Mtu gani alisababisha upate kazi?

Mtu gani alisababisha upate kazi?

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2017
Posts
1,011
Reaction score
1,915
Habari,

Tunajua kwenye maisha Yetu kila kitu ni Mungum

Hebu Tuambie Mtu unaye mu admire alisababisha wewe upate kazi unayofanya au uliyowahi kufanya kupata maisha.

Mimi nilikuwa kitaa kuna binti mmoja alinitumia tangazo la kazi kwenye WhatsApp akiniomba nimsaidie kuaplai kazi nikafanya kazi aliyonituma nami pia nikaamua kuaplai ni ajira za NGOs ya afya.

Aisee Mimi ndo niloyeitwa kwa interview na nikapata ile kazi.

Ashukuriwe sana Yule binti J.

Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
 
Wanangu J,

ananipigia simu kuwa ameambiwa Bank Z (sio jina halisi) kuna kazi, Chap bila kuchelewa natimba nakutana na Mama K, akaniunganisha na wengine waliokuwa wanasubiri kupiga interview.

Nikapiga interview baada ya wiki nikaitwa kwenda training.... nikaanza kazi baada ya miezi kadhaa nishazoea kazi J akaniletea mteja wake anataka mkopo nikamfanyia chap kwa haraka.

Yule jamaa kumbe ni HR taasisi moja ya Govt....akanambia kama niko tayar niandike barua kuna kazi kwenye taasisi yake...nikavunga kidogo lkn baada ya kuwa advised na washua na other relative nikaandika barua, nikaitwa kwa interview wakati ule ajira hazijawa fully centralised.

Nikapiga interview baada ya miezi kama 5 hv nikaitwa kazini... aisee sitoacha kumshukuru mwanangu sana J maana yy ndiye source ya mafanikio haya!
 
Mimi Pana mlinzi mwenzangu tulitoka lindo asubuhi akaniambia panono wametangaza nafasi za kazi gazette lipo home twende ukaaply.

Nilienda nikaaply nilifanikiwa ikabdili maisha yangu tukaja kutana na my ex security guard mwenzangu Chuo tukalamba degree jamaa nae alipata mishe nono baada yangu
 
Kuna kazi nyingine natarajia kuianza mwezi ujao Binti j pia amehusika niipate pia.

Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
He,nyie mnabahati bhana Mimi ninadegree ya accountacy mwaka wa tano huu na aply naona nipumzike,nikiaply Naitwa interview Ila swali ninaloulizwa inakuaje mpaka leo haujaajiriwa na matokeo yako yapo vizuri najitetea pale Ila wengi nahisi wanakuwa hawaamini kuwa Sina kazi wengine wanahisi Kuna tatizo upande wangu nachoka kabisa
 
Nilikuwa msibani baada ya bro wangu kupotezea maisha. Rafiki yangu akanidokeza kuwa ofisi flani wametangaza nafasi ya kazi. Nikampa vyeti atoe copy na nikamwomba aniandikie barua kisha apeleke. Baada ya wiki nikaitwa usaili na yeye hakuitwa hata kufanya usaili. Baadae nikapata kazi.
 
Mungu amrehemu na ampe pumziko la amani, alishatangulia mbele ya haki. Ila sitokuja kumsahau milele na sitoacha kumwombea dua njema.

Alinitafutia kazi kipindi nimemaliza tu chuo kikuu, maisha yashanipiga kitanzi cha shingo na kimekaza kisawasawa, sina dira wala mwelekeo wa maisha. Na chuo kwenyewe nlikua natoka ghetto kwa miguu mpaka chuo umbali wa Kilometa 8 au Kilometa 9 bila hata kuwa na hela ya kula wala ya maji ya kunywa.

Home washaanza kupiga kelele na kunitukana kinoma, fulani yupo yupo tu dar, anazurura tu na kujihusisha na magenge ya wahuni... kamaliza chuo ila hataki kutafuta kazi, mtoto kalaaniwa yule, michango ya familia hatoi, kazi kufanya starehe, angalia mtoto wa fulani amemaliza chuo ana kazi yake na nyumba yake sasa hivi... Anakesha kubeti tu!!!

Ukweli mtaani hakuna ajira, kibanda cha kubeti hata sikijui, sio mtu wa viwanja, mfukoni hela ya kula hata buku mbili sina, mapenzi yamenikamata kwasababu ya stress demu ndio akanikolezea kunikamata vizuri... Masela nliomaliza nao degree wengine washakata tamaa ya maisha kwasababu hakuna ajira, na hapo washakua madereva wa bodaboda tena.... Nani wa kukupa mchongo? Stress zilinijaa mpaka nikapata depression kufikia hatua nlitamani nife, kikwazo cha kufupisha maisha yangu ilikua dini yangu, ni dhambi kubwa sana kujitoa uhai, ni kumkufuru muumba... Dah!!

Yule mzee hakua ndugu yangu wala hatukua hata na undugu wa mbali, ila alinipigia sim moja tu, from no where asubuhi ya siku ya alhamisi, maongezi yalikua;

Mzee : Hujambo? Nlijua umelala kijana. Haya mtafute huyu jamaa mwenye hii number kesho ijumaa saa moja kamili asubuhi, usiache. Nakutumia namba!

Mimi: Hapana, naamka saa 11 alfajr kila siku... Sawa mzee wangu, ntafanya hivo kumtafuta! Ila kuna nini mpaka unanihimiza hivi??

Mzee: Usiulize, ukishamtafuta na kuonana nae utajua. Kwaheri!

Nakutana na jamaa siku ya pili ijumaa ananiambia, mzee fulani amekuombea kazi, amekusifia uko vizuri darasani na pia kwenye kujituma na kazi, unatakiwa kuanza jumatatu bila kukosa! Mkataba wako huu! Mshahara 1.5 mil take home + laki 2 ya kodi + laki 1 usafiri + chakula = 1.8 Mill total!!!! Ila utakua chini ya uangalizi kwa muda wa mwezi mmoja tu juu ya utendaji wako wa kazi!!

Mwezi huo nlifanya kazi kama mbwa aisee!! Na kila nikiwaza maisha nliotoka baada ya hapo ndio nikazidisha kujituma vibaya sana! Kijijini huko ndugu na wazee wakaanza kuniita baba, sio tena nimelaaniwa!

Baada ya mwaka na nusu, mzee yule akaugua cancer na kufariki! Dah haya maisha!

God bless him!
 
Zamani huko 2004 ...
Hakusababisha..alinibeba kabisa aisee...!

Aliambia piga namba hii ongea na huyu mchina..mshahara laki 6...

Nikapiga huyo nikaingia job kumbe ilikua kazi yake kaacha kaenda kampuni ingine ndio akamwambia mchina naleta mtu kama mm atacover nafasi yangu ila usimlipe chini ya 600k imagine 2004...

Nikapiga miaka miwili....

Akaniambia sa hv umeiva apply kazi sehemu flani kumbe yeye ndio boss pale...akanivujishia na maswali kabisa

Sasa ile written nikapasua, ile ya practical nikaichana mbaya kabisa...kwenye oral hakua na access wale wazungu wakabaki mdomo wazi maana niliwaacha hoi kabisa

Dada mmoja akasema no...this is too good to be true....

Nikapewa nyingine..maswali yamebadilishwa

Nikaipasua...akakosa cha kusema!

Next time....mm nikambeba jamaa nilipata kazi mahali nikamrecomend yeye....nilijua kabisa ile kazi singeiweza!
 
He,nyie mnabahati bhana Mimi ninadegree ya accountacy mwaka wa tano huu na aply naona nipumzike,nikiaply Naitwa interview Ila swali ninaloulizwa inakuaje mpaka leo haujaajiriwa na matokeo yako yapo vizuri najitetea pale Ila wengi nahisi wanakuwa hawaamini kuwa Sina kazi wengine wanahisi Kuna tatizo upande wangu nachoka kabisa
Ukitaka kuajiriwa .

Mungu kwanza .

Jitahidi kutengeneza Cv Kutokana na mahitaji ya mwajiri

Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
 
Mimi mwanamke ninayeishi nae alinisisitiza sana jaribu na hii baada ya kula za uso mara nyingi mnoo.Niliomba,nikaitwa na niko kazini.Nakimbiaje na mafaili nalala nayo ,natembea nayo ni mafaili kwa kwenda mbele.2032 ntaiacha hii kazi nikiwa hai.
 
Baada ya mnyama PCB kunichakaza matokeo ya kidato cha Sita Shemeji yangu akaniambia Nenda kasome Diploma ya mechanics engineering
Nilivyomaliza Tukaenda nyumbani kwa kigogo mmoja akamwambia kuwa mm ni mechanics anifanyie mpango niingie kwenye hiyo Mamlaka ilikuw Ijumatano jumatatu nikalipoti kazini kigoma

Shemeji yangu ni mfupi kama mnavyojua matatizo ya watu wa fupi lkn hapa aliupiga mwingi


Nitaleta muendelezo jinsi sifa zilivyoniponza mpaka nikapokonywa ukuu wa idara ya mechanics hapo job
 
He,nyie mnabahati bhana Mimi ninadegree ya accountacy mwaka wa tano huu na aply naona nipumzike,nikiaply Naitwa interview Ila swali ninaloulizwa inakuaje mpaka leo haujaajiriwa na matokeo yako yapo vizuri najitetea pale Ila wengi nahisi wanakuwa hawaamini kuwa Sina kazi wengine wanahisi Kuna tatizo upande wangu nachoka kabisa
.
20230408_220002.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom