Mtoto atoroshwa ndani ya kikapu Muhimbili

Jamani leo nimeumia sana ndani ya moyo wangu, kwa hili tuweke siasa pembeni kwanza. Ni hivi:

Leo majira ya jioni mimi na ndugu zangu tulienda hospitali ya Muhimbili kumuona mgonjwa, saa ya kuondoka tukapanda daladala ya Buguruni. Kwakuwa watu walikua ni wengi na daladala imeshajaa akaja mama mmoja na kikapu chake, kondakta akapokea kile kikapu yule mama kwa sauti ya upole akamwambia konda hicho kikapu nakuomba kiweke vizuri kina vitu vya kuvunjika.

Konda akajibu hakuna tatizo, lakini yule mama alionekana hana nguvu. Kuna jamaa akampisha akae kwenye siti alipokaa tu kwenye siti akaomba kikapu chake, mara akamtoa mtoto! Watu wote tukamshikia bango kwamba ameiba mtoto haiwezekani.

Yule mama akatujibu amefanyiwa operesheni na anadaiwa laki saba kwahiyo alichofanya ni kumuweka mtoto kwenye kikapu na 'kusepa' nae. Kuna wamama walisema aoneshe hiyo operesheni na akafanya hivyo. Kwakweli imeniuma sana, yule mama anatia huruma sana tumemchangia elf40 na ameshukia Buguruni malapa.

Kwa hyo Muhumbili hospitali waangalie, leo kuna mgonjwa katoroka na mtoto kwenye kapu lakini pia wekeni utaratibu mzuri wa kukagua vifurushi vinavyotoka hapo hospitali maana mtu anaweza kutoka na mtoto sio wake. Sisi tuliokuwepo kwenye daladala tulijiridhisha tu kwamba yule mtoto ni wake.

Najua kabisa hapa ni sehemu ya great thinkers na huwa mnahitaji evidence lakini nilishindwa kuchukua picha kutokana na hali ilivyokuwa. Ila hii ni serious ishu Muhimbili waangalie utaratibu wao.
Wengine watoto wao wanakufa katika uzazi. Huyu alitakiwa arudishwe hospitali ikathibitishwe. Naomba ukatoe taarifa polisi.
 
Wamama hebu acheni roho mbaya. Hivi unafikri kama angepelekwa POLISI yangeishia hapo? Huyo mama lazima angerudishwa Muhimbili pamoko na kutokuwa na hela. Walichotakiwa kufanya labda wangejitolea wababa wachache wakamsindikiza mpaka mtaani kwake na kuchukua anwani ya makazi ili ilitokea kesho yake mtu analia kuibiwa mtoto Muhimbili iwe rahisi kumnasa! Hii ni changamoto kwa serikali inayojinasibu kwamba imeboresha maeneo ya huduma iweje huduma ya uzazi ulipiwe maelfu? Wacha wamama watoroke!
Usicheze na akili za mwanamke. Huyu mama anaweza akawa kaiba mtoto. Naomba hii taarifa ipelekwe polisi. Kama ni wa kwake tutamchangia bili yake.
 
Jamani leo nimeumia sana ndani ya moyo wangu, kwa hili tuweke siasa pembeni kwanza. Ni hivi:

Leo majira ya jioni mimi na ndugu zangu tulienda hospitali ya Muhimbili kumuona mgonjwa, saa ya kuondoka tukapanda daladala ya Buguruni. Kwakuwa watu walikua ni wengi na daladala imeshajaa akaja mama mmoja na kikapu chake, kondakta akapokea kile kikapu yule mama kwa sauti ya upole akamwambia konda hicho kikapu nakuomba kiweke vizuri kina vitu vya kuvunjika.

Konda akajibu hakuna tatizo, lakini yule mama alionekana hana nguvu. Kuna jamaa akampisha akae kwenye siti alipokaa tu kwenye siti akaomba kikapu chake, mara akamtoa mtoto! Watu wote tukamshikia bango kwamba ameiba mtoto haiwezekani.

Yule mama akatujibu amefanyiwa operesheni na anadaiwa laki saba kwahiyo alichofanya ni kumuweka mtoto kwenye kikapu na 'kusepa' nae. Kuna wamama walisema aoneshe hiyo operesheni na akafanya hivyo. Kwakweli imeniuma sana, yule mama anatia huruma sana tumemchangia elf40 na ameshukia Buguruni malapa.

Kwa hyo Muhumbili hospitali waangalie, leo kuna mgonjwa katoroka na mtoto kwenye kapu lakini pia wekeni utaratibu mzuri wa kukagua vifurushi vinavyotoka hapo hospitali maana mtu anaweza kutoka na mtoto sio wake. Sisi tuliokuwepo kwenye daladala tulijiridhisha tu kwamba yule mtoto ni wake.

Najua kabisa hapa ni sehemu ya great thinkers na huwa mnahitaji evidence lakini nilishindwa kuchukua picha kutokana na hali ilivyokuwa. Ila hii ni serious ishu Muhimbili waangalie utaratibu wao.
Hiyo operation alifanyiwa lini na huyo mtoto ni wa siku ngapi? Alienda kama fast track patient? Hiyo c- section ilikuwa imepangwa au emergency. Kwanini asijue gharama za operation? Mnavyomsupport kuvunja sheria mnajua hali yake ya kiafya ya mwili na akili?

Usione nakushambulia, sijapenda hii hata kidogo. Mimi siyo daktari wala mfanyakazi wa sekta ya afya, ninachoshindwa kuelewa basi zima hamna aliyekuwa na wazo kwamba wanamsaidia mtu kuvunja sheria. Ukubwa wa kosa hatuujui kwa sasa.
 
Back
Top Bottom