UZUSHI Mtu aliyechora tattoo hawezi kabisa kuchangia damu

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Habari Wakuu,

Hata hivyo kumekuwa na dhana kuwa mtu anayejichora tattoo hawezi kumchagia mtu damu na sababu za kutokufanya hivyo hazijawekwa bayana zikaeleweka

Je, ni kweli kwamba mtu aliyechora tattoo hawezi kuchangia damu? Na kama ni kweli zipo ni sababu za kisayansi ya kushindwa kufanya hivyo?

IMG_7236.jpeg
 
Tunachokijua
Damu ni kimiminika muhimu kwa maisha ya binadamu. Pamoja na kazi zingine, hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksijeni na virutubisho mwilini, huratibu mfumo wa kinga mwili katika kupambana na maambukizi mbalimbali ya magonjwa pamoja na kudhibiti joto kwenye kiwango cha kawaida kinachofaa kwa afya bora.

Pamoja na uwepo wa mapinduzi makubwa katika uwanda wa sayansi, teknolojia na tiba, hadi sasa hakuna mbadala wa damu inayoweza kutengenezwa kwenye maabara. Mwili wa binadamu pekee ndio unaweza kuzalisha damu inayoweza kutumika kwa binadamu mwingine.

Wagonjwa wengi hutegemea damu ili kuokoa maisha yao hasa pale wanapokuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa za kiafya kama vile upasuaji, maambukizi makali ya magonjwa (mfano Malaria), ajali na matibabu ya saratani.

Mwili wenye afya unaweza kuzalisha upya, au kutengeneza damu nyingi zaidi katika muda wa wiki 4 hadi 6 hivyo kuchangia damu ni suala jema lisilo na athari kwa afya ya mchangiaji.

Masharti ya kuchangia damu
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), yapo masharti mengi yanayopaswa kuzingatiwa kwa watu wanaotaka kuchangia damu.

Pamoja na kwamba masharti haya hutofautiana kati ya nchi na nchi, WHO inashauri kuzingatia yafuatayo;
  1. Awe na umri wa kati ya miaka 18-65
  2. Awe na uzito unaofikia kilo 50 na kuendelea
  3. Awe na afya bora, asiwe na mafua au maambukizi ya mfumo wa chakula
  4. Kwa mwanaume, awe na damu inayofikia 13.0 g/dl na mwanamke 12.0 g/dl
  5. Asiwe na maambukizi ya VVU, Homa ya Ini, asiwe ametumia madawa ya kulevya pamoja na kushiriki matendo ya ngono zembe kwenye kipindi cha miezi 12
  6. Asiwe mjamzito au ananyonyesha
Tattoo na kuchangia damu
Kama ilivyobainishwa awali, uchoraji wa tattoo ni moja ya sanaa ambazo watu hutumia kuchora michoro mbalimbali mwilini mwao. Michoro inayoweza kuwa na kumbukumbu au maana kwao au hata kwa watu wengine.

Yapo maswali na mitazamo mingi inayozungumzwa kuhusu watu wenye tattoo na uwezo wao wa kuchangia damu.

Ukweli kuhusu dhana mbalimbali zinazohusiana na suala hili upoje?

JamiiForums imezungumza na wataalamu mbalimbali wa afya ya binadamu pamoja na kurejea tafiti na nyaraka za kitabibu na kubaini kuwa watu walio na tattoo hawakatazwi kuchangia damu, isipokuwa upo utaratibu mahsusi uliowekwa kwa ajili yao ili waweze kushiriki katika kuchangia.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mtu aliyechora tattoo haruhusiwi kuchangia damu kwa kipindi cha miezi 6 tangu siku ya kwaza ya kujichora. Hata hivyo, ikiwa uchoraji wa tattoo utafanywa na wataalamu wa afya waliosajiliwa kwa kufuata taratibu zote za kiusalama, tendo la uchangiaji wa damu linaweza kufanywa baada ya masaa 12 tangu kuchorwa kwa tattoo.

Aprili 2020, Taasisi ya Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC) ilitoa pia mwongozo mpya wa uchangiaji damu ili kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI. Katika mwongozo huo, CDC inashauri kusubiri kwa kipindi cha walau miezi 3 kuchangia damu baada ya kuchora tattoo.

Aidha, mwongozo wa Taasisi ya Msalaba Mwekundu ya Marekani haukatazi watu wenye tattoo kuchangia damu, bali huwataka wasubirie kwa miezi 3 tangu tarehe ya kwanza ya kuchora tattoo husika ili waweze kuchangaia damu.

Taasisi zingine pia kama San Diego Blood Bank hushauri mtu kusubiri kwa miezi 3, Taasisi ya Msalaba Mwekundu ya Australia hushauri kusubiri kwa miezi 4 na NHS hushauri kusubiri kwa miezi 4.

Masharti haya huhusika pia kwa watu wanaojitoboa miili kwa kutumia vifaa visivyotakaswa.

Sababu ya kutochangia damu baada ya kuchora tattoo
Sababu ya kusubiria kwa kupindi fulani kabla ya kuchangia damu ni kuzuia maambukizi ya magonjwa yanayoweza kutokea pindi mhitaji atakapopatiwa damu husika.

Uchoraji wa tattoo huhusisha matumizi ya vifaa vyenye ncha kali vinavyoweza kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa, hasa ikiwa vitakuwa havijatakaswa.

Baadhi ya magonjwa hayo ni homa ya Ini na VVU/UKIMWI

Madhara ya kuchangia damu
Hakuna madhara ya kuchangia damu, hata hivyo baadhi ya wachangiaji hupatwa na maumivu kidogo ya kichwa, kizunguzungu, uchovu pamoja na kuhisi maumivu eneo la kutolea damu.

Kwakuwa utaratibu wa kutengeneza damu mpya hufanyika kila siku, mwili hufidia kiasi cha damu kilichotolewa kila baada ya wiki 4-6.

Hivyo, kwa wastani, taasisi ya Cleveland Clinic inashauri kuwa kila baada ya siku 56, mtu aliyechangia damu awali anaweza tena kuchangia damu kwa mara nyingine.
Asante kwa ufafanuz

Kuna kitu nimekielewa pia kumbe ndo maana Marekani hawaruhusu mashoga kuchangia damu pamoja na kuwa wanapenda hyo jamii ya wafukua mitaro
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom