Kijana kumaliza degree na kuuza mahindi au kazi za umachinga ni kujidhalilisha

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Kijana kumaliza degree na kuuza mahindi au kazi za umachinga ni kujidhalilisha

Unasoma tokea huko shule ya msingi, sekondari, form 5 na six chuo kikuu unamaliza degree yako halafu unakuja kuwa mchoma mahindi, umachinga, kutembeza vitu, kuchimba mitaro na kazi za sulubu huko ni kujidhalilisha

Hizo ni kazi za kufanya waliokataa kusoma wakaishia la saba au walokomea form 4

Kwasababu ulimaliza la saba au form 4 na ulikua unasoma kwa bidii na kuna wana uliwaacha kitaa wao hawakua na time na shule then eti baada ya miaka mingi ya kusota kielimu unakuja kuwa sawa nao tu tena ajabu wanakuja kukuajiri na unakuta wamekuzidi

Sasa kuna mantiki gani ya elimu?Kama elimu yetu haimkomboi kijana kwanini tungangane nayo

Tulipaswa tuwe na elimu ya vitendo zaidi na stadi za maisha itakayomuandaa mtu akimaliza hata asipoajiriwa awe anajua nini cha kufanya tumekomaa na elimu za theory za what is communication verbal na non verbal sijui gesture sijui ninini

Japo kutegemea kuajiriwa sio jambo zuri lakini inauma mtu asome kwa bidii ajinyime kila kitu wazazi wauze hadi viwanja mashamba na ngombe mtoto aende shule halaf mwishowe wanakuja kuwa sawa na mtoto wa mama Mwajuma ambaye aliishia la saba B tu akaamua kujiingiza mtaani tokea akiwa na 14 years huko

Wasomi wengi wanapata msongo sana, maana huishia kuchekwa mtaani utaishia wanasema "kiko wapi sasa alikua anajifanyaga kusoma kwa bidiii na kupata one kiko wapi sasa?"

Serikali ijifunze kwa kikwete alifanyaje kupunguza tatizo la ajira.....Kwa kua hii mitaala mibovu ya theory ina baraka za serikali basi serikali ihakikishe watu wake wanaajirika na kupata ajira
 
Mkisha pata mshahara huko ofisini basi mnajiona mnayo akiri kuwazidi wengine, Umasikini umewajaa tu, mfano wafanyakazi wengi wakishatoka tu ofisini basi hata hela ya bando hamna, huwezi kumkuta Online hadi kesho muda wa kazi tena.
 
Inategemea umachinga unao define wewe ni huu wakutembeza vinguo viwili vitatu barabarani au kuwa na kiduka cha kawaida.Umachinga upo wa hali ya chini,kati na juu.Mimi naona inatengemea unataka kuwa wa juu au kati bado ni applicable kwa mtu mwenye degree kwani hata kuwa agent wa viwqnda vikubwa duniani bado ni umachinga but in different level.Mfano kuwa na kituo cha mafuta na unauza mafuta usioagiza wewe ,huo ni umachinga but in different version.Mimi mchaga hata niwe na PHD lazima niganye umachinga lakini kwa level ya juu
 
Degree holder unachimba mitaro ni kazi ila kiza ya kisenge kwa degree holder
Degree Holder Nicola Tesla aliwahi kufulia akawa kibarua wa kuchimba mitaro ya kupitishia nyaya za umeme za General Electric kampuni ambayo yeye mwenyewe ndiye alikuwa engineer mkuu kabla hajabuni Umeme wa AC.

Wewe degree holder wa Marketing ambaye hujawahi kuuza hata pipi ya tsh 50 unataka ujifanye Elon Munsk.?
 
Mkisha pata mshahara huko ofisini basi mnajiona mnayo akiri kuwazidi wengine, Umasikini umewajaa tu, mfano wafanyakazi wengi wakishatoka tu ofisini basi hata hela ya bando hamna, huwezi kumkuta Online hadi kesho muda wa kazi tena.
Ni sawa tu lakini nalia kivulini uhakika mwisho wa mwezi na sina stress kaz ipo wala haiyeyuki
 
Bado hujatafsiri maana ya elimu....omba Mungu yasikukute.
ni kweli hajui maana ya elimu anadhania elimu ni kuajiriwa kazi ya serikali au kwenye kampuni.

Atumie elimu kuboresha hiyo hiyo kazi ya kuchoma mahindi au chipsi, mfano kuweka mazingira mazuri, kufanya packaging au mbinu nyingine ya kuboresha ile biashara.
 
Shida kubwa ni kupeleka mambo bila mpango mkakati, suala hili la kutoangalia mwelekeo wa elimu na hatima ya elimu kesho yake linaanzia mbali sana kuanzia kwenye ngazi ya familia mpaka huko juu taifani.

Yaani watu kujifanyia mambo kwa kubahatisha bahatisha tu, yaani watu hawafikirii hivi tunafanya hili Jambo litakuwa na matokeo gani kesho.
 
Kwa hiyo unataka wawe wanalala tu wakati wanasubiria milango kufunguka mkuu? Au wawe ombaomba alafu muanze kuwatangaza kwa watu?

Naona la muhimu ni kuwatia moyo huku wakiwa focused na malengo ya maisha yao, nyakati ngumu huwa hazidumu.
 
Weka akiba ya maneno.
Waacha wachimbe mitaro na wazibue pia vyoo ,wapate Hela ya kula.
Nakupa
Mfano. Ukiuza chips sahani 20 *2500/ =50000/
Akipata faida buku TU .
20000/=
Zidisha mara 30

Jamani uzeni sana chips,mahindi. Machungwa mihogo.nk
Mtengeneze soko la bidhaa za wakulima yaani ,nyanya ,vitunguu,kabich,ndimu,nk
 
Back
Top Bottom