Mtu akifa roho yake huenda wapi

jisanja

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,078
2,000
Wasaalam wanajamvi,
sina maana ya kutaka kuchimbua imani za watu na nisingependa hata katika majadiliano watu waanze kukashifu dini za wengine.....
wengi wetu tunaamni kua mwili, nafsi na roho n vitu tofauti....
mtu akifa inakua na maana kua mwili umejitenga na roho...je roho hii iliyojitenga na mwili hua inaenda wap?
 
May 1, 2017
56
125
Roho haifi mwili ndio hufa so ukifa roho inabadilishiwa housing nyingine/mwili kisha inaendelea kula bata wakat wewe unaliwa na minyoo ndani ya gheto la ardhini.
Mkuu umevuta bangi nini,
Mwili ndio unakufa lakini wewe(roho) haufi, mtoa mada anataka kujua mwili ukifa wewe unaenda wapi?
 
smigo4u

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
3,255
2,000
Hujui ile theory ya mtu akifa hapa anazaliwa kwingine?
NB.Bangi natumia sana hasa ukitia ndimu na tui la nazi kachumbali pembeni
Mkuu hii ki2 ya roho kuhamia mwili mwingine ni faith ya ma budha huko na hindu (kwa ujumla buthisms wote) ila kwa dini nyengine not applicable
 
Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
29,448
2,000
Mkuu hii ki2 ya roho kuhamia mwili mwingine ni faith ya ma budha huko na hindu (kwa ujumla buthisms wote) ila kwa dini nyengine not applicable
Jana nimesikia redioni kisa cha mtoto nchini india aliye zaliwa mara mbili na wazazi tofauti hadi na mm nimeamini kabisa..
jina la redio silikumbuki hope itakua Coconut fm au chuchu fm zenji.
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
26,872
2,000
Ukifika kaburini.
Unarudishia roho yako.kama wa motoni adhabu inaanza pale pale,,
Na kama wa peponi raha zinaanza palepale.
Hyo imani ya uislam.
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,310
2,000
Wasaalam wanajamvi,
sina maana ya kutaka kuchimbua imani za watu na nisingependa hata katika majadiliano watu waanze kukashifu dini za wengine.....
wengi wetu tunaamni kua mwili, nafsi na roho n vitu tofauti....
mtu akifa inakua na maana kua mwili umejitenga na roho...je roho hii iliyojitenga na mwili hua inaenda wap?

Kwani huko ulikosikia au kusoma kuwa kuna kutengana wanasemaje kuhusu destinations za mwili na roho?
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,030
2,000
Wasaalam wanajamvi,
sina maana ya kutaka kuchimbua imani za watu na nisingependa hata katika majadiliano watu waanze kukashifu dini za wengine.....
wengi wetu tunaamni kua mwili, nafsi na roho n vitu tofauti....
mtu akifa inakua na maana kua mwili umejitenga na roho...je roho hii iliyojitenga na mwili hua inaenda wap?
Mkuu, suala la kwanza na muhimu kujiuliza na kujibu kabla ya kupata ufumbuzi wa swali lako ni je, unaamini katika roho? je mtu akifa si ndo mwisho wa kila kitu? kama unaamini kuna roho na maisha ya baadae sasa ni namna gani ulimwengu umedhibitisha uwepo wa roho? je roho ni nini na inakaa sehemu gani mwilini na ina kazi gani katika mwili? je wanyama wengine kama paka, ng'ombe, kuku nk wana roho pia?
 
jisanja

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,078
2,000
una maana
Ukifika kaburini.
Unarudishia roho yako.kama wa motoni adhabu inaanza pale pale,,
Na kama wa peponi raha zinaanza palepale.
Hyo imani ya uislam.

una maana jehanam ni kaburi ulilozikwa? na vipi wanaosema kua kuna siku moja ya hukumu.....ambapo wote tutahukumiwa!!
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
56,147
2,000
Mwili- Kaburini
Roho- Mbinguni/ motoni
Nafsi inaendaga Wapi? Maana mwanadamu ana nafsi, Roho na mwili
 
mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
26,872
2,000
una maana

una maana jehanam ni kaburi ulilozikwa? na vipi wanaosema kua kuna siku moja ya hukumu.....ambapo wote tutahukumiwa!!
pale ni mwanzo tu.na kaburi linabana na adhabu zipo.na kiama kipo.parapanda italia na wooooote tutafufuliwa kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho,mbingu zitakuwa milango tutakwenda kwa mungu kuhesabiwa na kulipwa.
 
jisanja

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,078
2,000
Mwili- Kaburini
Roho- Mbinguni/ motoni
Nafsi inaendaga Wapi? Maana mwanadamu ana nafsi, Roho na mwili

kwa jinsi nilivosoma soma kwenye vijarida....mwili n hii cover ya nje...nafsi n uhai/pumzi.....roho n nguvu ya ndan kabisa inayotuunganisha na Mwenyezi Mungu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom