Unataka kuolewa? fuata haya...

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517
‘Dodo’, ile ngoma la King Kiba, kalisikilize tena leo. Yawezekana hukuelewa jana na majuzi ile. Ni ngoma ambayo unaweza kuitumia kusaka ‘waifu’ flan hivi na ukafanaikiwa. Ni ngoma ambayo inakuwa tamu kadiri inavyoishi.

Yeah (Ye Baba)

Kupenda ni vitendo, Si maneno maneno, Leo nakupa kitengo, Kwa kufika malengo, Umeziba mapengo, Kwa upendo upendo, Eeh bwana wala huzingui, Anzeni vikao vya send off yeah. Maana we mrembo nakujuza...

‘Ene wei’. Hii ni kwa wenye ndoto ya kuolewa ‘Suni azi posibo’. Moja kati ya mtihani mkubwa kwa kina dada ni kusubiri kuchaguliwa ndipo waingie kwenye ndoa. Bahati mbaya waoaji wenyewe hata hawaeleweki wanataka nini kwa mwanamke.

Maana huwezi kujua masela wanataka nini kwa mwanamke. Mwenye mke mrembo anatembea na beki tatu asiyejua hata kujipulizia uturi mwilini. Anayemmiliki mke mwenye adabu zake kutwa yuko baa, akilewa tu anakuwa mali ya wahudumu.

Sasa siyo vibaya na nyinyi wanawake muwe mnajiongeza kujua muoaji. Maana hata nyinyi kama minyoo ‘samutaimu’ hamueleweki. Yule anayekupenda unampuuza unakomaa na jitu lisilokupenda na kuliweka kwenye ‘statasi’ kila siku.

Ukitaka kumjua mwanamume muoaji tazama sifa hizi. Kwanza hupenda sana kuamkiwa na watu. Ukimuona sema shikamoo, hata ukirudia mara tano kwa siku, siyo mbaya ndio linataka hivyo. Utakuwa unajisogeza karibu na ndoa.

Waoaji hawajibu meseji kwa wakati, na kama ni ya suala la pesa ndio hawajibu kabisa. Hawajui kuita majina ya mahaba kama baby, honey, sweetie wala my. Hawataki dem mpenda saluni wa ‘kuchati magrupuni’ au wa stori za insta na kuvaa mawigi.

Ukiwa naye matembezini usitazame vitu dukani wala kuulizia bei. Pita kama huoni kitu vile la sivyo ndoa itapepea. Mkienda baa agiza bia moja, ikizidi sana mbili au usiagize kabisa. Msosi ni chipsi kavu au akiulizia chakula wewe jibu “Noo baby nimekula nyumbani tayari” hata kama hujala. Hapo utafanya mlango wa ndoa uwe wazi zaidi. Na usiongozane na mashosti zako mkitoka naye. Marufuku.

Usiombe bando, nauli, pesa ya vicoba wala kumpa stori za shida za wazazi wako. Neno “Baby nikuambie kitu?” Stoop! Siyo neno rafiki kwenye sikio la kidume muoaji. Atajua wewe ni sehemu ya jamii ya ombaomba. Wale wa barabarani tumewazoea na tunajua tuishi nao vipi. Lakini kuna wale wa kidigitali wale. Ndio hawatakiwi.

Wale wa saa nane usiku anakuambia “Baby sijala...” Wale ndio kero kama nzige wale. Sasa usifanye mwanamume akadhani na wewe ni mmojawapo. Wanaomba hela ya nauli, ya saluni, ya msosi na ya vicoba. Kero zaidi ni lile neno lao la mwisho. Eti “Tuma na ya kutolea.”

Hawa ombaomba new model ni hatari bora hata kina Matonya kuliko hawa. Wanatufilisi na kutupa magonjwa juu. Ogopa! Ukimwimbisha asubuhi mchana anakuambia gesi imeisha. Ukimsomesha asubuhi jioni anakupa na mtoto kabisa. Utasikia “Mtoto wako anaumwa.”

Zamani kuvaa gauni refu ilikuwa kutunza maadili ya Kiafrika. Baadaye ikawa nguo ndefu ni kichaka cha kuficha miguu chelewa. Na wa miguu ya bia walivaa vimini kuanika miguu yao hadharani. Walionekana wahuni wenye kuleta majaribu kwa wakware.

Lakini hivi sasa wenye vimini ndio hutunza maadili kuliko wa gauni ndefu. Dada zetu siku hizi huvaa magauni marefu wenyewe huita dera. Ni vizuri kuliko vimini, tatizo wakichoka na kulinyanyua juu. Kwani hujui saizi yako mpaka ushikilie dera kama bibi harusi?

Ukijiuliza juu ya hili suala unaweza kupasuka kichwa aisee. Ujue ‘samtaimu’ hata wao pia katika hili hujishangaa. Unajiuliza kwani njia ina maji au matope? Hamna kitu ila kalishikilia kwa kulivuta mpaka juu juu usawa wa ikulu.

Hizi swaga ukiwa nazo mwanamke, tegemea kupata ushindani mkubwa sana wa kupata ndoa. Wanaume tuna ‘ditelizi’ ndogo ndogo sana za kufanya tumuelewe mwanamke wa kuwa mke. Wanawake wengi hawajui hili jambo, wanajikuta tu wanakosa au wanapata.

Kuna panya wa kiume aitwaye Magawa, alipata nishani ya dhahabu ya kubaini mabomu. Hivi sasa kastaafu kazi rasmi. Sasa tunawataka wahusika wamlipe mafao yake haraka. Sisi siyo wavulana, ni wanaume lazima tubebane.

Wasimcheleweshe kama wafanyavyo kwa wastaafu wengine. Magawa ni mzalendo, mtiifu, jasiri na mfia Taifa lake. Tunataka familia yake ifaidike na kiinua mgongo cha mzee wao. Sambamba na ulinzi mkali wa kudhibiti wadangaji.

Maana isijekuwa Magawa kapewa mapene mbuzi akaishia kuzitafuna na vicheche vya mjini. Maana wadangaji hawachezi mbali na fursa. Si ajabu walimdaka uwanja wa ndege na maneno ya: “Jamani napenda wanaume wenye pua kama ya Magawa akee...”

Magawa siyo kama panya wa kwenye mageto yenu. Waliokimbia umande na kuishi kwa wizi majumbani. Magawa alisoma vizuri kule SUA na leo atakuwa anakula mafao tu.

Pia ajengewe nyumba na vifaa vya kisasa vya ulinzi. Maana Wafipa na Wamakonde akili zao wanazijua wenyewe. Akatiwe bima ya maisha. Na watu wa Moro wajenge sanamu la Magawa kwa kuwatoa kimasomaso.

Kwa wale panya wataalamu wa kutegua pesa, nguo na vyakula vya majumbani mwetu. Tutaendelea kuwastaafisha kinguvu, kwa sumu na kuwafanya kuwa kitoweo cha mapakashume mitaani.

Magawa ni masomi, mbobezi ambaye anastahili heshima na alindwe kwa hali na mali. Na sisi kama wanaume lazima tusimame na Magawa, katuaminisha kama mtoto wa kiume. Makofi kwa Magawa tafadhali.

Sasa totozi mkae mkijua mpaka panya wa kiume wapo kwa ajili ya kulinda usalama. Sisi tumeambiwa tuwalinde na kuwapenda na ninyi mtupe heshima na kututii. Hiki ndicho kitu tunachotaka wanaume waoaji. Tumeambwa kutafuta pesa na wake.

Usisikilize ya watu. Wao ukiwa single lazima watauliza, kwa nini huna girlfriend/boyfriend? Ukiwa naye utasikia, ndoa lini? Ukifunga ndoa, utasikia tunataka wajomba na mashangazi! Mkizaa watakuja na hii, mtoto kakua mtafutieni dada/kaka yake!

Ukimtafuta, utasikia mbona mnazaa haraka haraka hamuogopi maisha? Ukinenepa, we unanenepa tu, huogopi magonjwa kuna presha na kisukari. Ukikonda, utasikia acha ubahili pesa zote hizo unakuwa bahili?

Ukinunua gari, utaambiwa gari la nini wakati hujajenga wala huna kiwanja? Ukijenga, utaambiwa usumbufu huu wa daladala mjini huna gari? Tushike lipi? Kwa wanaume sisi mara nyingi huwa tunakufa na tai shingoni.

Maisha ya mwanamume ni ya kila kitu kukitafuta kwa tochi udi na uvumba. Ukitaka kumiliki pisi kali lazima umtafute. Hata ukiwa na pisi nyingi nchi nzima, lakini ukitaka mke lazima umtafute. Kumbuka wote wanakutegemea, kwa hiyo pesa ya kula ni juu yako lazima uzitafute. Pia ili uweze kudumu nao, amani ya moyo lazima uitafute…

Kutokana na mihangaiko kuwa mingi kila siku, hata usingizi ili uupate lazima uutafute. Ndio maana wazee wengi hupiga mitungi ni sehemu ya kusaka usingizi. Na tunaambiwa ufalme wa mbinguni lazima tuutafute. Wanaume tutaingia mbinguni tukiwa tumechoka sana.

Tutapokewa na malaika tukiwa taabani ulimi nje kama jibwa la polisi. Hata kifo, wanaume wengi hutangulia, ili kwenda kutafuta sehemu ya kujenga mbinguni. Lakini hayo ndio majukumu yetu tumeumbiwa kama wanaume.

Sisi tunatakiwa kutafuta maisha, kutafuta pesa, kutafuta mke, na kutafuta amani ya mioyo yetu pande zote mbili. Wanawake kuhaha kwa waganga na kuhubiri kusaka mume ni kuvamia majukumu ambayo hayawahusu. Subiri wenye majukumu tuje kukuposa.

©Mwananchi
 
Mambo yamebadirika kwelikweli hii Leo ndoa zinasakwa kwa maostazi
Hii siyo kwa mademu tuu hata boys wanaangaika sana kwa waganga kusaka pisi kali
 
Asante
 
a lot of men are still boys
Wadada ambao hamjaolewa nawapa pole kuna changamoto kwakweli
And alot of women are still girls sikuhizi! Unataka uhudumiwe wakati uko kwa baba yako? Huduma rasmi zinatakiwa zianze baada ya kulipiwa mahari.

Responsibility ya kujua umekula, umevaa ni ya mume from that moment! Sio kabla
 
Upo sahihi kabisa.

Pia ongezea tendo la ndoa ni kwa ajili ya wanandoa,,usimuombe/asikuombe mapema kabla hujamlipia /hajalipiwa mahari.
 
Back
Top Bottom