Muafaka CCM na CUF, pande mbili za shilingi!

Mwafaka na CCM?

Hiyo ni ndoto .... CCM wataendelea ku-buy time mpaka 2010 ifike waingie tena kwenye uchaguzi wakati mpasuko uko pale pale. Maneno ya Makamba na Kingunge yalikuwa na msg nzito sana, na leo JK ameongezea kwamba hakuna haja ya kuweka deadline. So kinachofanywa na CCM ni kuendelea kuvuta muda maana nina uhakika CUF walitoa conditions ngumu ambazo CCM Zenji hawawezi kuzikubali na ndiyo maana mpaka leo hii hakuna kinachoendelea.
 
kwani cuf walipo mwandikia zile barua mbili mbona hakujibu,leo anatoa tamko ambalo alina kichwa wa miguu,mimi hii nchi sasa imenishinda hata dual citizenship sitaki tena
 
labda kwa ccm,lakini mwanchi wa kawaida kama mimi ni maumivu tu,umeona ile picha ya mtoto utumbo nje ?,
 
Juzi nimesoma kwa mara nyingine mazungumzo yamekwama kwa sababu Katibu Mkuu wa CCM yuko likizo!! Je tuamini kuwa hana kitabu cha matukio ya kila siku kama Katibu mkuu? Huu ni utani wanaofanyiwa CUF. Ndani ya CCM hakuna anayetaka suluhisho, kama lipo, kwa 'mgogoro' huu, nje ya kupiga kura. Bado naamini kuwa CUF wanapoteza muda kwani 2010 si mbali waje kwetu wapiga kura na kutuconvince umahiri wao. Piga ua CCM haitatoa suluhu mezani.
 
Posted Date::10/8/2007
Bazara Kuu CUF kujadili taarifa ya muafaka
Na Muhibu Said

BARAZA Kuu la Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, linatarajiwa kupokea taarifa ya mwelekeo wa mazungumzo ya kutafuta muafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar kati ya chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo hatima yake imeendelea kuwa kitendawili hadi sasa.


Mazungumzo hayo yaliyoanza Januari 17, mwaka huu, yaliendelea kwa siku tatu mfululizo, kuanzia Agosti 31 katika Hoteli ya Courtyard, jijini Dar es Salaam, baada ya kukwama kwa zaidi ya miezi miwili.


Habari kutoka Makao Makuu ya CUF jijini Dar es Salaam zilizothibitishwa na mmoja wa viongozi waandamizi wa chama hicho taifa, zinaeleza kuwa Baraza Kuu linatarajiwa kufanya kikao Oktoba 23, mwaka huu na moja ya agenda zinazotarajiwa kujadiliwa inahusu mazungumzo hayo ambayo usiri wake hivi sasa umeongezeka maradufu.


"Hakuna kiongozi wa chama aliyeelezwa lolote kuhusu maaendeleo wala mwelekeo wa mazungumzo hayo, imebaki kuwa ni siri ya wajumbe wa kamati ya mazungumzo. Tunatarajia watatueleza katika kikao cha Baraza Kuu tarehe 23," alisema kiongozi huyo mwandamizi wa CUF ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.


Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff, mwanzoni mwa mwezi uliopita, akiwa kisiwani Pemba, alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa Kamati ya mazungumzo ya CUF na ile ya CCM zimeshakubaliana tarehe ya kumaliza mazungumzo hayo.


Hata hivyo, mbali na Maalim Seif, hadi sasa hakuna kiongozi wala mjumbe yoyote wa kamati hizo aliyekuwa tayari kuelezea yaliyokwishajadiliwa katika vikao hivyo na tarehe ya mwisho ya kumalizika kwa mazungumzo hayo.


Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM, zinaeleza kuwa mazungumzo hayo takriban mwezi sasa, yamesimama.


Imeelezwa kuwa sababu za kusimama kwa mazungumzo hayo, inatokana na viongozi wa chama hicho kubanwa na heka heka za uchaguzi wa ngazi za wilaya, mikoa na taifa. Uchaguzi Mkuu wa chama hicho unatarajiwa kufanyika Novemba, mwaka huu.


Septemba 3, mwaka huu gazeti hili lilimkariri mmoja wa wajumbe wa kamati za mazungumzo hayo (jina linahifadhiwa) akisema kuwa, chini ya uongozi wa makatibu wakuu, Yusufu Makamba (CCM) na Maalim Seif (CUF), katika awamu yake ya pili, mazungumzo hayo yalifanyika kwa amani na kwamba taarifa ya maendeleo yake ingetolewa kwa pamoja na kamati hizo wakati wowote baada ya Ijumaa ya Septemba 7, mwaka huu.


Mbali na hilo, mjumbe huyo alisema mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru ambaye ni mjumbe wa kamati ya mazungumzo kutoka CCM na kwamba, pande zote zilikubaliana kuwa zingewasilisha ripoti siku hiyo.


Mazungumzo hayo yaliendelea baada ya CUF kutoa tamko la kuitikia wito wa Rais Jakaya Kikwete aliyekiomba chama hicho kukubali kuendelea na mazungumzo na CCM na kuachana na msimamo wake wa awali wa kuiomba Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati kuyanusuru mazungumzo hayo.


Mmoja wa wajumbe wa kamati ya CUF, Hamad Rashid Mohamed, alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa katika vikao na wenzao wa CCM, walitarajia kupanga programu ya kumaliza mazungumzo hayo.


