Mtoto atoroshwa ndani ya kikapu Muhimbili

Mtoto atoroshwa ndani ya kikapu Muhimbili

Mkuu hivi unajua maana ya "k" kweli? Ulivyoandika 7k? K maana yake ni thousand, hapo maana yake ni 7 x 1000 = 7,000/= Nadhani wewe ulimaanisha 700, 000/= ambayo ingefaa iwe 700k.
Isomeke kama ulivyosahihisha.
Heri ya sikukuu mkuu.
 
Jamani leo nimeumia sana ndani ya moyo wangu, kwa hili tuweke siasa pembeni kwanza. Ni hivi:

Leo majira ya jioni mimi na ndugu zangu tulienda hospitali ya Muhimbili kumuona mgonjwa, saa ya kuondoka tukapanda daladala ya Buguruni. Kwakuwa watu walikua ni wengi na daladala imeshajaa akaja mama mmoja na kikapu chake, kondakta akapokea kile kikapu yule mama kwa sauti ya upole akamwambia konda hicho kikapu nakuomba kiweke vizuri kina vitu vya kuvunjika.

Konda akajibu hakuna tatizo, lakini yule mama alionekana hana nguvu. Kuna jamaa akampisha akae kwenye siti alipokaa tu kwenye siti akaomba kikapu chake, mara akamtoa mtoto! Watu wote tukamshikia bango kwamba ameiba mtoto haiwezekani.

Yule mama akatujibu amefanyiwa operesheni na anadaiwa laki saba kwahiyo alichofanya ni kumuweka mtoto kwenye kikapu na 'kusepa' nae. Kuna wamama walisema aoneshe hiyo operesheni na akafanya hivyo. Kwakweli imeniuma sana, yule mama anatia huruma sana tumemchangia elf40 na ameshukia Buguruni malapa.

Kwa hyo Muhumbili hospitali waangalie, leo kuna mgonjwa katoroka na mtoto kwenye kapu lakini pia wekeni utaratibu mzuri wa kukagua vifurushi vinavyotoka hapo hospitali maana mtu anaweza kutoka na mtoto sio wake. Sisi tuliokuwepo kwenye daladala tulijiridhisha tu kwamba yule mtoto ni wake.

Najua kabisa hapa ni sehemu ya great thinkers na huwa mnahitaji evidence lakini nilishindwa kuchukua picha kutokana na hali ilivyokuwa. Ila hii ni serious ishu Muhimbili waangalie utaratibu wao.
Nyoote ni mazuzu.

1. Una hakikisha vipi kuwa operation ni ya uzazi?

2. Je kama amefanya hila ili amrubuni mmewe kuwa kajifungua kwa op, na mtoto kaiba?

3. Badala ya kumpeleka kituo cha Polisi ambapo naamini baada ya kugundulika ni wake angewezeshwa zaidi, wahisani wangeongezeka. Nyie mmeamua mchange bila kujiridhisha.

4. Suppose kesho ikatoka taarifa kuwa kuna mama kaibiwa mtoto au kabadilishiwa mtoto, mtajisikiaje ikiwa nyie mmemsaidia mwizi kutoroka?

Hamjatumia akili, na unaweza kutafutwa uisaidie polisi kwa kitu kinaitwa parts of offence. Nyie mmemsaidia kukamilisha wizi wake
 
watanzania ni wajinga sana .yaani situation kama hiyo mnamsaidia muhalifu? je kama kweli kajifungua mtoto wake kafariki akaiba wa mwenzake je? kwanini asingepelekwa polisi then apate msaada huko polisi? kwani polisi wangemrudisha muhimbili?
Wewe ndo wa kwanza umefikiria. Soma post yangu hapo juu kabla ya hii yako niliyo i quote. Umelitendea haki jukwa
 
Atakuwa anakablood chakipalestina aisle dah
 
Nyoote ni mazuzu.

1. Una hakikisha vipi kuwa operation ni ya uzazi?

2. Je kama amefanya hila ili amrubuni mmewe kuwa kajifungua kwa op, na mtoto kaiba?

3. Badala ya kumpeleka kituo cha Polisi ambapo naamini baada ya kugundulika ni wake angewezeshwa zaidi, wahisani wangeongezeka. Nyie mmeamua mchange bila kujiridhisha.

4. Suppose kesho ikatoka taarifa kuwa kuna mama kaibiwa mtoto au kabadilishiwa mtoto, mtajisikiaje ikiwa nyie mmemsaidia mwizi kutoroka?

Hamjatumia akili, na unaweza kutafutwa uisaidie polisi kwa kitu kinaitwa parts of offence. Nyie mmemsaidia kukamilisha wizi wake

Kwenyebasiii walijaawehuu hatamimii mwishoo wastory nasubiria nisome wakaishia polisii aisee
 
Na mimi nina mawazo kama yako anaweza kuwa kachukua wa mtu au ni wake kweli ipaswa apelekwe polis sasa walichokifanya kimenishangaza sana
Ndo ujinga mkuu, lowasa kudai elimu elimu elimu was right.

Fikiria psychological torture watakayo pitia kesho wakisikia mtoto kaibiwa Muhimbili. Yaani kitakachowasaidia ni Mello tu anayekataa kutoa taarifa za watu kama hawa wanaojitoa fahamu. Eti analinda uhuru wa habari/kujieleza
 
watanzania ni wajinga sana .yaani situation kama hiyo mnamsaidia muhalifu? je kama kweli kajifungua mtoto wake kafariki akaiba wa mwenzake je? kwanini asingepelekwa polisi then apate msaada huko polisi? kwani polisi wangemrudisha muhimbili?
Sasa kama hujui police watafanyaje unachangia kitu gan? Yaani wampeleke police alafu wamwachie!umevurugwa wewe.
 
Kweli sisi Watanzania ni wajinga nakubaliana nawewe,hilo swala liliibuka la kwenda polisi lakin baada ya maelezo ya yule mama na wamama waliokuwepo kuridhika kwamba ana opesheni na watu walianza kupinga swala LA polisi si unajua sisi wabongo tulivyo na mioyo midogo ndugu yangu.
Kaa kimya unaendelea kuonesha ulivyo 1:4
 
Yani hakuna watu wabishi kama wabongo sijui Mungu alituumbaje hilo swala liliibuka lakin wabongo tunahuruma jamani mpka bas, ninachosisitiza hapa ni utaratibu wa Muhimbili kukagua vifurushi vinavyotoka huwez jua yametokea mangapi hayo
Watu wana hila, mtu anaweza kununua dr wa operation, akanunua nurse, akanunua walinzi getinu, kila kitu akanunua, kisa kukuza pendo kwa mmewe. Mmeshindwa kuisaidia nchi.

Yaani ungekuwa mjanja ungepiga kelele za hatari, ili gari lipelekwe polisi.
 
watanzania ni wajinga sana .yaani situation kama hiyo mnamsaidia muhalifu? je kama kweli kajifungua mtoto wake kafariki akaiba wa mwenzake je? kwanini asingepelekwa polisi then apate msaada huko polisi? kwani polisi wangemrudisha muhimbili?
Mawazo yako ni "useful" sana. Mimi nilifikiria vingine, tena kwa kumhurumia sana huyo manzi. Lakini wewe umezama sana tena kwa kutulia! Kweli penye wengi hapaharibiki jambo.
 
Kumbe wakina mama hawana akili? Sikujua hilo siku nyingne nitawaweka na makofi ili tumpeleke polisi,lakin jifikirie huyu MTU alipitaje toka kitandani mlango wa wodi had geti LA nje halaf ukirud nilaumu mm
Hakuna linaloshindikana duniani kwa wanadamu isipokuwa kuzuia kifo, kuhuisha mufu na kwenda peponi tu. Vingine vyote human fiction inaweza tena kwa usahihi hadi 100% accuracy
 
Kabisa angepata msaada hata me ningemchangia halafu laki saba alilala siku ngapi?
Chagga, ajili ya mshono mama. Visu hivi madaktari vinawapatia ulaji sana na hawana huruma na mgonjwa linapopatikana suala la upasuaji.
 
Bibi, uliwahi kusoma story ya suleman na makahaba wawili wanaogombea mtoto??? Kwa mujibu wa mleta mada huwezi kuhojiii. Hata Kama kafiwa na mtoto, wewe ungekubali kupelekwa polis na mshono??"
Kwani polisi kuna nini mpk uogope kwenda km si mhalifu?
 
Mkuu hivi unajua maana ya "k" kweli? Ulivyoandika 7k? K maana yake ni thousand, hapo maana yake ni 7 x 1000 = 7,000/= Nadhani wewe ulimaanisha 700, 000/= ambayo ingefaa iwe 700k.
Simble hiyo ya lugha gani ama ni kiswahili kitarafa "kilo"?
Ushasikia wapi k/kitarafa kinasahihishwa?
 
Sijui ni wangapi huwa mnaenda Muhimbili na kujionea palivyo. Nitawapa scenarios 3 nilizoziona recently.

1. Nilimkuta kijana amepata ajali na amepona. Hana hata senti anadaiwa hela alipe na hapo alipo hana hata nauli ya kupanda daladala afike kwao. Nilimkuta katoroka asubuhi walinzi wakamkamata wakamrudisha wodini maana alikuwa na makovu usoni hivyo ni rahisi kumjua yeye ni mgonjwa. Anadaiwa elf 50, Hana ndugu wala nini. Nikasema nikirejea kumwangalia patient wangu mchana nitamlipia hiyo hela aruhusiwe. Mchana ule sikumkuta mgonjwa wangu na sikumuona ila namkumbuka mpaka leo.

2. Nimehudhuria ibada za Muhimbili pale kanisani. Wanakuja wagonjwa walioruhusiwa na hawana hela ya kulipia au hawana nauli ya kuondokea pale. Wengine hukaa zaidi ya week wakusibiria msaada au msamaha. Ni mateso. Wengine wanafiwa hawana hata hela ya sanda au jeneza, na bill juu unadaiwa. Sad.

3. Nimeenda kumuangalia mgonjwa mwingine. Pembeni ya mgonjwa wangu kuna mama anaongea kilugha alifanyiwa operation ila amepona. Namsikia ila hajui namsikia. Mwanaye anasema mama nauza ile pikipiki ila sipati mteja. Wanadaiwa 2m. Mama anamwambia wapigie basi fulani na fulani. Mama asubuhi hadi jioni asubuhi hadi jioni, pikipiki haitoki na hana hela ya kulipa bill.

Huyo mama aliyetorosha mtoto, kwanza hospitali imezembea sana. Pili huenda ikawa ni kweli mtoto ni wake.
 
Jamani leo nimeumia sana ndani ya moyo wangu, kwa hili tuweke siasa pembeni kwanza. Ni hivi:

Leo majira ya jioni mimi na ndugu zangu tulienda hospitali ya Muhimbili kumuona mgonjwa, saa ya kuondoka tukapanda daladala ya Buguruni. Kwakuwa watu walikua ni wengi na daladala imeshajaa akaja mama mmoja na kikapu chake, kondakta akapokea kile kikapu yule mama kwa sauti ya upole akamwambia konda hicho kikapu nakuomba kiweke vizuri kina vitu vya kuvunjika.

Konda akajibu hakuna tatizo, lakini yule mama alionekana hana nguvu. Kuna jamaa akampisha akae kwenye siti alipokaa tu kwenye siti akaomba kikapu chake, mara akamtoa mtoto! Watu wote tukamshikia bango kwamba ameiba mtoto haiwezekani.

Yule mama akatujibu amefanyiwa operesheni na anadaiwa laki saba kwahiyo alichofanya ni kumuweka mtoto kwenye kikapu na 'kusepa' nae. Kuna wamama walisema aoneshe hiyo operesheni na akafanya hivyo. Kwakweli imeniuma sana, yule mama anatia huruma sana tumemchangia elf40 na ameshukia Buguruni malapa.

Kwa hyo Muhumbili hospitali waangalie, leo kuna mgonjwa katoroka na mtoto kwenye kapu lakini pia wekeni utaratibu mzuri wa kukagua vifurushi vinavyotoka hapo hospitali maana mtu anaweza kutoka na mtoto sio wake. Sisi tuliokuwepo kwenye daladala tulijiridhisha tu kwamba yule mtoto ni wake.

Najua kabisa hapa ni sehemu ya great thinkers na huwa mnahitaji evidence lakini nilishindwa kuchukua picha kutokana na hali ilivyokuwa. Ila hii ni serious ishu Muhimbili waangalie utaratibu wao.
Mtoa mada kama ni kweli umeshiriki ktk tukio hilo ni uhalifu na wengine ktk daladala.

Kama huyo mama ameiba mtoto je utajuaje na pia yeye kama yeye ana operation huoni kama kuna MTU anaweza kuwa amekosa haki yake kwa nyie abiria kuhadaiwa na ushahidi hafifu wa huyo mama ujasiri.

Mlitakiwa mkabidhi Polisi kama mlishakuwa na mashaka naye kuhusu huyo mtoto kuweka ndani ya kikapu.

Mantiki ya kuunganisha na gharama za Muhimbili haziingi akilini kabisa kwa mzazi kwani Sera ya wazazi inajulikana kabisa ni free cost,watoto under 5 na wazee.
 
Back
Top Bottom