Mubarak refuses to stand down

yani hawa mafarao wanataka kumtoa mubarak na kuweka serikali ya kijeshi...hivi kweli wana akili?
 
Mubarak aelekea Sharm el sheikh, mji ulio karibu kabisa na mpaka wa Israel na Saudia tayari kwa safari ya lala salama.
Habari za uhakika ni kua jeshi chini ya mkuu wa jeshi Tantawi limechukua nchi. Habari zinaeleza pia Mubarak anataka kuhutubia Taifa kwa njia ya redio kumwachia nchi Suleiman lakini jeshi limekataa. Katika kikao cha supreme Council Mubarak na makamu wake hawakuepo. Tetesi pia zinasema Rais wa muda atakua (jina sikulipata sawa sawa, linaishia Hassan) na makamu wake atakua katibu mkuu wa Arab League Amr Mousa. Brotherhood website wanasema Mubarak ameondoka kabisa Egypt na hotuba inayo daiwa ataitoa ni pre-recorded.

Huo nao uongo. In deed hiyo site yao inasema "President Mubarak will announce constitutional procedures before handing over his powers to the vice president."
 
Wenzetu mnaangalia wapi maana tv zetu tunasubiria aseme na watu bado wamekusanyika kahaa:twitch::twitch::twitch::twitch:
 
Hizo source zako hazina tofauti na Tanzania Daima, au Mwanahalisi! Mubarak yuko Misri na atahutubia Taifa usiku huu huenda akaachia madaraka kwa mujibu wa Katibu mkuu wa chama tawala cha Misri! na sasa naangalia live Aljazeera English hakuna hicho unachokipakazia! angalia hapa: Al Jazeera English: Live Stream - Watch Now - Al Jazeera English

Na hii issue haina uhusiano wowote na TZ! sisi tunayo Serikali iliyochaguliwa na Wananchi na sio haki kulinganisha Utawala wa Egypt chini ya Hosni Mubarak alie tawala nchi hiyo miaka zaidi ya 30 sasa!

Sisi katiba yetu hairuhusu Rais kutawala zaidi ya miaka 10! na nchi yetu ni ya vyama vingi sio kama Egypt huko hakuna demokrasia wala uhuru wa vyombo vya habari! TZ uhuru huo upo ndio maana magazeti kama Mwanahalisi yanaweza kumuita Rais Jakaya kuwa ni mwizi na fisadi!

Hivyo msichanganye mambo! h

Ndivyo unavyojidanganya?? subiri uone moto wake. Misri hawakujua kuna siku watafanya walichokifanya itakuja kuwa Tz??? subirini moto utakapowaka utabaki unajiuliza hivi ni kweli. Wewe unafikiri watanzania bado wajinga kama w&&*%%^^. Hii ni njia mbadala ya kukomboa taifa. Kuna watu wataondoka watasahau na watoto wapenzi wake wakwe nakadhalika nakadhalika including you!
 
Mubarak anasubiriwa muda wowote atatoa hotuba kutoka kwenye "Palace" yake.
Source MSNBC-Hardball with Criss Mathews.
Therefore habari kuwa yuko nje ya nchi zinaweza kuwa uzushi?
 
Mubarak hataki kung'oka madarakani, atangaza kuendelea, jamaa ana roho ya paka (live speach inaendelea)
 
Mubaraka anazungumza sasa hivi,siasa nyingi tu,anajidai yuko upande wa wananchi wanaotaka mabadiliko,anaongea kwa unyenyekevu sana,anaelezea historia yake yeye kama baba mwenye familia na pia raisi aliyeiongoza nchi hiyo kwa miaka sitini kwa nyakati mabaya na nzuri.Anasema malalamiko ya wananchi ni legitimate na hivyo atawaongoza kwa usalama ili kuwepo na peacefull transition,nadhani mnaodai anajiuzulu leo ama eti yuko London mmetupiga changa la macho.Aljazeera waongo?
 
Mubarak hataki kung'oka madarakani, atangaza kuendelea, jamaa ana roho ya paka (live speach inaendelea)


...ha ha ha, na wananchi wamelegeza videvu wanamsikiliza blah blah zake. Hii ni 'political hypnotism!' wallah
 
Kasema atakaa madarakani hadi september,kwa wakati huu atasimamia reforms kwasababu anadai wananchi wana malalmiko ambayo ni "legitimate and just",na kwamba sasa ameanzisha a national dialogue,kubadili katiba na kuandaa mazingira mazuri kwa uchaguzi huru na wa haki!yani ni vituko tu mwenyewe nashangazwa na haya mazingaombwe kwasababu wananchi wao wanataka aondoke sasa hivi,yeye anazungumza yale yale tu,sioni jipya hapa!However nashangazwa na hizi tetesi ama mabadiliko ya ghafla ghafla ya maamuzi ama taarifa zinazotolewa na credible individual ama taasisi nyeti amabazo zinapelekwa kwenye news outlets....Kwasababu CIA walitoa taarifa kuwa jeshi linachukua nchi,nadhani kumefanyika majadiliano kwasababu ni juzi tu Dick Chenney alisema Mubarak ni US ally,mvutano ni mkubwa tusubiri reaction ya wananchi kwasababu wenye maslahi na taifa hilo ni wengi sana na inabidi wawe makini.
 
anwar_sadat4311.jpg

mwishowe nahisi utakuwa kama walivyomfanyia Anwar Saadat 1981.

 
Last edited by a moderator:
Kamaliza hotuba!Kamalizia kwa kusema kuwa wananchi wa Misri ni kama "Watoto wake" Hata hivyo wananchi hawataki abakie hadi september,wanataka aondoke sasa hivi!na yeye kasema atalilinda taifa lake kwa kila hali na hivyo haendi mahali....Sasa sielewi ana maana gani na wakati ameshasema malalmiko ya wananchi hao ni "Legit and just" Ndio maana nikasema ni blah blah tu!Ama kweli madaraka matam!
 
Back
Top Bottom