muhosni
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 1,108
- 152
Mama!
Nakuheshimu mama.
Umetoka shamba, umechoka, umembeba mdogo wangu mgongoni na ujauzito. Jembe lako hukuacha shambani, umeleta kuni na mboga za majani. Mimi ndo nimerudi shule, sijala na sielewi kiasi ulivyochoka. Mimi ni mtoto wa kiume baba kanikataza kuingia jikoni.
Mama umejitahidi kupika umenituma nikateke maji, kisha nikanunue mafuta ya kupikia koroboi moja. Hatimaye tukala. Unampenda baba mama, ukamwachia chakula.
Giza limeingia, unaogesha mtoto na mimi unaniharakisha nioge baba asije kukugombeza. Mafuta ya taa yamekwisha mama, hakuna pesa ya kununua. Moto unatusaidia mwanga.
Baba anaingia anaimba, amelewa! Anakuita kwa sauti ya ukali, unaitika kwa heshima, unatoka kwenda kumfungulia nyumba yake. Unamfunulia chakula na kumkaribisha. Anatazama chakula anahamaki "Chakula gani hiki wewe mwanamke, hata ukimpa mbwa hali?"
Maneno yanayofuata siwezi kuyarudia mama, pole sana. Baada ya kusikiliza hotuba ndefu, na baada ya baba kupitiwa na usingizi, unafunga mlango wake unakuja kwetu kulala mama.
Mara narudi nyumbani, nakuta hakuna mtu. Shangazi ananiambia mama kalazwa hospitali, "kapewa mtoto". Mara baada ya miaka kadhaa mama, ukanipatia wadogo zangu saba.
Ulipenda tusome mama, hukuwa na uwezo
Ulipenda tuwe na afya mama, hukuwa na uwezo
Ulipenda uvae vizuri mama, hukuwa na uwezo
Mtoto wa nane mama, ukaaga naye dunia. Nyerere angekuwa bado madarakani mama usingekufa kwa sababu hizo. Kukosa huduma, muuguzi hakujali.
Baada ya kifo chako mama, hadithi ni chungu zaidi na ndefu sana.
Kokote uliko mama, nakupenda sana na leo ni siku yako tukufu!