Mtu akifa anaenda wapi?



mkuu wewe ulimwambia yule jamaa kwamba dini za asili zinahusisha kafara kwamba sio upendo - --- mimi nikakupa mfano huo wa kwenye cross, kama ukiona mfano wa kwenye cross upo sawa, mimi sina tatizo ila ukafute ule usemi wa mwanzo mkuu


unataka kuleta double standard za namna gani?
 
ukiweka logic unaonekana huna spiritual mkuu, mimi wangekua wanasema "hilo sjui" nisingekua na shida sana ila kitu kikiwa hakileti mantiki anakimbilia spiritual huu ni utapeli wa wazi
Hii spiritual ya kuambiwa tuikate kabisa mpaka hiyo spiritual ya kweli kama ipo ione wivu ijitokeze iache uoga na kujificha😅
 
naam mkuu
Kabisa na hakuna haja ya kujiuliza ukifa unaenda wapi na wakati ulipotoka yenyewe haupajui .

Yani mimi niweje roho inayodaiwa haifi halafu yote haya nisiyajue ?

Na kama ukifa unakua roho na sio mwili iweje yesu baada ya kufufuka alichomoka na mwili wake kaburini , au ule mwili uliliwa na fisi akachomoka kama roho?
 
Kwahiyo kuna uwezekano tukiwa usingizini sometimes nafsi na roho zetu hutoka kwenda kutembea tembea huko ndo maana hua tunaota ndoto?
 
hiyo ya kufa na kufufuka mimi siwezi ikubali mkuu ---

kama hatukujadili kabla ya kuja hapa duniani, mi naona watu wakaushe tu 😁
 
Hivi vitu vyote unavyovitaja haviwezi kuwepo baada ya kifo. Viumbe hawana hisia, ndoto wala akili wakishakufa.
Roho ni dhana tu. Hakuna kitu kinaitwa roho.
Hata kingekuwepo, wewe unajuaje kama binadamu ana roho ila wanyama wengine hawana?
 
Hivi vitu vyote unavyovitaja haviwezi kuwepo baada ya kifo. Viumbe hawana hisia, ndoto wala akili wakishakufa.
Roho ni dhana tu. Hakuna kitu kinaitwa roho.
Hata kingekuwepo, wewe unakuaje kama binadamu ana roho ila wanyama weng



1. Mhubiri 3:19–21



Biblia zenyewe wanazijua basi , hapo unapigia mbuzi gitaa tu.
 

Meneja wa makampuni nimekuunga mkono 100 kwa 100 pamoja na kuwa umeandika kwa kutumia Biblia.
Hata kwa mujibu wa Quran utaratibu ni huo huo japo umeelezwa kwa namna tofauti kidogo. Watu waovu wata anza mateso tangu ile siku wamezikwa hadi siku ya hukumu na baada ya hukumu mateso yataendelea...
Watu wema wata anza kufurahia Neema ya Mungu tangu ile siku wazikwa na hata baada ya hukumu watahamia peponi kuendelea kufurahia Neema za Mungu.
SIKU ZA MWISHO ZITAKUWA NGUMU SANA JAPO WANADAMU WANACHUKULIA KIMCHEZO MCHEZO (Miaka 60 -80) TULIYOPEWA HAPA DUNIANI NI MICHACHE SANA. Hatujiulizi waliokufa miaka mamia iliyopita wapo wapi? TUMUOMBE MUNGU ATUPE MWISHO MWEMA!!!
 
Kwahiyo kuna uwezekano tukiwa usingizini sometimes nafsi na roho zetu hutoka kwenda kutembea tembea huko ndo maana hua tunaota ndoto?


Ndoto ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko na hisia ambao unatokea akilini, kwa kawaida bila makusudi, katika hatua fulanifulani za usingizi
brain is randomly playing back memories and thoughts, and then trying to make sense of it all, creating a story or scenario, which is the dream.
 


1. Mhubiri 3:19–21




Biblia zenyewe wanazijua basi , hapo unapigia mbuzi gitaa tu.
Naomba tusome hii mistari ya aya nzima:
Mhubiri 3
1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa;

3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza;

5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia;

6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa;

7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena;

8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.

9 Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?

10 Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.

11 Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.

12 Mimi najua ya kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi, na kufanya mema maadamu wanaishi.

13 Tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote.

14 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.

15 Yale yaliyoko yamekuwako; na hayo yatakayokuwako yamekwisha kuwako; naye Mungu huyatafuta tena mambo yale yaliyopita.

16 Zaidi ya hayo, nikaona tena chini ya jua ya kwamba, Mahali pa hukumu upo uovu, Na mahali pa haki upo udhalimu.

17 Nikasema moyoni mwangu, Mungu atawahukumu wenye haki na wasio haki; kwa kuwa kuna wakati huko kwa kila kusudi na kwa kila kazi.

18 Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.

19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.

20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

21 Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?

22 Hivyo nikaona ya kwamba hakuna jema kupita mwanadamu kuzifurahia kazi zake; kwa sababu hili ni fungu lake; kwa maana ni nani atakayemrudisha tena ili ayaone yatakayomfuata baadaye.
 
Sisomi utumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…