Mtumia mafuta ya rays kukinga ukimwi

Cassava

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
282
36
Jamani wadau wa JF hasa hili jukwaa la mapenzi, poleni na kazi.
Nimeona niwashirikishe hili swala manake linaniacha njia panda.

jana nilienda salon moja kunyoa nywele hapa Dodoma mjini. Nikiwa nimekaa jamaa ananinyoa akaingia mzee wa makamo mnene tena muongeaji kweli kweli.

Basi, akaanza kuhadithia kuhusu rafiki yake mmoja ambaye yeye katika maisha yake hakuwahi kutumia kondom akiwa anafanya mapenzi. Anasema huyo jamaa yeye anatembea na kichupa cha RAYS (mafuta fulani ya mgando yaitwayo RAYS).

Anapotaka kuvunja amri ya 6, huupaka ukuni wake na kisha kuipaka K, akimaliza kiupaka tu kitu mwake mwake.

Jamaa anasema huyo jamaa alishapima pamoja na utundu wake wa mademu hajawahi kukutwa na maambukizo ya virusi kwa kuwa kichupa cha rays kilikuwa kinamsaidia. Ila akasema huyo mtumia RAYS alishakufa kwa ajali ya gari na anaamini alikufa akiwa hana virusi manake alikufa siku chache baada ya kupimwa.

Sasa wadau na wataalam, je Mafuta ya rays yanaweza kukinga maambukizo ya VVU?

Nawasilisha.
 
Alipokufa walimsachi hawakumkuta na rays?? joke, Nafikiri hii haijathibitishwa wala sijawahi kusikia ila hizi jell kama za ky na nyinginezo nimesikia pia watu wanatumia ila nakushauri usiamini hivyo vitu condom ni bora zaidi. ukimwi umejaa sana kuweza kufanya majaribio ya Rays.TUMIA CONDOM PLS Cassava
 
Hata hivyo nafikiri hakua msuguaji sana..pengine inahitaji utaalamu jinsi ya kusugua! maana kama wenzangu na mimi wanaosugua kwa kasi kama cherehani..hapo michubuko haikosi
 
Alipokufa walimsachi hawakumkuta na rays?? joke, Nafikiri hii haijathibitishwa wala sijawahi kusikia ila hizi jell kama za ky na nyinginezo nimesikia pia watu wanatumia ila nakushauri usiamini hivyo vitu condom ni bora zaidi. ukimwi umejaa sana kuweza kufanya majaribio ya Rays.TUMIA CONDOM PLS Cassava

Mshauri aoe na akae na mke wake tuu bila kuchakachua nje.
 
Hiyo haina ukweli wowote, njia sahihi ni kutumia condom kwa usahihi vinginevyo ni kujidanganya.
 
watanikoma


Mkuu by any means kama hiyo issue ina ukweli basi ni kwamba huyo jamaa katika pitapita zake zote hakuwahi kukutana na muathirika... Kwani kwa hesabu 7% ina maana katika watu 100 kuna wazima 93... Hivyo kuna uwezekano mkubwa hakuwahi kukutana na muathirika katika sarakasi zake. Ningekubaliana na hiyo hoja kama ningepata uhakika kuwa kamcharaza mwenye ngoma live kwa kutumia hiyo rays tena zaidi ya mara 3 na akatoka mzima, vinginevyo ni kupotosha umma....
 
Du! jamaa alikuwa mbunifu kweli!!
Ila alikuwa anacheza na moto! Ngoma bado hatari, sijui ile dawa waliotangaza Mwananchi gazeti kuwa imegunduliwa Marekani imefikia wapi!?....au ilikuwa geresha tu za wazungu?
 
Back
Top Bottom