7 years sasa kitu kinaahirishwa na siku zinavyokwenda najihisi kuwa huru zaidi nikiwa single namna hii.......ya nini mtoto kzualiwa safari za kwa mkemia mkuu zianze.....kumbuka hapa hatuangalii mtoto tu......kuna kisonono,Gono,Pangusa na Ukimwi....Usisogeze goal mbele kisingizio kubambikiwa mtoto labda kama hujadhamiria kuoa kutokana na mambo mengine.
Kuna haja ya kuwa mkali(siyo cris brown style) kwa mamaa kuwa kuna DNA na akikubambikia mtoto utapata ukweli ili ajue mumewe moto chini!
Hakuna haja ya kuzini nje wakati umo kifungoni ila mambo yanatokea sana kwenye mazingira tunapoishi!..
Nilianza 2002 nakumbuka niliona demu wa msela anachemka na watu nikaona woote wako hivyo.....sitaki presha....nikavuta aka 2 nakuta bado wako vile vile tena ndio kama wamechanganyikiwa....ikavutwa mpaka 2008-now naona mauza uza tu nimeweka hapo labda iwe inanikumbushaMake sure unaoa hiyo 2010, eti mwanaJF Yo Yo bwanaharusi mtarajiwa!..I can imagine maana utakuwa unawaza DNA DNA tu! Haitokei kwa kila mtu pia usimcheke mtu kesho yakakukuta halafu uelewe vizuri kashkash za maisha!..
Hello,
Nilitoa habari yangu katika forum hii na kupata maoni mbalimbali kutoka kwenu wadau.
Napenda kuwashukuru wote mliochangia na kunishauri, kwa wale walionipa pole asante sana. Ni kama mtu aliyepata ajali vile kwa hiyo nakubali pole zenu na hata wale waliokuwa wakali kidogo.
Kwa sababu fulani sitaweza kuendelea kuchangia katika hii mada. Ila napenda kuwaeleza msimamo wangu baada ya kupata ushauri wenu.
Msimamo wangu hautokani na sababu hizi hapa chini:
-Kujiona mkosa sana;
-Kwa sababu mimi ni mwanamke;
-Nina woga wa maisha ya baadae;
-Ni selfish na sifikirii wengine, nk
Nimeamua kusema hili kwa sababu tu NAMPENDA MUME WANGU na siwezi kuendelea kumdanganya maisha yote, hivyo NITAMUELEZA ukweli. Hata hivyo nitatazama muda muafaka na nitazingatia ushauri wenu mliotoa wa jinsi ya kuendea jambo hili. Nitakapokuwa tayari, hapo tu ndio nitafanya hivyo na nitaheshimu uamuzi wake atakaoutoa. Sitazamii lolote, Mungu atanisaidia.
Siwezi kuahidi kama nitarudi kuwaeleza matokeo kutokana na mazingira, ila nitajaribu kama itawezekana. Nashauri muwe waangalifu katika maisha yenu, hasa katika mambo kama haya.
ASANTENI SANA.
Acha kumuingiza mwenyezi Mungu kwenye upuuzi wa namna hio......shetani ndio ana play part hapo...Dada amini usiamini utashangaa jinsi Mungu atakavyokupigania maana msema ukweli ni mpenzi wa Mungu,na katika hili Mungu ataangalia dhamira yako usishangae mume wako akakuonea huruma kuliko ulivyo fikiria maana umesumbuka kwa muda mrefu.
Lakini mimi ningekuomba swala hili liwe lako na mumeo iwe siri ya watu wawili,
hao wazee waheshima kumbuka binadamu tulivyo ukiniona mimi msiri wako kumbuka na mimi nina mtu ambaye ni msiri wangu tena ndo maana wahenga walisema Siri ni ya mtu mmoja/fanyeni hilo wewe na mmeo kwanza nyie ni mwili mmoja maumivu yako ndo maumivu yake japokuwa kwa namna tofauti.
Acha kumuingiza mwenyezi Mungu kwenye upuuzi wa namna hio......shetani ndio ana play part hapo...
7
Nilianza 2002 nakumbuka niliona demu wa msela anachemka na watu nikaona woote wako hivyo.....sitaki presha....nikavuta aka 2 nakuta bado wako vile vile tena ndio kama wamechanganyikiwa....ikavutwa mpaka 2008-now naona mauza uza tu nimeweka hapo labda iwe inanikumbusha.....kisa ya Saleh wa clouds nimeisikiliza imenifanya nife moyo kabisaaaaa
Sikiliza Dullonet Tanzania | Sikiliza Hekaheka toka mtaani na CloudsFMHicho kisa cha Saleh sikijui, nipe hints kidogo nipate mwangaza!..
Sasa Mungu hapo anahusika vipi kwenye uzinifu huo? unajua kwenye dhambi Mungu hayupo yuko Iblisi.....YoYo
Wakati shetani ana pray part hapo Mungu alikuwa wapi?.Ukidanganywa na shetani unarudi kwake au una kwenda kwa Mungu kutafuta suruhisho?.Mungu pekee ndo anaweza kuleta suluhisho.
YoYo kama kungekuwa hakuna kukosa basi kusingekuwa na kutubu, kwahiyo mungu alivyotuumba alijua kuwa tutakosea na ndipo toba ikawepo, hivyo binadamu anapokosea kimbilio lake ni kutubu na kumshirikisha mungu katika toba zake!!
kuhusu kuogopa kuoa kwa mikasa ya watu sio suluhisho, muombe mungu akupe mke mwema nawe uwe mume mwema ni hilo tu, hao wenye watoto na wake za watu pengine ni waume za watu au wanaume kama wewe na pengine miongoni mwao wapo wanawakosoa na kuwahukumu akina maindamainda!!
Maindainda,
Hukupashwa hata kusema jambo hilo humu. Funga mdomo wako bibie. Baki na Mungu wako. Ukifikiri ukweli ni ukweli always, shauri yako hata Yesu aliulizwa 'ukweli ni kitu gani?' Na chamoto alikiona. Akalia sana kwa uchungu. Nakushauri, acha kabisa kuongelea zaidi suala hilo unless umechoka kuishi happily ktk ndoa yako hiyo. DON'T TELL HIM
god eeeh hii mada imenishangaza na imeniuma sana na imeniacha hoi
kwa ushauri wangu moja ulikosea sana kujihusisha na mapenzi nje ya ndoa na hayakuwa salama sikushauri umwambie mmeo kwani hujui ni jinsi gani atalipokea hili ..
pili nini kilikutuma ukamwambie huyo mwanaume wako wa nje una mimba yake ..kosa la pili ambalo hukufikiria ulikuwa unampenda saana au???
Ni mwanzo wa mfurugiko wa ndoa yako na umesema mmeo anakupenda sana utakapoliongea hili kwa mmeo ..ndugu watakapojua itakuwaje ..
jamii inayokuzunguka
dada umeniiacha hoi pole sana na tatizo hili ni tatizo ..mwache mtoto aendelee kutunzwa na huyo babaake anayemjua
Vp mpaka leo hii hakurudi kutuambia kipi aliamua? bado tunaendelea kutoa ushauri? au hii ni kwa faida ya wengine?
Vp mpaka leo hii hakurudi kutuambia kipi aliamua? bado tunaendelea kutoa ushauri? au hii ni kwa faida ya wengine?
Vp mpaka leo hii hakurudi kutuambia kipi aliamua? bado tunaendelea kutoa ushauri? au hii ni kwa faida ya wengine?
Huu ni uhamuzi mbaya, na madhara yake ni makubwa kuliko faida, msishangae mkisikia hawa mabwana wawili kwa sasa wanaburuzana mahakamani au wameisha uana,alishatoa uamuzi wake na akasema atasema mwezi unaofuatia, alitoa hiyo post April kwa hiyo inawezekana mumewe tayari amesha jua ukweli....labda tumuombe Mainda aje hapa kutu habarisha hitima ya hii soo
Ndugu na rafiki zangu wa Jamii Forums,
Naomba msaada katika jambo hili.
Nina ndoa ya kama miaka kumi. Nina mume wangu ambae najua ananipenda, nami pia ninampenda. Miaka kadhaa iliyopita nilikutana na jambo ambalo limenitia simanzi sana na sijui hata nifanyeje, kuna wakati siamini kama ni jambo lililonitokea mimi maishani.
Kwa kifupi ni kwamba nina mtoto ambae najua si wa mume wangu! Amelelewa na huyu baba bila kujua kwa upendo mkubwa, kulipa ada za shule na mahitaji yote. Kusema kweli haijakuwa jambo rahisi maana kila anapomuita baba mimi moyo wangu hujaa simanzi. It happenned that I was at a wrong place with a wrong guy and it happenned. Si tabia yangu na wala sikujidhania kwamba siku moja naweza kuisaliti ndoa yangu. .
Huyo baba mwenye mtoto ana mke, simpendi kimapenzi na wala hatuhusiani tena, ikiwa ni pamoja na kuwa hajawahi kumtunza mtoto huyu ingawa anaweza. Sikutaka afanye hivyo. Tatizo ni kuna wakati fulani aliwahi kusema kuwa atakuja kumchukua mtoto wake siku moja, kivipi sijui. Naona ana fujo maana sioni uwezekano wa jambo hili labda avunje ndoa yangu kwanza. Sio kutokana na sababu hii ila kwa muda mrefu tangu nikiwa na mimba ile nimetaka kumwambia mume wangu ukweli lakini nimeshindwa. Maisha ya masikitiko na kuwaza jamani naona nashindwa na nataka nimwambie ukweli na atoe hukumu yake.
Naomba mnishauri hasa wanaume- ingekuwa wewe ungefanyaje? Nimwambie au niache?
Hili ni tukio la kweli, naomba ushauri usiwe katika yafuatayo:
1. Kusema kwamba mimi msaliti na mke mbaya-hilo nalijua na wengi wenu mnayajua haya na haitanisaidia sana.
2. Kusema nimefanya ngono zembe nikapime ukimwi - nimepima na sina
Naomba msaada.