Hata hivyo, Hamad alisema katika vikao vya ngazi za juu vya chama chake vilivyofanyika kwa nyakati tofauti Agosti, mwaka huu, walikubaliana kuwa mazungumzo hayo yawe ya wazi badala ya kuendelea kuwa ya siri kama ilivyokuwa awali na kuahidi kuwa msimamo wao huo, wangeufikisha katika vikao na wenzao wa CCM ili waujadili kabla ya kutekelezwa.


Mazungumzo hayo yalikwama kwa zaidi ya miezi miwili baada ya makatibu wakuu wa vyama hivyo kukubaliana kwa maandishi kwamba, Agosti 15, mwaka huu, yawe yamekwisha.


Kabla ya kukwama, makatibu wakuu wa vyama hivyo walikutana na mchakato wa mazungumzo ulianza kwa kuzingatia ajenda tano, ikiwamo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 30, 2005 na taathira zake.


Ajenda nyingine, zilikuwa ni usawa na haki katika kuendesha siasa, masuala ya utawala ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), njia za kuimarisha mazingira ya maelewano ya kisiasa na uendeshaji wa uchaguzi huru na wa haki Zanzibar, na utaratibu wa kutekeleza Programu ya Utekelezaji wa Makubaliano yatakayofikiwa katika mazungumzo hayo.


Kwa mujibu wa makubaliano ya vyama hivyo, mazungumzo ya msingi yangefanywa na Kamati ya Mazungumzo, lakini pale ambapo kamati ingekwama, makatibu wakuu wangeingilia kati kutoa mwongozo.


Rais Jakaya Kikwete katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Agosti 14, mwaka huu, alisema mambo yote yameshajadiliwa katika mazungumzo hayo na kufikiwa hatua nzuri, ambayo ni pamoja na usawa na haki katika kuendesha siasa, masuala ya utawala ya SMZ, njia za kuimarisha mazingira ya maelewano ya kisiasa na uendeshaji wa uchaguzi huru na wa haki Zanzibar.

source: mwananchi
 
Wachunguzi wa JF napatwa na mshangao sana kuona mazungumzo haya yanendelea kwa mida mmwingi na hapa JF nimeweka manyanga kwa namna dondoo zinavyopachikwa wanasema copy to write au kama ilivyo ndivyo iwekwavyo.
Sasa mashushu wa JF nawapa changamoto hiyo kuweza kupenya security ya Makatibu Makamba na Seifu ambao wamebana mdomo na hakuna kinachojulikana katika mazungumzo yao ni punde tu wamemaliza mkutano na waandishi wote walitimuliwa na Makamba ili ibaki kuwa ni siri.
Baadae wamesema wananchi wakae mkao wa kula yaani sina la kusema kuhusu usiri yaani JF imegonga ukuta kupata ronyo.:confused:
 
mimi wameshanichoshwa na hizi bla bla za muafaka?
Ni nini hicho wanachokiongelea kischoisha au wasichoafikiana?
2010 inakaribia, na asilimia kubwa the same story zitajirudia, then CUF wataandamana na kutaitishwa muafaka.Then circle itaanza upya!
Hizo pesa wanazotumia kwenye kuafikiana ni bora waziinvest kwenye maendeleo ya nchi au vyama vyao!
 
TAMKO la Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), kuhusu hatima ya Mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar, limezua mapya, baada ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chama cha Wananchi (CUF), kuliita kuwa ni ufisadi na usanii wa kisiasa.


Kauli hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wahadhiri wa UDSM waliozungumza na Mwananchi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alipozungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu chama hicho, jijini Dar es Salaam jana.


Wakati wasomi na CUF wakitoa maoni yao, Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba aliiambia Mwananchi jana kuwa uamuzi wa CCM kuamua kuendesha kura za maoni utazidi kuwagawa Wazanzibari badala ya kuwaunganisha.


Wahadhiri hao, Maalim Seif na Jaji Warioba walitoa kauli hiyo kufuatia tamko la NEC juu ya suala la Mwafaka lililotolewa juzi baada ya kuhitimisha kikao chake katika Kijiji cha Butiama, mkoani Mara, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ilitaka ifanyike kura ya maoni visiwani Zanzibar ili kupata ridhaa ya wananchi kuhusu kuundwa kwa serikali ya mseto visiwani humo.


Warioba alisema kwamba suala la maamuzi wa serikali ya mseto liko ndani ya viongozi na kwamba wasikwepe majukumu yao." Suala la kutekeleza Mwafaka liko ndani ya uongozi, hivyo wasikwepe wajibu wao," alisema.


Alisema kimsingi hana matatizo kama viongozi wana nia ya kuboresha mchakato wa Mwafaka, lakini ana wasiwasi kwamba mchakato huo ukifika hadi wakati wa uchaguzi unaweza usiwe na maana inayokusudiwa.


"Matatizo ya Zanzibar yanatokana na uchaguzi, hivyo hayawezi kutatuliwa kwa uchaguzi," alisisitiza Jaji Warioba.


Warioba alitoa mfano wa Chama cha ANC cha Afrika Kusini ambacho kilishinda kwa wingi wa kura, lakini kikashirikisha vyama vingine kwa lengo la kuunganisha wananchi. "Vyama vikiungana kwa mtindo wa serikali ya mseto, hata wananchi pia wataungana," alisema.


Alisema mfano mzuri ni visiwani Zanzibar ambapo kabla ya viongozi wa CUF na CCM kuanza mazungumzo ya kuleta Mwafaka visiwani humo, wananchi walikuwa hawazikani kwa sababu za kiitikadi, lakini viongozi wao walipoanza kuzungumza na wananchi nao walipunguza chuki baina yao.


Profesa Mwesiga Baregu wa Sayansi ya Jamii, Idara ya Siasa ya UDSM, alisema kitendo cha CCM kutaka suala la Mwafaka kupigiwa kura ya maoni na wananchi baada ya kukaa nalo kwa miaka miwili sasa, ni uhuni unaoweza kulipeleka taifa katika migogoro.


�CCM wanafanya uhuni na huu ni mchezo mbaya sana kwa sababu yaliyoharibika Kenya yalitokana na wananchi kukosa imani na serikali kutokana na uhuni wa aina hiyo,� alisema Profesa Baregu.


Alisema tabia ya Serikali ya CCM kuanzisha michakato mizito ya kitaifa na kufanya ghiliba za makusudi kisha kuiacha kwenye utata, ni ufisadi wa kisiasa na hatari kwa uhai wake na maendeleo ya taifa.


�Tofauti na ufisadi wa uchumi ambao bado unazungumzwa, kitendo hicho ni ufisadi wa kisiasa na kama serikali haisimamii haki, haistahili kuaminiwa wala kuheshimika na matokeo hayo yote ni watu kuchukua sheria mkononi,� alisema.


Alisema uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM kurudisha mjadala wa mwafaka kwa Wananchi wa Zanzibar wakati wajumbe wake ni viongozi wa CUF na CCM Taifa ni ujanja wa kuukataa mwafaka.


�Uamuzi huo unaondoa imani na dhamira njema ya CCM kuhusu mwafaka. Kwa nini hatima ya mazungumzo hayo yakafanywe na Wazanzibari tu wakati walioshiriki ni makatibu Wakuu wa vyama vyenye wanachama Bara na Zanzibar?� alihoji Baregu.


Profesa Baregu alisema kama kuna umuhimu kura za maoni ziendeshwe kuhusiana na kutungwa kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar badala ya kupoteza fedha nyingi kuendesha kura za maoni kuhusu mwafaka tena katika mazingira ambayo jamii inafahamu kuwa CCM inaukataa.


Profesa mwingine wa kitivo hicho, Ernest Mallya alisema uamuzi wa CCM kutaka hatma ya mwafaka kuamriwa na wananchi wa Zanzibar kwa kura za maoni, ni ishara kuwa hawakuwa na nia thabiti kuutafuta.


Alisema kura za maoni haziwezi kutoa mwelekeo unaotarajiwa kuhusu mwafaka badala yake zitaongeza uhasama baina ya pande mbili zinazovutana kuhusu suala hilo.


�Kura ya maoni ni uchaguzi ambao ni wazi CCM itashinda kwa mbinu zilezile wanazotumia kushinda chaguzi zingine. Hiki ni kigezo ambacho chama hicho kinataka kukitumia kuukataa na CUF wasikubali, wakatae,� alisema Profesa Mallya.


Profesa Mallya alitaka CCM kuanzisha mchakato wa kura za maoni katika kero zote za muungano kama ina nia njema na taifa badala ya kukazania kura za maoni kuhusu mwafaka ambazo tayari imejiandalia ushindi wa kuukataa.


Kauli ya Profesa Mallya iliungwa mkono na Mhadhiri Msaidizi wa idara hiyo Bashiru Ally aliyesema kuwa kura za maoni haziwezi kuleta mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar.


Alisema kama suala hilo limeshindwa kufikia tamati katika mikutano ya viongozi wa vyama viwili vinavyopingana, halitaweza pia kukamilika kwa kura za maoni kwani kura ndizo zilizokuwa chanzo cha mgogoro huo.


Alieleza kuwa utaratibu wa kura za maoni hauna tofauti na kampeni za Uchaguzi Mkuu unaowagawa watu katika makundi mawili yanavutana na kuongeza mgogoro badala ya suhulisho.


Ally alisema hakuna maana nyingine zaidi ya �danganya toto� kuanzisha mchakato wa kura za maoni kuhusu mwafaka wakati kuna matatizo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.


�Kwa nini tutumie fedha kuwauliza wananchi kuhusu mwafaka na kuacha mambo ya msingi kama matatizo ya ardhi, madini, uraia na maeneo mengine yenye utata kama siyo kuvuta subiri na kuwadanganya wenzao wa CUF?� alihoji.


�Kuwauliza wananchi kuhusu mwafaka ni kuongeza chumvi kwenye kidonda, kwani hadi sasa Watanzania bado hawajajua hatima ya wizi wa EPA na kamati za madini,� alisema.


Mhadhiri wa sheria chuoni hapo, Dk Sengondo Mvungi alisema matumizi ya rasilimali za umma katika mpango wa kupata kura za maoni ni aina nyingine ya ufisadi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete.


Alisema hakuna sababu za msingi kuitisha kura za maoni kuhusu serikali ya mseto visiwani Zanzibar wakati Katiba haikatazi.


�Tunawauliza wananchi ili watupe majibu gani kuhusu serikali ya mseto wakati tayari Katiba haipingani nayo?� Kama watafanya na wakatumia fedha za umma tutawapigie kelele kwani huo ni ufisadi,� alisema


Dk Mvungi alisema kuitisha kura za maoni sio kosa na inaruhusiwa kikatiba, alibainisha kuwa matumizi ya rasilimali za umma katika mambo binafsi ya wanasiasa ni kosa kisheria.


Mhadhiri Msaidizi wa kitivo hicho cha sheria, Makarios Tairo alisema kura za maoni VIsiwani Zanzibar zisiendeshwe kwa ajili ya mwafaka bali ziendeshwe kwa upana zaidi kulinda maslahi ya Wazanzibari na Watanzania wote.


Alisema historia inaonyesha kuwa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi visiwani Zanzibar vyama vya CUF na CCM vimekuwa vikishindana kwa tofauti ndogo ya kura jambo ambalo linaleta umuhimu wa kuwa na serikali ya mseto baina ya vyama hivyo viwili.


Wakati wahadhiri hao wakisema hayo, CUF, imepinga hoja ya CCM ya kutaka ifanyike kura ya maoni Zanzibar ili kupata ridhaa ya wananchi ya ama iundwe au isiundwe serikali ya mseto visiwani humo.


Badala yake, CUF imeitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo, ikiwa ni pamoja na kutia saini makubaliano hayo na kuyatekeleza mara moja.


Katika mazungumzo yao yaliyochukua takriban miezi 14 na vikao 21, pamoja na mambo mengine, CUF ilidai kuwa walikubaliana na CCM kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, maarufu kama "serikali ya mseto" itakayoshirikisha pande mbili za vyama hivyo.


Mbali na hilo, CUF pia imepinga hoja ya kufanywa kwa marekebisho katika baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo, ambayo CCM imeiagiza kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF ili kujadili mapendekezo hayo.


Katika tamko lake lilisomwa na Maalim Seif jana, CUF imesema hoja hizo ni usanii wa kisiasa, ubabaishaji na upotoshaji uliofanywa na CCM kwa lengo la ama kuendelea kurefusha muda hadi mwaka 2010 au kuyakataa makubaliano ambayo wajumbe wake wameshiriki kuyaandaa katika miezi 14 ya mazungumzo kati ya vyama hivyo.


"Kwa msingi huo CUF haikubaliani na hoja hizo zote mbili," alisema Maalim Seif.


Maalim Seif alisema kinachosikitisha zaidi ni kuwa tofauti na ilivyoelekezwa, pendekezo la kutaka kura ya maoni, halikuwa limeibuliwa na wajumbe wa NEC, bali lilikuwamo katika taarifa ya Kamati ya CCM inayoshiriki mazungumzo, likiwa ni pendekezo walilotaka liridhiwe na Kamati Kuu (CC) ya NEC.


"Hivyo, ni wazi liliandaliwa mapema kutokana na kile kamati hiyo ya CCM ilichokiita 'kuipiku CUF katika ubunifu wa kujenga'," alisema Maalim Seif.


Alisema kitendo cha Kamati ya CCM kuwasilisha kitu kipya nje ya makubaliano yaliyofikiwa, ni upotoshaji mkubwa wenye lengo la kulifanyia usanii wa kisiasa suala kubwa linalogusa maslahi ya taifa na watu wake moja kwa moja.


Alihoji kama pendekezo la kura ya maoni lina nia njema ya kuwashirikisha wananchi, kwa nini wajumbe wa Kamati ya CCM wasiliwasilishe katika vikao vya mazungumzo na badala yake wakaamua kuliingiza kama mtego wa kisiasa wenye lengo la kuipiku CUF?


Maalim Seif pia alihoji iwapo kura ya maoni itaendeshwa na chombo kipi na kwa utaratibu upi, hasa ikitiliwa maanani tayari CCM na CUF wamekubaliana kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Daftari la Kudumu la Wapigakura, vina matatizo ya msingi ambayo yanahitaji kurekebishwa?


"Ni vipi basi tume hiyo chini ya daftari bovu lililopo itaweza kuendesha kura ya maoni ambayo itakuwa huru na ya haki?," alisema Maalim Seif na kuongeza:


"Sisi tunaona suala hilo ni mbinu chafu yenye lengo la kuendelea kupoteza muda ili makubaliano yaliyofikiwa yasiweze kutiwa saini na utekelezaji kuanza. Kwa lugha yao CCM waliyoandika katika waraka wao ni njia ya kuipiku CUF na kamwe haikusudiwi kupata maoni ya wananchi".


Kuhusu marekebisho katika baadhi ya mapendekezo ya Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo ambayo CCM imeiagiza kamati yake kukutana na wajumbe wa CUF kujadili mapendekezo hayo, Maalim Seif alisema hawaungi mkono suala hilo kwa kuwa CCM haijataja ni maeneo gani inataka yafanyiwe marekebisho.


Alisema hoja hiyo inashangaza kwa sababu wajumbe wa Kamati ya Mazungumzo kutoka CCM, walikuwa wakiwaarifu wajumbe kutoka CUF kwamba, walikuwa wakiwasilisha taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vikao vya CC na NEC na kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na kupata maelekezo na miongozo inayohitajika.


"Hata taarifa ya karibuni kabisa ya CCM iliyokuwa ikikanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba mheshimiwa Amani Karume si kikwazo cha kufikiwa makubaliano ya mwafaka iliweka mkazo na msisitizo kwamba katika kila hatua viongozi hao wameshauriwa ipasavyo. Hatua hii ya mwisho ilikusudia kubariki makubaliano hayo yaliyokuwa yakifikiwa hatua kwa hatua na siyo kufungua mjadala mpya kupitia mpya ya mazungumzo," alisema Maalim.


Hata hivyo, alisema pamoja na kushtushwa na usanii wa kisiasa katika suala hilo, wamepata faraja kwa kuwa suala hilo limewawezesha Watanzania kujua ni nani kati ya CCM na CUF asiyeitakia nchi mema, amani, utulivu na siasa za maelewano na mashirikiano.


Alisema jambo hilo limeonyesha kuwa CCM iliingia katika mazungumzo hayo ikiwa haina dhamira ya kweli na ya dhati ya kuupatia ufumbuzi wa kweli mpasuko wa kisiasa Zanzibar.


Badala yake, alisema imeonekana kuwa lengo pekee la CCM katika mazungumzo hayo, lilikuwa ni kuwahadaa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kwa kujidanganya kwamba wangeweza kuidhibiti kisiasa CUF kupitia utaratibu wa kuwapa matumaini ya uongo na kurefusha mazungumzo kadri inavyowezekana hadi kipindi kinachokaribia Uchaguzi Mkuu ujao pasi na kuchukua hatua zozote za maana kwa lengo la kutoa ufumbuzi wa kweli wa mpasuko huo.


Kutokana na hali hiyo, alisema CUF ambayo imefanya kila lililomo katika uwezo wake kuinusuru hali tete ya kisiasa Zanzibar isichafuke, imevunjwa moyo na Rais Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM.


"Imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa nchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa imetetereka sana," alisema Maalim Seif na kuongeza:


Kutokana na hali hiyo, alisema CUF haiko tayari kushirikiana na CCM kuwafanyia Watanzania usanii wa kisiasa akisema kwamba huo sio utaratibu wa CUF katika uendeshaji wa siasa na akaitaka CCM kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya vyama.


Alisema kinyume na hayo, CUF inatoa wito kwa marafiki wa Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua madhubuti za uhakika na za haraka kuingilia kati suala hilo ili kuhakikisa makubaliano yaliyofikiwa yanatiwa saini.


Aliwashukuru viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, taasisi na jumuiya za kijamii, mabalozi na vyombo vya habari, hususan magazeti huru kwa mchango wao mkubwa walioutoa na ambao ulisaidia kufanikisha mazungumzo hadi hatua za kukamilishwa na kuwataka wanachama na wapenzi wa CUF kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki wakijua chama hicho kiko upande wa amani, ukweli na haki.


Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe alisema kwamba uamuzi wa CCM kuhusu mwafaka ni hatari kwa taifa na kuishiwa kisiasa. " Maamuzi ya CCM yanaonyesha kwamba viongozi wengi wa chama hicho wamefilisika kisiasa na uwezo wao una mashaka makubwa," alisema Zitto

Suala la mwafaka lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kuamuliwa na NEC baada ya kudumu kwa takribani miaka miwili chini ya makatibu wakuu wa vyama hivyo, Yusuf Makamba na Maalim Seif Sharrif Hamad.


Imeandaliwa na Muhibu Said, Kizito Noya na Rehema Rajabu
 
CUF na wao wapige kura ya maoni kama wanataka Mseto au mchele tu (kipande chao cha ardhi)
 
Naomba kunukuu baadhi ya maneno ya Maalim Seif:

“CUF imevunjwa moyo sana na Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa wananchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, imetetereka sana.

“Kitendo cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya uenyekiti wake kukataa kupitisha makubaliano yaliyofikiwa na kamati ya mazungumzo ya CCM na CUF na badala yake kuja na hoja mpya za ajabu ajabu zenye lengo la “kuipiku CUF”, kisiasa kinamwonyesha Rais kikwete ama hakuwa mkweli na mwaminifu tokea mwanzo na kwamba alikuwa akifanya usanii wa kisiasa wakati alipotangaza kuwa anasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar au ni kiongozi dhaifu asiye na udhibiti wa chama anachokiongoza. Yote mawili hayampi sifa ya kiongozi ambaye nchi inamhitaji inapopita katika vipindi vigumu,” alisema Maalim Seif.


---mwisho wa kunukuu ----

Kadri siku zinavyokwenda watu wengi zaidi wanazidi kumjua JK ni mtu gani, Je yuko makini na anachozungumza? Huwa anamaanisha hicho?
 
Naomba kunukuu baadhi ya maneno ya Maalim Seif:

“CUF imevunjwa moyo sana na Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa wananchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, imetetereka sana.

“Kitendo cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya uenyekiti wake kukataa kupitisha makubaliano yaliyofikiwa na kamati ya mazungumzo ya CCM na CUF na badala yake kuja na hoja mpya za ajabu ajabu zenye lengo la “kuipiku CUF”, kisiasa kinamwonyesha Rais kikwete ama hakuwa mkweli na mwaminifu tokea mwanzo na kwamba alikuwa akifanya usanii wa kisiasa wakati alipotangaza kuwa anasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar au ni kiongozi dhaifu asiye na udhibiti wa chama anachokiongoza. Yote mawili hayampi sifa ya kiongozi ambaye nchi inamhitaji inapopita katika vipindi vigumu,” alisema Maalim Seif.


---mwisho wa kunukuu ----

Kadri siku zinavyokwenda watu wengi zaidi wanazidi kumjua JK ni mtu gani, Je yuko makini na anachozungumza? Huwa anamaanisha hicho?

Maalim Seif,

hamkuwa mkimfahamu Kikwete tangu mwanzo au mliamua tu kutomfahamu makusudi mkitegemea angekiuka katiba ya sisiem?Kama kuna mwana-CUF yeyote humu arejee kusoma ile thread ya Mwanakijiji inayoongelea Ibara 15.something...

after all who's Kikwete anyway?
 
Naomba kunukuu baadhi ya maneno ya Maalim Seif:

“CUF imevunjwa moyo sana na Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa wananchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, imetetereka sana.

“Kitendo cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya uenyekiti wake kukataa kupitisha makubaliano yaliyofikiwa na kamati ya mazungumzo ya CCM na CUF na badala yake kuja na hoja mpya za ajabu ajabu zenye lengo la “kuipiku CUF”, kisiasa kinamwonyesha Rais kikwete ama hakuwa mkweli na mwaminifu tokea mwanzo na kwamba alikuwa akifanya usanii wa kisiasa wakati alipotangaza kuwa anasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar au ni kiongozi dhaifu asiye na udhibiti wa chama anachokiongoza. Yote mawili hayampi sifa ya kiongozi ambaye nchi inamhitaji inapopita katika vipindi vigumu,” alisema Maalim Seif.


---mwisho wa kunukuu ----

Kadri siku zinavyokwenda watu wengi zaidi wanazidi kumjua JK ni mtu gani, Je yuko makini na anachozungumza? Huwa anamaanisha hicho?

Maalim Seif,

hamkuwa mkimfahamu Kikwete tangu mwanzo au mliamua tu kutomfahamu makusudi mkitegemea angekiuka katiba ya sisiem?Kama kuna mwana-CUF yeyote humu arejee kusoma ile thread ya Mwanakijiji inayoongelea Ibara 15.something...

after all who's Kikwete anyway?
 
Naomba kunukuu baadhi ya maneno ya Maalim Seif:

“CUF imevunjwa moyo sana na Mheshimiwa Jakaya Kikwete akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, imani tuliyokuwa nayo kwake kama kiongozi wa wananchi na ambayo tulibaki nayo hadi CCM inaelekea katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, imetetereka sana.

“Kitendo cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM chini ya uenyekiti wake kukataa kupitisha makubaliano yaliyofikiwa na kamati ya mazungumzo ya CCM na CUF na badala yake kuja na hoja mpya za ajabu ajabu zenye lengo la “kuipiku CUF”, kisiasa kinamwonyesha Rais kikwete ama hakuwa mkweli na mwaminifu tokea mwanzo na kwamba alikuwa akifanya usanii wa kisiasa wakati alipotangaza kuwa anasononeshwa sana na mpasuko wa kisiasa Zanzibar au ni kiongozi dhaifu asiye na udhibiti wa chama anachokiongoza. Yote mawili hayampi sifa ya kiongozi ambaye nchi inamhitaji inapopita katika vipindi vigumu,” alisema Maalim Seif.


---mwisho wa kunukuu ----

Kadri siku zinavyokwenda watu wengi zaidi wanazidi kumjua JK ni mtu gani, Je yuko makini na anachozungumza? Huwa anamaanisha hicho?


Kwan nyie hamkujua kwamba JK ni bonge la Kanjanja?Yaani mlimtumainia kwa mambo mema?
 
Wapendwa ndugu zangu waTZ

Sote tukiwa kama wapenda amani na tunaitakia mema nchi yetu tumesikitishwa sana na maamuzi ya CCM juu ya muafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar. Binafsi nimesikitishwa zaidi kwa kujua kwamba hali ya amani huko visiwani hivi sasa iko mashakani.

Mimi ni mmoja kati ya wanaopendelea Zanzibar kuwe na Serekali ya mseto kwa kuwa naamini hatua hiyo itasaidi sana kupunguza mgawangiko uliopo kati ya sisi waunguja na ndugu zetu wapenzi kutoka Pemba. Vilevile hatua hiyo itapunguza jazba za kisiasa na uhasama usiokuwa na maana. Ni kweli kwamba CCM hawakufanya maamuzi ya busara juu ya suala la muafaka lakini kabla ya kuihukumu CCM katika hili naomba tuelewe kwamba matatizo ya kisiasa ya Zanziabar hajachangiwa na CCM tu bali hata hiyo CUF ambayo wengi humu JF wanaona ndio chama chenye SERA bora zilizolenga kuleta maendeleo ya Zanzibar na watu wake. Ili muafaka uwezekane CUF nayo pia nahitaji kuwajibika na kubadili mfumo wake wa kiitikadi ambao kwa kiasi fulani unatupa mashaka sisi watu wa Unguja.

Tatizo kubwa ambalo lipo Zanziabr hivi sasa ni mgawanyiko wa jamii ya kizanzibari. CCM wanachofanya sasa ni kuongeza gap liliopo lakini linapokuja sula la nani ahukumiwe katika kuleta ubaguzi huko Zanzibar lawama pia wanazibeba CUF/Maalim na sio CCM peke yao. Maalim kwa kutaka kwake kukubalika kisiasa aliibuka na slogan ya Upemba, na kwa kweli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kubrainwash ndugu zetu, akawajaza chuki, uhasama na kuwabadilisha kabisa roho zao. Kisiasa Maalimu hawaakilishi watu wa Unguja na mara zote akisimama kwenye majukwaa anaanza na statement ya ndugu zangu WAPEMBA……. Maalim anahitaji kubadili msimamo wake hapo ikiwa kweli anataka sisi watu wa Unguja tuamini kwamba yeye ni kwa Wazanzibar na si wapemba

Tuje kwenye suala la Mapinduzi ya mwaka 1964. Sisi watu wa Unguja tunaamini kwamba Mapindizi ya mwaka 1964 ndiyo yaliyomkomboa muafrika au "MAGOZI" kutokana na madhila ya ukoloni (Magozi ni very irritating terminology iliyokuwa ikitumiwa enzi hizo kabla ya mapinguzi kurefer watu weusi wa ASP, is very interesting to note same terminology inatumika na wana CUF). Kwetu sisi watu wa Unguja muarabu alikuwa ni mkoloni lakini kwa wezentu wa kisiwa cha pili under influence ya Maalim mapinduzi ni haramu na muarabu hakuwa mkoloni bali alikuja kuleta ustaarabu na maendeleo kwa so called "MAGOZI" ambao kwa wakati huo walikuwa wakiishi maisha ya kishenzi na kitwana. Maalim mara nyingi amekuwa akitamka bayana dhahir shahir kwamba mapinduzi wa mwaka 1964 ni haramu na mwaka 1999 yeye na Juma Duni walinukuliwa wakisema kwamba serikali ya mtu mweusi Zanzibar mwisho wake mwaka 2000. Sasa hebu tujiulize mseto utapikikaje ikiwe upande moja unaamini wao ni waafika na mapinduzi ndiyo yaliyowakomboa na upande wapili wanalaani mapinduzi???. Ni uzuri Maalim akatueleza msimamo wake wa sasa juu ya mapinduzi ya mwaka 1964

Mara nyingi kuwekuwa na malalamiko kwamba Pemba imekuwa nyuma kimaendeleo kitu ambacho ukweli wake uko mashakani. Zanzibar kama zilivyo nchi nyingi za Afrika, infrastructures zote ni zilezile walizoziacha wakoloni kwa ufupi Zanzibar yote haina maendeleo. Lakini naomba tunote kwamba walioanza kuwapuuza katika kuwaletea maendeleo ni hawo ambao wao wanasema walikuja kuleta maendeleo na ustaarabu. "Waleta maendeleo na ustaarabu" walibase makazi yao Unguja na ndo mana kuna tafauti kubwa ya Unguja na Pemba na kutokana na Sera za CCM na wao wakashindwa kuleta mabadiliko yoyote si kwa pemba tu bali kwa Zanzibar yote.

Tukija kwenye maendeleo mengine wenzetu hawa wamesoma zaidi kuliko sisi watu wa Unguja. Wamefanya mambo mengi sana pale elimu ya juu Zanzibar wenyewe wanayajua lakini kutokana na tabia yao ya kupinga najua na hili watalipinga, lakini ukweli unajulikana. Pamoja na yote hayo sisi watu wa Unguja hatuna chuki nao sababu ni ndugu zetu lakini wao kutokana na kasumba za Maalim wanatuona sisi maadui. Kwenye biashara wao ndo hao, wao wemechangia pia katika kuifilisi BPZ (bank) kwa kupeana mikopo ya mamilioni kwa collateral za vibanda vya mbavu za mbwa, hawayasemi hayo na bado wanaona wanayanyaswa. Unguja wapo na wanaishi kwa amani na hatuwabagui lakini waunguja walioko Pemba wana maisha ya taabu sana. So kabla hatujazungumza mseto, Maalim ana jukumu kubwa sana la kuwabadili ndugu zetu, naamini kwa influence yake kama alivyoweza kuwatia sumu ya ubaguzi anaweza pia kuwafanya wawe na ile imani yaliyokuwa nayo hapo kabla.

Ndugu zetu hawa kuna kipindi walisusia kabisa shuguli zote za kimaendeleo kwa mfano wakipelekewa huduma za uzazi salama argument inakuja…..CCM inataka wasizae ili wasiwe wengi kwenye kupiga kura,....wakipelekewa dawa wa mtende na mabusha (kunradhi hakuna neno mbadala) wanasema uzazi utatoka watakuwa hawawezi kuzaa and so on. Maalim alikuwa mstari wa mbele katika kuwashawishi wagomee shughuli zinazoletwa na CCM. Hebu tujiulize kiongozi gani huyo??? Kweli anawatakiwa wananchi wake mema. Mimi sijawahi kusikia Zitto akiwaambia watu kule Kigoma wasishiriki maendeleo na badala yake amekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wananchi wake. Sote tumeona alivyolisimamia kidete suala la buzwagi. Hao ndo mfano wa viongozo tunao wataka na sio wale ambao wasimama kwenye majukwaa kuwagawa ndugu ambao hapo kabla tulikuwa tunaishi kwa upendo na ummoja, vilevile hatutaki viongozi wenye kusimama kwenye majukwaa na kupotosha historia eti mapinduzi ya mwaka 1964 yalikua ni haramu??. Nani anataka kusikia hayo katika karne hii ya 20, ambapo nchi zote za afrika zimeacha historia kama iliyo na zinangalia mbele. Inawezekana kweli CCM imewabagua wapemba lakini wakubali kuwa na Maalim pia amechagia katika kuzorotesha maendeleo yao.

Maalim amechangia sana kuwafanya ndugu zetu hawa wajione wao ni waarabu na si waafrika. Ndugu zetu hawa hivi sasa wao ni "coconuts" they are dark outside white inside. Kwao wao muafrika ni gozi, "the more dark your are the less human you are". Kwao wao msaudia, muomani, sharjah nk ni binaadamu waliokamilika na wana haki ya kuishi Zanzibar na wanakaribishwa kwa mikono miwili lakini neighbours next door….mmaafia, mbagamoyo, mrufiji, mnyamwezi, msukuma nk hao ni kero katika jamii.thamani yao ni ya nusu mtu...wao ni washenzi, machogo na ni bughudha katika jamii, si kwa lolote lile bali kwa rangi ya ngozi yao. Lakini kwetu sisi watu wa Unguja hao ni sehemu ya watanzania na ni waafrika wenzetu

Tunapojadili suala la muafaka ndugu zangu wapendwa naomba muelewe kwamba siasa za Zanzibar si sawa na za bara, bara wapinzani wanazungumzia sera mbovu za CCM na pace ndogo ya maendeleo lakini kwa kwetu CUF inazungumzia hitoria iliyopita miaka 40. Ni ukweli uliodhahiri kwamba CCM imeshindwa kuleta maendeleo Zanzibar lakini CUF chini ya Maalim Seif nayo pia haiwezi kuleta maendeleo bali inataka kuturejesha nyuma tulikotoka. Viongozi wa CCM hawatutendei haki sisi wazanzibari kwa kushindwa kutuletea maendeleo na tutawahukumu kwa hilo. Lakini Maalim ametuumiza sana sisi wazanzibar kwa kutugawa na kutubagua, kwa kupotosha historia ya nchi yetu na kutuacha tunaishi katika chuki watu ambo hapo nyuma tulikuwa ni wa moja.

Yanayotokea sasa kwa Maalim ni kile alichokisema Mwalimu JK Nyerere (mungu ampunzishe kwa amani) naomba kunukuu "dhambi ya ubaguzi ukiitenda haitakuwachia itakuandama tu" na yeye dhambi ya kutubagua sisi Wazanzibar inamuandama na haitamuachia.....
 
Ni kweli kwamba CCM hawakufanya maamuzi ya busara juu ya suala la muafaka lakini kabla ya kuihukumu CCM katika hili naomba tuelewe kwamba matatizo ya kisiasa ya Zanziabar hajachangiwa na CCM tu bali hata hiyo CUF ambayo wengi humu JF wanaona ndio chama chenye SERA bora zilizolenga kuleta maendeleo ya Zanzibar na watu wake

CCM imekosea wapi? Maana CCM haijapinga Serikali ya Mseto; Infact imepitisha ilichofanya cha zaidi ni kutoa pendekezo kwa wenzao namna ya utekelezaji? Ndio suala la kura ya Maoni.

Na CCM wako sawa kwa maana wewe muunguja na huenda mwanaCCM utapiga kura ya ndio kwa serikali ya Mseto... hivyo CCM are on track!!!
 
CCM imekosea wapi? Maana CCM haijapinga Serikali ya Mseto; Infact imepitisha ilichofanya cha zaidi ni kutoa pendekezo kwa wenzao namna ya utekelezaji? Ndio suala la kura ya Maoni.

Na CCM wako sawa kwa maana wewe muunguja na huenda mwanaCCM utapiga kura ya ndio kwa serikali ya Mseto... hivyo CCM are on track!!!

Wait and see. Chama cha mapinduzi kwa sasa kina udhaifu mkubwa, kwenye suala la muafaka kurudisha kwa wananchi ni kuchemsha, kwa mtu yeyote anayependa madaraka huwa hakubali ku-share madaraka, lakini kama ku-share madaraka kuna manufaa ya taifa kunatakiwa kufanyike bila mtu au kundi fulani kupenda!

Muafaka Zanzibar ni must, delay tactics zinaiumiza Zanzibar kwa ujumla.
 
Wewe wacha kukurupuka ,hizo ni siasa za CCM ,labda nikukumbushe tu hapa watu wanakwenda na rejea .hizo maneno iko kumpachika kiongozi wa juu ambae alikuwa gogo la CCM ni za uwongo,karibu mikutano yote naisikiliza tokea ya bara mpaka huko Zanzibar na ya London ndio usiseme na si CUF hata ya CCM.
Slogan ya Upemba katika uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi Zanzibar wapemba walitimuliwa na Mapuri ndie mhusika mkuu na alifika kutunga kitabu ambacho kilichomwa moto uwanjanikwa uwongo kama ulioandika hapo.Na si kweli kuwa Maalim akianza huanza na ndugu zangu wa Pemba huo ni uwongo.
Kusema Mapinduzi haramu sio kosa maana hadi hii leo faida ya mapinduzi haijaonekana kwa mwananchi wa kawaida na uharamu ulitokana na kuwaua baadhi ya wasomi waliokuwemo ndani ya baraza la mapinduzi na walikuwa mstari wa mbele.Majina siwajui lakini nasikia kuna anaitwa Othman Sharif,Hanga na wengineo hao labda uwaeleze watu wa JF ,watu hao wako wapi na nini kiliwasibu.Ndipo tunaweza kusema kama yalikuwa halali.
Kusema serikali ya mtu mweusi sijawahi kusikia na hilo linawezekana kusemwa ikiwa kipimo kitakuwa bora kuliko utawala tulio nao,sasa unataka kutwambia Juma Duni ni mwarabu ,Machano ni Mwarabu,Mloo umaarufu wanamwita kuchi ni Mwarabu ,yuko yule aliekuwa jaji mkuu nae ni mwarabu ,kama huwajui magogo wa Afro Shiraz basi itazame na ichambue CUF kwa kina utaona CCM kuna wapiga debe tu lakini hakuna Afroshirazi,Juma Duni mikono yake imejaa damu kwa kuilinda ASP ,ila watu hayo ndio wanayotaka kuyaweka kando na kuiweka Zanzibar mpya kila mmoja atabeba mzigo wake mwenyewe.
Unajua naona hoja hizi zako kuzijadili ni kurudisha nyuma muwamko wa watu haya ni mambo ambayo hayana nafasi tena Zanzibar.
Tatizo.
1 ) Tatizo la Zanzibar na CCM ndilo linalotaifuna Zimbabwe
2 ) Tatizo la CUF na Zanzibar ndilo lilopelekea machafuko Kenya.
Sasa nakupa kibarua ya kufanya equation ya mambo hayo mawili hapo juu ili urudi na hesabu ya jawabu hilo.Mambo ya tararira hayana nafasi na huwezi kumdanganya mtu kwa leo kwa kumuimbia sijui hapo zamani za kale unasikitisha sana yaani umikuja jambo Forum kuja kusema uchovu wa hadisi za alfu lelalela.Pole sana.
 
Back
Top Bottom