Niliamua kumfurahisha mtoto wa mama mkwe kwa ujumbe huu

Mr sule

JF-Expert Member
Oct 14, 2021
607
1,097
Kuandika ujumbe ndefu si kawaida yangu kwa huyu mtarajiwa wangu. vijana haya mambo si ya kupuuza hata kama unaongea nae kila siku lakini jumbe kama hizi anakuwa nazo na atarudia kusoma mara kwa mara

Mke wangu
leo nimetafakari sana kuhusu wewe. mwanamke ambae umetokea katika maisha yangu na kujiona tu mimi pekee ndie nina mke mzuri na ninaependwa.

Kama nilivyokuambia mke wangu, vipaumbele vyangu katika maisha yetu ni kufanya uwe na furaha, Amani, Tabasabau, kicheko na kufanya kuishi maisha ya ndoto zako, kwani nimeapa kupigania ndoto zako kwa uwezo niliona na nguvu zangu zote nilizonazo.

Ninavyokupenda nahisi kabisa wewe una moyo wangu, kwaiyo ni jukumu langu kkupigia hadi mwisho wa toni ya Jasho langu, niko tayari kwa lolote, nimejipanga kulinda mpenzi wangu. kwa chochote. Hili hata wewe mwneywe unalijua sana.

Nitakuwa mume bora sana kwako, nitakuwa mume ambae utajivunia kuwa nae katika maisha yako yote. Nitakuwa mume ambae nitakufanya experience maana ya Upendo, nitakuwa mume ambae ni baba bora kwa watoto wako, nita linda familia kimaadili, kiuchumi kmaendeleo na kuwa na mahusiano mazuri kwa familia za pande zote mbili na watu wengine.

Najua unajua kila siku nakumbia nahitaji familia yenye furaha na Amani, na leo nigependa kutumia fursa hii kukumbusha kwamba, Daima tuendele kumuomba Mungu wetu, atuepussha na tamaa, anasa na vitu vingine ambazo zinaweza kuweka doa safari yetu hii ya kufa na kuzikana na atupe neema na baraka tele, kizazi ambacho ni mfano kwa watu wengine, atuwekea upesi wa kutimiza malengo yetu hasa biashara na mambo Mengine.
Hakika mambo yote hayo tukisimama na Mungu tutashinda.

Maneno haya si mageni kuyasikia kutoka kwangu ila nakukumbusha tena na tena hata kama unajua hili lakini nina wajibu wa kukumbusha.

Mwisho niseme tu nakupenda sana mtoto wa mama mkwe wangu.

Baada ya ujumbe huu nilipewa zawadi nzuri sana.
 
FB_IMG_16870188220058448.jpg

Naona huyo mtoto wa mama mkwe amefanikiwa kupata mshamba mmoja hivi wa mapenzi.

Basi akikuangalia na gazeti lako anasema hi!
 
Kama nilivyokuambia mke wangu, vipaumbele vyangu katika maisha yetu ni kufanya uwe na furaha, Amani, Tabasabau, kicheko na kufanya kuishi maisha ya ndoto zako, kwani nimeapa kupigania ndoto zako kwa uwezo niliona na nguvu zangu zote nilizonazo.
Pigania ndoto zako na furaha yako ndugu yangu, hii tahadhari ni kwa faida yako tu lakini.
 
Kwanza kuna kitu ulimkosea ndiyo ukashusha hilo gazeti ama ulianza tu? Na je baada ya hayo maneno ukamalizia na "will you marry me?" Au stori stori tu , nice message though atakua anakukumbuka na kubaki anatabasamu tu.

Sijamkosea
Mtoto wa mama mkwe uwa ananifurahisha sana.

Nilikaa tu nikaamua kumpa maua yake.

Nimeshatoa posa so tuko kwenye level nyingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom