MUALIKO: The JF 'Rock City Wing'

Rock City

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,266
501
Salaam wakuu,

Karibuni The JF Rock City Wing.

Hii ni kuwaarifu wadau wote wa Mwanza na ng'ambo kuwa, tunataraji kufanya kikao chetu cha wing yetu hii mpya siku ya Jumatano 01.05.2013 tujaaliwapo. Muda ni kuanzia saa kumi kamili jioni.

Baada ya mashauriano ya karibu kabisa yaliyofanyika miongoni mwa wadau wa JF jijini, tumependekeza mjumuiko wetu ufanyike katika eneo la Rock Beach Hotel, katika sehemu za ndani zinazotazama ufukwe wa ziwa. Eneo hili ni jirani kabisa na Kamanga Ferry (kama unapandisha/unashuka Capri Point). Tutazidi kutoa muongozo.

Tunapenda kuwashukuru wote kwa michango yenu, changamoto zenu, maangalizo yenu na uzoefu wenu katika uanzishwaji wa wing yetu hii mpya. TUNAWASHUKURU.

Mnaweza kuwasiliana moja kwa moja na Rock City, charminglady au Elizabeth Dominic kwa maelekezo, muongozo na ufafanuzi zaidi.

Kwa pamoja, TUTAWEZA.

Ahsanteni sana na KARIBUNI.


Mwanza Oyeeeeee!!!
 
Last edited by a moderator:
Ntakuja kama mgeni "maalum"
Copy: charminglady ; Kwa ajili ya huduma ya malazi na huduma zingine za "kimwili" na kiroho.
 
Last edited by a moderator:
Rock City Nawatakia kila lililo la kheri katika kikao chenu, bahati mbaya nitakuwa na udhuru tarehe uloitaja; kwa hivyo sitaweza kuhudhuria kikao!.
 
Last edited by a moderator:
Ntajitahidi sana nihudhurie japo bandiko lako halitoi maelezo ya kutosha, pale mahali siku hizi hapaitwi Rock beach, pana jina la kichina sijalikariri, japo nimepaelewa kwa sbb nipo Mza kitambo! Pili, haujatoa angalizo la muda wa kukutana, tatu, angalau agenda za kuanzia kabla ya michango ya wadau! Ntashukuru km ukilijaza nyama bandiko lako kwa manufaa yetu sote. Ahsante
 
Thanks you for your thoughts , and swit creative ideas!
Even if the "wing" only is no longer enough !
Niulize kwa nini ? Ntakujibu.
Nway wabeja sana mwanawane! Tuli wana Ng'wanza lu'uluh, dohoo shida.
Wi aksepti inviteshen.
Bt note some clear information, such as date, venue, time.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom