MUAJI YA KINYAMA ARUSHA: Mwema, Nahodha na Kikwete Mjipime Kubakia Madarakani

Waziri Mkuu kama msimamizi mkuu wa shughuli za serikali hajatoa tamko mpaka hivi sasa. Hebu fikiri tena kuhusu credibility na accountability ya viongozi wetu wa Africa.
Huyu mzee ni hypocrite kama mara ya mwisho anakataa gari mpya ambayo ishanunuliwa na inatumika na mtu mwingine as we speak.
Wakati Mr president anaendelea na cocktail party kama hakuna kilichotokea.ridiculous!!!!!

Aheri mtu ukose hela mfukoni kuliko kukosa busara kichwani.

Kuna mtu alitoa kauli ya aina hii hapa jf na sasa napata kukubaliana nayo. Inasikitisha kweli hivi. Hata kwa hali ya kawaida tu mtu huwezi kuendelea na sherehe za harusi wakati nyumba ya jirani kuna msiba hata kama unaona msiba wenyewe haukuhusu kitu.

Sherehe kwanza, uhai na usalama wa raia wa Tanzania baadaye????
 
CCM mkiacha tukatia miili hii ya wafu wetu udongoni bila ya wahusika kuchukua hatua stahili basi niwahakikishieni kwamba mtakuwa mmeuza nafasi ya muhimu sana kwa bei rejareja machoni mwa jamii yetu ya Tanzania.

Hivi kumbe aibu na utamaduni wa watu kuwajibika uliondoka zamani na mzee Mwinnyi siku hizi kumebaki waganga njaa tu!!
 
BAADA YA CCM KUUMBUKA NA KUKODI 'BAKWATA VUVUZELA' ARUSHA, NDIO TUSEME MAREHEMU WETU WAMEGOMA KUONEWA KATI WAFU WAO HADI KABURINI??

Jamani, nilichelewa kuona taarifa hii hapa ya BAKWATA. Mbona aibu ya mwaka kwa CCM!! Aibu hii yote wenzetu CCM watapeleka wapi uso wao mbele ya jamii ya Tanzania? BAKWATA halisi ya mjini Arusha na ile ya makao makuu Dar es Salaam wamekana wahuni waliokodishwa na CCM kutoa taarifa za kukinzana na tamko la maaskofu kumkataa Meya wa Kuchonga wa CCM Arusha.

Kwa siku za jirani kidogooo naona nyota kutoka mashariki na inasema hivi kwamba wajumbe wengi ndani ya bunge hili karibia watashinikizwa na wapiga kura wao ama wakihame hili jahazi MV UFISADI linalozama kwa uongo na janja za nyani kwa jamii na kwamba wasiposikia sauti hizo kwa wakati mwafaka na basi wabakie wazame nayo.

Pia kwa mitaji hii ya mikashfa mizito mizito nchini kama vile Maruani Dowansi, EPA, MEREMETA, Mauaji ya Kinyama Arusha, Rushwa kwa familia ya Marehemu Ismael, 'BAKWATA' wa Kukodisha Arusha, 'Diwani wa Kuchonga' Chatanda, na Uchakachuaji wa Uchaguzi Mkuu, dalili zote zinaonyesha ya kwamba sehemu kubwa ya Wabunge wa CCM Uadilifu watapiga kura za chuki dhidi ya CCM Kikwete na kupitisha muswada wananchi kujiandikia wenyewe katiba mpya bila udalali.

Hiyo CCM Kikwete ambayo wabunge wengi wataiasi bungeni Dodoma sawa sawa na jinsi ambavyo mawaziri wengi tayari wamekwishaonyesha njia, wakati mwingine hujulikana kama CCM UFISADI aka Wanamtandao / Wachacharikaji / CCM Rostam Aziz ambao husemekana kwamba ndio walioufadhili mauaji ili kututisha wananchi tusiendelee kuwabana kwenye katiba mpya amba mpaka sasa imewafanya waitwe CCM Chama Cha Mauaji.

Kitakachowasambaratisha ambayo tayari imeshaondo madiwani 3 nchini kutofungamana na hiki kikundi ni HOFU KUBWA YA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YENYE DAMU MIKONO YOTE wakati utamaduniwa Ki-Tanzania hata siku moja haivumili sura ya kumwagana damu katika jamii yetu yenye upole, na ustaarabu katika haki.
 
Popote pale duniani sababu kuu ya kuwepo kwa chombo kinachoitwa SERIKALI katika jamii fulani ni kuhakikisha wakati wote kwamba wanawalinda raia wote salama na mali zao kwa usawa.

Sasa pale ambapo SERIKALI ndiyo inayoonekana kufadhili udhalimu katika chaguzi mbali mbali nchini, kuwanyima wananchi fursa ya kuwakilishwa jinsi wachaguavyo wenyewe kwa hiari yao, na kuamua kuwashamubulia kwa risasi za moto, kujenga mazingira ya kusababisha uharibifu wa mali na hata kuua kabisa kinyama kama ilivyotokea hivi karibuni mkoani Arusha, basi hapo mantiki ya kuwa na kitu SERIKALI haipo tena.

Kwa msingi huu wa kushambuliwa mara kwa mara raia nchini mwetu na kuuaua, viongozi wao kudhalilishwa, huduma za kiserikali kutolewa kwa raia kwa misingi ya itikadi zao kisiasa basi NI SHARTI WATU KUWAJIBIKA MARA MOJA kwa sababu waliokufa Arusha sio nzi, Walioua UDOM na kufichwa sio panzi na yule alieuaua Shinyanga na polisi wala sio mende hivyo kuwajibika viongozi wa juu hapa hakuna mjadala.

HOJA YANGU:


Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri Bora Utawala Mzee Tyson, Waziri Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Serikali za Mitaa George Mkuchika, IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Meya wa CCM Arusha na Mama Chitanda, nyote kwa pamoja, wakati umefika wa nyinyi kwa nafasi zenu wenyewe KUJIPIMA KWA MISINGI YA MAUAJI HAYA YA KINYAMA JIJINI ARUSHA na muone kama kweli bado ni sahihi kwenu kuendelea kuongoza katika taifa hili TUPENDE TUSIPENDE.

Haya mauaji ya raia kwa kasi kubwa hii ya ajabu si mambo madogo na kuyapuzia mbali hata kidogo kama bado tunaipenda kweli nchi yetu na kuitakia ustawi mzuri huko tuendako. Tukumbuke usemi wa wahenga; mdharau mwiba miguu huota tende, tuliwataka kujiuzulu wakati mlipompiga na kudhalilisha mbunge wa Arusha akiwa kazini jimboni kwake na mkaipuuzia mbali bila hata mtu mmoja kuwajibika na hivi sasa taifa zima hatushinikizi tena bali tunawaangalieni kwa karibu sana katika hili!!!

kujiuzuru viongozi waliopatamadalaka kwaruswa nikazi sijuwi ulio wataja kamanimiongoni
 
Popote pale duniani sababu kuu ya kuwepo kwa chombo kinachoitwa SERIKALI katika jamii fulani ni kuhakikisha wakati wote kwamba wanawalinda raia wote salama na mali zao kwa usawa.

Sasa pale ambapo SERIKALI ndiyo inayoonekana kufadhili udhalimu katika chaguzi mbali mbali nchini, kuwanyima wananchi fursa ya kuwakilishwa jinsi wachaguavyo wenyewe kwa hiari yao, na kuamua kuwashamubulia kwa risasi za moto, kujenga mazingira ya kusababisha uharibifu wa mali na hata kuua kabisa kinyama kama ilivyotokea hivi karibuni mkoani Arusha, basi hapo mantiki ya kuwa na kitu SERIKALI haipo tena.

Kwa msingi huu wa kushambuliwa mara kwa mara raia nchini mwetu na kuuaua, viongozi wao kudhalilishwa, huduma za kiserikali kutolewa kwa raia kwa misingi ya itikadi zao kisiasa basi NI SHARTI WATU KUWAJIBIKA MARA MOJA kwa sababu waliokufa Arusha sio nzi, Walioua UDOM na kufichwa sio panzi na yule alieuaua Shinyanga na polisi wala sio mende hivyo kuwajibika viongozi wa juu hapa hakuna mjadala.

HOJA YANGU:


Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri Bora Utawala Mzee Tyson, Waziri Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Serikali za Mitaa George Mkuchika, IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Meya wa CCM Arusha na Mama Chitanda, nyote kwa pamoja, wakati umefika wa nyinyi kwa nafasi zenu wenyewe KUJIPIMA KWA MISINGI YA MAUAJI HAYA YA KINYAMA JIJINI ARUSHA na muone kama kweli bado ni sahihi kwenu kuendelea kuongoza katika taifa hili TUPENDE TUSIPENDE.

Haya mauaji ya raia kwa kasi kubwa hii ya ajabu si mambo madogo na kuyapuzia mbali hata kidogo kama bado tunaipenda kweli nchi yetu na kuitakia ustawi mzuri huko tuendako. Tukumbuke usemi wa wahenga; mdharau mwiba miguu huota tende, tuliwataka kujiuzulu wakati mlipompiga na kudhalilisha mbunge wa Arusha akiwa kazini jimboni kwake na mkaipuuzia mbali bila hata mtu mmoja kuwajibika na hivi sasa taifa zima hatushinikizi tena bali tunawaangalieni kwa karibu sana katika hili!!!

Mauaji ya Arusha ni ya kinyama na ni sababu tosha ya kufukuzwa kazi kwa Saidi Simwema kwani anaendeleza yale aliyoyafanya Mbeya kwa kusababisha vifo vya mahabusu 21. Mtetezi taasisi, ninayoiongoza, ilitoa tamko kali sana juu ya mauaji haya lakini magazeti mengi yaliogopa kuitoa. Kutokana na umuhimu wake naomba nitawatumieni kesho nitakapokuwa nayo karibu.
 
Mauaji ya Arusha ni ya kinyama na ni sababu tosha ya kufukuzwa kazi kwa Saidi Simwema kwani anaendeleza yale aliyoyafanya Mbeya kwa kusababisha vifo vya mahabusu 21. Mtetezi taasisi, ninayoiongoza, ilitoa tamko kali sana juu ya mauaji haya lakini magazeti mengi yaliogopa kuitoa. Kutokana na umuhimu wake naomba nitawatumieni kesho nitakapokuwa nayo karibu.

Ni mshangao wa kila mtu hapa kwamba mpaka dakika hii hamna wa kuwajibika serikalini kwa damu isiyo na hatia iliyomwagwa na mwenye jukumu la msingi kulinda uhai wa kila mmoja wetu.
 
kujiuzuru viongozi waliopatamadalaka kwaruswa nikazi sijuwi ulio wataja kamanimiongoni

Kama kweli kikwazo kwa watu kuwajibika wanapofanya makosa katika kazi za umma hutokana na ukweli kwamba vyeo vyao wamevigharamia kwa fedha binafsi kuvipata basi bado tunashida kubwa ambayo inaweza tu ikaondolewa na wananchi kujiandikia katiba mpya nchini.
 
Ni mshangao wa kila mtu hapa kwamba mpaka dakika hii hamna wa kuwajibika serikalini kwa damu isiyo na hatia iliyomwagwa na mwenye jukumu la msingi kulinda uhai wa kila mmoja wetu.

Anaetakiwa kuwajibika ni yule aliye waambia waandamane.
 
Anaetakiwa kuwajibika ni yule aliye waambia waandamane.

Aliyeruhusu wananchi kuandamana, nijuavyo mimi ni KATIBA ya sasa ikieleza ya kwamba ni haki yao kufanya hivyo na kwamba polisi ni WAKUPEWA TU TAARIFA (SI CHOMBO CHA KUOMBWA KURUHUSU) KUWEPO KWA MKUTANO WA HADHARA. Lengo la kuwataarifu ni kwa ajili tu ya kuja kulinda.

Sama mlinzi anapojigeuza gafla kutaka aonekane bosi yeye wakati bosi halisi ambaye ndiye anayemlipa mshahara kwa kodi anadiriki kumfyatulia risasi, hii ni dhahiri dalili za watu kulewa madaraka na kuchanganyikiwa tu!!

Ninayo uhakika kwamba hata wewe hapo ukweli huu unaufahamu sana tu lakini kwakuwa tunaishi katika zama za KIFISADI basi kila kitu watu kama wewe huzigeuza up-side down kwa maslahi ya tumboni kwako tu.

Hii ndio tunasemea kwamba ni uongozi mahiri unaozingatia uwezo mkubwa wa kufikiria kila kitu KUPITIA MAELEKEZO YA TUMBO na wala si kwa uwezo wa akili inavyosema.
 
Mimi bado naamini kuwa IGP Mwema ametumiwa tu - yaani amepokea order kutoka juu na kama ilivyo ada, ili aweze kuendelea kukalia kiti chake alikuwa hana budi kutii amri ya wakulu... ndio vyeo vyetu vya bongo hivyo . Cheo kikubwa lakini mtu huna say. Ukijifanya kichwa ngumu yanakukuta yaliyomkuta Tido Mhando
Serikali ndiyo wavunjifu wa amani ya Tanzania, wakisaidiwa na Mheshimiwa "Mwema na watu wake" Viongozi wetu wamekua wanahubiri demokrasia isoyoonekana! Wanawaua wenzetu kama wanyama wa pori lisilolindwa!! Hii tunasema hatukubaliani nao kabisa, lazima wawajibike! Chadema waliandaa maandamano ya amani, na walitembea kilomita 2 bila kuleta vurugu, sasa kilomita chache zilizobaki kufika uwanjani ndiyo wangeleta hizo vurugu? kwa kweli polisi ndiyo walioleta vurugu, IGP na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha mnatakiwa kuwajibika mara moja. Watanzania siyo wapole kama mnavyofikiri, tunazijua haki zetu, na Polisi mkiendelea kuwaua ndugu zetu itafika mahali tunashindwa kuvumilia "Point of no return" na mtapambana na nguvu ya uma!
 
IGP Mwema si mwema kwetu hapa hata kidogo.

Katika masuala ya kipolisi nchini mwetu huyu ndugu yetu ndiye polisi namba tatu baada ya Mhe Kikwete na Nahodha.

Na kwa mujibu wa dhana zima ya utawala bora na mazingira yote yaliotufikisha hapo ni kwamba wote watatu wanatakiwa waende nyumbani kwa kushindwa utumishi kwa vigezo vilivyowekwa na katiba ya sasa.

Endapo watagoma kufanya hivyo basi doa hilo litakuwa zito mno kulifuta katika jamii yetu hii na kwa vizazi vijaavyo.
 
Wapendwa wanaJF na watanzania wenzangu wote,

Nichukue fursa hii kutoa pole zangu za dhati kwa watanzania wote kwa msiba mkubwa uliolikumba taifa kutokana na mbinu dhaifu, zilizopotoka na mbaya za ulinzi zilizotumiwa na jeshi letu la polisi kwa maelelkezo ya viongozi wao na kusababisha maafa ya raia wema mkoani Arusha tarehe 5 January 2011 wakati wakitekeleza kwa vitendo haki yao ya msingi ya kukutana na kuandamana kwa mujibu wa katiba.

Binafsi sikuwepo nchini wakati hayo yakiokea na nilifuatilia tukio zima kupitia mitandao ya internet. Niseme tu kuwa najua hivi sasa marehemu wamekwishaagwa na kuzikwa huku wakipewa heshima wanayostahili na chama cha demokrasiaa maendeleo CHADEMA na wakazi wa Arusha na vitongoji vyake na hata miji jirani. Ila nimesikitishwa sana na kutojitokeza kwa kiongozi yoyote wa serikali na wa chama cha mapinduzi kushiriki waziwazi kwenye msiba huo. Kuna wakati inabidi hata mchawi mwenyewe kuhudhuria msiba kwani ni katika matukio kama hayo dhamira ya kweli ya umoja na undugu hudhirika.

Pia nimeshangazwa sana na kitendo cha waziri mkuu kushindwa kutoa tamko lolote la serikali hadi wakati huu, si kwa uchaguzi wa meya wala wa machafuko yaliyosababisha umwagaji wa damu zisizo na hatia. Hali kadhalika sijasikia kauli thabiti ya wahusika kukemea na kukosoa jeshi la polisi kwa mashambulizi dhidi ya raia kwenye maandamano ya amani kwa kutumia risasi za moto. Yote haya kwangu yanadhihirisha udhaifu wa uongozi na ulegevu katika kuchukua hatua madhubuti pale zinapohitajika.

Nakumbuka wakati IGP mstaafu Omary Mahita aliposhutumu wabunge kujipendelea kwa mishahara na posho kubwa huku askari wake wakiwa na maisha na zana duni, haraka haraka aliomba radhi baada ya kubanwa na kamati ya bunge iliyokuwa chini ya mh Simpasa. Binafsi nilichukizwa kuona askari akiomba radhi mwanasiasa, lakini kwa hili la Arusha naamini itakuwa heshima viongozi wa jeshi hasa IGP mwenyewe akiwaomba radhi wananchi wote wa Tanzania kwa jeshi lake kushindwa kulinda usalama na badala yake kushambulia hata pale palipokuwa hakuna tishio lolote la kiusalama. Hata kama ni kwa kupotoshwa na taarifa za kiintelijensia, bado anapaswa si tu kuwachukulia hatua waliompotosha, bali pia kuwajibika kwa kutoa maagizo yaliyopelekea maafa kwa raia wema na uharibifu wa mali.

Kumhusu waziri Nahodha, mie binafsi sijapata kufurahishwa na uongozi wake tangu alipokuwa waziri kiongozi huko Zanzibar. Ni kwamba sijajua vigezo vilivyotumika kumweka hapo alipo, lakini kwa hili la arusha na lile la zanziba wakati wote akiwa madarakani na kuhusika moja kwa moja na matukuio yote mawili, naye anapaswa si tu kuwajibika , bali kjichunguza kama kweli anaweza kuwa kongozi wa dhamana ya kiwango alichonacho na bado akawa ni wa kutumainiwa. Tathmini hiyo yafaa pia kufanywa na rais kikwete na iwe ni dira ya kumuongoza katika kuteua wasidizi wake kwa siku zijazo.

Mwisho niupongeze uongozi wa CHADEMA kwa kutoyumba katika kutetea kile wanachoamini na kuwapa heshima waliyostahili ndugu zetu wote waliotutoka. Ni changamoto kama hizi ndio zimebadili sehemu nyingine za dunia na kuwa na demokrasia za kupigiwa mfano. aidha chama cha mapinduzi nacha chapaswa kujitafakari namna kinavyoendesha siasa zake hasa miongoni mwa watu wa tabaka za chini. nafikiri ni wakati muafaka sasa wa CCM kujihoji pia kama bado inamhitaji luteni makamba kuendelea kuwa katibu mkuu wake. Matatizo kama haya yalihitaji umakini wa kiuongozo ili kuayepuka na hata watu wadogo kinafasi na kiwadhifa kama mary chatanda leo wasingekuwa wanjulikana kiasi hiki. Kule kushindwa kutokea kwenye msiba, kunadhihirisha kuwa CCM na serikali yake wamewaachia CHADEMA msiba wao. Hili ni kosa na hata kama hawataelewa leo, wataelewa kesho.

Nimalizie tena kwa kutoa pole kwa wafiwa na majeruhi wote na kumuuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. amina
 
dah,am sure umeandika mambo mazuri ila tatizo ni ndefu kweli na nawahi kujenga nchi,thanks
 
Waliouawa na polisi waagwa na halaiki


*Viongozi wa dini wasema wamekufa wakitetea taifa
*Freeman Mbowe adai mauaji hayo yalikuwa yamepangwa


Na Glory Mhiliwa, Arusha.

MAELFU ya wakazi wa Arusha na mikoa ya jirani jana walijitokeza katika kuaga miili ya
watu waliouawa na polisi kwa risasi kwenye maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yaliyofanyika Januari 5, mwaka huu.

Ibada za kuaga miili ya Denis Shirima na Isimal Omar ilifanyika jana katika Uwanja wa NMC baada ya maandamano yaliyotokea katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, saa nane na robo.

Ibada hiyo iliongozwa na viongozi wa dini wa madhehebu ya kikristo na kiislamu, ikiwashirikisha viongozi wa Taifa wa CHADEMA, wabunge wa chama hicho, wanachama, rafiki, ndugu, jamaa na wananchi wengine.

Katika ibada hiyo alianza Ustadh Alawi kuuombea dua mwili wa marehemu Ismail Omar kwa kusema amekufa kutokana na kupigania haki ya taifa kuwa na katiba mpya.

Alifutiwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini Dayosisi ya Mjini Kati Askofu Thomas Laizer ambapo alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni kupigania haki ya Watanzania.

"Sisi viongozi wa dini tutaendelea kuishauri serikali na kutoa maoni yetu maana na sisi pia ni sehemu ya jamii namshangaa Bw. Makamba anapotukejeli kwa kauli anazozitoa huku akitumia vifungu vya kwenye biblia, uelewa wake kwenye biblia kwanza ni mdogo sana, haelewi hata maana ya neno tiini mamlaka iliyo juu yenu," alisema Askofu Laizer.

Alisema kuwa inashangaza kuona hata Katibu wa Mkoa wa Arusha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Mary Chatanda kuambukizwa na Bw. Makamba ambaye amekuwa akiwakejeli viongozi wa dini.

Aidha katika ibada hiyo pia alikuwemo Diwani wa Kata ya Sombetini kupitia TLP, Bw. Michael Kivuyo ambaye hivi karibuni alijivua unaibu meya na kuungana na CHADEMA kwa madai ya kuwa hawezi kuongoza manispaa hiyo ikiwa katika dimbwi la damu.

Ndugu wa marehemu pamoja na viongozi wa CHADEMA pekee ndio walioruhusiwa kuwaaga miili ya marehemu hao baadaye mwili wa Isamil Omar ulikwenda kuzikwa Lekitatu, Usa River Arumeru na mwili wa Dennis Maiko Shirima ulisafirishwa kwenda Rombo Kilimanjaro kwa mazishi yanayofamyika leo.
 
Hongera Mbunge, isinge kuwa busara kwenda pale maana ndo wenyewe wamesababisha mauaji haya.
 
itakuwa ndoto kwa viongozi wa tanzania kujiuzulu hata kama wangekuwa wame sababisha mauaji ya watoto wao
 
Hawajapiga risasi wao why wajiuzuru? hata waliosign mikataba mibovu isiyo na tija ndio hao hao viongozi wetu

167109_175117322524527_135719259797667_317209_3652943_n.jpg
 
Well said!
Hicho chama chenu kingekuwa na watu wengi kama wewe, mbona nchi hii ingekuwa mbali!
Mkuu karibu huku ... ccm is a sinking ship!
 
Back
Top Bottom