Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
Popote pale duniani sababu kuu ya kuwepo kwa chombo kinachoitwa SERIKALI katika jamii fulani ni kuhakikisha wakati wote kwamba wanawalinda raia wote salama na mali zao kwa usawa.
Sasa pale ambapo SERIKALI ndiyo inayoonekana kufadhili udhalimu katika chaguzi mbali mbali nchini, kuwanyima wananchi fursa ya kuwakilishwa jinsi wachaguavyo wenyewe kwa hiari yao, na kuamua kuwashamubulia kwa risasi za moto, kujenga mazingira ya kusababisha uharibifu wa mali na hata kuua kabisa kinyama kama ilivyotokea hivi karibuni mkoani Arusha, basi hapo mantiki ya kuwa na kitu SERIKALI haipo tena.
Kwa msingi huu wa kushambuliwa mara kwa mara raia nchini mwetu na kuuaua, viongozi wao kudhalilishwa, huduma za kiserikali kutolewa kwa raia kwa misingi ya itikadi zao kisiasa basi NI SHARTI WATU KUWAJIBIKA MARA MOJA kwa sababu waliokufa Arusha sio nzi, Walioua UDOM na kufichwa sio panzi na yule alieuaua Shinyanga na polisi wala sio mende hivyo kuwajibika viongozi wa juu hapa hakuna mjadala.
HOJA YANGU:
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri Bora Utawala Mzee Tyson, Waziri Mambo ya Ndani Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Serikali za Mitaa George Mkuchika, IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Meya wa CCM Arusha na Mama Chitanda, nyote kwa pamoja, wakati umefika wa nyinyi kwa nafasi zenu wenyewe KUJIPIMA KWA MISINGI YA MAUAJI HAYA YA KINYAMA JIJINI ARUSHA na muone kama kweli bado ni sahihi kwenu kuendelea kuongoza katika taifa hili TUPENDE TUSIPENDE.
Haya mauaji ya raia kwa kasi kubwa hii ya ajabu si mambo madogo na kuyapuzia mbali hata kidogo kama bado tunaipenda kweli nchi yetu na kuitakia ustawi mzuri huko tuendako. Tukumbuke usemi wa wahenga; mdharau mwiba miguu huota tende, tuliwataka kujiuzulu wakati mlipompiga na kudhalilisha mbunge wa Arusha akiwa kazini jimboni kwake na mkaipuuzia mbali bila hata mtu mmoja kuwajibika na hivi sasa taifa zima hatushinikizi tena bali tunawaangalieni kwa karibu sana katika hili!!!