Mimi Na Mama Damu Damu Campaign

ndo vile

Member
Mar 11, 2023
25
12

MIMI NA MAMA DAMUDAMU COMPAIGN.​

NOTE DHANA (CONCEPT NOTE)

UTANGULIZI​

Pamoja na ukuaji mkubwa wa kiteknolojia na gunduzi nyingi zinazofanywa katika sekta ya afya na utabibu bado haiwezekani kuunda damu katika maabara.Uchangiaji wa damu kwa hiari ndiyo njia pekee inayotegemewa duniani kote katika kuokoa maisha ya watu wenye kuhitaji damu kama njia ya matibabu,wamama wajawazito,waathirika wa ajali,wagonjwa wa saratani,pamoja na watu wenye magonjwa yanayosababisha upungufu wa damu mara kwa mara wanaweza kuokolewa maisha yao kwa uwepo wa damu salama na yakutosha katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Kila mchangia damu anaweza kuokoa maisha hadi ya watu watatu na kuchangia damu kwa hiari ni wazo jema linaloonyesha kujali,upendo,utu na ubinadamu.”Upatikanaji wa damu salama naya kutosha ni sehemu ya utekelezaji wa lengo la huduma kwa afya kwa wote lakini pia ni kipengele muhimu katika utendaji kazi wa mifumo ya afya kote duniani” kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO).

Pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali na sekta binafsi katika kuhamasisha watanzania kuchangia damu kwa kutumia kampeni na matukio mbalimbali bado muitikio wa watanzania kujitokeza na kuchangia damu salama ni mdogo,kampeni ya MIMI NA MAMA DAMUDAMU ni kampeni ya kitofauti na kimapinduzi inayokuja kuamsha ari na kujenga utamaduni mpya kwa watanzania kuwa wachangia damu salama kwa hiari wa mara kwa mara.

KWA NINI MIMI NA MAMA DAMUDAMU CAMPAIGN?​

Mama yetu mpendwa ambaye ndiye Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hasani ametuonyesha kwa vitendo jinsi anavyojali maisha ya watanzania kwa uboreshaji mkubwa alioufanya katika sekta ya afya tena ,kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani yamefanyika maboresho makubwa katika sekta ya afya,ujenzi na upanuzi wa mahospitali,vituo vya afya,zahanati,uwepo wa vifaa tiba na wataalamu wa afya,uwepo wa madawa ya kutosha katika maeneo mbalimbali nchini ni ushahidi wazi unaoonyesha ni kwa kiasi gani Mh.Rais anajali maisha ya watanzania anaowaongoza.

Kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa damu salama kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za afya mheshimiwa Raisi Samia Suluhu Hasani ameamua kutoa bure mifuko inayotumika kukusanyia damu salama katika halmashauri zote 184 nchini Tanzania,hii inaonyesha ni kwa kiasi gani Mama yetu mpendwa anajali maisha ya watanzania.

Kwa kuwa Mama yetu Mh. Samia Suluhu Hasani ameshaonyesha kwa vitendo jinsi anavyojali maisha ya watanzania kwa maboresho makubwa aliyoyafanya kwenye sekta ya afya “KAMPENI YA MIMI NA MAMA DAMUDAMU”itatoa fursa kwa watanzania kusimama pamoja na mama yetu mpendwa na kumtia moyo kwa kazi kubwa na za kizalendo anazozifanya katika kutatua changamoto za watanzania haswa katika sekta ya afya kwa kujitokeza kwa wingi na kuchangia damu salama kwa hiari.

MIMI NA MAMA DAMUDAMU CAMPAIGN​

Kampeni ya uhamasishaji uchangiaji wa damu salama kwa hiari yenye lengo la kuongezaupatikanaji wa damu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuweza kuchochea utoaji wa huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu salama ya kutosha kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Njia za uhamasishaji katika kampeni hii ni za kitofauti na za kipekee na kampeni nyingine za uhamasishaji wa uchangiaji wa damu wa hiari zilizowahi kufanyika Tanzania,hivo kwa kupitia kampeni hii tunatarajia watanzania wengi kuhamasika zaidi kujitokeza kuchangia damu kwa hiari na kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa damu salama katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo kumtia moyo na nguvu Raisi wetu na kumuonesha kwa vitendo jinsi watanzania wapo pamoja naye na wanaziona jitihada kubwa na za kizalendo anazozifanya katika kutatua changamoto zinazowakabili watanzania haswa katika sekta muhimu ya afya.

MALENGO​

Watanzania kusimama pamoja na Raisi wetu Mama Samia Suluhu Hasani na kuunga mkono jitihada zake za kizaendo za utatuzi wa changamoto zinazowakabili watanzania haswa katika sekta ya afya kwa kuchangia damu kwa hiari.

Kujenga utamaduni mpya kwa watanzania kuwa wachangiaji damu wa mara kwa mara ili kuongeza upatikanaji wa damu salama katika vituo vyetu vya afya na kuokoa maisha ya watanzania.

Kutoa elimu juu ya uchangiaji wa damu salama kwa hiari,kiafya,kijamii,kiuchumi,na kisaikolojia na kuondoa dhana potofu walizonazo baadhi ya watanzania kuhusiana na uchangiaji wa damu salama kwa hiari.

UTEKELEZAJI​

Tumezoea kuona kampeni nyingi za uhamasishaji wa uchangiaji damu kwa hiari zikitumia watu maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii zetu kama wanasiasa,viongozi wa dini,wanamichezo,wanamuziki katika uhamasishaji wa uchangiaji wa uchangiaji wa damu salama,watu hawa wenye ushawishi katika jamii hujumuika na wananchi wa kawaida na kuchangia damu kwa hiari,kitendo cha watu hawa maarufu kujumuika na wananchi wa kawaida na kuchangia damu huwavutia wananchi wengi kujitokeza na kuchangia damu salama kwa hiari.

Kampeni ya “MIMI NA MAMA DAMUDAMU” pia itawatumia watu maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii katika kuhamasisha uma wa watanzania kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ila itawatumia kwa namna tofauti na ilivyozoeleka katika kampeni na matukio mengine ya uhamasishaji wa uchangiaji damu wa hiari.

Kwa kawaida utaratibu wa uchangiaji wa damu unajumuhisha hatua nne​

  1. Kujaza dodoso la mchangia damu na kupima uzito,
  2. Kupima shinikizo la damu,kupima wingi wa damu na kufanya majadiliano kuhusu afya ya mchangia damu,
  3. Mchangia damu kuchangia damu yenye ujazo wa miimita 450,
  4. Baada ya kuchangia damu mchangiaji kupata mapumziko ya dakika 5 na kupewa kinywaji.

Katika kampeni ya “MIMI NA MAMA DAMUDAMU” watu maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii hawatachangia damu kama iivyozoeleka kwenye kampeni na matukio mengine ya uhamasishaji wa uchangiaji damu bali watashiriki moja kwa moja katika hatua ya kwanza na ya nne za utaratibu wa uchangiaji damu.

Wanasiasa,viongozi wa dini,wanamuziki,wafanyabiashara wakubwa,wanamichezo,wasanii,watahusika moja kwa moja katika kampeni hii ya “MIMI NA MAMA DAMUDAMU”kwa kujaza madodoso ya wananchi watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiari na kwa kushirikiana na wataaamu wa afya watu hawa maarufu na wenye ushawishi watashiriki katika kupima uzito wananchi watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiari,(hatua ya kwanza ya utaratibu wa kuchangia damu).

Kwa mfano wananchi wa Dar es salaam watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiari taarifa zake za awali kama jina,umri,jinsia,zijazwe na Mtume mwamposa,halafu uzito apimwe na Diamond.

Pia watu hawa maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii watahusika moja kwa moja kwenye hatua ya nne ya utaratibu wa uchangia damu,ambapo kwa kawaida mchangia damu baada ya kuchangia damu katika hatua ya tatu, hupata mapumziko ya dakika 5 na kupewa kinywaji,wagawaji wa vinywaji katika hatua ya nne watakuwa watu hawa maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii.

Kwa mfano wananchi wa Dodoma watakaojitokeza kuchangia damu wakati wa mapumziko ya dakika 5 wapewe vinjwaji na Mandonga,Nandy,Morisson n.k

KUZINGATIA(FOCUS)​

Hatua ya pili na ya tatu katika utaratibu wa uchangiaji damu zinazojumuhisha kupima shinikizo la damu,wingi wa damu majadiliano kuhusu afya ya mchangia damu na mchangia damu kuchangia damu zitaratabiwa na kusimamiwa na wataaamu wa afya kwa asilimia 100.

Kitendo cha watu hawa maarufu na wenye ushawishi kushiriki kwenye hatua hizi mbili za utaratibu wa kuchangia damu,hatua ya kwanza na ya nne itaongeza amasa ya watanzania wengi kujitokeza na kuchangia damu kwa hiari kwa sababu hii itakuwa ni moja ya fursa adimu kwa watanzania kukutana kwa karibu na kupata wasaa wakuonana pamoja na kuongea kwa uchache na watu ambao wanawapenda na kuwashabikia,nafasi ambayo siyo rahisi kuipata kwa njia nyingine.

Kampeni ya “MIMI NA MAMA DAMUDAMU” itatoa fursa hii adimu ya kwa watanzania watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiari ya kuwaona kwa karibu,kuongea na kupiga picha watu wanaowapenda na kuwashabikia.

MATUKIO MENGINEYO KWENYE KAMPENI YA “MIMI NA MAMA DAMUDAMU”​

Kuelezea kwa wananchi watakaojitokeza kuchangia damu mafanikio ya kijamii,kiuchumi,kidemokrasia kimiundombinu,yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hasani kwa kutumia runinga na vipeperushi.

Utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa uchangiaji damu kijamii,kiuchumi,kisaikolojia n.k. Utoaji wa chanjo ya uviko 19.

Photo shoot,wananchi watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiariwatapata fursa ya kupiga picha za kumbukumbu na watu wanaowapenda na kuwashabikia.

Burudani za muziki,live band,djs session,celebrites appearances.

MATARAJIO​

Jamii ya watanzania kusimama pamoja na Mh.Raisi Samia Suluhu Hasani katika kuifanya Tanzania yenye maendeleo,upendo,na amani.

Itajenga utamaduni mpya wa watanzania kuwa wachangiaji damu wa hiari wa mara kwa mara na kuokoa maisha ya watanzania.

Wananchi watapata elimu juu ya umuhimu wa uchangiaji damu na kuondokana na dhana potofu walizonazo baadhi ya watanzania kuhusiana na uchangiaji damu.

Itasaidia serikali kupata takwimu za magonjwa mengine kama maambukizi ya virusi vya ukimwi. Utatoa fursa ya watu maarufu kukutana kukutana na mashabiki zao na kubadilishana nao mawazo. Undugu,umoja,mshakamano,na upendo baina ya watanzania utaimarika maradufu.

WALENGWA​

Wizara ya afya,Mpango wa taifa wa damu salama, Chama cha mapinduzi,

Sekta binafsi na asasi za kiraia, Watu maarufu na wenye ushawishi,

Vyombo vya habari na Wananchi wote.

COLLINS AUDAX KARANI, 0656996116, 0788947141,​

MIMI NA MAMA DAMUDAMU COMPAIGN.​

NOTE DHANA (CONCEPT NOTE)

UTANGULIZI​

Pamoja na ukuaji mkubwa wa kiteknolojia na gunduzi nyingi zinazofanywa katika sekta ya afya na utabibu bado haiwezekani kuunda damu katika maabara.Uchangiaji wa damu kwa hiari ndiyo njia pekee inayotegemewa duniani kote katika kuokoa maisha ya watu wenye kuhitaji damu kama njia ya matibabu,wamama wajawazito,waathirika wa ajali,wagonjwa wa saratani,pamoja na watu wenye magonjwa yanayosababisha upungufu wa damu mara kwa mara wanaweza kuokolewa maisha yao kwa uwepo wa damu salama na yakutosha katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Kila mchangia damu anaweza kuokoa maisha hadi ya watu watatu na kuchangia damu kwa hiari ni wazo jema linaloonyesha kujali,upendo,utu na ubinadamu.”Upatikanaji wa damu salama naya kutosha ni sehemu ya utekelezaji wa lengo la huduma kwa afya kwa wote lakini pia ni kipengele muhimu katika utendaji kazi wa mifumo ya afya kote duniani” kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO).

Pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali na sekta binafsi katika kuhamasisha watanzania kuchangia damu kwa kutumia kampeni na matukio mbalimbali bado muitikio wa watanzania kujitokeza na kuchangia damu salama ni mdogo,kampeni ya MIMI NA MAMA DAMUDAMU ni kampeni ya kitofauti na kimapinduzi inayokuja kuamsha ari na kujenga utamaduni mpya kwa watanzania kuwa wachangia damu salama kwa hiari wa mara kwa mara.

KWA NINI MIMI NA MAMA DAMUDAMU COMPAIGN?​

Mama yetu mpendwa ambaye ndiye Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hasani ametuonyesha kwa vitendo jinsi anavyojali maisha ya watanzania kwa uboreshaji mkubwa alioufanya katika sekta ya afya tena ,kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani yamefanyika maboresho makubwa katika sekta ya afya,ujenzi na upanuzi wa mahospitali,vituo vya afya,zahanati,uwepo wa vifaa tiba na wataalamu wa afya,uwepo wa madawa ya kutosha katika maeneo mbalimbali nchini ni ushahidi wazi unaoonyesha ni kwa kiasi gani Mh.Rais anajali maisha ya watanzania anaowaongoza.

Kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa damu salama kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za afya mheshimiwa Raisi Samia Suluhu Hasani ameamua kutoa bure mifuko inayotumika kukusanyia damu salama katika halmashauri zote 184 nchini Tanzania,hii inaonyesha ni kwa kiasi gani Mama yetu mpendwa anajali maisha ya watanzania.

Kwa kuwa Mama yetu Mh. Samia Suluhu Hasani ameshaonyesha kwa vitendo jinsi anavyojali maisha ya watanzania kwa maboresho makubwa aliyoyafanya kwenye sekta ya afya “KAMPENI YA MIMI NA MAMA DAMUDAMU”itatoa fursa kwa watanzania kusimama pamoja na mama yetu mpendwa na kumtia moyo kwa kazi kubwa na za kizalendo anazozifanya katika kutatua changamoto za watanzania haswa katika sekta ya afya kwa kujitokeza kwa wingi na kuchangia damu salama kwa hiari.

MIMI NA MAMA DAMUDAMU CAMPAIGN.​

Kampeni ya uhamasishaji uchangiaji wa damu salama kwa hiari yenye lengo la kuongezaupatikanaji wa damu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuweza kuchochea utoaji wa huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na ukosefu wa damu salama ya kutosha kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Njia za uhamasishaji katika kampeni hii ni za kitofauti na za kipekee na kampeni nyingine za uhamasishaji wa uchangiaji wa damu wa hiari zilizowahi kufanyika Tanzania,hivo kwa kupitia kampeni hii tunatarajia watanzania wengi kuhamasika zaidi kujitokeza kuchangia damu kwa hiari na kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa damu salama katika vituo vya kutolea huduma za afya hivyo kumtia moyo na nguvu Raisi wetu na kumuonesha kwa vitendo jinsi watanzania wapo pamoja naye na wanaziona jitihada kubwa na za kizalendo anazozifanya katika kutatua changamoto zinazowakabili watanzania haswa katika sekta muhimu ya afya.

MALENGO​

Watanzania kusimama pamoja na Raisi wetu Mama Samia Suluhu Hasani na kuunga mkono jitihada zake za kizaendo za utatuzi wa changamoto zinazowakabili watanzania haswa katika sekta ya afya kwa kuchangia damu kwa hiari.

Kujenga utamaduni mpya kwa watanzania kuwa wachangiaji damu wa mara kwa mara ili kuongeza upatikanaji wa damu salama katika vituo vyetu vya afya na kuokoa maisha ya watanzania.

Kutoa elimu juu ya uchangiaji wa damu salama kwa hiari,kiafya,kijamii,kiuchumi,na kisaikolojia na kuondoa dhana potofu walizonazo baadhi ya watanzania kuhusiana na uchangiaji wa damu salama kwa hiari.

UTEKELEZAJI​

Tumezoea kuona kampeni nyingi za uhamasishaji wa uchangiaji damu kwa hiari zikitumia watu maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii zetu kama wanasiasa,viongozi wa dini,wanamichezo,wanamuziki katika uhamasishaji wa uchangiaji wa uchangiaji wa damu salama,watu hawa wenye ushawishi katika jamii hujumuika na wananchi wa kawaida na kuchangia damu kwa hiari,kitendo cha watu hawa maarufu kujumuika na wananchi wa kawaida na kuchangia damu huwavutia wananchi wengi kujitokeza na kuchangia damu salama kwa hiari.

Kampeni ya “MIMI NA MAMA DAMUDAMU” pia itawatumia watu maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii katika kuhamasisha uma wa watanzania kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ila itawatumia kwa namna tofauti na ilivyozoeleka katika kampeni na matukio mengine ya uhamasishaji wa uchangiaji damu wa hiari.

Kwa kawaida utaratibu wa uchangiaji wa damu unajumuhisha hatua nne​

  1. Kujaza dodoso la mchangia damu na kupima uzito,

  1. Kupima shinikizo la damu,kupima wingi wa damu na kufanya majadiliano kuhusu afya ya mchangia damu,

  1. Mchangia damu kuchangia damu yenye ujazo wa miimita 450,

  1. Baada ya kuchangia damu mchangiaji kupata mapumziko ya dakika 5 na kupewa kinywaji.

Katika kampeni ya “MIMI NA MAMA DAMUDAMU” watu maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii hawatachangia damu kama iivyozoeleka kwenye kampeni na matukio mengine ya uhamasishaji wa uchangiaji damu bali watashiriki moja kwa moja katika hatua ya kwanza na ya nne za utaratibu wa uchangiaji damu.

Wanasiasa,viongozi wa dini,wanamuziki,wafanyabiashara wakubwa,wanamichezo,wasanii,watahusika moja kwa moja katika kampeni hii ya “MIMI NA MAMA DAMUDAMU”kwa kujaza madodoso ya wananchi watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiari na kwa kushirikiana na wataaamu wa afya watu hawa maarufu na wenye ushawishi watashiriki katika kupima uzito wananchi watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiari,(hatua ya kwanza ya utaratibu wa kuchangia damu).

Kwa mfano wananchi wa Dar es salaam watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiari taarifa zake za awali kama jina,umri,jinsia,zijazwe na Mtume mwamposa,halafu uzito apimwe na Diamond.

Pia watu hawa maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii watahusika moja kwa moja kwenye hatua ya nne ya utaratibu wa uchangia damu,ambapo kwa kawaida mchangia damu baada ya kuchangia damu katika hatua ya tatu, hupata mapumziko ya dakika 5 na kupewa kinywaji,wagawaji wa vinywaji katika hatua ya nne watakuwa watu hawa maarufu na wenye ushawishi kwenye jamii.

Kwa mfano wananchi wa Dodoma watakaojitokeza kuchangia damu wakati wa mapumziko ya dakika 5 wapewe vinjwaji na Mandonga,Nandy,Morisson n.k

KUZINGATIA(FOCUS)​

Hatua ya pili na ya tatu katika utaratibu wa uchangiaji damu zinazojumuhisha kupima shinikizo la damu,wingi wa damu majadiliano kuhusu afya ya mchangia damu na mchangia damu kuchangia damu zitaratabiwa na kusimamiwa na wataaamu wa afya kwa asilimia 100.

Kitendo cha watu hawa maarufu na wenye ushawishi kushiriki kwenye hatua hizi mbili za utaratibu wa kuchangia damu,hatua ya kwanza na ya nne itaongeza amasa ya watanzania wengi kujitokeza na kuchangia damu kwa hiari kwa sababu hii itakuwa ni moja ya fursa adimu kwa watanzania kukutana kwa karibu na kupata wasaa wakuonana pamoja na kuongea kwa uchache na watu ambao wanawapenda na kuwashabikia,nafasi ambayo siyo rahisi kuipata kwa njia nyingine.

Kampeni ya “MIMI NA MAMA DAMUDAMU” itatoa fursa hii adimu ya kwa watanzania watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiari ya kuwaona kwa karibu,kuongea na kupiga picha watu wanaowapenda na kuwashabikia.

MATUKIO MENGINEYO KWENYE KAMPENI YA “MIMI NA MAMA DAMUDAMU”​

Kuelezea kwa wananchi watakaojitokeza kuchangia damu mafanikio ya kijamii,kiuchumi,kidemokrasia kimiundombinu,yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hasani kwa kutumia runinga na vipeperushi.

Utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa uchangiaji damu kijamii,kiuchumi,kisaikolojia n.k. Utoaji wa chanjo ya uviko 19.

Photo shoot,wananchi watakaojitokeza kuchangia damu kwa hiariwatapata fursa ya kupiga picha za kumbukumbu na watu wanaowapenda na kuwashabikia.

Burudani za muziki,live band,djs session,celebrites appearances.

MATARAJIO​

Jamii ya watanzania kusimama pamoja na Mh.Raisi Samia Suluhu Hasani katika kuifanya Tanzania yenye maendeleo,upendo,na amani.

Itajenga utamaduni mpya wa watanzania kuwa wachangiaji damu wa hiari wa mara kwa mara na kuokoa maisha ya watanzania.

Wananchi watapata elimu juu ya umuhimu wa uchangiaji damu na kuondokana na dhana potofu walizonazo baadhi ya watanzania kuhusiana na uchangiaji damu.

Itasaidia serikali kupata takwimu za magonjwa mengine kama maambukizi ya virusi vya ukimwi. Utatoa fursa ya watu maarufu kukutana kukutana na mashabiki zao na kubadilishana nao mawazo. Undugu,umoja,mshakamano,na upendo baina ya watanzania utaimarika maradufu.

WALENGWA​

Wizara ya afya,Mpango wa taifa wa damu salama, Chama cha mapinduzi,

Sekta binafsi na asasi za kiraia, Watu maarufu na wenye ushawishi,

Vyombo vya habari na Wananchi wote.

COLLINS AUDAX KARANI, 0656996116, 0788947141,​

Msuli tembo matokeo sungura

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom