Mtoto atoroshwa ndani ya kikapu Muhimbili

Mtoto atoroshwa ndani ya kikapu Muhimbili

Kuwatangazia wanawanchi kuwa huduma ni Bure vitu vyote vipo hospitali, nawasihi maneno ya kuazima kutoka kwa viongozi wenu changanya na akili ya mwewe, uhai hauna spea, nunua vifaa ufikapo hospitali, watoa huduma za Afya wanapposema vifaa hakuna amin ni kweli wala hawafichi
 
Jamani leo nimeumia sana ndani ya moyo wangu, kwa hili tuweke siasa pembeni kwanza. Ni hivi:

Leo majira ya jioni mimi na ndugu zangu tulienda hospitali ya Muhimbili kumuona mgonjwa, saa ya kuondoka tukapanda daladala ya Buguruni. Kwakuwa watu walikua ni wengi na daladala imeshajaa akaja mama mmoja na kikapu chake, kondakta akapokea kile kikapu yule mama kwa sauti ya upole akamwambia konda hicho kikapu nakuomba kiweke vizuri kina vitu vya kuvunjika.

Konda akajibu hakuna tatizo, lakini yule mama alionekana hana nguvu. Kuna jamaa akampisha akae kwenye siti alipokaa tu kwenye siti akaomba kikapu chake, mara akamtoa mtoto! Watu wote tukamshikia bango kwamba ameiba mtoto haiwezekani.

Yule mama akatujibu amefanyiwa operesheni na anadaiwa laki saba kwahiyo alichofanya ni kumuweka mtoto kwenye kikapu na 'kusepa' nae. Kuna wamama walisema aoneshe hiyo operesheni na akafanya hivyo. Kwakweli imeniuma sana, yule mama anatia huruma sana tumemchangia elf40 na ameshukia Buguruni malapa.

Kwa hyo Muhumbili hospitali waangalie, leo kuna mgonjwa katoroka na mtoto kwenye kapu lakini pia wekeni utaratibu mzuri wa kukagua vifurushi vinavyotoka hapo hospitali maana mtu anaweza kutoka na mtoto sio wake. Sisi tuliokuwepo kwenye daladala tulijiridhisha tu kwamba yule mtoto ni wake.

Najua kabisa hapa ni sehemu ya great thinkers na huwa mnahitaji evidence lakini nilishindwa kuchukua picha kutokana na hali ilivyokuwa. Ila hii ni serious ishu Muhimbili waangalie utaratibu wao.


Huyu aliyepost habari si ndiyo chombo chetu cha usalama alipaswa kutwambia amechukua hatua gani badala ya kutupasha!!! mbona namwona kama ndiye kwenye profile pic!
🙄😕
 
Good mama mtoto...., umevunja rekodi ya mwaka 2016.…!. Ningekujua ningekupa zawad. Ila big up sn.
 
Kwakweli imeniuma sana, yule mama anatia huruma sana tumemchangia elf40 na ameshukia Buguruni malapa.

Kwa hyo Muhumbili hospitali waangalie, leo kuna mgonjwa katoroka na mtoto kwenye kapu lakini pia wekeni utaratibu mzuri wa kukagua vifurushi vinavyotoka hapo hospitali maana mtu anaweza kutoka na mtoto sio wake.

Nakuona kama unauma na kupulizia;
  • Umemchangia mgonjwa, sawa jambo jema
  • Lakini unamfichulia siri na kuonekana umekerwa na aina utoroshwaji wa mtoto
 
Yani hakuna watu wabishi kama wabongo sijui Mungu alituumbaje hilo swala liliibuka lakin wabongo tunahuruma jamani mpka bas, ninachosisitiza hapa ni utaratibu wa Muhimbili kukagua vifurushi vinavyotoka huwez jua yametokea mangapi hayo
Uko sahihi mazingira yalisababisha pamoja na hali ngumu ya maisha ya wa Tanzania walio wengi mkafanya hiyo bahati mbaya ya kumuachia bila ya kuwa na hakika
 
Huyo mama huenda kweli ni mtoto wake,lakini lawama lazima wapewe serikali kwasasabu laiti ingelikuwa matibabu ni bure kwa watu wote nadhani asingefanya ivyo uyo mama,lawama tuipe serikali laiti matibabu yangelikuwa bure uyo asingejificha,mfano mdogo kuna mtoto wa dada yangu alilazwa hapo Muhimbili mwishoni ikaja bili yakuwa anadaiwa shilingi laki tatu,basi akakaa hospitali wakati amesharuhusiwa mpaka deni lote lilipoisha ndipo aliporuhusiwa kutoka,nami ningeliweza kufanya ivyo ningefanya tu,Jamani mkumbuke maisha magumu uku mtaani iyo laki saba kuipata ni inshu mjue

nov 2016 kuna mama alikaa KCMC siku mbili zaidi baada ya kuruhusiwa, mtoto wake alilazwa, ana miaka kama 13 hiv, watu wakawa wanamshauri mama amtoroshe huyo binti, ila mama alisema huyo mtoto huwa naumwa mara kwa mara na huwa analazwa hapo. akaopgopa kutoroka akidhan siku akiumwa tena watamdaka.

