Mtu wa Kwanza Duniani Ambaye Hana Jinsia

Kuna kesi moja inayohusu mambo ya ndoa nchini Uingereza walisema kwamba jinsia ya mtu "is determined at birth" kwahiyo huyo ni mwanamme kwa mujibu wa hiyo kesi. Wazungu wanaamua tu kuchezea akili za watu.

Na hiyo kesi mwanamme alioa mtu akidhani ni mwanamke halisi kumbe alijibalisha kwa upasuaji kutoka uanaume kwahiyo ndoa ikatenguliwa na Mahakama kwamba hakukuwa na ndoa hapo.
 
What about biologically

alizaliwa kama mwanaume, akajibadilisha kuwa mke. Kufikiri, kuwaza, matendo yake lazima ni kiume na hiyo ndiyo jinsia yake. Wazungu mapunguwani tu. such simple issue wanaifanya ngumu kutambua.
 
foolish............ kabisa sasa mshasema alizaliwa mwanaume wat else do we need
 

4235818.jpg

Norrie May-Welby

Mlowezi wa kiingereza nchini Australia ameingia kwenye rekodi za dunia kwa kuwa mtu wa kwanza kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote si ya kiume wala ya kike.
Norrie May-Welby mwenye umri wa miaka 48, Muingereza anayeishi nchini Australia amekuwa mtu wa kwanza duniani kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote.

Madaktari nchini Australia walishindwa kumuweka Norrie kwenye fungu la wanawake au wanaume kutokana na hali yake ya kutokuwa na viungo vyovyote vya siri.

Norrie alizawaliwa kama mwanaume lakini alifanya operesheni ya kubadilisha jinsia yake kuwa mwanamke mwaka 1990 wakati huo akiwa na umri wa miaka 28.

Lakini baada ya kutokuwa na furaha katika hali yake mpya ya uanamke, Norrie aliamua kufanya operesheni nyingine na kuondoa uke alioupandikiza ili asiwe na jinsia yoyote.

Katika pasipoti yake mpya kama raia wa Australia, ilibidi maafisa wa serikali waongeze fungu jingine la watu wasio na jinsia baada ya madaktari kusema kuwa wanashindwa kuthibitisha Norrie ni jinsia gani.

"Mimi si mwanaume wala mwanamke, mimi nimeona bora nisiwe na jinsia yoyote", alisema Norrie.

Kutokana na uamuzi huo wa maafisa wa Australia, Norrie amekuwa mtu wa kwanza duniani kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote.

Mtu wa Kwanza Duniani Ambaye Hana Jinsia

<tbody>
</tbody>

kumbe hapo ni suala la uamuzi wa watu kukufanya wewe hauna jinsia yoyote.me nilijua kazaliwa hana kitu yaani kazibwa kila sehemu kumbe yuko poa..hao wanajaribu kupingana na mungu tu hawana lolote hao...
 
Mimi sio mjuvi sana wa baolojiai ila kuna vitu ni rahisi kueleza. jinsia ya mtu inayotambulika ni ile aliyozaliwa nayo. Vilevile hata kama kaondoa sehemu za nnje, bado za ndani zanaweza kumtambulisha kuwa ni mtu wa aina gani. Huwezi badili kila kitu bana. huyo ni dume, na hao madaktari wa australia wamekosa u-serious.
 
huo ni uzushi huyo jamaa ni mwanaume si wamesema alizaliwa mwanaume ila akahangaika kujiharibu mwenyewe.pia ukimwangalia maumbile yake ya nje uwezi kataa kua ni mwanaume.
 
Back
Top Bottom