Mtoto wa Msukuma apata 'A' zote kwenye matokeo ya kidato cha pili

Pongezi nyingi kwake, aendelee na jitihada hiyo hiyo hadi chuo kikuu.
Huyo ndio kiongozi wetu bora wa badae.
anafaa kuigwa na watoto wengine.
 
Kama mbunge kweli anatetea wanyonge,na ameona ni vyema kumpeleka mtoto wake shule yenye mkondo wa kiingereza(English medium school),basi ni vyema akapeleka muswada binafsi bungeni "Serikali ibadilishe mfumo wa elimu ili Watanzania waweze kunufaika na shule kuwa na michepuo ya kiingereza",na aombe kujua ni lini Serikali itafanya utafiti na tathimini ya namna ya kubadili mfumo wetu ili nchi iwe na vijana wenye kuweza kushindana kimataifa katika kutafuta maisha na fursa katika nchi za mataifa mengine.
 
Mmmmh hili hapana.
nimesoma shule za mchanganyiko, wengi wanachelewa kupevuka na kujua nini kilichowapeleka kule, wengi wanawaza wakimaliza wajiunge na jeshi tuu.Halafu wengi wao wanapoteza muda kufanya mambo ya kuonekana wao ni wajanja kwa wanawake,nawazungumzia vijana wa kiume
 
Back
Top Bottom