Mtu gani alisababisha upate kazi?

Mungu amrehemu na ampe pumziko la amani, alishatangulia mbele ya haki. Ila sitokuja kumsahau milele na sitoacha kumwombea dua njema.

Alinitafutia kazi kipindi nimemaliza tu chuo kikuu, maisha yashanipiga kitanzi cha shingo na kimekaza kisawasawa, sina dira wala mwelekeo wa maisha. Na chuo kwenyewe nlikua natoka ghetto kwa miguu mpaka chuo umbali wa Kilometa 8 au Kilometa 9 bila hata kuwa na hela ya kula wala ya maji ya kunywa.

Home washaanza kupiga kelele na kunitukana kinoma, fulani yupo yupo tu dar, anazurura tu na kujihusisha na magenge ya wahuni... kamaliza chuo ila hataki kutafuta kazi, mtoto kalaaniwa yule... Anakesha kubeti tu!!!

Ukweli mtaani hakuna ajira, kibanda cha kubeti hata sikijui, mfukoni hela ya kula hata buku mbili sina, mapenzi yamenikamata kwasababu ya stress demu ndio akanikolezea kunikamata... Masela nliomaliza nao degree wengine washakua madereva wa bodaboda. Nani wa kukupa mchongo? Dah

Yule mzee hakua ndugu yangu wala hatukua hata na undugu wa mbali, ila alinipigia sim moja tu, from no where asubuhi ya siku ya alhamisi, maongezi yalikua;

Mzee : Hujambo? Nlijua umelala kijana. Haya mtafute huyu jamaa mwenye hii number kesho ijumaa saa moja kamili asubuhi, usiache. Nakutumia namba!

Mimi: Hapana, naamka saa 11 alfajr kila siku... Sawa mzee wangu, ntafanya hivo kumtafuta! Ila kuna nini mpaka unanihimiza hivi??

Mzee: Usiulize, ukishamtafuta na kuonana nae utajua. Kwaheri!

Nakutana na jamaa siku ya pili ijumaa ananiambia, mzee fulani amekuombea kazi, amekusifia uko vizuri darasani na pia kwenye kujituma na kazi, unatakiwa kuanza jumatatu bila kukosa! Mkataba wako huu! Mshahara 1.5 mil take home + laki 2 ya kodi + laki 1 usafiri + chakula!!!! Ila utakua chini ya uangalizi kwa muda wa mwezi mmoja tu juu ya utendaji wako wa kazi!!

Mwezi huo nlifanya kazi kama mbwa aisee!! Na kila nikiwaza maisha nliotoka baada ya hapo ndio nikazidisha kujituma vibaya sana!

Baada ya mwaka na nusu, mzee yule akaugua cancer na kufariki!

God bless him!
Basi kijali kiazaz chake kilichobaki mkuu
 
Baada ya mnyama PCB kunichakaza matokeo ya kidato cha Sita Shemeji yangu akaniambia Nenda kasome Diploma ya mechanics engineering
Nilivyomaliza Tukaenda nyumbani kwa kigogo mmoja akamwambia kuwa mm ni mechanics anifanyie mpango niingie kwenye hiyo Mamlaka ilikuw Ijumatano jumatatu nikalipoti kazini kigoma

Shemeji yangu ni mfupi kama mnavyojua matatizo ya watu wa fupi lkn hapa aliupiga mwingi


Nitaleta muendelezo jinsi sifa zilivyoniponza mpaka nikapokonywa ukuu wa idara ya mechanics hapo job
Naikumbk connection uliyonipa ila mpaka sasa ubao unasoma 0
 
Mwanangu R. Aliniambia kuna bidhaa flani dili sana, kuna siku tulikua dubai akaniambia walijaribu tafuta kiwanda wakapata ila wanatengeneza kwa oda.
Nikaweka akilini hiyo.

Siku moja nikaona video mtu amepost anauza katika soko letu.
Nikaingia alibaba nika search jina la hiyo product nikakutana na same video nikajua hao wanachukua kwa huyu supplier.
Tukawasiliana nikaagiza mzigo wa kwanza pc 3. Faida laki 9 kila pc.
Zimefika zikaisha.
Nikaongeza 5 zikafika zikaisha.
Sa hivi kila mwezi nina wastani wa kuuza same product angalau pc 5.

Best business ever. Unakaa na mzigo ila siku ukiuza ni kicheko
 
He,nyie mnabahati bhana Mimi ninadegree ya accountacy mwaka wa tano huu na aply naona nipumzike,nikiaply Naitwa interview Ila swali ninaloulizwa inakuaje mpaka leo haujaajiriwa na matokeo yako yapo vizuri najitetea pale Ila wengi nahisi wanakuwa hawaamini kuwa Sina kazi wengine wanahisi Kuna tatizo upande wangu nachoka kabisa
Kuna sehemu nzuri Mungu anakuandalia.
Don't give Up!!
 
Mwanangu R. Aliniambia kuna bidhaa flani dili sana, kuna siku tulikua dubai akaniambia walijaribu tafuta kiwanda wakapata ila wanatengeneza kwa oda.
Nikaweka akilini hiyo.

Siku moja nikaona video mtu amepost anauza katika soko letu.
Nikaingia alibaba nika search jina la hiyo product nikakutana na same video nikajua hao wanachukua kwa huyu supplier.
Tukawasiliana nikaagiza mzigo wa kwanza pc 3. Faida laki 9 kila pc.
Zimefika zikaisha.
Nikaongeza 5 zikafika zikaisha.
Sa hivi kila mwezi nina wastani wa kuuza same product angalau pc 5.

Best business ever. Unakaa na mzigo ila siku ukiuza ni kicheko
Bro ww ulikuw Ushatoboa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom