Mtoto wangu amerithi tabia yangu ya utotoni ananipa gharama kulipa vitu vya watu kila siku

kijanamtanashati

JF-Expert Member
Aug 22, 2014
516
890
Nakumbuka mimi nilipokuwa na umri 6-13 nilikuwa mkorofi natukana sana watu sichagui mkubwa au mdogo, nilikuwa na matusi hatari na kupenda kurushia watu mawe, pale mtaani wakawa wanamwita mama yangu 'mama mawe'. Hadi watu wazima wakawa waniogopa kwa matusi. Mtu akinichokoza mbona ataisoma namba yeye na familia yake, nakusanya mawe mengi halafu naenda kurusha juu ya bati na mlangoni kwao basi huko ndani zinatoka sauti 'wee mama mawe mwao ameanza mkataze mwanao'.

Nyumbani kulikuwa na shamba la mipapai basi majirani wakija kuomba mapapai kama mama hayupo wakinikuta mimi wanagairi hata kuomba. Au wakimkuta mdogo wangu na yeye anawaambia muombeni kaka, basi wanagairi utasikia 'mtoto ana matusi yule unatafuta kuporomoshewa matusi'. Kuna kipindi mpaka wazazi wa pale mtaani waliwakataza watoto zao wasicheze na mimi. Ila baadae nilibadilika baada ya kumaliza shule ya msingi nikawa mtoto wa kawaida mpaka watu wakawa wanashangaa.

Sasa hivi nina mtoto wa kiume miaka 5, kila siku naletewa kesi zake amevunja vitu vya watu kwa mawe. Ugomvi wake wa mawe akichokozwa anaporomosha mawe. Aliwahi kuvunja kioo cha gari cha watu nikaletewa kesi ilinibidi nilipe. Amevunja vioo nyumbani kwa majirani mara tatu na jana amempasua mtoto wa jirani kichwani kwa jiwe mpaka ikabidi tumpeleke hospitali. Mama ake anampiga sana lakini hasikii, anapigwa leo kipigo cha mbwa mwito kesho anarudia tena kurusha mawe akichokozwa. Mimi pia nimeshampiga mara kadhaa, nimemtishia kumpeleka polisi lakini wapi. Ukimuliza kwanini unapiga watu mawe anajibu 'wenyewe wananichokoza'. Mama yake anadai tumpeleke bording labda atabadilika lakini mimi sikubaliani na wazo hili, mtoto wa miaka 5 bado mdogo sana kukaa mbali na wazazi. Halafu watoto huko bording wanaharibika sana hasa hawa wa kiume. Wakuu nisaidieni nifanye ili huyu mtoto aache hii tabia maana huko anakoelekea anaweza kuja kuua mtu kwa mawe.
 
Malipo ni hapahapa dunia, kuwa mpole mkuu ufidiefidie japo kidogo hasara uliyosababisha wazazi wako.
Mungu aliposema nitakupa wa kufanana nawe hakumanisha mke tu. Sasa imekua kwa mtoto kafanana nae vizuri sana

Pole sana Baba Mawe

Uzuri unajua tatizo linatokea wapi. Hiyo ni hatua ya kwanza kulitatua.

Msalimie Bibi Mawe(mamaako) mwambie umempokea jina sasa wewe ndo baba Mawe mtaani na mkeo ndo mama mawe
 
Una moja kati ya haya matatizo manne. Na yanarithiwa. ADHD, Oppositional Defiant Disorder (ODD), Asperger’s Syndrome, or a mood disorder. Mtoto wako amerithi hiyo hali.

Kinachofanyika ni kwamba, anakuwa amevurugwa kimawazo (mood and emotions). Na akivunja kitu, ndio anapata ahueni ya muda mfupi. Ndio sasa haachi kuvunja. Sababu inampatia nafuu ya hiyo hali.

Ni genetic na issue ya kisailolojia. Inabidi utafute psychiatrist akusaidie hapo.

Tanzania watu wanasema ukorofi wa mtoto nk. Hapana. Ni chemical imbalances ndani ya miili yenu haziko sawa.

Hata sasa hivi ww umekuwa lakini najua ni mtu wa HASIRA SANA HAPO HOME KWAKO. Na sometimes hata sasa hivi umri umeenda lakini najua bado unavunja vunja vitu sometimes kwa hasira.
 
Mbinu ulizotumia wewe kuacha kuwa mkorofi zitumie kwa mwanzo na yeye atabadiliki
Mimi sikutumia mbinu yoyote nilijikuta tu naacha kuwa mkorofi nilipoanza shule ya secondary. Nikisema nimuache na yeye hadi afike secondary bado ana miaka kama 7, nikimuacha si ataua mtu au kuzidi kuniletea hasara ndani ya hii miaka 7
 
Baba Mawe haraka ya nini? Subiri mpka amalize std 7 atatulia tu!
 
Usiwaze mkuu Mungu kaona akuonjeshe tu raha uliyokuwa unawapa wazazi wako enzi zako...sio kesi wala nini
 
Una moja kati ya haya matatizo manne. Na yanarithiwa. ADHD, Oppositional Defiant Disorder (ODD), Asperger’s Syndrome, or a mood disorder. Mtoto wako amerithi hiyo hali.

Kinachofanyika ni kwamba, anakuwa amevurugwa kimawazo (mood and emotions). Na akivunja kitu, ndio anapata ahueni ya muda mfupi. Ndio sasa haachi kuvunja. Sababu inampatia nafuu ya hiyo hali.

Ni genetic na issue ya kisailolojia. Inabidi utafute psychiatrist akusaidie hapo.

Tanzania watu wanasema ukorofi wa mtoto nk. Hapana. Ni chemical imbalances ndani ya miili yenu haziko sawa.

Hata sasa hivi ww umekuwa lakini najua ni mtu wa HASIRA SANA HAPO HOME KWAKO. Na sometimes hata sasa hivi umri umeenda lakini najua bado unavunja vunja vitu sometimes kwa hasira.
Kweli mkuu mimi ni mtu wa hasira lakini mara nyingi nafanikiwa kujizui hasira zikinipanda, sivunji vitu kwa sasa, hizo mambo nilikuwa nafanya utotoni. Huyu dogo nikimpeleka kwa psychiatrist atapona kabisa hili tatizo?
 
Problem in tanzania psychiatrist hawajabobea sana. Also inategemea how much imbalance he has physiologically. Ukimpata mzuri na aliyebobea atakusaidia. Hata asipopona full, itapungua kwa asilimia kubwa sana kwa namna ambayo haita-affect maisha yake na ya wale waliomzunguka.
 
Back
Top Bottom