Machozi ya mtoto wa jirani yangu yamenisikitisha sana

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Jun 20, 2022
1,215
2,992
Habari muda huu Wana JF,

Kuna kisa nilileta hapa kuwa mtoto wa Jirani yangu amezoea kuniita baba.

Jana majira ya saa 5 asubuhi, ilibidi niwaage Jirani zangu baadhi ambao tumeishi vizuri muda wote niliokuwepo hapa, sehemu niliokuwa naishi Ina nyumba 3 Ila ziko kwenye fensi moja Jirani yangu mwenye yule mtoto alionizoea kuniita baba, anaishi nyumba ya pili Kati ya hizi 3 tuko karibu Sana Mana nyumba zetu zinatazamana kila siku lazima tuonane, tumezoeana kiasi sababu me ni mcheshi Sana, salamu nyingi na mazoea kwa limit.

Tukawa tumekutana nje baada ya salamu, ikabidi nimwambie A to Z kuwa naondoka mazingira haya Kuna emergency imetokea job kwa muda sitakuwepo hapa na wife anarudi kwa muda home, kwa ufupi tunahama mazingira haya.

Baada ya kumpa taarifa iyo niliona Kama amekosa amani hivi ukicheki tulizoeana, nadhani unaelewa kuagwa ghafla na mtu mliozeana Kuna hali flani hivi inatokea ya huzuni ukicheki mlikuwa mnaishi vizuri.

Ikabidi anipe kheri na baraka nyingi uko niendako (tumpe Jina O la mtoto wake) akasema....Maskini mwanangu O alishakuzoea sijui itakuwaje asipokuona.

Nikwambia tuko pamoja leo tumekutana hapa tumeishi vizuri, kesho tunaweza kukutana sehemu nyingine na tukawa majirani tena kwa Mara nyingine, akacheka😁.

Ila naamini O mwazoni itakuwa ngumu Ila badae atazoea ni utoto tu akipata uelewa atanisahau na maisha yataendelea. Maongezi mengine yakaendele tukaishia hapo akanipa na contact zake.(Nina heshima Sana na wake za watu mazoea kwa limit)

Leo majira ya saa 7 mchana baada ya wife kutangulia home, nikawa nahamisha vitu kadhaa vilivyobaki ili niweze kukabidhi nyumba ya watu, ghafla nashangaa yule mtoto akaja kunikumbatia huku analia baba (uncle) mbona unaniacha wakati nishakuzoea (anajua kuongea kwa kiasi chake)

Mama amenimbia unaondoka urudi tena ikabidi nimbembeleza pale uongo na ukweri akatulia, nikampa na hela ili anyamaze kulia.

Kufupisha story muda wa kuondoka yule mtoto akawa analia Sana kila nikijitahidi kumtuliza akawa hataki anataka tuondoke wote, ikabidi mama yake aje kumchukua kwa nguvu akamfungie ndani huku akilia Sana, mama yake O nikampa 30k amnunulie zawadi 0 ya sikukuu nikamuaga na kuondoka.

Moyo wangu uko na ubaridi leo sijui O yuko na hali gani, Ila Sina jinsi maisha lazima yaendelee.

Ulikuwa rafiki yangu wa muda wote Princess O nakupenda Mungu akujalie afya njema na ubaki salama inshallah 🙏

Nb: Mume wa Jirani yangu anakujaa Mara moja moja na tunaishi vizuri ni mtu powa Sana.

Thread: Mtoto wa Jirani amezoea kuniita baba
 
Sawa umetoa 30k 0 apate zawadi ya pasaka, ila nakuhimiza fanya hivo hivo kwa wazazi kama wapo, au ndugu yako yoyote mkuu mwenye uhitaji walau wafurahie pasaka

Kama una ndugu kijijini mpe priority aisee Kule maisha ni magumu! Aisee kipindi Cha mvua nilifanya kilimo nikawa nimeweka nyapara asimamie kazi zangu aisee Kule maisha ni magumu, ukipewa kazi ya buku Tano lazima jasho litoke mpaka kwenye Tako, nikajifunza kitu, huku mjini tunajifanya wa kishua kutoa favours kwa wadada izi 50 50 wakati Tuna ndugu wengi kijijini wanataabika

Naamini hukosi ndugu kijijini ambae ukimtumia 30k atapata furaha isiyo na kifani na milango ikafunguka!! Ni ushauri tu mkuu maana najua pesa ni za kwako usije nishukia kama mwewe
 
Umeandika ukweri mkuu natamani kila member humu apite kusoma comment yako.

Ndugu wapo na tunawasaidia tunapoweza mkuu,Ile 30k nimetoa kama ukumbusho anaweza akamnunulia shati au sketi ya O ikawa Kama kumbukumbu kwao.
Sijui Kama nimekujibu kwa kueleweka mkuu
 
Back
Top Bottom