Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,827
- 3,569
Nimetoka kuzungumza na mpwa wangu sasa hivi anaomba msaada wa cherehani akajifunze kushona nguo, ndio mradi aliobuni baada ya kusota miaka 2 bila ajira. Amesoma ana degree Bachelor of Arts in Community and Development Studies.
Kaniambia ameshapata mtu wa kumfundisha na mahali pa kujifunzia (baraza fulani hivi). Ninavyofahamu huyo fundi cherehani atakayekuwa anamfundisha mpwa wangu kushona ana elimu ya darasa la saba tu, jamani! Huyu fundi atapata ujumbe gani kuhusu kusomesha mtoto?
Hivi kweli ni sawa kijana asome hadi elimu ya university aishie kuja kufundishwa ushonaji na mtu wa la saba? Kulikuwa na sababu gani ya kupoteza gharama na muda wote huo, si bora tu angeenda ushonaji alipomaliza la saba, labda sasa hivi angekuwa mbali sana. Au kuna mahali tunakosea katika elimu hizi, tuna universities nyingi na courses nyingi lakini kumbe wanachohitaji watu ni ufundi cherehani tu! Tunahangaika na mambo makubwa ya gharama kubwa bure tu!
Interestingly mpwa wangu ana shauku kubwa ya kutekeleza mpango wake huu, anauchukulia serious kabisa, anaanza kesho rasmi! Namtakia kila la heri lakini kwa kweli nashangaa tu, mimi katika makuzi yangu niliona degree ni level kubwa sana, si ya kutumia kwenye cherehani. Lakini basi ndiyo imeshakuwa hivyo.
Tunakwama wapi?