Mtu ukiwa na pesa, somesha mwanao international schools, achana na hizi exam based schools or education

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,735
2,000
Mtu ukiwa na hela ya kueleweka ama kama unataka kuwekeza kweli kwa watoto wako, wasomeshe international schools au shule zenye mitaala ya kimataifa.

Hizi shule zenye mitaala ya kimataifa zinawajenga watoto kwenye analytical skills, reasoning, logic, creativity, competence na mambo kama hayo.

Ukikutana na mtoto wa darasa la 6 wa hizi shule, reasoning yake ama analytical skills zake ni sawa na kijana wa form six wa necta schools.

Shule hizi hazilengi kuona mtoto anapata nini au maksi gani darasani bali kuibua talents nyingine alizonazo mtoto sio hizi za necta ambazo zimejikita kwenye ufaulu tu wa mwanafunzi.

Ukitaka kuwekeza kwenye elimu ya kweli kwa mwanao na kama uwezo upo peleka mwanao shule zenye mitaala ya kimataifa.
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
4,008
2,000
Mbona wengine tumesoma hizi hizi shule za sirikali, tena shule ya msingi kijijini kwa babu kuongea kilugha mwanzo mwisho lakini tumefanikiwa kupata scholorship kusoma Masters na PhD kwenye international universities ambazo zipo kwenye world ranking ya 10 bora, what happened?
 
Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,735
2,000
Daah nilikutana na mtoto wa shule hizi nikamuuliza una ndoto ipi akaniambia I want to be a UN SECRETARY.
Nikasema hawa kweli wanawaza international level.
Hawa watoto hawasomi kwa kutoboa, kukariri maswali ya physics sijui hesabu za mody physics.

Hawa wanajifunza elimu ya kuwasaidia kukabiliana na mazingira yanayowazunguka ambalo ndio dhumuni kuu la elimu.

Hizi za NECA eti unakuta hadi wanazuia wazazi kwenda kumuona mtoto eti utamharibia concentration, sasa hiyo elimu ama ujinga, kwamba mzazi ukitembelea mtoto utamvuruga asifanye vizuri? Ujinga ujinga mtupu kwenye elimu ya NECTA.
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
4,480
2,000
Unajifariji tu. Scholarship unapata lakini haina maana kuwa ubora wako uko kama wa graduate wa IST. Walimu wanafundisha hapo chuo kikuu lakini hawawezi kujieleza kwa Kiingereza na wamepata skolaship za UK, US, Australia.. wamefanya PhD nk huko.
Mbona wengine tumesoma hizi hizi shule za sirikali, tena shule ya msingi kijijini kwa babu kuongea kilugha mwanzo mwisho lakini tumefanikiwa kupata scholorship kusoma Masters na PhD kwenye international universities ambazo zipo kwenye world ranking ya 10 bora, what happened?
 
6321

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
307
500
Mtu ukiwa na hela ya kueleweka ama kama unataka kuwekeza kweli kwa watoto wako, wasomeshe international schools au shule zenye mitaala ya kimataifa.

Hizi shule zenye mitaala ya kimataifa zinawajenga watoto kwenye analytical skills, reasoning, logic, creativity, competence na mambo kama hayo.

Ukikutana na mtoto wa darasa la 6 wa hizi shule, reasoning yake ama analytical skills zake ni sawa na kijana wa form six wa necta schools.

Shule hizi hazilengi kuona mtoto anapata nini au maksi gani darasani bali kuibua talents nyingine alizonazo mtoto sio hizi za necta ambazo zimejikita kwenye ufaulu tu wa mwanafunzi.

Ukitaka kuwekeza kwenye elimu ya kweli kwa mwanao na kama uwezo upo peleka mwanao shule zenye mitaala ya kimataifa.
Sisi tuliosoma mchafukoge sec school tuna uwezo mkubwa Sana wa kukariri, swala la kuelewa utalikuta kazini.
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,090
2,000
Kuwa mjumbe wa Bodi wa Shule kumenisaidia kufahamu mengi juu ya hizi shule za serikali.Hizi shule za serikali siku hizi zimejaa siasa na mihemuko. Syllabus haifuatwi,kuna wataalamu wa elimu wanaojiita wakuu wa shule na maafsa elimu wa halmashauri kutwa kubuni vitu vya ajabu ajabu mara;

Wanafunzi wanakatazwa kusoma masomo mengine wasome Civics na Kiswahili eti wapate 'D' mbili za cheti.

Kuna baadhi wanaambiwa waache kabisa kusoma somo la hisabati. Wengine wanakatazwa walimu wasifundishe badala yake wawape wanafunzi mitihani na wasolve! Jumlisha mitihani ya inter- school, pre - mock, Mock, pre NECTA , Terminal, Mid-term nk. Kunawafanya walimu wasifundishe kabisaa.

Maagizo ya mara kwa mara toka kwa wabunifu wa wilayani na ubunifu wa mkuu wa Shule yasiyofuata na kuzingatia syllabus sio tu yanapunguza maana ya mtaala pia malengo yaliyokusudiwa.
 
logframe

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
3,721
2,000
Kuwa mjumbe wa Bodi wa Shule kumenisaidia kufahamu mengi juu ya hizi shule za serikali.Hizi shule za serikali siku hizi zimejaa siasa na mihemuko. Syllabus haifuatwi,kuna wataalamu wa elimu wanaojiita wakuu wa shule na maafsa elimu wa halmashauri kutwa kubuni vitu vya ajabu ajabu mara;
Wanafunzi wanakatazwa kusoma masomo mengine wasome Civics na Kiswahili eti wapate 'D' mbili za cheti.

Kuna baadhi wanaambiwa waache kabisa kusoma somo la hisabati. Wengine wanakatazwa walimu wasifundishe badala yake wawape wanafunzi mitihani na wasolve! Jumlisha mitihani ya inter- school, pre - mock,Mock,pre NECTA ,Terminal,Mid-term nk. Kunawafanya walimu wasifundishe kabisaa. Maagizo ya mara kwa mara toka kwa wabunifu wa wilayani na ubunifu wa mkuu wa Shule yasiyofuata na kuzingatia syllabus sio tu yanapunguza maana ya mtaala pia malengo yaliyokusudiwa.
Bila shaka hiyo shule ipo Arusha.
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
4,008
2,000
Unajifariji tu. Scholarship unapata lakini haina maana kuwa ubora wako uko kama wa graduate wa IST. Walimu wanafundisha hapo chuo kikuu lakini hawezi kujieleza kwa Kiingereza.
Mkuu kuna world scholars kibao ambao hawajakanyaga hizo international schools na wanaheshimika kwenye field zao. Nafikiri hizo shule zimeanzishwa purposely kwa ajili ya watoto wa mabalozi kwenye nchi husika, hakuna jipya...
 
nduza

JF-Expert Member
Feb 7, 2019
709
1,000
Mtu ukiwa na hela ya kueleweka ama kama unataka kuwekeza kweli kwa watoto wako, wasomeshe international schools au shule zenye mitaala ya kimataifa.

Hizi shule zenye mitaala ya kimataifa zinawajenga watoto kwenye analytical skills, reasoning, logic, creativity, competence na mambo kama hayo.

Ukikutana na mtoto wa darasa la 6 wa hizi shule, reasoning yake ama analytical skills zake ni sawa na kijana wa form six wa necta schools.

Shule hizi hazilengi kuona mtoto anapata nini au maksi gani darasani bali kuibua talents nyingine alizonazo mtoto sio hizi za necta ambazo zimejikita kwenye ufaulu tu wa mwanafunzi.

Ukitaka kuwekeza kwenye elimu ya kweli kwa mwanao na kama uwezo upo peleka mwanao shule zenye mitaala ya kimataifa.
Lakini mbona kibongo talent nyingi zinatoka kwa watu ambao ni masikini na wasio na elimu kubwa
Mbona hatuoni hao international wakiongoza kwenye fani nyingi zinazotumia vipaji sana
 
andjul

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
17,420
2,000
Mbona wengine tumesoma hizi hizi shule za sirikali, tena shule ya msingi kijijini kwa babu kuongea kilugha mwanzo mwisho lakini tumefanikiwa kupata scholorship kusoma Masters na PhD kwenye international universities ambazo zipo kwenye world ranking ya 10 bora, what happened?
Usinikumbushe mapito niliyo pitia.
Ile naanza na form five tu mwalimu wa kemia mzungu,mmarekani na Mjapani,hesabu ni mchina wa kimarekani na Mhindi,nageukia Fizikia nakutana na mzee Ngui sijui kabila gani masikini muda wote ni kufoka tu. Halelujaaa GS hii hapa na mzee Mwangoka anafundisha kwa kinyakyusa na stori zake za Tukuyu na kufukuzwa chuo kikuu kwa migomo...
Ikawa mwanzo mwisho ni kumeza tu....
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
4,480
2,000
Wewe ulitaka world-class scholars wote watoke international schools? Nani kasema hivyo? Your argument is based on a false premise. Twambie watoto wangapi wanasoma shule za kawaida na wangapi kati ya hao ni world-class scholars halafu twambie wangapi wanasoma international schools na wangapi kati ya hao ni world-class scholars. Wanaopita international schools is just a fraction ya wale wanaopita shule za kawaida. Unapofanya ulinganifu ni lazima uwe na numerators (x) na denominators (y). Hawezi kulinganisha mabilioni ya watoto wanaopita shule za kawaida na elfu kadhaa wanaopita katika international schools kwa idadi ya hao wachache waliokuwa world-class scholars kutoka katika mabilioni ya waliosoma huko kayumba.
Mkuu kuna world scholars kibao ambao hawajakanyaga hizo international schools na wanaheshimika kwenye field zao. Nafikiri hizo shule zimeanzishwa purposely kwa ajili ya watoto wa mabalozi kwenye nchi husika, hakuna jipya...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom