Simulizi ya ubaharia wa Lemutuz_Superbrand

Dr am 4 real PhD

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
6,494
11,982
Screenshot_20230406-163411_1.jpg

ZE AKILI ZANGU ZA ASUBUHI LIVE U KNOW: ..Hii picha nilipiga loongtime ago in the 90s nikiwa Seamen au Baharia (Ass. Engineer) katika meli ya "MV. LUXEMBOURG" ya kampuni ya Celestie Belgique Maritime (CMB) Shirika la Meli la Taifa la Belgium lipo mjini Antwerpen ambako niliishi kwa Miaka 5 ya masomo na kazi ya Ubaharia ....niwafahamishe Vijana wa sasa kwamba enzi hizo maisha Bongo yalikua Tight sana na ndio hasa chanzo cha neno "BONGO" neno Bongo lilianzishwa na Mabaharia ...wakati huo kulikua na njia mbili tu muhimu za Kijana kuondokana na Umasikini nazo zilikua ni ..(1). UBAHARIA & (2). KUCHEZA SOKA YANGA AU SIMBA ...hakukuwa na options zingine kama sasa zilikua ni enzi za Awamu ya Kwanza yaani Kijana kuvaa Jeans na Raba tu ilikua a Big Deal ...binafsi mambo ya Ubaharia nilikutana nayo katika Shule ya Msingi ya Jamhuri Mnazi Mmoja niliposoma Primary School Vijana 2 Marehemu RAJA KAKA na JUMA JAGAN BURR (now in Canada) ndio walionifundisha maana ya Ubaharia na mimi nikajiunga na ndoto za kuwa Baharia ...nikaanza Ugomvi mkubwa sana na Mzazi wangu ambaye hakutaka kabisa kusikia hizi habari lakini kwa kuwa niliendelea na ndoto mwishoni Mzazi wangu alilegeza kamba na kunishauri kwamba nitafute Ubaharia wa Elimu sio ule wa kuzamia Meli ...nilipomaliza High School nikachomoka mpaka Brussels/Belgium nakumbuka nilirukia Terminal One na ndege ya LUFTHANSA AIRLINES kwa nauli ya Tsh. 90,000 enzi hizo USD Moja ilikua sawa na Tsh.11 tu! ...ni kweli nilijiunga na Shule ya Ubaharia ya Zeemanhuis College Antwerpen Sheria za masomo ya Meli ni Miezi 6 Darasani then 6 mingine Baharini baada ya Miaka 5 nilikua nimemaliza masomo na tayari maisha ya Baharini yalikua yamenichosha nilikua ndani ya Meli Singapore nikaachana na Ubaharia for good nikarudi Bongo for 2 Month na kuhamia New York City/USA ....MY POINT nimeona maneno mengi ya uongo sana hivi karibuni kuhusu Mabaharia ...HOWEVER I am Super Impressed that kwa mara ya kwanza Tanzania we are celebrating "UBAHARIA" nimeona mpaka Baadhi ya Mawaziri wakijiita MABAHARIA it is great to see that... na NAWAOMBEA VIJANA WENGI WALIOPOTEZA MAISHA (NAWAFAHAMU WENGI SANA) WAKIPIGANIA KUWA MABAHARIA MUNGU AWAREHEMU! AMEN - @lemutuz_superbrand


#copy
 
Anasema miaka hiyo kutoka ilikuwa kupitia soka na ubaharia 😃
Soka hapa bongo kumbe limeanza kulipa muda
Siyo kweli hayo ni mawazo yake, watu wanaomzunguka huo ndio ulikuwa upeo wao wa mwisho kufikiri, ni sawa na mbunge kwa sasa hawezi kuona kama kuna maisha nje ya ubunge au siasa na ukapiga pesa nzuri tu.
 
Sijawahi kujitambulisha hapa JF my true identity, lakini Baharia mwenzangu Le Mutuz kaniangusha, yeye kasoma Belgium, Mimi nimesoma DMI Bongo, lakini usahihi ni Seaman.
You mean Dar es salaam Marine Institute (DMI)

Mkuu kumbe na wew ni Baharia... hongeraah 😊
 
Hapo hapo watu wanaangukia pua huwezi amini, mtu Anaishi nyumba ya kupanga 20 yrs, anawatafutia watu pesa yy anakufa chokambaya.... bila connection dar utapoteza mda
Kwel mkuu ni peponi Kwa baadhi ya watu ni Jehanamu Kwa wengine wengi ...
 
Back
Top Bottom