Njanga Tz
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 843
- 654
Jamani leo nimeumia sana ndani ya moyo wangu, kwa hili tuweke siasa pembeni kwanza. Ni hivi:
Leo majira ya jioni mimi na ndugu zangu tulienda hospitali ya Muhimbili kumuona mgonjwa, saa ya kuondoka tukapanda daladala ya Buguruni. Kwakuwa watu walikua ni wengi na daladala imeshajaa akaja mama mmoja na kikapu chake, kondakta akapokea kile kikapu yule mama kwa sauti ya upole akamwambia konda hicho kikapu nakuomba kiweke vizuri kina vitu vya kuvunjika.
Konda akajibu hakuna tatizo, lakini yule mama alionekana hana nguvu. Kuna jamaa akampisha akae kwenye siti alipokaa tu kwenye siti akaomba kikapu chake, mara akamtoa mtoto! Watu wote tukamshikia bango kwamba ameiba mtoto haiwezekani.
Yule mama akatujibu amefanyiwa operesheni na anadaiwa laki saba kwahiyo alichofanya ni kumuweka mtoto kwenye kikapu na 'kusepa' nae. Kuna wamama walisema aoneshe hiyo operesheni na akafanya hivyo. Kwakweli imeniuma sana, yule mama anatia huruma sana tumemchangia elf40 na ameshukia Buguruni malapa.
Kwa hyo Muhumbili hospitali waangalie, leo kuna mgonjwa katoroka na mtoto kwenye kapu lakini pia wekeni utaratibu mzuri wa kukagua vifurushi vinavyotoka hapo hospitali maana mtu anaweza kutoka na mtoto sio wake. Sisi tuliokuwepo kwenye daladala tulijiridhisha tu kwamba yule mtoto ni wake.
Najua kabisa hapa ni sehemu ya great thinkers na huwa mnahitaji evidence lakini nilishindwa kuchukua picha kutokana na hali ilivyokuwa. Ila hii ni serious ishu Muhimbili waangalie utaratibu wao.