Mkuu
Mkandara
Nyerere hakujenga misingi na kuwaachia Wananchi, alijenga misingi na kuhakikisha viongozi wanaishi na kuihubiri. Tatizo la sasa si Wananchi, ni viongozi wasiojali masilahi ya Nchi
Yote yajadiliwe iwe udini au ukanda, lakini la Zanzibar hapana! hili tuliache tu, kama sivyo tuanze na wewe
1. Hivi ni nani kati ya Tanganyika na Zanzibar aliyeanzisha ubaguzi! Mkandara ulibaini chanzo lini!
2. Hivi ni lini Mkandara uliwahi kuuliza ikiwa KERO za Muungano zililenga kujenga Class na kuibagua Tanganyika
3. Wakati Zanzibar wanasema ni Koloni la Tanganyika na wanataka waachwe! mkandara uliandika wapi
4. Katiba ya JMT 1977 ilipovunjwa wazi wazi na Wazanzibar 2010 Mkandara ulikuwa wapi na ulishauri nini!
5. Wakati Zanzibar inapewa nafasi maalumu za Ajira, Masomo n.k. kwanini hukuona huo kama ubaguzi
6. Zanzibar n ilipoanzisha madai ya Tanganyika, kwanini Mkandara alisimama kuatetea bila kujali ubaguzi
7. Juzi, Zanzibar wametanganza kuanzisha shirika lao la ndege! juzi kushinda jana. Hivi huko si kujitenga!
Kuwalaumu Watanganyika kwa kudai kuchoshwa na ubaguzi si kuwatendea haki. Mwiba hutoka ulipoingilia
Kuhusu udini, nikukumbushe kidogo. Nyerere akitajwa Zanzibar wote wanaitikia Laanatullah kwa maana laana ya Mwenyezi mungu iwe juu ya Nyerere. Hayo hukuyoana wakati huo, leo unayaona kwa SSH!
Haya unayoyazungumzia hayakumea kama uyoga, yameanza taratibu na kupaliliwa na viongozi! na miongoni mwao ni wale waliotaka umaarufu bila kujua wanapanda mbegu mbaya