MTOTO MFU NDANI YA BOKSI

SteveMollel

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
8,430
23,750
Mnamo mwaka 1957 tarehe 25 mwezi wa pili, mwili wa mvulana mdogo ulikutwa ndani ya boksi sehemu ambapo haparuhusiwi kutupia vitu huko eneo la Philadelphia, Marekani. Mtoto huyo anakadiriwa kuwa na miaka 4-6, urefu wa futi tatu na inchi tatu. Akiwa uchi ila amefunikwa na blanketi zito.

Na nywele zake, rangi ya dhahabu iliyofifia, zilikuwa zimekatwa ikisadikika muda mfupi kabla hajauawa, na pia mwili wake ukiwa umesafishwa vema, pia ikisadikika ni muda mfupi kabla ya kuuawa kwake.

Kwenye mwili wake kulikuwa na majeraha madogo, kidevuni, kando kidogo ya sehemu za siri na hata kwenye enka ya mguu wake wa kushoto, lakini, kutokana na ripoti ya kiuchunguzi, majeraha makubwa ya kichwani ndiyo yaliyopelekea kifo chake.

Ila hakukuwa na shahidi yeyote yule wa hilo tukio…

Basi hapo ambapo mwili wa mtoto huyo ulipotupwa, akatokea kijana mmoja na kuuona, akiwa ni mtu wa kwanza kabisa kufanya hivyo. Lakini baada ya kuuona, ikamchukua karibu siku nzima kabla ya kutoa taarifa yoyote ile. Uzuri baadae alikuja kutoa taarifa hizo.

Bila shaka alikuwa kwenye hali ya taharuki, maulizo ama woga.

Ila akiwa kwenye hali hiyo, kabla hajatoa taarifa, mwanaume mwingine akauona mwili wa mtoto huyo lakini yeye akahofia kabisa kutoa taarifa polisi kwa kutokutaka kuhusishwa kabisa na maiti hiyo. Kwa mwanaume huyu alihofia huenda akaulizwa maswali juu ya uwepo wake katika hilo eneo na akajikuta anashindwa kuyajibu.

Nadhani hii ni desturi ya watu walio wengi, kuogopa kutoa taarifa kuhusu jambo fulani kwa kuhisi wanaweza kuhusishwa kinamna moja ama nyingine na hiyo kesi. Zile za ‘staki ushahidi!’ nadhani wazijua.

Basi kutokana na hali ya hewa kuwa baridi sana kipindi hiko, ilikuwa ni ngumu kubashiri kwa uhakika juu ya muda halisi ambao mtoto yule alikuwa amefariki.

Polisi walipouchukua mwili huo, wakasambaza vipeperushi takribani laki nne ili yeyote anayemfahamu mtoto huyo akapate kufika kituoni kutoa taarifa. Na vipeperushi hivi vikasambazwa Marekani nzima, lakini juhudi hizo hazikuleta matunda yoyote yale.

Sasa ikabidi wataalamu hao wa usalama wachukue hatua za mbele zaidi kumtambua mtoto huyo. Wakafananisha nyayo za miguu za mtoto huyo na pia wakatumia ‘fingerprint’ za maiti kutambua kama zitafanana na rekodi yeyote ile, lakini hamna rekodi yoyote iliyopatikana!

Hakukuwa na rekodi ya mtoto huyo popote pale.

Basi hapa ikaanza kuwalazimu wapelelezi watumie vitu vilivyokuwa vinapatikana kwenye eneo la tukio kuona kama watapata chochote kitakachowasaidia kwenye upelelezi wao. Na kitu cha kwanza kabisa kuhangaika nacho kikawa ni boksi lililohifadhi maiti.

Kwenye boksi hilo kulikuwa na ‘serial number’ ambayo wapelelezi waliitumia kutambulia boksi lilitokea kwenye kiwanda gani, JCP store, ambayo ilikuwa inapatikana maili kumi na tano mbali na eneo la tukio.

Kabla ya kubebea maiti hiyo, wapelelezi wakatambua kuwa boksi hilo lilibebelea kichwa cha kitanda, ikiwa ni miongoni mwa maboksi kumi na mawili ambayo yalienda maeneo mbalimbali, lakini sasa bado ikawa ngumu kutambua ni nani haswa aliyepokea boksi hilo kwani wateja wote hao, kumi na wawili, walilipa kwa ‘cash’ hivyo hakukuwa na rekodi ya makaratasi.

Ila kama bahati basi, kati ya wateja kumi na wawili, nane wakatoa taarifa polisi baada ya kuona tangazo. Na kati yao kuna ambao wakasema bado maboksi yao walikuwa nayo, na wengine wakisema wanayatumia kuhifadhia takataka nyumbani.

Baada ya tafiti zaidi, wapelelezi wakaja kubaini kuwa boksi hilo lililobebelea maiti lilibebelea kichwa cha kitanda toka JCP store kwenda eneo linaloitwa Upper Darby, karibu tu na Philadelphia.

Na vipi kuhusu lile blanketi?

Upelelezi ukaenda mbele zaidi kwa kuanza kulifuatilia na lile blanketi ambalo lilifunika maiti ya mtoto yule. Utafiti huo ukafanywa na taasisi ya mambo ya utengenezwaji wa nguo ya Philadelphia na kubaini kuwa aidha lilitokea Granby, Quebec huko Canada au Swannanoa, North Carolina.

Ilikuwa ni ngumu kubaini haswa limetokea wapi kwasababu mablanketi kama hayo mengi hutengenezwa na kutumwa, hivyo upelelezi kwa kutumia blanketi ukawa ni mgumu zaidi na ukaishia hapo. Sasa wakahamia kwenye kitu kingine kilichopatikana kwenye eneo la tukio.

Kitu hicho si kingine bali kofia ambayo ilipatikana hatua kumi na tano tokea pale ambapo boksi lilikuwapo. Kofia hiyo ilikuwa rangi ya bluu saizi 7 1/8 na yenye chapa iliyosomeka ‘EAGLE HAT & CAP COMPANY’ ambayo ni kampuni inayopatikana huko Philadelphia kusini.

Hapa upelelezi ulipofanyika juu ya kofia hiyo, Muuzaji aitwaye Hannah Robbins akasema anamkumbuka mwanaume aliyenunua kofia hiyo kwake, ambapo akamweleza mwanaume huyo alikuwa na nywele nyeupe, makadirio ya miaka 26 - 30. Alilipia kwa cash na hajamuona tena tangia hapo mpaka leo hii. Wapelelezi wakatembelea maduka mbalimbali ya kofia wakiulizia lakini bado hawakubahatika kupata kitu.

Kwenye mwili wa mtoto yule kulikuwa pia na mabaki ya nywele maeneo kadha wa kadha. Mmoja wa wasanii wa kipelelezi (Forensic Artist) kwa jina la Frank Bender akaamini kuwa kuna uwezekano mtoto huyo alilelewa kama msichana sababu kwamba alikuwa na nywele ndefu ambazo zilionekana kukatwa kwanguvu.

Na pia mpelelezi wa kesi hiyo bwana Bill Kelly alitumia wasanii ambao walichora picha ya mtoto huyo kwenye mwonekano wa kisichana kuona kama atatambulika lakini bado haikuzaa matunda.

SASA NANI ALIMUUA MTOTO HUYU?

Ebu tutazame hapa …

MAELEZO YA KWANZA

Nadharia ya kwanza ni kutoka kwa waandishi wawili Lou Romano na Jim Hoffman ambao wanasema waliwahi kukutana na mtu tokea Philadelphia ambaye aliwahi sema kwamba aliwahi kumkodishia nyumba mwanaume mmoja aliyewahi kumuuza mtoto wake wa kiume.

Je mtoto huyo ndiye yule aliyeokotwa akiwa mfu?

wapelelezi wakafanya jitihada kumpata mwanaume huyo ila wakaambulia kumpata mwanaye wa kiume, yaani ambaye anadhaniwa anaweza kuwa kaka yake na yule mtoto mfu. Wakafanya vipimo vya DNA lakini wakiwa hawajamtaarifu kaka yule kama wanafananisha vinasaba na yule mtoto mfu.


MAELEZO YA PILI …


Daktari aitwaye Remington Bristow alipeleleza kesi hiyo ya mtoto kwa takribani miaka thelathini na sita akiwa anakusanya kila taarifa ambayo inakuja mbele yake. Akitumia pesa nyingi na masaa mengi mno akijaribu kumtambua mvulana huyo.

Alisafiri kutoka Philadelphia mpaka Arizona na Texas kufuatilia tu. Pia hata akakutana na mtu anayezaniwa amerukwa na akili ambaye alidhani anaweza kumpatia taarifa yoyote ile kumhusu huyo mtoto. Na kwa urahisi zaidi wa kukusanya taarifa, bwana Remington akawa anatembea na kinyago chenye kufanania uso wa mtoto yule mfu.

Kwa mujibu wa bwana huyu Remington, mtoto yule alikuwa amekufa kiajali tu. Kucha za mtoto huyo zilizokuwa zimekatwa vema zilimfanya aamini mtoto huyo alikuwa anapata matunzo mazuri toka kwenye familia yake, na pengine familia yake ikaogopa kujitokeza sababu ya kuhofia kufunguliwa mashtaka.

Lakini zaidi bwana huyu akaenda kukutana na familia ya karibu na eneo la tukio, familia ambayo tayari hata polisi walishawafanyia mahojiano. Hapo bwana Remington akaona kitanda cha mtoto mdogo ambacho alidhani labda kichwa chake ndicho kile kilicholetwa na lile boksi toka JCP store.

Hivyo basi Remington akasema kuwa inawezekana huyo mtoto aliyekufa ni mtoto haramu, yaani wa nje, wa binti wa familia hiyo ambaye alikuja kumtupa mwanaye ili asibainike kuwa ‘single mother’.

Baadae kidogo, bwana Remington akafariki na basi mpelelezi aitwaye Tom Augustine akachukua kesi hiyo kuifanya kazi.

MAELEZO YA TATU … Ebu hapa uskize kwa umakini …

Kuna mwanamke aitwaye Martha ambaye aliwasiliana na mpelelezi Augustine na akasisitiza aongee na polisi.

Martha aliwaambia polisi kuwa mama yake alikuwa akimtumikisha kingono ‘sexual abuse’ na pia mama yake alikuwa anamfanyia vivyo hivyo na mtoto yule wa kiume.

Na kwa mujibu wa maelezo ya Martha, mama yake alimuua mtoto yule kwa kumpiga baada ya kupambania kumwogesha. Baada ya hapo akawaendesha Martha na huyo mvulana kwenda kumtupa.

Maelezo haya ya Martha yakaonekana kuwa na kiini cha ukweli kutokana na kufanania na baadhi ya taarifa zilizokusanywa hapo mwanzo, maelezo na hata pia anwani. Kwenye maelezo ya Martha, mtoto huyo alipewa kipigo baada ya kula maharage yaliyookwa. Na kwenye mwili wa mtoto huyo, kooni mwake alikutwa akiwa na vitu nyeusi kuonyesha alitapika ama kutapishwa.

Lakini baadae ilikuja kugundulikana kuwa Martha ni mgonjwa wa akili na walipomtafuta zaidi kuhakikisha maneno yake kwa ushahidi, hakuonekana.


**





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaburi lililohifadhi mwili wa mtoto huyo likiwa limeandikwa BABA WA MBINGUNI MBARIKI MTOTO HUYU ASIYEJULIKANA..
images-9.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laiti wapelelezi wetu wangepeleleza kwa kutumia 10% ya juhudi iliyotumika kubaini muuaji wa huyo mtoto, bila shaka:
1.Muuaji wa Akwilina angeshatiwa korokoroni badala ya kukimbilia kufunga jalada.
2. Tungeshajua kilichompa Ben Saanane
3.Waliomfyatulia risasi mh.Lissu wangeshahukumiwa.
 
Back
Top Bottom