Siku ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika - 16 Juni, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Siku ya Mtoto wa Kiafrika ni tukio la kila mwaka linaloadhimishwa tarehe 16 Juni tangu maandamano ya Soweto nchini Afrika Kusini mwaka 1976 walioandamana kupinga Elimu duni huko Soweto Nchini Afrika Kusini. Tunaenzi ujasiri na uthabiti wa watoto wa Kiafrika na tunasisitiza umuhimu wa kukabiliana na changamoto wanazokabiliana nazo.

Mwaka huu mashirika 8 yameungana kwa pamoja kuandaa tukio maalum la matembezi ya watoto nchini Tanzania kwa ajili ya kusherehekea na kuwawezesha watoto wa Kitanzania.

Lengo kuu la tukio hili ni kusisitiza maelekezo ya Serikali ya kufanyia marekebisho Sheria ya Ndoa (1971) kwa kusikiliza sauti za watoto.

Mashiriki Yaliyohusika Kuandaa Matembezi Ya Siku ya Mtoto wa Kiafrika:Tai Tanzania, C-Sema, Jamii Forums, Missing Child Tanzania, Msichana Initiative, Tanzania Ending Child Marriage Network (TECMN), Children Dignity Forum (CDF), na Flaviana Matata Foundation (FMF).

Karibu kufuatilia maadhimisho haya.

IMG_20230616_071331_431.jpg


Matembezi ya watoto yameanza kutoka hapa viwanja vya Aghakani kuelekea Viwanja vya Farasi.

Msafara wa watoto umefika darqja la Tanzanite, watoto wakiwa wameshika mabqngo yenye jumbe mbalimbali, moja ya jumbe hizo zinasema. NIPE ELIMU USINIPE MUME, SHERIA YA NDOA INAKIUKA HAKI ZETU.

IMG_20230616_104843_292.jpg


Matembezi ya watoto tayari msafara umewasili viwanja vya farasi, maadhimisho ya siku hii yanaenda na kauli mbiu isemayo Mpe nafasi msichana badili sheria ya ndoa.

Matembezi na Watoto hawa yanalenga kuwarithisha tunu muhimu ya kudai haki. Haki iliyodaiwa na watangulizi wetu toka kwa Makaburu Siku kama ya leo 1976

Pia, kupinga kwamba zaidi ya asilimia 30 ya Wasichana Nchini Tanzania huolewa kabla ya kutimiza Miaka 18 (Demographic and Health Survey and Malaria Indicator Survey 2016)

Kwa mujibu wa UNICEF, Tanzania inashika nafasi ya 11 Duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya Watoto wanaoolewa kabla ya kutimiza Miaka 18

IMG_20230616_104843_729.jpg
IMG_20230616_104843_729.jpg
IMG_20230616_104843_292.jpg
IMG_20230616_104843_953.jpg


Sajenti Eva Simon Mbesere wa Kituo cha Polisi Kanda Maalum (Dawati la Jinsia) akizungumza na Watoto mbalimbali kwenye Uwanja wa Farasi-Dar katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, amesema "Mtoto unapotumwa hautakiwi kukataa kwa kuwa siku moja nawe utakuwa mzazi, wajibu wako ni kusoma na kutimiza kazi za jamii zinazokuhusu"

Anaongeza kuwa unapokuwa likizo ni wajibu wako kusaidia wazazi kazi ndogondogo, usikubali kutumikishwa iwe kingono au kwa namna nyingine yoyote.

Elimu imetolewa kwa watoto juu ya wao kufahamu haki zao kama watoto, moja ya haki zao ni kupata elimu, kupata huduma za afya na kulindwa. Watoto wamehusiwa juu ya kutambua nao wana wajibu kwa wazazi ikiwa pamoja na kuwatii na kushiriki kazi jamii kama usafi nyumbani, kama kuosha vyombo kufua nk, watoto wameambiwa waache kiburi na watambue kuwa wao ni tunu ya taifa ivyo wanatakiwa kuwa na maadili.

Pia wamepewa wamafundishwa kutqmbua ishara za namna ya kutambua watu wanaotaka kuwafanyia ukatili, wasiruhu waguswe kwenye maeneo nyeti ya miili yao hiyo ni kwa jinsia zote kike na kiume. Pia wameambiwa wawafikishie ujumbe watoto wenzao na pia kuwaambia wazazi kuwa wageni wakija nyumbani wasiwalaze na watoto wao kwani wageni wengine wanaweza kuwa na tabia za ukatili kwa watoto.

Sajenti Eva Simon Mbesere wa Kituo cha Polisi Kanda Maalum (Dawati la Jinsia): Kuna mazingira ambayo Mtoto unatakiwa uyatolee taarifa kama vile Mzazi wako akiwa mkali kupitiliza au matendo yoyote mabaya ambayo hauna mtu wa kumwambia, unatakiwa kufika kwenye Dawati la Jinsia kwenye Kituo chochote cha Polisi au Shuleni kwa Mwalimu wako.

Sajenti Eva Simon Mbesere wa Kituo cha Polisi Kanda Maalum (Dawati la Jinsia): Kwa Watoto wa kiume mnapokuwa shuleni msiingie msalani wengi, choo ni kwa ajili ya mtu mmoja. Mwingine anatakiwa kupanga foleni kama matundu hayatoshi

Pia, Watoto wa kiume mnapoona kuna mtu anafanya ukatili wa kulawiti Watoto wengine mnatakiwa kutoa taarifa, unapokaa kimya ipo siku anaweza kukurudia wewe kwa kuwa ameona hakuna hatua zinazochukuliwa.

WATOTO WANAITAKA KESHO ILIYO SALAMA ZAIDI KWAO NA VIZAZI VIJAVYO

Wapo wanaosema 'kuozesha Watoto wa miaka 14 huu ni utamaduni wetu' na wengine wanasema kwamba 'ni mila na desturi zetu', kauli hizo kwa bahati mbaya zinatoka kwa Viongozi ambao familia zao haziozeshi Watoto wa umri huu

Watoto wanaitaka kesho iliyo salama zaidi kwa ajili yao na vizazi vyao, wameamua kuzungumza kwa vitendo na hili limejidhihirisha kwa kuwaenzi Watoto wenzao waliofanya hivyo kutetea haki zao Mwaka 1976 nchini Afrika Kusini

JAMII FORUMS: UTETEZI WA HAKI ZA MTOTO NI SEHEMU YA MAJUKUMU YETU

Afisa Program wa JamiiForums, Eileen Mwalongo akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Uwanja wa Farasi, Dar anasema "Haki za Mtoto ni sehemu ya majukumu yetu ambayo tumekuwa tukifanya kwa miaka mingi. Tukiwa Wadau ambao tunapambania Haki za Mtoto tumeshiriki katika maadhimisho haya ili kuendelea kuelimisha jamii kuhusu Haki za Mtoto hasa Mtoto wa kike

Ameongeza, "Tunaamini kwa ushirikiano wetu pamoja na Wadau wengine tunaweza kuongeza nguvu ya kushawishi Serikali kufanya mabadiliko ya vifungu vya 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa vinavyomruhusu mtoto wa kike kuolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18"
 

Attachments

  • 693A9931.jpg
    1.1 MB · Views: 2
  • 693A9916.jpg
    2.1 MB · Views: 1
  • 693A9939.jpg
    758.6 KB · Views: 1
  • _MG_1871.jpg
    554.4 KB · Views: 1
Mtoto ana haki ya kutoa maoni & kusikilizwa. Ni marufuku mtoto kunyimwa haki hii ya msingi

mtoto.jpeg
 
Ningependa kujua kama haya maadhimisho yanafanyika kwa Dar tu au na mikoa mingine. Kama ni Dar tu naona bado ugumu wa mtoto aliye Nanjirinji, Sitimbi, Mlalo, Mlola, Chumvini, Nkwenda, Mabira, Mpigamiti etc kukombolewa.

Watoto wa vijijini ndio wanahitaji walau kupata maadhimisho kama haya maana kwa mazingira ya kijijini ndiko kuna matukio mengi sana ya ukiukwaji wa haki za watoto kama kubakwa, kunyimwa elimu, kazi za utotoni, kipigo na ujinga mwingine.

Watoto hasa wa vijijini wanahitaji kuhakikishiwa elimu bora, afya bora, lishe, mazingira ya kuishi yanayoridhisha etc.
 
Back
Top Bottom