Njiapanda: Mtoto wa mke wangu niliyemlea tangu ana miaka 2 ameenda kutoa mahari bila kunishirikisha

Chabrosy

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
2,618
3,083
Habari wana jamvi!

Natumaini ni wazima wa afya, ni hivi niende kwenye mada husika hapo juu mimi ni kijana mwenye umri was miaka 39, nina mke na watoto 6 ila mke wangu nilimkuta akiwa na mtoto wa kiume wakati tunaoana mwaka 2002, jumla ukijumlisha tuna watoto 7.

Kiukweli huyo kijana mtoto wa mke wangu (my step son) nimemtafutia kazi Serikalini now anafanya kazi vizuri, alipata kazi mwaka juzi akiwa na miaka 19 tu, huyu kijana nimemlea mimi tokea akiwa mdogo maana nilianza kuishi na mama yake dogo akiwa na miaka 2.

Kwanini nimekuja kwenu leo, mke wangu anajua simuelewi, amekuwa msiri sana na huyu kijana wake. Wanafanya vitu vya siri siri, sishirikishwi kwa chochote nikiwa kama mzazi. Kuna siku kijana kamfata mama yake waende wakanunue eneo mimi sijaambiwa sikumaind, maana ni jambo la kawaida tuu.

Kubwa kuliko ni kijana kaenda katoa mpaka mahari, lakini kijana mimi hajaniambia kama baba yake ambae nimemlea tokea mdogo, mpaka kazi mimi ndio nimemtafutia lakini hanishirikishi kwenye jambo la kuoa.

Nilipochoka wametoa mpaka mahari lakini taarifa sijapewa ni hivi mimi niko nao mbali, mimi niko mkoa wa Arusha kikazi, saizi wife na familia wapo Pwani, Kibaha. Kijana wangu kazi anafanyia Morogoro huyo kiukweli hiki kitu kimeniuma sana.

Nikifikiria huyu mke wangu tulikuwa tunapendana sana na tumetoka mbali sana, tokea kipindi iko tunaishi Iringa nilimkuta akiwa dada wa kazi za ndani ana mtoto mimi nikiwa msaidizi pia kaka wa kazi za ndani. Ila tukapendana hivyo hivyo Mungu akanisaidia nikapata ajira mwaka 2000, 2002 tukaoana tukiwa wadogo sana.

Tena nilimuoa hata ile ruksa ya mimi kupata kutoka kazini sikupata ruksa ya kuoa lakini nilimuoa hivyo hivyo mpaka leo tuna watoto 7 ukijumlisha na wake, lakini leo kijana wake mambo yanakuwa mazuri wanaanza nitenga nashindwa elewa nimewakosea nini!

Maana mimi huwa sishindi nyumbani naweza nikakaa miezi hata mitatu sijarudi home hii yote kutokana na nature ya kazi yangu ambayo kijana wangu my step son amenirithi, kiukweli naumia sana.

Yani tunaelekea uzeeni wife ndo ananza nificha hivi, mke wangu alikuwa na tabia nzuri tuu nashindwa elewa izi tabia kazitoa wapi za kunificha sijawai mfumania ajawai nifumania sina mtoto wa njee sina mwanamke njee japo nilishawai kuwa mchepuko nilipigaga mara mbili tatu onetime nikatemana nae lkn mke wangu hakujua sasa nashindwa kuelewa why wife amebadilika hivi?

Kitu kingine kijana huyu nikimpigia simu hapokei au akipokea hana story na mimi kama zamani kiukweli hiki kitu kina nitesa sana yani natamani hata nistaf mapema ili niwe karibu na wife lakini mimi kustaafu bado mpaka mwaka 2045.

Kiukweki sina furaha natamani nirudi nikakae karibu na familia yangu sijawai fikiria kama mapenzi yatanitesa hivi jinsi mm na wife tulivyopendana sijui nimemkosea wapi mpaka amenitenga ananificha baadhi ya vitu yeye na kijana wake.

Kitu kingine nasikia wife anajenga huko Mbande lakini hajaniambia. Hii sina uhakika maana nipo mbali naye. Ukiangalia kama miradi mingi mimi na wife tumeshirikiana ifanya na iko hatua nzuri kiukweli nataka nichukue leave ya mwezi mzima nikakae home nitulize akili mana wife simuelewi anashida gani kwann ananificha ficha vitu vyake sikuizi.
 
Habari wana jamvi..!Natumaini ni wazima wa afya, ni hivi niende kwenye mada husika hapo juu mimi ni kijana mwenye umri was miaka 39, nina mke na watoto 6 ila mke wangu nilimkuta akiwa na mtoto wa kiume wakati tunaoana mwaka
Nyie wanajeshi mnakuwaga wajinga hamjui caring Hadi mnaoa single mother

Then sio busara kulilia mapenz at ur age 49+ yrs Ni Aibu Sana kiukweli huyo dogo umemuingiza jeshini then ameanza kukuona hufai

Cha kufanya kuwa na Amani moyoni huyo dogo kavimba kisa mwanajeshi
 
Hapa ndipo unaposikiaga baba kaua mama na mwanaye wa kufikia.

Anachofanya mkeo ni ushenzi wa grade A.

Huenda kijana hana kosa ni msukumo wa mama yake tu.

Bahati nzuri wewe ni mjeshi, na huyo mwanao ni mjeshi, bado una nafasi ya kumkanya huyo step son wako iwe kama baba ama kama senior wake.

Akileta jeuri ongea na wakubwa zake wampige chini. Asilete dharau hapa, eboooh!
 
Bila shaka wewe ni askari wa bakabaka, Anyway inauma lakini hakuna namna we mchane tu mkeo maana dogo lazima anapata kiburi toka kwa wife wako mueleze ukweli kabisa kua haupendezwi na tabia zake za hovyo na za kichawi, maake uchawi si lazima mpaka aloge.

Ukimaliza kumchana wife, mpigie na dogo umchane
 
Nyie wanajeshi mnakuwaga wajinga hamjui caring Hadi mnaoa single mother
Then sio busara kulilia mapenz at ur age 49+ yrs Ni Aibu Sana kiukweli huyo dogo umemuingiza jeshini then ameanza kukuona hufai

Cha kufanya kuwa na Amani moyoni huyo dogo kavimba kisa mwanajeshi
Nani kasema mwanajeshi mbn unakurupuka hivyo mkuu nimesema wapi mimi no mwanajeshi???
 
Mkuu we nimtu kazi auvip mzee wangu..sasa cha kufanya nenda mpanda mroge huyo mtoto awe kichaa halafu wakati mkeo amechanganyikiwa na homa ya mtoto,tumia nafasi hiyo kujua hyo nyumba kajenga wapi.

Then mroge nayeye wafanye ndondcha then utakufa kwa amani.
 
Hapa ndipo unaposikiaga baba kaua mama na mwanaye wa kufikia...

Anachofanya mkeo ni ushenzi wa grade A...

Huenda kijana hana kosa ni msukumo wa mama yake tu..

Bahati nzuri wewe ni mjeshi, na huyo mwanao ni mjeshi, bado una nafasi ya kumkanya huyo step son wako iwe kama baba ama kama senior wake.

Akileta jeuri ongea na wakubwa zake wampige chini... Asilete dharau hapa, eboooh!!!
Nzuri iyo safi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom