudu, kulea watoto wao kidini, na kuwadhoofisha kiuchumi wachungaji na maaskofu wa Kanisa hilo. Kwa hiyo, Samia anatekeleza sera ya kuua familia za Kikristo kwa njia ya mzunguko. Huu ni ukiukwaji wa Katika ya nchi.

17. Security forces outsourcing for domestic oppressions:

Samia anatekeleza sera ya kuhemea majeshi ya kigeni na kuyaingiza nchi kinyume cha taratibu zinazofahamika kisheria. Kuna ushahidi usiokanushika kwamba wakati wa wiki ya uchaguzi Samia aliingiza majeshi kutoka Uganda, DRC, na Zambia.

Wanajeshi hawa walikuwa hawaguswi na mapolisi wa usalama barabarani mara tu baada ya kuonyesha vitambulishi vyao vya kijeshi vilivyotolewa na nchi zao.

Walipofika nchini mwetu kazi yao ilikuwa ni moja tu. Kufanya “spree shooting.” Walikuwa ni wauaji wa kukodi.

Kwa hiyo, haya yalikuwa na mauaji ya kupanga yakiwa yanajumuisha idara nyingi za serikali. Hata hivyo, majeshi yote ya kukodi hayakuwa yanawajibika kwa CDF. Badala yake, yalikuwa yanaratibiwa na Mtoto wa Samia aitwaye Andul.

Huu ni uvunjifu mkubwa wa Katiba ya nchi inayoweka jukumu la kulinda uhai wa Taifa mikononi mwa JWTZ. Samia anayo kesi ya kujibu mbele ya makapteni.

III. MPASUKO KATI YA MATARAJIO NA UHALISIA

Mpaka hapa, ni wazi kuwa kuna mpasuko kati ya matarajio ya watu kuhusu uendeshaji wa nchi kwa mujibu wa katiba na na mang’amuzi yao kuhusu hali halisi ilivyo.

Tayari mara kadhaa Samia amemfahamishwa kwa udadavuzi wa maandishi laini kwamba anapaswa kuendesha nchio kwa kufuata misingi ya maadili asilia inayotajwa katika katiba ya nchi. Mfano, amewahi kupewa ushauri ifuatao:

“Specifically, in every human person’s nature there are natural inclinations that are the origin of our moral choices and actions, as opposed to our immoral choices and actions, namely: (1) Natural inclination to the good as opposed to an aversion to the evil; (2) Natural inclination to preserve life as opposed to an aversion to intentionally causing death of an innocent person; (3) Natural inclination to preserve health as opposed to an aversion to sickness; (4) Natural inclination to copulation as opposed to an aversion to predication; (5) Natural inclination marriage as opposed to an aversion to celibacy; (6) Natural inclination to knowledge of truth as opposed to an aversion to ignorance; (7) Natural inclination to live in society as opposed to an aversion to solitude; (8) Natural inclination to self-integration as opposed to an aversion to self-disintegration; (9) Natural inclination to ownership as opposed to an aversion to material poverty; (10) Natural inclination to technology as opposed to an aversion to technological aversion; (11) Natural inclination to personal self-determination as opposed to an aversion to subjugation; (12) Natural inclination to order as opposed to an aversion to chaos; (13) Natural inclination to peace as opposed to an aversion to violence; (14) Natural inclination to coherence as opposed to an aversion to incoherence; (15) Natural inclination to culture; (16) Natural inclination to the common good as opposed to an aversion to the common evil; and (17) Natural inclination to knowledge of religious truth as opposed to an aversion to religious ignorance.

Hata hivyo, Samia haonekani kusikiliza ushauri wowote wakati hii ni misingi ya madili asilia iliyotajawa kwenye Katiba ya nchi ambayo Samia aliapa kuilinda.

Kuna mpasuko usioweza kusuluhishika kati ya fikra za Samia na Timu yake, kwa upande mmoja, na fikra za umma, kwa upande mwingine. Hatimaye, Samia ameamua kupanga mauaji ya wakosoaji wake na anajigamba kwamba “tuki tayari kuua tena.”

Hivyo, napendekeza kwamba, ni sahihi kuhitimisha kwamba, Samia amepoteza uhalali wa kukaa ikulu.

IV. HITIMISHO NA MAPENDEKEZO

Hivyo basi, kwa kuwa watu huunda serikali kwa ajili ya kuitumia kama nyenzo ya kulinda uhai wao na haki zinazoambatana na uhai;

Kwa kuwa watu wanayo haki ya kubadili serikali inayohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kusimika serikali mpya, ambayo, kwa maoni yao, itaweza kukuza na kuhami haki zao;

Kwa kuwa watu wanayo haki ya kufuta muundo wa kiserikali unaohatarisha haki zao kwa utaratibu endelevu, na katika nafasi yake kubuni na kuweka muundo mpya wa serikali mpya, ambao kwa maoni yao utaweza kukuza na kuhami haki zao;

Na kwa kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya Samia na muundo wa serikali mbili vimethibitika kuhahatarisha haki za watu kwa utaratibu endelevu, tangu 2015;

Hivyo basi, natoa mapendekezo yafuatayo, kwa ajili ya utekelezaji kabla ya tarehe 01 Januari 2026:
  1. Mosi, napendekeza kwamba, Samia akubali kwa hiari yake kuvunja serikali na Bunge ili kutengenza mazingira rafiki kwa mchakato wa maridhiano ya kitaifa.
  2. Pili, napendekeza kwamba, Samia akubali kuunda serikali ya mpito itakayosimamia mchakato wa maridhiano ya kitaifa.
  3. Tatu, napendekeza kwamba, Samia akubali kujiuzulu na kuipa nafasi serikali ya mpito kusimamia mchakato wa maridhiano ya kitaifa, kuundwa kwa katiba mpya na kusimamia uchaguzi mtakatifu chini ya Katiba Mpya.
  4. Na nne, kama Samia hakubaliani na mapendekezo haya, wakati ushahidi wote uliowasilishwa unaonyesha bayana kuwa ameshindwa kuendesha nchi kwa mujibu wa Katiba, basi, bila kuvunja Katiba ya nchi, JWTZ wasimamie mchaka wa mapinduzi ya kidemokrasia kama ilivyofanyika huko Zimbabwe mwaka 2017.
Nawasilisha.
Shida Form Four Failure, haelewi kitu hapo!
 
Barua ya Kijasiriadola kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama: Muda wa Samia Kukaa Ikulu Ulikwisha Siku Alipouliza Hivi, ‘Kama hamkutaka serikali iwaue watoto wenu kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani?’

Nawasilisha.
Mkuu Doctor Mama Amon. Kwanza asante kwa bandiko hili, ubarikiwe sana!.

Mimi ni mtu wa prevention which is better than cure, hivyo nilisikia sauti HII nikaileta humu, ila haikuwa.
P
 
Mosi, napendekeza kwamba, Samia akubali kwa hiari yake kuvunja serikali na Bunge ili kutengenza mazingira rafiki kwa mchakato wa maridhiano ya kitaifa.
Hizi ni ndoto za mchana
Pili, napendekeza kwamba, Samia akubali kuunda serikali ya mpito itakayosimamia mchakato wa maridhiano ya kitaifa.
Ikimpendeza kwani hili ni jambo la hiari yake.
Tatu, napendekeza kwamba, Samia akubali kujiuzulu na kuipa nafasi serikali ya mpito kusimamia mchakato wa maridhiano ya kitaifa, kuundwa kwa katiba mpya na kusimamia uchaguzi mtakatifu chini ya Katiba Mpya.
Hili nalo ni hiari yake, ikimpendeza atafanya, ikiwa hataki atabakia madarakani.
Na nne, kama Samia hakubaliani na mapendekezo haya, wakati ushahidi wote uliowasilishwa unaonyesha bayana kuwa ameshindwa kuendesha nchi kwa mujibu wa Katiba, basi, bila kuvunja Katiba ya nchi, JWTZ wasimamie mchaka wa mapinduzi ya kidemokrasia kama ilivyofanyika huko Zimbabwe mwaka 2017.
Hili wangefanya kabla ya MO29 na hawakufanya, wafanye leo? Kwa lipi?

Nimesema mahala pengine hapa JF kwamba Samia ama atabakia hadi 2030 au ataondoka lakini kwa hiari kwa kutokea jambo ambalo anakuwa ameondoka automatically kwa mujibu wa katiba.

Nakupongeza kwa kutumia haki yako ya kikatiba kutoa maoni. Kila mtu anayo haki ya kutoa maoni kwa mujibu wa katiba ya JMT 1977.
 
Nilidhani uko serious na andiko lako mpaka niliposoma point ifuatayo:

Bahati mbaya mfumo wa “Shariah Law” inaruhusu mauaji holela, kwa kuwapiga mawe watuhumiwa hadi wafe, hata bila kufuata mfumo wa kimahakama, inahalalisha utekaji na utesaji wa watuhumiwa kwa kuwachapa viboko hadi 100, na kadhalika. Kwa ufupi mfumo wa “Shariah Law” hautambui ukuu wa tunu ya uhai.

Utekaji, mauaji na utesaji wa raia unaoendelea nchini ni ushahidi kuwa sasa mfumo wa “Shariah Law” umerasimishwa kinyemelea nchini Tanzania.

Nikaconclude kuwa wewe ni mdini uliyejimask kama msomi. Umeonyesha ujinga wa kiwango cha juu au chuki kali dhidi ya waislamu.

Baada ya kusema hayo, mimi naamini Samia ni incompetent, hatoshi kwenye hiyo nafasi, kaingia kwenye hiyo nafasi kwa uchaguzi feki na wa kimagumashi na naamini analo la kujibu juu ya mauaji ya wananchi yaliyotokea Octobe 29 na siku kadhaa baadae.
 
‘Kama hamkutaka serikali iwaue watoto wenu kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani?’
Aliyatamka haya maneno kwa kinywa chake; kweli?

Unacho kipande cha hotuba hiyo kinachoonyesha bayana kuwa aliyasema haya maneno?

""Kama hamkutaka serikali tuwaue kwa nini mliwaruhusu waingie barabarani?"
Sijasoma mengine uliyoandika huko chini, lakini nashindwa kabisa kuamini kuwa mtu mwenye akili timamu tu, anaweza kudiriki kusema maneno ya namna hii, tena hadharani!

Kwa hiyo, wazazi ndio waliowaruhusu serikali kuua watoto, ambao hata wazazi wao walitaka watoto hao wakauliwe na serikali!

Ni vigumu sana kuamini, lakini mtu mwenyewe ni Samia, lolote linawezekana.
 
To make long story short

7. Inquiry commissions dramas:

Samia anatekeleza sera ya kutumia Tume za Uchgunguzi kuwazunga wananchi. Mfano mzuri ni Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 2025 wakati wa uchaguzi mkuu.
  • MKurugenzi wa uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi wapo na wanajua kilichotokea vituoni nchi nzila,
  • Mkuu wa Jeshi la Polisi na Ma-RPC wapo na wanajua kilichotokea barabarani chini ya usimamizi wa Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Hajj,
  • Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Uporaji Mkubwa (Special Anti-Robber Unit-SARU) yupo na anajua kikosi chake kilifanya nini mitaani katika wiki ya uchaguzi na kwa maagizo ya nani,
  • Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa yupo na amekusanya taarifa za kilichotokea kwenye makaburi ya halaiki wakati intaneti na umeme vimekatwa,
  • Mkuu wa JWTZ yupo na anajua kilichotokea mitaani nchi nzima,
  • Wakuu wa Wilaya na Kamati za Ulinzi na Usalama wanazoziongoza wapo na wanajua kilichotokea kwenye wilaya zao katika wiki ya uchaguzi, na
  • Mkurugenzi wa JUkwaa la Wahariri na Waandishi wa habari wapo na wanajua matukio yote muhimu japo hayajachapishwa magazetini
 
Ni kweli sahivi ikulu yuko Padre Kitime.

Kweli nyumbu ni chakula cha mamba hamma akili
Nguruwe kama wewe, hata akina Padre Kitime wote mtawaua, bado utataka kugeukia nguruwe wenzio, mradi tu pawepo na vurugu. Nguruwe huwa hana muda wa kutulia na kutumia akili.

Samia anaweza kuwaua wote hao nyumbu, lakini bado utakuwa huridhiki.
 
To make long story short

7. Inquiry commissions dramas:

Samia anatekeleza sera ya kutumia Tume za Uchgunguzi kuwazunga wananchi. Mfano mzuri ni Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 2025 wakati wa uchaguzi mkuu.
  • MKurugenzi wa uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi wapo na wanajua kilichotokea vituoni nchi nzila,
  • Mkuu wa Jeshi la Polisi na Ma-RPC wapo na wanajua kilichotokea barabarani chini ya usimamizi wa Kamishina wa Operesheni wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Hajj,
  • Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Uporaji Mkubwa (Special Anti-Robber Unit-SARU) yupo na anajua kikosi chake kilifanya nini mitaani katika wiki ya uchaguzi na kwa maagizo ya nani,
  • Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa yupo na amekusanya taarifa za kilichotokea kwenye makaburi ya halaiki wakati intaneti na umeme vimekatwa,
  • Mkuu wa JWTZ yupo na anajua kilichotokea mitaani nchi nzima,
  • Wakuu wa Wilaya na Kamati za Ulinzi na Usalama wanazoziongoza wapo na wanajua kilichotokea kwenye wilaya zao katika wiki ya uchaguzi, na
  • Mkurugenzi wa JUkwaa la Wahariri na Waandishi wa habari wapo na wanajua matukio yote muhimu japo hayajachapishwa magazetini
Interesting observation.
 
2. Elevation of Shariah Law over the Natural Moral Law:

Samia anatekeleza sera ya kuendesha nchi kwa kutumia mfumo wa sheria za kiislamu uitwao “shariah law,” ambao ni mfumo rasmi wa sheria za kuendesha nchi katika mataifa ambayo ni wanachama wa Jumuiya ya Waislamu iitwayo “OIC”.

Ukweli uko hivi: Katiba ya nchi (1977) inakataza uhalifu wa kijinai kama vile utekaji, mauaji holela, na ubadhirifu wa fedha na mali za umma, isipokuwa kama uhalifu huu ukifanywa na Rais mwenyewe.

Ruhusa hii ya kikatiba inapatikana kwenye ibara ya 46 ya Katiba inayompatia Rais kinga dhidi ya mshtaka yoyote ya kijinai. Rais anaweza kujizuia kufanya uhalifu huu kwa sababu za kimaadili tu.

Kama Rais ni Mkristo atatumia maadili ya Kibiblia yaitwayo “Amri Kumi za Mungu”.

Na kama Rais ni Muislamu atatumia maadili ya Kikurani yaitwayo “Shariah Law.”

Bahati mbaya mfumo wa “Shariah Law” inaruhusu mauaji holela, kwa kuwapiga mawe watuhumiwa hadi wafe, hata bila kufuata mfumo wa kimahakama, inahalalisha utekaji na utesaji wa watuhumiwa kwa kuwachapa viboko hadi 100, na kadhalika. Kwa ufupi mfumo wa “Shariah Law” hautambui ukuu wa tunu ya uhai.

Utekaji, mauaji na utesaji wa raia unaoendelea nchini ni ushahidi kuwa sasa mfumo wa “Shariah Law” umerasimishwa kinyemelea nchini Tanzania.

Lakini, kwa mujibu wa ibara ya 3 ya katiba ya Tanzania (1977), Tanzania ni dola isiyofungamana na upande wowote wa kidini, na unayopaswa kuongozwa kwa kufuata misingi ya maadili asilia, kama inavyotafsiriwa na sisi Watanzania wenyewe.

Tukisema hizi harakati zenu zinaendeshwa na chuki dhidi ya Uislam na Waislam sio kwamba sisi ni wapotoshaji. Tunaelewa tunachosema. Cha kusikitisha kuna baadhi ya ndugu zetu Waislam hawajashtuka na hili au wanapuuzia.

Wewe ni mtu mwenye chuki dhidi ya Uislam na ni mpotoshaji kwa ujinga au chuki au vyote viwili ila umezificha ndani ya maneno meeeeeeeeeeeeeeeeeengi na falsafa uchwara.
 
People dont read between the lines....

Ule mstari ndio ilikuwa kauli ya ajabu kuliko zote. Unawalaumu wazazi kwa vifo vya watoto wao? Hivi yule mama wa kule Mbeya binti yake aliyepigwa risasi wakati anaenda kumtumia hela mama yake anajisikiaje?
 
Back
Top Bottom