Afrika ni ngumu mtoto wa maskini kuendeleza kipaji chake kwa support kutoka kwa baba yake

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Kipaji ni zawadi iliyopo ndani yako ambayo mungu mwenyewe kakupa kujua una kipaji gani hilo ni jukumu lako wewe mwenyewe tena.

Lakini kiafrika afrika ni ngumu sana kipaji cha mtoto kuendelezwa na kupata support kutoka kwenye familia sio kwa sababu hawataki kipaji chako kiwe kikubwa ila tu " MFUMO WA MAISHA NDO UPO HIVYO".

hata wengi waliofanikiwa hawakupata support kutoka kwenye familia zao ukisikiliza history ya SADIO MANE kutoka BANBALI utagundua kuwa ni juhudi zake na ukaidi wake ndo umemfanya awe pale alipo leo .

Ukisikiliza history za wachezaji waliolelewa na mzazi moja wa jinsia ya kike kama DEPAY utagundua kuna upande moja ulikuwa unambeba history yake ipo tofauti kidogo na wachezaji kama SADIO na KICHUYA .

kwanini nasema kuna wachezaji malezi ya mzazi wa kike yanawabeba . katika rika la ukuaji sana sana watoto wa kiume inakuwa ngumu sana kuonana na baba yani baba katoka asubuhi karudi jioni kwahiyo tunakuwa na ukaribu sana na mama zetu. na tunaona upendo wa mama ni mkubwa sana.

kuliko baba zetu lakini tukikua wakubwa baadae sana ndo tunaanza kuuona upendo wa baba pale maisha yanapoanza kutupa tuition ya bila malipo.

Sasa katika umri wa utoto ukijulikana una kipaji na mama akijua una kipaji mara nyingi atakusupport tu ila baba hawezi kukusupport kwa sababu

👇👇👇👇👇👇
Mama ni moyo ana mapenzi ya dhati yaliyovuka mipaka kwa mwanae, leo hii hata mama yako ukimwambia unataka kuwa msanii atakupa support.

mapenzi ya dhati kuna muda huwa yanapofusha kushindwa kuona uhalisia, hapo unakuta mtu hana kipaji wala bidii, hana connections, n.k

Baba ni kichwa, mlinzi na mtafutaji, leo hii ukimwambia unataka kuwa msanii atatafakari na kuona mbali maana ukiwatoa kina Diamond, Kiba, Harmonize na wasanii wengine wachache waliofanikiwa.

kuna lundo kubwa sana la wasanii miaka nenda rudi wamesota (kwa ambao tumekaa na wasanii tunajua msoto wake).

atakupa makavu ( ukweli mchungu) na hatakusupport atakwambia ni bora akutafutie jembe ukalime uwe na uhakika hata wa kula na kuja kilisha familia yako.

Hapo ukitumia hisia utaona mama anakupenda ila ukitumia akili unaona baba anakujali.

ila kadri umri unavyoenda mtoto wa kiume akiacha kuwa tegemezi na kuanza kujitegemea.

kuhama, kujitaftia ridhiki, kuwa na familia, n.k basi hapo ukaribu kwa baba unaongezeka maana wanaanza kufanana, mtoto na baba wote wanajitaftia ridhiki, mtoto na baba wote wameoa, mtoto na baba wote walihama kwao kujitegemea, n.k.

yote kwa yote wote wana umuhimu, ukipatwa na tatizo mama atakuwa karibu na wewe sana huku mzee akihangaika huko nje kukunasua kwenye tatizo kadri ya uwezo wake wote.

hapo ndipo wengi wanakosea wanadhani mama ndie mwenye umuhimu zaidi.

lakini wanasahau baba yupo nje anapambana ili kuwanasua kwenye matatizo ya ujinga kwa kuwapa mahitaji ya elimu, kuwaondolea njaa kwa kuwalisha, kuwasitiri kwa kuwavisha, kuhakikisha hamlali nje kwa kulipia kodi ya nyumba au kujenga, kuwatoa uvivu kwa kuwapa kazi za kufanya nyumbani, kuwanusuru katika maamuzi mabaya yanayoweza kuwapeleka jela kwa kuwatia adabu tangu mkiwa wadogo, n.k.

mchango wa baba ukitaka kuujua kama wewe ni mtoto wa kiume anza kujitegemea na kisha uwe na familia yako, ila kama bado unaishi kwenu bado hujawa mwanaume wa kuondoka kwenye kiota ukajitegemee hapo itakua kazi kuona mapenzi ya baba.

kwahiyo vijana wa afrika support kutoka kwa upande wa baba zetu tutaipata kwa wingi baada ya wajukuu zetu wajukuu wao kufa lakini support haiwezi kupatikana kama mfumo wa maisha bado utakuwa upo hivi hivi.
 

Attachments

  • 1661680713013.jpg
    1661680713013.jpg
    50.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom