Mtoto wa miaka nane auawa Njombe

Mtoto wa miaka nane auawa Njombe

NJOMBE WAMEUA MTOTO TENA.


Kuna taarifa zinasambaa kwamba kuna mtoto ameuwawa tena kijiji cha matembwe Jimbo la Lupembe na timu ya ulinzi na usalama ya Mkoa imehamia huko usiku wa Leo kwa ucgunguzi

Kwa taarifa zaidi nitawajuza

Updates
Huyu mtoto anaitwa Rachel, Ni mtoto wa miaka nane.
Alipotea majira ya mchana, walimtafuta Bila mafanikio mpaka ilipofika jioni waliukuta mwili wake msituni akiwa ameuwawa na kutolewa macho na sehemu za siri.Ros

my take
Hawa wauaji ni watu majasiri sana, pamoja na Naibu Waziri wa mambo ya ndani kuwepo hapa siku za hivi karibuni na kukemea kwa nguvu na kuahidi watakiona na mtema kuni watakaokamatwa Bado Bila uoga wanaendelea kuua.



Sent using Jamii Forums mobile app

Rose nilikueleza kuwa maombi hayasaidii sababu hawa watu hawana dini. Hapa ni nyumba hadi nyumba kufanya searching.
 
Kwanini waganga wasifutiwe leseni zao hawa ndiyo chanzo cha machafuko kwenye jamii, albino wanauliwa sababu ni hawa waganga watoto, watu wazima wanauliwa sababu ni hawa kisa masharti yaokwa ntu mwenye kutaka utajiri wa haraka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishangaa sana..
Badala uite viongozi wa vijiji na vitongoji.... Uite wachungaji na wainjilist wa level ya chini kabisa unawaita kina Dr Mwandulami na Dr Mkongwi...... Hii nchi....... Ila naumia kwa vile Njombe is my home land
 
Mnaweza kuwa mnabwabwaja hapa kumbe hao jamaa zenu muaonao bungeni,wake kwa waume njia hizi ndio zimewafikisha hapo.

Sasa inapombidi kupambana na jini analolijua inakuwa ngumu kidogo maana,usiku litamfuata akiwa amelala.

Kuna mambo duniani hapa ni magumu sana,kama sio yatajiishia kiasili kama yalivyokuja basi labda neema ya Mungu iingilie kati.rip watoto,njia ni moja ya wote.
 
Tumia akili acha ushabiki wa kishamba, nani asiyejua kuwa kuna mauji makubwa yanayosimamiwa na watawala wa awamu hii?
Uko chini ya kiwango. Nilidhani utajilazimisha kuinuka. Hivi unasoma sekondari gani wewe?
 
Why haya mambo hutokea kila mwaka Wa uchaguzi au tunapokaribia uchaguzi!? It means wanasiasa wetu si waadilifuama!? Maana tulikuwa tunalia na watu wenye ulemavu Wa ngozi tukajenga mpaka hostels kuwahifadhi, sasa watoto wetu tuwaweke wapi!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutegemea uchawi ili kufanikiwa kwa kukatisha maisha ya wengine eti ndio utafanikiwa ni uvivu wa kufikiri na uvivu wakujituma katika kujiletea maendeleo.

Pia kuna haja ya serikali kuwatazama kwa jicho la tatu hawa waganga wakienyeji.

Mauaji haya yanafanyika kwa maelekezo kutoka kwa waganga wakienyi hivyo serikali inatakiwa iwe macho na jamaa hawa ikiwezekana itangazwe kupiga marufuku waganga wakienyeji nchi nzima.
 
Jaman let us pray for innocent children Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni, utupe leo mkate wetu wa kila siku, utusamehe makosa yetu kama tunavyowasamehe walio tukosea, usitutie ktk kkishawishi lkn utuopoe na yule muovu Amina.
 
Sio kila sehemu unaleta habari za Uchama na siasa fwala wewe...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kawaida yake Lissu ataanza "Serikali ya Magufuli inaua watu inawaweka kwenye viroba na kuwatupa baharini. Na sasa imeanza kuua watoto, kuwang'oa viungo na kuwatupa msituni, na hakuna uchunguzi unaofanyika" Kwani ya Rufiji na haya yanatofauti gani?
 
Mh. Rais wangu, kamata waganga wa kienyeji na wachawi wote mkoa wa Iringa na ukianzia na Njombe, piga ndani, hutaona tena mauaji haya, huu ni ushirikina mkubwa huko Iringa.. Dawa ni kuwamaliza wachawi wanaojiita waganga wa kienyeji.. [emoji15][emoji25][emoji24]
Mimi ndiyo nilishauri hivo

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom