Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,163
- 64,224
Ili apate cha kuiba; wengine wanakuombea mabaya, mfano:-
- Daktari anataka uugue ili aende kukutibu
- Wakili anataka uwe na kesi ili aweze kusimamia
- Muuza majeneza anataka ufe ili auze majeneza
- Nabii anataka urogwe ili akutoe mapepo
- Mganga anataka urogwe na wachawi ili akupe tiba
- Askari anataka ukosee ili wakukamate
- Mama ntilie na wenye hoteli wanataka usikie njaa wakuuzie chakula
- Kiongozi anataka uwe mjinga ili akutawale
- Fundi magari anataka gari iaribike ili aitengeneze
- Dereva bajaji anataka jua likuchome ili upande usafiri wake
- Muuza mwamvuli anataka unyeshewe na mvua ili ununue mwamvuli
- Askari magereza anataka ufungwe ili apate kazi
- Fundi viatu anataka kiatu chako kiharibike ili akishone
- Muuza madawa anataka uugue ili akuuzie dawa
- Mchungaji anataka usifanikiwe ili kila siku uwe muumini wake
Hatari sana, mambo ni mengi; kwa kweli tuwaombee wezi waishi miaka mingi kwa kutuombea mema na mafanikio.
Kama wewe ni mwizi, nyoosha mkono juu nikununulie pepsi
Kama wewe ni mwizi, nyoosha mkono juu nikununulie pepsi