nafikiri hili swala la matibabu serikali liangaliwe upya.
 
operesho dna? yaani wewe mtu mzima unazidiwa akili na kina mama?
Wamama hebu acheni roho mbaya. Hivi unafikri kama angepelekwa POLISI yangeishia hapo? Huyo mama lazima angerudishwa Muhimbili pamoko na kutokuwa na hela. Walichotakiwa kufanya labda wangejitolea wababa wachache wakamsindikiza mpaka mtaani kwake na kuchukua anwani ya makazi ili ilitokea kesho yake mtu analia kuibiwa mtoto Muhimbili iwe rahisi kumnasa! Hii ni changamoto kwa serikali inayojinasibu kwamba imeboresha maeneo ya huduma iweje huduma ya uzazi ulipiwe maelfu? Wacha wamama watoroke!
 
Huyo mtoto sipati picha akija kuwa kiogozi mkubwa wa hii nchi wahuni wote wa pale LUMUMBA na CCM jinsi atakavyo walamba kitanzi
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu swissme kati ya watu ambao nimewaona hawaipendi ccm kutoka uvungu wa moyo wako basi ni wewe.....

Heshima kwako mkuu, ukiweza kuwaambukiza watu spirit yako wallah bongo kunageuka syria sasa hivi.....
nampendaga sana huyu swiss me
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu swissme kati ya watu ambao nimewaona hawaipendi ccm kutoka uvungu wa moyo wako basi ni wewe.....

Heshima kwako mkuu, ukiweza kuwaambukiza watu spirit yako wallah bongo kunageuka syria sasa hivi.....
 
Wee jaman hapo kuna mawili my dears inawezekana ni wake ama kamuiba ktk kipindi cha kunyonyesha ward 36 you never know so ilitakiwa apelekwe police then police wangedecide kama kumkagua hyo scisor au la
 
Hii ni mpya mm nilijifungulia muhimbili tena kwa operation na sikutozwa hata 100 sijui huo utaratibu wa wajawazito kulipa umeanza lini? Pia unapojifungua kwa operation Muhimbuli huwa kuna chumba maalum ambacho watoto huwekwa na huruhusiwi kuingia kama sio mzazi coz watoto kuna alama huwa wanavalishwa kwenye mikono yako inayoshabihiana ya mama mzazi wa Huyo mtoto kama sikosei na nipo tayari kusahihishwa mzazi anayetozwa gharama za operation ni yule from the beginning alikuwa na special doctor wake hapo ndio huwa wanatozwa gharama za operation so inawezekana huyo maza kaiba mtoto wa mwezie swali kamuiba katika mazingira gani coz kwa muhimbili walivyostrict na watoto wa operation nashindwa pata picha
Wewe kweli ni Dada wa pekee "unique Dada" miaka uliyozaa wewe inafanana na walio zaa wenzio pakini wengine wakalipa ila wewe hukulipa hata 100, hebu muda mwingine tuache upashkuna jamani
 
Huduma ya Afya ni haki ya kila mtanzania, Tunawaambia kina ummy Mwl na Boss wake tunataka haki yetu, mambo yakutuvisha vifo huku tunatamani tuendelee kula ugali wa maharage hatutaki, msiwatie mikosi watoto kiasi cha kuwekwa kwenye kikapu kama shombo la samaki
 
Ndio utaratibu Wao na ukigoma kukopa hawakupi sijui report sijui release kwahio next time Ukija hawakuhudumii. Ni kweli we had the same case tulikua na Ndugu yetu hapo Muhimbili Ward ya Watoto yaani ikabidi atuambie ndio tukalipa na ukumbuke ana Kadi ya Bima ya Afya. Haya twende Kazi. Ni story inayoumiza Sana
 
My dear sijajua umejifungua lini ila mimi nilijifungua mwaka mmoja uliopita tulilipia kila kitu mpaka sindano za maumivu, nilishuhudia mtu ganzi imeisha mshono unamuuma wanamuambia dawa hakuna ikabidi nimlipie yule dada!!! Sasa bure hiyo ya wapi?? Kuhusu kule juu nakumbuka nilivyotoka kwenye chumba cha upasuaji nesi akaniambia mwangalie mtoto vizuri umkariri.....siku hiyo hiyo jioni mzazi akawa hamuoni mwanae nikaogopa mnoo kesho yake nikaongea vizuri na dr wakanipa chumba na mwanangu nilale nae. Kwa mazingira ya pale ukitaka kumuiba mtoto inawezekana kabisa!!!! Kwanza mkienda nyonyesha mnaeza msimkute nesi sasa hapo utashindwa chukua mtoto??
2010 my dear ndio nilijufungua that's why nashangaa lakini hii ni awamu nyingine so inawezekana huo utaratibu ukawepo wa wajawazito kulipia
 
Kiongozi hali ya uchumi ni ngumu,mama muuza vitumbua atatoa wapi laki saba,Hayo mambo yapo si walisema kujifungua bure?Sasa mama mzazi akifanyiwa operation kwanini alipe?Halafu viongozi wa dini wanaghilibu wananchi maisha yamekuwa rahisi,mungu atawachoma moto kwa unafiki wenu, so sad mungu tusaidie.
Sema maaskofu.
 
Back
Top Bottom