Mtu msomi ni nani?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,482
40,495
Msomi ni nani?

Katika kusoma makala mbalimbali pamoja na kufanya tafiti binafsi, kumeonekana kuna changamoto katika kusema fulani ni msomi.

Wapo wanaoamini, katika kufikia hatua fulani ya elimu anakuwa yuko sahihi kuitwa msomi.

Wengine wanaamini msomi, ni yule anayetumia rasilimali vitu, watu, fedha na kutengeneza fursa pamoja na kutatua changamoto za jamii.

Wengine wanaamini, kuwa na utitiri wa vyeti vingi ndio njia sahihi ya wao kuitwa wasomi.

Ilibidi nichimbue zaidi vitabu na makala mbalimbali, ili kupata mitazamo tofauti tofauti kuhusu neno msomi.

Na uchambuzi wangu, umejikita kwa makundi haya katka mtazamo wa neno msomi:-

Ambao hawakwenda shule kabisa

Hili kundi wanaamini mtu msomi, ni yule aliyeajiriwa au kuongea kiingereza au mtu mwenye mali.

Ambao wanajua kusoma na kuandika

Hapa niliwatazama wale waliofanikiwa sana kuliko walioenda shule, hawa mtazamo wao wanamchukulia mtu msomi kama mtu aliyeenda shule ili kuweza kujinusuru na changamoto za maisha kwa kuajiriwa; wao wanaona wasomi kama watu wanaopindisha mambo ili waweze kujihami na ugumu wa maisha.

Ambao wana elimu ya kawaida

Hapa niliwatazama wale waliohitimu elimu ya sekondari mpaka 'degree' moja. Wao wanaamini msomi ni yule mtu anayeweza kuchambua mambo; kwa hiyo kama kati yao wanaweza kuchambua mambo, anakuwa yuko sahihi kuitwa msomi.

Ambao wana elimu ya juu

Hapa niliwatazama wenye elimu ya 'masters' na PhD; katika kundi hili wengi wao wanaamini wao ni wasomi na wako sahihi kuitwa wasomi; katika kuhoji kwa nini wanashindwa kutatua chamgamoto za kijamii ingawa wao wapo na wanajiita wasomi; wengi hutoa visingizio vingi, mara ''lack of capital, lack of skilled labour, lack of power, lack of government support n.k''

Ambao wako level ya u-professor

Hili ndio kundi la mwisho linaloamini wao ndio wasomi zaidi na hakuna mtu anayeweza kuwa-'challenge' kama hujafikia hatua yao ya kielimu.
Ni kweli ni hatua ya juu ya kielimu, lakini swali lilikuwa, ni kwa nini mpaka leo katika vyuo vyetu bado tunatumia vitabu vingi kutoka kwa wazungu iwe ni ''financial management, managemeni in general, law, operation management n.k''.

Pia, uwepo wao unawasaidiaje jamii katika kutatua changamoto zao?
Jibu linalokuja, ''You are incompetent you can't argue with a professor?''

Hapa nilipo sijielewi wakuu; nipeni jibu, mtu msomi ni nani?


Update
NB:
''Accordance with eqnx ..../ according to eqn x...'' kama kwenye maandiko ya watu, hutumiki kwenye hiyo ''phrase'', usijihangaishe kujiita wewe ni msomi.​
 
Kwamba shahada sio Elimu ya juu mpaka MTU ajifariji?
Duniani pote MTU mwenye shahada anaelimu ya juu

Wewe unachanganya Elimu ya juu na Ajira, hayo ni mambo mawili tofauti.
Wengi tumeudhuria madarasani tukaondoka na magamba tu, leo hii tukiambiwa tutetee usomi wetu, tunabaki tukijing'ata ng'ata tu
 
Back
Top Bottom