nipeni mistari ya kuongezea basi wakuu!!
Nimeanza hivi!
Naongea na cha usiku, Mtoto wa ngeleja
mwambie mshua, mbona giza kila siku lini litaisha?
Mtaani umeme hakuna, kazi zimesimama
Bila umeme kuwaka, uchumi wetu unakwama.
Dogo, mwambie mshua, tumemchoka!
Naanza kwa ustaarabu, kwa kumtungia wimbo.
Aondoke kwa taratibu, kabla hatujamtoa kwa fimbo
dogo, babako anazingua, mwambie atoke.
Hakuna alichosaidia, tutaja mtoa kwa mateke.
Mchana kiza usiku kiza, asituletee mapepe.
Ametudanganya richmond, dowans na sasa simbion
bado umeme hatuuon, hadi sasa tupo gizani
dogo mwambie mshua aende, uwezo wake mdogo
ajjaribu kazi ingine, na akili zake ndogo
aache kutudanganya, asituone wote madogo.