Uchaguzi 2020 Mtu timamu hawezi kushangilia matokeo haya

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,340
2,000
Kituo chenye wapiga kura 125,239 (registered voters) msimamizi anatangaza wamepiga kura 437,980, hata wizi hauko hivyo.

Uchaguzi ambao karibu nusu ya wagombea ubunge nchi nzima aidha wametekwa, wanashikiliwa na polisi au kujeruhiwa kwa silaha, utashangiliaje matokeo haya.

Matokeo ya uchaguzi ambao karatasi za kura feki zimezagaa mitaani nchi nzima.

Uchaguzi ambao wakati wa kuhesabu kura polisi wanaingia vituoni wanawatoa mawakala wote wa vyama vingine anabaki wakala wa CCM na msimamizi wa kituo wakihesabu peke yao.

Uchaguzi ambao OCD anaingia kituo cha kupigia kura anakwapua ballot box na kuondoka nalo.

Uchaguzi ambao matokeo yanaonyesha wagombea wote wa ubunge toka CCM wameshinda, matokeo ambayo yanakwenda kuunda bunge la chama kimoja.

Hata mwana CCM mwenye akili timamu hawezi kushangilia matokeo ya uchaguzi huu yanayokwenda kuligawa taifa.
 

Mr Tyang

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
1,234
2,000
Mleta mada si Rais wenu wa mtandaoni aliwambia kuwa atawaingiza barabarani, una lialia nini sasa?

Labda tu nikuulize baada ya Kamanda mkuu kutangazwa kuwa kashindwa mpaka Sasa hivi Makamanda wake mmeshaingia barabara ngapi?
 

Gmox

JF-Expert Member
Mar 31, 2014
298
500
Hakika ukiona mtu anasimama na kijivuna juu ya matokeo haya yafaa ajichunguzee, maana kinachofuata hapa ni kilio tu na wakutusemea akuna maana 89% ya hao viongozi watakuwa hawajachaguliwa na wananchi hii ni hatari sana aisee!
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,551
2,000
Hizi kura "Za Nyongeza" sio kote zimeshtukiwa. Na hata Kawe tuseme hicho alichokiona Mdee ni kituo kimoja, what about others?

Karatasi zilizobambwa ni "Genuine" kabisa, ndo kusema kua Tume walichapisha na karatasi za ziada wakawapa CCM.

Tumeingia gharama kubwa kuandaa haya maigizo. Ni heri tukawa hatuna Uchaguzi hizi hela zikaenda kwenye kazi zingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom