Jamani jana alikuja wifi/shemeji yenu toka kijijini kwani nilimwacha baada ya kupata kibarua hapa mjini, kama ilivyo kawaida ya wanaume tulio wengi haturidhiki(mungu atusamehe) niliamua kuwa na mpenzi mwingine hapa town wa kutuliza mashetani ya kipanda, kosa nililofanya ni kumleta mpaka sehemu ninayoishi akawa anakuja mara kwa mara mpaka kuzoeana na watoto wa mama mwenye nyumba, sasa jana my waifu katia timu mjini kutokana na kubanwa na shughuli za ofsini nikamtuma jamaa yangu akamchukue ampeleke nyumbani kizazaa kilianza baada ya kufika nyumbani kuna kitoto pale nyumbani kina miaka kama 6 hivi kamemwambia kila kitu, nimetoka kazini nikakuta waifu kasepa kurudi nyumbani na amesema hataki ndoa tena, nimekoma jamani nimejitetea mpaka basi lakini hanielewi naogopa ndoa yangu kuvunjika.