Habari za Masiku wana-JamboForum, soma hii habari kuhusu Mkutano wa CCM na CUF!
MAKATIBU Wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi (CUF), leo wanakutana pamoja kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu muafaka katika Hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mara ya mwisho CUF ilipokutana na waandishi wa habari, ilisema imeridhishwa na hatua iliyofikiwa katika mazungumzo yanayoendelea baina yake na CCM yenye lengo la kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar.
CUF kilisema mazungumzo hayo yaliyoanza Januari 17, mwaka huu, yanaendelea vizuri na hadi sasa hakuna kiongozi yeyote aliyekwenda nje ya mstari katika mazungumzo hayo.
Kauli hiyo, ilitolewa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alipokuwa akisoma maazimio ya kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho, kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 27-28, mwaka huu.
Akisoma maazimio hayo, Profesa Lipumba alisema kutokana hali hiyo, Baraza Kuu limeiagiza timu ya CUF katika mazungumzo hayo, kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa yanafanikiwa.
Wakati CUF wakisema wamefurahishwa na mazungumzo hayo, kamati ya vyama vya CCM na CUF inayoshughulikia mazungumzo ya muafaka, mwezi uliopita, wajumbe wa vyama hivyo walijichimbia Bagamoyo, lakini habari za ajenda zilizojadiliwa ndani, ziligubikwa na usiri mkubwa.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Kingunge Ngomable-Mwiru, zilieleza kikao cha kamati hiyo kilifanyika katika Hoteli ya Oceanic kwa maelewano makubwa.
Wajumbe wa CCM katika mazungumzo ya Bagamoyo, waliongozwa na Kingunge ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia siasa na uhusiano wa jamii, na CUF waliongozwa na kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed.
Tokea Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani, amekuwa akirudia mara kwa mara kwamba mpasuko wa Zanzibar ni ajenda yake kuu. Hata hivyo, siku za hivi karibuni alisema kwamba mazungumzo baina ya vyama hivyo yako katika hali nzuri.
Hivi karibuni Kamati Kuu ya CCM iliyoketi jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine, ileleza kufurahishwa kwake na ripoti ya maendeleo ya mazungumzo hayo na ikaagiza kuwa kasi ya mazungumzo hayo iendelee.
Haijulikani ni mbinu zipi hasa zinazotumika kuondoa kutokuelewana kwa CCM na CUF visiwani Zanzibar, ingawa CUF wamekuwa wakipendekeza siku zote kuwa njia ya pekee ya kumaliza mpasuko uliopo ni kuunda serikali itakayoshirikisha watu kutoka vyama vyote viwili.
Hata hivyo, upande wa CCM visiwani wamekuwa wakipinga kwa nguvu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, siku zote wakisema ushindi wao katika uchaguzi unawapa mamlaka ya kisheria ya kuunda serikali
Makatibu wakuu CCM, CUF wakutana