Muafaka CCM na CUF, pande mbili za shilingi!

Haya ndio maneno, at last CUF wanaanza kutuonyesha tulichokuwa tukisubiri miaka yote!...
 
lipumba seif.jpg
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam jana, kuhusu mazungumzo ya muafaka kati ya CUF na CCM. Kulia ni Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad. (Picha na Zuberi Mussa)

http://www.majira.co.tz/
 
Nimemsikilia Katibu Makamba; hana jipya mambo ni yale yale ya CCM kuwafanya Watanzania wajinga. CCM wanaongoza kwa kuwahadaa watanzania; Mwenyekiti wa CUF anasema CUF wamejitoa; yeye anasema Mazungumzo Yanaendelea...sasa yanaendelea kati ya CCM na chama gani?

Then, hadaa nyingine anasema hakuna mgogoro wa kusuluhisha; Mwenye akili ajiulize walikuwa wanakutana wanajadili nini...kwani ulikuwa mkutano wa kujadili posa ule?

CCM hizi tactics zenu zina mwisho; tena sio mbali wananchi wameshaanza kushtuka.
Mzee Makamba alikuwa anajibu tu kisiasa na kwa kwa juu juu- CCM kuna ukweli wanaupotosha! Ni vyema CUF wamekuwa open na kusema. Hii naona ni strategy ya CUF kuwachagiza CCM wawe serious- na warudi kwenye mazungumzo!
 
CUF wajitoa rasmi kwenye mazungumzo ya muafaka na CCM.

Kwa habari za uhakika ni kuwa chama cha CUF leo kimejitoa rasmi kwenye mazungumzo ya muafaka yaliyokuwa yanaendelea na CCM juu ya mpasuko wa kisiasa kule Zanzibar .

Tamko rasmi la chama hicho limetolewa na mwenyekiti wake Prof> Lipumba leo majira ya saa sita mchana .

Nalitafuta tamko then ntaliweka ila atakayelipata mapema basi aliweke.

Duh sasa kuna sababu zozote zilizotolewa kwa kujitoa huko?

Najua hi ni game lakini kati ya CUF na CCM kunatakiwa kuwepo na mutual agreement na mutual benefit kwa wote sasa inawezekana CUF hawajaridhishwa na mchezo wa CCM. Ila hili ni tatizo na ni hatari si kwa Zanzibar tuu bali pia kwa Tanzania nzima.
 
Walipaswa kujitoa kwani kila wakati CCM panmoja na viongozi wao wamekuwa wakitoa kauli tete na mwenyekiti wa chama ambaye ni rais hajawahi kusikika akiwakemea wala kutoa msimamo wake juu ya kauli hizo za makamba,kingunge na seif khatibu.

Jambo baya ni kuwa CCM wakiwa kwa wafadhili waliwza kujichotea billion kumi na tatu 13 billion kwa ajili ya muafaka na huenda wamechukua nyingine nyingi zaidi kutoka kwa wafadhili.
 
Tamko lenyewe hili hapa ,

(CUF – Chama Cha Wananchi)
TUSIPOZIBA UFA ZANZIBAR, TUTAJENGA UKUTA TANZANIA
Zikiwa zimebaki siku saba tu kabla ya kufikia mwisho wa mazungumzo kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi (CUF) yaliyokusudiwa kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar, Chama chetu kimelazimika kuwatangazia Watanzania wote na ulimwengu kwa ujumla kuwa mazungumzo hayo ambayo yameshachukua miezi minane yamekwama kwa kipindi kirefu sasa na hakuna dalili zozote za kuweza kukwamuka.

Kukwama kwa mazungumzo hayo kumetokana na CCM kuingia katika mazungumzo haya kikiwa hakina dhamira ya kweli na ya dhati ya kuupatia ufumbuzi wa kweli mpasuko huo na pia kumetokana na Rais Jayaka Kikwete kushindwa kuyasimamia ipasavyo na kuyapa uongozi na mwongozo wa kisiasa unaohitajika.
Inaonekana lengo pekee la CCM katika mazungumzo haya lilikuwa ni kuwahadaa Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwa kujaribu kuidhibiti kisiasa CUF kupitia utaratibu wa kuwapa matumaini ya uongo (strategic engagement) na kuyarefusha mazungumzo hayo kadiri inavyowezekana hadi kipindi kinachokaribia uchaguzi mkuu ujao pasina kuchukua hatua zozote za maana zenye kulenga kutoa ufumbuzi wa kweli, wa haki na wa kudumu wa mpasuko uliopo.

Huku ni kucheza na amani na utulivu wa nchi yetu. CCM imeonesha wazi wazi kuwa haiitakii mema Tanzania yetu na wala haitaki kuona umoja wa kitaifa na utulivu wa kudumu vinapatikana Zanzibar ambayo ni sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano.

Tunachukua nafasi hii kuwahakikishia Watanzania na ulimwengu kwa jumla kuwa CUF kwa upande wake imechukua kila juhudi kuona mazungumzo haya yanafanikiwa. Imetoa kila ushirikiano unaohitajika kwa CCM na hata kuachia madai yake makuu (kutoa ‘concessions’) ili kuyanusuru mazungumzo hayo na kuyafanikisha. CCM haionekani kujali au kuthamini juhudi hizo.

CUF imemuandikia barua mbili Rais Jakaya Kikwete kumtaka aingilie kati mazungumzo hayo lakini haoneshi kujali. Barua hizo amezipuuza na hatukupata majibu yoyote. Hatuelewi kama Rais Kikwete amesalimu amri kwa wahafidhina ambao walikwishaapa kuwa watahakikisha mazungumzo haya yanakwama au na yeye mwenyewe ni sehemu ya mpango wa kuyakwamisha.

Rais anapaswa ajue kuwa heshima ya ofisi yake na uadilifu wake binafsi uko katika mtihani na majaribu makubwa kutokana na kushindwa kusimamia kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa kwa Watanzania kupitia hotuba yake ya Desemba 30, 2005 Bungeni na pia ahadi aliyoitoa na kuirejea mara kadhaa kwa marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa katika ziara zake za nje ya nchi kila mara pale alipoulizwa kuhusiana na mgogoro wa muda mrefu wa kisiasa Zanzibar.
Maelezo ya kina kuhusu nini kilichojiri katika mchakato mzima wa mazungumzo haya tutayatoa kwa Watanzania na ulimwengu wa kimataifa baada ya kumalizika muda waliokubaliana kwa maandishi Makatibu Wakuu wa CCM na CUF, Mhe. Yussuf Makamba na Maalim Seif Sharif Hamad, kukamilisha mazungumzo ambayo ni Agosti 15, 2007.

Mkutano huu wa leo una dhamira moja tu ya kuendeleza juhudi za CUF za kuyanusuru mazungumzo haya hata katika siku chache zilizobaki kabla hayajafikia tarehe ya mwisho tuliokubaliana. Tunataka Watanzania wote na jumuiya ya kimataifa wawe mashahidi kuwa CUF imefanya kila liliomo katika uwezo wake kuinusuru hali tete ya kisiasa Zanzibar isichafuke. Hali ya kisiasa Zanzibar ni mbaya sana kutokana na wananchi kukatishwa tamaa na tabia ya kigeugeu, hadaa na hiyana ya CCM inayolenga kuendelea kuibakisha Zanzibar katika migogoro. Kumbukumbu za wananchi za hujuma za CCM na Serikali zake kuvuruga Muafaka I na II zinaonekana kuthibitishwa na hatua za sasa za kuyakwamisha na kuyavuruga mazungumzo haya. Mgogoro wa kisiasa unaambatana pia na hali ngumu ya maisha kwa Wazanzibari inayosababishwa na hali mbaya ya uchumi na ufisadi wa hali ya juu unaofanyika Zanzibar.

Yote haya yamewaweka Wazanzibari katika hali ya kukata tamaa. Hii ni hatari. Watu waliofikishwa hapo wanaweza kuchukua hatua zozote zinazoweza kuigharimu nchi yetu pakubwa na kuiondolea sifa tunayojitangazia kuwa ni kisiwa cha amani katika Afrika. CCM imeifikisha Zanzibar katika hali ambayo imeziingiza nchi nyingine za Kiafrika katika vurugu kubwa. Sisi katika CUF hatutaki tufike huko.

Mazungumzo haya ya CCM na CUF yamekwama. Juhudi za CUF kuyakwamua na kuyafikisha tamati kwa kupata ufumbuzi wa haki na wa dhati haziungwi mkono na CCM. Imedhihirika kuwa vyama hivi viwili vinavyovutana na vinavyoshiriki mazungumzo haya haviwezi wenyewe kujikwamua. Rais Kikwete ameshindwa kuchukua hatua za kuingilia kati.

Kutokana na hayo basi, CUF imeamua kujitokeza hadharani kutoa wito kwa Watanzania, marafiki wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti na za uhakika kuingilia kati hali hii sasa ndani ya kipindi hiki cha siku saba zilizobaki kuyanusuru mazungumzo hayo.

Baada ya Tanzania yenyewe kushindwa katika utatuzi wa mgogoro wake huu wa muda mrefu, sasa ni wakati muafaka kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kwa kuchagua Mpatanishi wa Kimataifa anayeheshimika kuja kuyasimamia hadi kuyafikisha ukingoni kwa kuhakikisha makubaliano ya dhati yanafikiwa yatakayotoa ufumbuzi wa kweli na wa haki wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar.

Jumuiya ya Kimataifa iepuke fedheha iliyoipata katika nchi nyengine za Kiafrika ambazo iliziachia hadi hali ikachafuka na ndipo ikaingilia kati. Hali ya Zanzibar ni mbaya. Ilitulia kwa sababu ya matumaini ya Wazanzibari na Watanzania kwamba mazungumzo ya CCM na CUF yataleta suluhisho la utulivu na umoja. Mazungumzo hayo sasa yanaposhindwa na yanapokosa uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yanahitaji kuona jumuiya ya kimataifa inaingilia kati kwa hatua za wazi na madhubuti kuinusuru Zanzibar na Tanzania isitumbukie kule nchi nyingine za Kiafrika zilipotumbukia.
TUSIPOZIBA UFA ZANZIBAR, TUTAJENGA UKUTA TANZANIA.

Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa Taifa
Agosti 7, 2007.
 
Sijaelewa hapa. Hivi cuf wamejitoa ama la? Maana naona blah blah tu hapo kwenye tamko uchwara.
 
Kama CUF wameng'amua janja hiyo ni ajabu sana maana walionekana kuwa wake kwenye lepe zito la usingizi. Ni kama ile tuliyokuwa tunasikia danganya toto. Lakini ntaamini kama kweli wameng'amua, maana ninachojua ni kuwa wateleta vuzrugu kidogo pale mji mkongwe wakati wa uchaguzi, watapigwa mikwaju halafu unaitwa mwafaka unarushwarushwa hadi unapokuja uchaguzi mwingine, and on and on and on.....sasa kama wameng'amua janja hiyo hongera. Nadhani tunaweza kutegemea a long term solution as a result of this.
 
Huu Muafaka ilikuwa ni janja ya CCM tu kubuy time hadi uchaguzi ufike walikuwa hawana nia ya muafaka waliwatia CUF katika ntego na wao wakaingia - sasa watakuwa na cha kusema kuwa CUF ndio waliovunja Muafaka ule.

Seif khatibu si kesha sema kuwa Muafaka waliufanya tangu 1964 so kwa sasa hakuna Muafaka mwengine, yote ni geresha tu.

Hata akiletwa msuluhishi kutoka nje haitosadia kitu madhali CCM hawajawa tayari kuletea amani Zanzibar, kwani si alikuja msuluhishi kutoka umoja wa madola na akaleta suluhu zanzibar na matokeo yake sote ni mashuhuda.

Wanachoogopa CCM bara ni kuwa iwapo CCM itashindwa zanzibar (kutokana na Muafaka)kwa sababu Muafaka utaweza kuwawekea mazingira mazuri CUF kushinda zanziba, basi na CCM bara watakuwa katika hali ngumu.
 
Duh! Kumbe muafaka ni kwa ajili ya kuwawekea cuf mazingira mazuri ili washinde uchaguzi zanzibar!!! Kwa mtaji huo hata kama ningekuwa hao ccm, nisingekubali kabisa.
 
Duh! Kumbe muafaka ni kwa ajili ya kuwawekea cuf mazingira mazuri ili washinde uchaguzi zanzibar!!! Kwa mtaji huo hata kama ningekuwa hao ccm, nisingekubali kabisa.

ndio maana hawataki Muafaka - wanawachezea kuf tu
 
Nawapa 5 CUF kujitoa, kwa sababu CCM hawakuwa serious.kutatua matatizo ya Zanzibar, CCM inatakiwa inanze kwanza kutafuta KATIBU MKUU mwingine mwenye visison.
 
Kimsingi hata mantiki ya hii kitu muafaka siioni. Na tatizo silioni. Hapa suala ni madaraka tu ambayo sidhani kama yanawasaidia wananchi isipokuwa hao wanasiasa uchwara na njaa zao zisizoisha.

Nilitegemea kama cuf wamegundua kwamba wanachezewa shere, wangetangaza kwa ujasiri kwamba wamejitoa, ila sasa kwa kuwa wanajua kwamba wanahusika kwa asilimia kubwa kuvuruga amani huko Zanzibar ndiyo maana wanalilia jumuiya ya kimataifa iuendeleze muafaka mfu na wakati jamaa walishakuja na wakagundua ni janja ya nyani tu. Nawahurumia sana maana sasa wanaelekea kubaki historia.

Hawa jamaa (cuf) wana ubinafsi sana, na kama siyo kupigiwa kelele na kulaaniwa walikuwa wameamua kuwatenga wabunge wengine wa vyama vya upinzani katika kuunda kambi ya upinzani bungeni. Mabaguzi kweli kweli haya majitu. Yaani mijitu haina mbunge hata mmoja Tanzania Bara, halafu inajifanya kuunda kambi ya upinzani ambayo haina hata sura ya kitaifa. To hell with their muafaka.

Muafaka muafaka kitu gani! Si bora wakafanya kama pelipehutu ili kikaeleweka badala ya mikwara bubu tu. Huo ukuta tuone jinsi utakavyojengwa. Yaani wameona mafungu ya muafaka hayatoki tena ndiyo wanalia sasa hivi, mbona wakati posho zipo walikuwa wakishirikiana na ccm kuficha taarifa za huo muafaka butu. It's time kwa Lipumba na Seif kung'atuka ili chama kikapata watu makini wa kukipa mwelekeo vinginevyo hakuna cuf tena.
 
Makamba ,makamba,makamba,alichosema kwenye interview na BBC ni aibu kwa ccm na taifa kwa ujumla eti kuwa Lipumba hawezi kuzungumzia muafaka kwa kuwa yeye siyo mjumbe ni aibu?

Akasome katiba ya CUF ajue msemaji mkuu wa chama ni nani?
 
Makamba ,makamba,makamba,alichosema kwenye interview na BBC ni aibu kwa ccm na taifa kwa ujumla eti kuwa Lipumba hawezi kuzungumzia muafaka kwa kuwa yeye siyo mjumbe ni aibu?

Akasome katiba ya CUF ajue msemaji mkuu wa chama ni nani?



Of course, Seif hawezi kupinga jambo ambalo linampa maslahi. Lipumba hapo anafanywa mbuzi wa kafara tu ili mambo yakiharibika yeye ndiye awajibike. Kawaida ya Seif ni kuuandaa moto na kumweka Lipumba mbele ili auwashe, na ukishawaka ukalipuka Seif uingia mitini na kuwaacha wenzake wakiugulia maumivu. Baadae anarudi na kuanza kuwatembelea na kujifanya anawaonea huruma kumbe yeye anajua anachokitafuta.

Lipumba jihad inaelekea kumshinda na siku si nyingi atatupwa pembeni kama Mapalala.
 
ilongo kweli ndugu yangu una songo na hawa jamaaa.

lakini kuwa binaadam kidogo halfu soma tena alama.
 
Waungwana naogopa mno ninapoona kuwa nasi JF tuna Tabia ya kutojali mambo yanayohusu maisha ya wenzetu.Utofauti wa Msomi na yule asiyeenda shule ni Ustaarabu na kujua ku-value Utu wa mwenzake.Suala la Mtafaruku wa Zanzibar tunaliangalia kwa upeo Mdogo,Kutakuja tokea matatizo ambayo tunaweza kabisa kuyatafutia Ufumbuzi Leo!.Viongozi wetu wana tabia ya kutojali kwa yale mambo wasioyapenda,Wameweza kuwakana Vijana huko Ukraine wakati Vigezo vyote vimeonyesha kuwa wao ndio waliwapa Go ahead ya kwenda kutafuta Elimu Huko.Leo wanapuuzia Muafaka(II) Kati yao na Chama cha CUF,Hii ni Hatari na linaweza kusababisha vifo!!!

Kwa wale mtakaokuwa na kumbukumbu nzuri,mtakumbuka kuwa Hotuba
ya kwanza ya JK Bungeni ile 30/Desemba/2005 ,alisema atatumia nguvu zake zote kumaliza matatizo ya Zanzibar!,Kama kawaida kaingia (Ikulu) madarakani na jukumu la Matatizo hayo kampa Kingunge na Makamba,Watu hawa hawapendi mabadiliko,wanataka kuona CCM ndio yenye kuongoza Daima,hata kama inakosa Ridhaa ya wananchi,wameshindwa kujenga mazingira ya Chama hichi kupendwa Pemba na Unguja,na ndiyo hiyo iliyoleta Mtafaruku wa kuuliwa watu kule Pemba (Enzi za Mkapa).Muafaka (I) Ulimalizika bila makubaliano,na huu Muafaka(II)Unaonekana unafikia ukingoni bila maamuzi ya maana!,Hali hii itakwenda hivi mpaka lini?.

Siku Muungwana JK alipomchagua Makamba kuwa Katibu Mkuu wa CCM alisema amemchagua ili akajibu mapigo ya Wapinzani!,Makamba anajibu mapigo kwa kiswahili cha mtaani,Uwezo wake wa kujadili mambo kwa kina ni Mdogo,yeye ni mtendaji zaidi kama askari polisi ,lakini sio Negotiator!!,Kwa Mtazamo wangu Mzee Mangula alikuwa mtu mwenye akili ya kuweza kuzungumza na kutatua matatizo kwa majadiliano lakini sio huyu Makamba!.Sasa tunarudishwa nyuma,na tunarudisha hali ya wenzetu Wazanzibari nyuma pia,kwa sababu wao ndio waathirika zaidi!.Muafaka huu umezungumzwa kwa miezi 8 bila kufikia makubaliano!,Nafikiri sasa ni muda Muafaka kwa jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kabla hali haijakuwa mbaya zaidi!.

Wanaoumia hapa sio Seif,Lipumba au hao CCM,wanaopata matatizo ni raia wa kawaida,kwani sehemu kama Pemba ambayo haina uwakilishi wa CCM imeachwa hata katika miradi ya Maendeleo.Waungwana Tuujali Utanzania wetu kuliko Itikadi za Vyama vyetu!!Balaa hili la CCM na CUF litaleta Mmomonyoko Mkubwa kwenye Muungano!,wale mnaomshauri JK,p/se mwambieni aende huko Zanzibar na kulifanyia kazi hili kwa Uwazi!!!Suala liwe Utanzania wake na sio Itikadi zake za Uccm!!

Ni Imani yangu kuwa tutalijadili hili kwa uwazi hapa tukijali UTAIFA wetu.Tuweke TAIFA mbele kabla ya Itikadi zetu za Vyama!.
 
1. Kulikuwa na rule zimewekwa kuhusu huu muafaka, kwamba wasemaji watakuwa makatibu wakuu tena sio mmoja mmoja bali wote wawili? swali hii rule imetenguliwa lini, mpaka ikabidi wenyeviti wa vyama ndio waongelee muafaka?

2. Mazungumzo yamfuaka yalitakuwa wayabreak makatibu wakuu!!!

Tuwe makini sana kuangalia mwenendo wa wanasiasa wetu otherwise watatuchezea michezo wanaowachezea wananchi kila siku!

3.The fact kwamba muafaka huu hauna neutral person/institution on it,,,say for example third party, this is the very very weakness of the ongoing muafaka.

4. Accordingly to previous set rules, CUF wametengua rule walizokubaliana na CCM, kwamba mazungumzo hayo ni siri.


Maoni yangu tu!
 
Nadhani mpaka sasa naweza kusema kutokana na hali iliyopo Tanania sio rahisi issue ya Zanzibar kupatiwa long term solution. Uongozi wa CCM sasa hivi naweza kusema una nguvu kabisa katika historia ya chama katika siku za karibu, lakini vilevile huenda ni uongozi uliokosa vision kabisa, pamoja na kuwa kuna manifesto na wanachokiita vision 2025, lakini kwa miaka hii miwili inaonekana yote yamewekwa kando. Katibu mara nyingi ndiye nguzo ya uongozi wa chama, maana yeye nadiye anashughulikia mambo ya kila siku ya chama. Katibu aliyepo sasa hivi anaonesha kuwa ni mtu ambaye hajai-master manifesto na hata vision 2025 haiko karibu naye. Anakuwa kama ni demagogue politician. Ukiangalia na make up nyingine ya chama unaweza kuwa na hofu zaidi kama long term solution itapatikana.
 
View attachment 499

Hati ya Muungano iko wapi? Mimi kwa sasa nafahamu waasisi wetu walikuwa wanashinikizwa na "western na eastern blocks" kwa manufaa ya wakati ule na sio sasa. Siasa za ujamaa zilikwishawekwa kapuni siku nyingi sasa mambo ni ku-mix tu na kuangalia mawazo mapya.

Suala la Zanzibar ni la kihistoria na siasa zote za sasa Tanzania zinataka mabadiliko.

Ni vijana wa kisasa ndio wanahitajika kubadilisha siasa za Tanzania.

Lets go to "basics".
 
Back
Top Bottom