Mtumishi wa umma mbaroni kwa kuchana na kuchoma Quran, Waziri Jafo aagiza asimamishwe kazi

Wafahamishe kwamba Qur'an,imetaja pia Injili,Zaburi,Taurati(Torati),ni vitabu vya Mungu,na vingine havikutajwa majina,lakini pia waislamu tunatakiwa tujue vipo vitabu vya Mungu.
Hao masheikh ubwabwa lazima wapige kelele maana ndiyo wenye kutumia hicho kitabu kinawahusu,na nimekwambia kwenye hicho kitabu hakisemi tu Qur'an ndiyo ya Mungu bali kumeeleza vingi tu kuwa ni vya Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama hoja ni hiyo si jeshi la polisi tayari limemkamata na watamfungulia mashtaka kwa mujibu wa katiba? Kusimamishwa kazi kunakujaje? Kwani amevunja sheria za kazi?
Nadhani umeshajifunza kitu mpaka Sasa. Tofautisha Sheria za utumishi wa Uma na Sheria za makosa ya jinai, na hizi wakati mwingine husomwa kwa pamoja. Kwa Mfano Mh. Rais amemfuta kazi jamaa yako kwa kutumia Sheria ya utumishi wa Uma lakini masuala ya kijinai ameziachia mamlaka husika ziendelee nae. Hivyo Basi huenda kule akamalizana nao aidha ikibainika amepatwa na hatia au la lakini kwenye utumishi alishajiharibia, yaani ameishushia hadhi aidha Taaluma yake au tasnia ya watumishi wa Uma. Nina Imani alichokitaka huenda ikawa ameshaanza kuvipata, Ninamwomba Kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya utumishi wa Uma.
 
Back
Top Bottom