Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Kuna watu hawataki kuamini kuwa chama cha CUF kinaelekea ikulu kutokea upinzani. Silazima iwe kesho au keshokutwa, kwakuwa inaeleweka kuwa demokarasia ina mikondo mingi ya kupita mpaka kufikia ufukweni salama. Nikimkumbuka Abdulaye Wade alivyo suffer na PDS yake tokea mwaka 1974, wakati bado Leopard Sedar Senghor mwenyewa yu hai, Wade kawa mpinzani tokea siku zote hizo, na alishindwa katika chaguzi 4 katika kitu cha urais, mpaka kizazi kipya cha Wasenegal kinafumbua macho na kumuelewa(baada ya kufa au kupoteza dira kwa wahafidhina) mwaka 2000 ndo PDS ya Wade na Wade mwenyewe wanaingia ikulu.
Kwa hiyo kufikia mafanikio kuna taka mipango ya muda mfupi na muda mreefu kama PDS ya Wade na usatahamilivu wa kuwavumilia wananchi katika kipindi cha mpito kuelekea demokarasia ya kweli,ambacho wengine hawajaifahamu hada madhumuni yake na vyama vinavyotawala vinatumia hila na vitimbi kuchezea ridhaa na matakwa ya wananchi walioifahamu hiyo demokarasia ya uchaguzi na wananchi kubakia kimya wakiwaachia viongozi wao wa vyama vya siasa wapege kelele.
Ila kwa kumalizia, chama cha Mapinduzi kisitazamie kutawala nchi hii comfortably miaka yote, kama UNIP ya Kaunda kama KANU ya Moi n.k kuna siku kitapumzishwa na siku zenyewe zinaanza kusogea taratiiibu. time will tell.
Binafsi nilikuwa mmoja wa watu walioamini kwamba Lipumba angeunda serikali ya kitaifa mwaka 2000, na yeye mwenyewe alitangaza hadi Baraza lake la Mawaziri. Wakati huo CUF ilishirikiana na Chadema katika kampeni zake. Baada ya hapo na hasa baada ya matatizo ya CCM/CUF Zanzibar, na hadi mwaka 2005, CUF ikaanza kupoteza mwelekeo na walizidi kuingia katika mtego wa mwafaka wa CCM ambao ni mtego mbaya kama nilivyosema ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
Nimekatishwa tamaa zaidi na kuibuka kwa siri nyingi mbaya za ndani ya CUF ambazo kwa maslahi ya Taifa, si vyema kuzijadili humu jamvini. Kwa kifupi kama hakitabadilika na kugeuka nyuma na kuamua kukataa mambo laini na kufuata mambo magumu, CUF haitoshinda. Walio ndani wanajua, na wanajua nini maana yake.
Mwa maslahi ya Taifa, CUF lazima wabadilike. Warudi kwenye ile CUF yenye kujitegemea na kutegemea zaidi wapenzi wake wa ndani na nje ya nchi na si ilivyo sasa. Hata kama hapo awali (1995-2000) walikua hivi, sasa waache.