Mtoto wa Membe ahamishwa ofisi asipoteze ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa Membe ahamishwa ofisi asipoteze ajira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Oct 10, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Wakati sakata la watoto wa vigogo likiendelea kutafutiwa ufumbuzi baadhi ya mashirika mbali yameendelea kuwajibika katika hili na kutia simanzi kwa jinsi hali ya kung'ang'ania watoto wa vigogo inapoendelea .....

  Habari zaidi za kusikitisha zinasema mtoto wa waziri wa mambo ya nje Mh MEMBE ameishangaza jamii ...hivi karibuni katika shirika moja la ndege la tanzania pale lilipotangazwa zoezi la redandas ..mtoto wa mh membe gafla aliamishiwa katika kitengo fulani na yule aliehusika kurudishwa pale alipokuwepo mtoto wa mh membe...wakati tulipoanza kufwatilia ukweli halisi tuliambiwa kijana huyu aliamishiwa kitengo cha mjini toka ofisi zao za aport sehemu ambayo alikuwepo mtu mmoja tu....tulipomtafuta mhusika mwenyewe aliweza kukataa kujibu kabla ya kuanza kueleza ""mimi hata waseme nini hili zoezi aliwezinigusa"na kama unashida zaidi kamuulize bosi wangu alienihamisha

  hili lilitudhihirishia wazi kweli kuna kitu kama hicho....

  Tukiwa kama watanzania waliofundishwa ustaarabu ...uongozi wa kampuni hii auna budi kujisafisha kwa hili...haya yanadhihiirisha uchafu gani unaotokea katika mashirika ya umma kwa kuwalinda watoto wa vigogo....
  tulipofwatilia ofisi zao za mjini tulipewa namba ambayo mhusik alipokea na alipotusikiliza alikata simu...tunaomba wale wanaopewa dhamana kwa mashirika ya umma wajue tunapowapigia waandishi tunawasaidia na si kuwaharabia kama wanavyotukatia simu
   
 2. R

  Risk taker Member

  #2
  Oct 10, 2009
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wakuu,
  Ni kweli kabisa hilo limefanyika na hiyo kampuni ni ATCL na huyo mfanyakazi anaitwa John Membe
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kwa heshima ya Bernard Membe Ningemshauri amuondoe huyo mtoto au hata amtaftie shule nje ya nchi kama wengi wanavyofanya... maana siri si siri tena!!
   
 4. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mwandishi anatoa hukumu wakati taarifa za kuthibitisha hana. Mtu kuhamishwa kituo kuna sababu kadhaa, ni wapi imethibitishwa kahamishwa ili kukwepa redundance?...Ungesema hana sifa za kazi, au hakuajiriwa kwa kufuata taratibu, pengine ingekua issue. Watu najua tupo frustrated na maisha, ila kutaka watoto wa viongozi wasipewe fursa ya kufanya kazi kwenye mashirika kama watanzania wengine ni choyo isiyo na msingi. Nao ni watanzania, na kama ilivyo kwa mtu yeyote atajaribu kuadvance career yake. What is wrong with that?

  Its high time waandishi muka concentrate on issues za kitaifa, maana sikuhizi hii obscession yenu kwa personalities na kutaja majina imefika mahali inakera... Ni name dropping tu kila siku. Hivi hakuna issues za kuandika bila the so called fulani fulani na watoto zao kutajwa tajwa?...

  Halafu kachumbari za udaku nyingii, eti kitendo "kilichoishangaza jamii"...na kwamba kuhamisha mtu kituo cha kazi ni moja ya "uchafu wa mashirika ya umma".

  Petty issues tu kila siku...majungu majunguuu aaarrrrgh!
   
 5. s

  shabanimzungu Senior Member

  #5
  Oct 10, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nepotism tanzania stinks
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Sioni tatizo kwa John kuhamishwa, cha msingi anazo sifa zinazomuwezesha kubaki katika hiyo ajra mpya.
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kama jamaa kahamishwa halafu shortly kunatokea redundancy kule alikotoka, halafu hii move imefanywa kwake tu basi watu tutaweka one and one kupata two, tutaona special treatment moja kwa moja.
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  majungu yako kwa wabeba mabox huku tunasaidiana kuambiana ukweli...hakuna majungu...kama majungu si umesikia yaliowakuta BOT..
  swala muhimu sababu za kuhamishwa walikuwa hawana...huyo alieamishwa aiasemekena amekuwa hapo 2 yrs..na yuko mwenyewe hiyo posn.iweje leo hii watangaza ridandas anahamishwa mtu gafla....huo uhuni wa kifadhihina...................??
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ni lazima ku pursue kila story iliyo na harufu ya unfairness.Sasa hivi tuna magazeti ya kutosha kufuatilia mpaka udaku, kwa nini tusifuatilie mambo ya kujenga society inayoheshimu rule of law?
   
 10. s

  saidhorizons Member

  #10
  Oct 11, 2009
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  MTM,
  Mimi niliposoma ujumbe huu haraka haraka nilidhani unatoka kwenye gazeti la Mwanahalisi, lile ligazeti letu linalotoaga "habari nyeti na zenye uhakika" yaani Saidi Kubenea. Niliporudiya na kusoma vizuli nikagunduwa kumbe mwandishi sio shujaa wetu Kubenea; yeye hapendagi kuandika umbeya.

  Mwanahalisi wa JF naona pengine ubadirishe jina lako la bandia kwasababu ukiendeleya na ku post Udaku kama huu unaweza kumharibia shujaa wetu Kubenea na gazeti lake lenye kuleta vitu vya uhakika. Tafadhali lifikirie ombi langu.

  Kabula ya kuwa waziri, Membe alikuwa jirani yangu pale Mikocheni. Ninawafahamu watoto wake wote. Ana watoto wawilli wakiume. Mmoja anitwa Richard ambaye anasoma university na wa pili anaitwa Denis ambaye anasoma primary. Nakuhakikishia kuwa Membe hana mtoto anayeitwa John.

  Kabula ya kumutumia shutumu zetu kuhusu hilo suala la ATC ni vizuri Mwanahalisi wa JF atufafanuliye. Huyo John alimuzaa lini? Una hakika na source yako au mvuto wa kuandika Udaku umekushinda nguvu? Kwa taarifa tu sio lazima mtu yoyote mwenye jina la pili la "Membe" lazima awe mtoto wa waziri Membe, nadhani unalielewa hilo. Tukitumiya standard hiyo mbona wafanyakazi wote wanaoitwa Mushi, Moshi, Massawe, Masanja nk watakuwa kwenye matatizo! MODS itakuwa vizuri mkifuta huu udaku au uhamishiwe huko kwenye kabrasha la umbeya!
   
 11. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa maneno muruwa ya Kiswahili chako
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu na wewe ni mtoto wa Kigogo nini? Je upo shirika gani BOT au..... tehetehe.... Watoto wa Masikini wanamaliza mavyuo vikuu na madigirii yao wanasota mtaani watoto wa vigogo hata kabla hawajahitimu tayari na ajira ina msubiri...hakuna usawa hata kidogo....
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dah hivi hata watoto wa wakulima nao wamehamishwa au kahamishwa mmoja tu?
   
 14. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 776
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 80
  It either wewe wa kuja, yaani mjini huna hata miaka 5 toka ulipotoka bara au mkimbizi kwani wapo wengi tuu wamejificha baada ya vita hawataki kurudi tena kwao.Now tell us who are u? and please usiharibu lugha yetu which is the first native African language kutumiwa na watu wengi katika nchi mbalimbali.
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Watoto wa Vigogo,
  Baba zenu wameuwa mashirika yote ya serikali. Kuna siku kama si nyie basi wajuu wenu watakuja kusota tu. SIdhani kama nyie wote mtakuja kuwa Mawaziri kama baba zenu. Inabidi ifike sehemu muanze kuwaamia baba zenu kuwa "Kuuwa nchi ni kuuwa future yenu pia". Inawezekana sasa hivi vigogo wanatesa kwa kuwa na dola milioni moja ila kwa miaka kadhaa ijayo itakuwa si kitu. Kama hela mtaani zitakuwa nyingi basi always kutakuwa na chance hata za wajukuu wenu na wao kuzipata. Ila siku wakija Wachina/Wazungu /Waarabu na kuishika hii nchi, hata nyie tutakuwa wote tukifua chupi zao na kulea watoto wao maana ni kazi pekee itatufaa.

  Akiba ya taifa ndiyo akiba ya uhakika kwetu wote. Walau ule uhakika wa kusema ntasoma na ntatibiwa wakati wowote bila ya kujali sina au nina pesa. Sasa ATCL ikifa, si hao watoto wa vigogo nao watakosa sehemu ya kufanya kazi? Siku wakija wageni na kushika nchi itakuwa ni kupewa kazi wakati baba yako ni Waziri. Akiondolewa, basi wanakufukuza kazi na wewe...... too sad.
   
 16. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kiswahili chake anakandamiza hadi kwenye kuandika..........
   
 17. N

  Nwaigwe JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 776
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 80
  Sikonge just being curious, hivi hiyo signature yako ina maanisha?au mzee una-info kwamba ndiye watakaye msimamisha kugombea?
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Hiyo sahihi yangu inawakilisha mawazo yangu tu. Dr Slaa wala hahusiki. Mie ni watu ambao wanaamini kuwa huyu jamaa akisema anagombea basi ntawajulisha ndugu na jamaa wengi wampigie. Vinginevyo basi hata mwakani mie kwene uchaguzi sidhani kama ntahusika.

  Hivyo, nakaribisha na wengine wawe na sahihi kama hiyo. Kama tukiwa wengi, inawezekana Dr. Slaa akafikiria na kuanza kuchukua form. Inawezekana hapendi kuingia kwenye jambo ambalo hana uhakika nalo. Ila tukiwa wengi, basi itakuwa rahisi kumshawishi. Hadi sasa ni kiongozi pekee ambaye ana uchungu na nchi yake na hajakamatwa au hata kusingiziwa na UFISADI wowote ule.
   
 19. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  hii ni kashfa sana kwa kiongozi kama Membe kufanya kitu ambacho ni kosa na uonevu kwa wengine, hata kama Membe hakuusika aangalie jinsi ya kutoka kwenye kashfa hii
   
 20. s

  saidhorizons Member

  #20
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Naigwe,
  Wewe na Congo hamujakosea kabisa. Mimi natokaga huko ndani Usukumani na nimekuja Dalisalamu miaka ya kalibuni. Marafiki zangu huwa wananiambiaga kuwa mimi ni mshamba. Na naamini hawajakosea kwasababu luga ambayo nimeizoweya ni Kisukuma ila ninajitahidi kunyoosha Kiswahili changu ili muweze kunielewa bila matatizo. Wakati ninajifunza, itabidi munivumiliye.

  I have really taken your (you and Congo) criticism and words of advice to heart. Even though you have noted that my Kiswahili is less than perfect (which unfortunately is not a new revelation), I believe there is (my linguistic shortcomings notwithstanding) plenty of elbow or wiggle room that allows me to get the thrust of my message across to the intended audience, which to me is the most important take away message from this exchange.

  A perfect symbiosis seems to be at work here: I am learning from your advice and criticism, while at the same time you are giving me the opportunity to get my message across. It demonstrates, if nothing else, that in this forum it is possible to exchange views and ideas as brothers and sister not only without insulting each other, but with a sense of enormous fulfillment and for that we all have to be thankful for being Tanzanians.
   
Loading...