Mtoto wa miaka 2 anyongwa Geita!!

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,636
37,850
Wakuu,

Kwenye nipashe asubuhi leo nimepata habari ya kusikitisha ya watoto wa miaka 12 mpaka 13 wamemnyonga mtoto mwezao wa miaka 2

Kisa kimetokea wakati watoto hao wakicheza Kaka wa marehemu (12) alituhumiwa kuiba goroli na wenzake 2 wa rika lake.

Wale rafiki zake wawili wakamkimbiza lakini yule mtuhumiwa (kaka wa marehemu) akawazidi mbio akatokomea.

Basi wale Vijana kwa hasira wakamrudia mdogo wake ( 2) wakamchukua na kumpeleka kichakani wakamfunga kamba shingoni wakamninigiza hadi kifo chake, alipofariki wakamfungua kamba wakambwaga chini wakampiga na tofali wakatokomea zao.

Mama mzazi wa marehemu amethibitisha mauaji haya.

Mwenye habari zaidi atupatie kwamba je vijana hawa wamekamatwa?
 
Pole sana wazaz wa mtoto marehemu. Hii inanikumbusha mbali sana kwani mwaka 1992 nikiwa na umri wa miaka kama 10 hv nikaenda kuoga ziwa nyasa na mdogo wangu mpendwa Jonathan Napiya (7). Ghafla kwa mapenzi ya mungu dogo alikufa kwenye maji, alipoopolewa kashakufa almanusura niambiwe kwamba mie ndie nimeua. Nashukuru mungu ndugu walijua kwamba ni mungu ndo anapanga juu ya kfo.
 
Mungu wangu...yani watoto wadogo wanakua wakatili kiasi hicho!!!!??!
RIP kamalaika ka watu kasiko na hatia!!Yani nimesoma hii habari mwili ukasisimka!!Maskini!
 
Inasikitisha sana
umri walionao kufanya mauaji ni mbaya
masikini kichanga naamini upo peponi

 
Back
Top Bottom