Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature currently requires accessing the site using the built-in Safari browser.
anapandwa kama mbegu za mazao mengine.
Swali kuhusu mtoto anatoka wapi huwa linaulizwa na watoto walio wengi. Wanamwuliza baba au mama kwamba mtoto anatoka wapi? Mtoto anayeuliza ni wa miaka mitatu au minne. Naomba mchango kuhusu jibu sahii la kumpa mtoto?
Wanapatikana hospitalini baada ya kuchomwa sindano nyiiiingi
i do hope some other people will contribute...haya maswali ni real life kabisa, wazazi tusaidiane kujiandaa na majibu yanayoeleweka...na hii mitandao watoto hawachelewi kuingia na kuona live how babies are born..ukaja kuulizwa with details macho yanakutoka!!
Swali kuhusu mtoto anatoka wapi huwa linaulizwa na watoto walio wengi. Wanamwuliza baba au mama kwamba mtoto anatoka wapi? Mtoto anayeuliza ni wa miaka mitatu au minne. Naomba mchango kuhusu jibu sahii la kumpa mtoto?
My 6yr old daughter has been relentless for the past 2weeks asking this question.We have got to the part anauliza mtoto anaingiaje tumboni kwa mama?Jasho linanatoka mama yake anamwambia mi na kazi kamuulize babako
Jamani kwa utamaduni wetu wa Kitanzania/Kiafrika mtoto mwenye umri huo hastahili kuambiwa process yote ya jinsi mtoto anavyopatikana.
Baba:Mama yako alimeza mtoto wakati wewe umelalaMtoto: Mama hataumia?
Baba: Anaweza kuumia kidogo.
... Marvelous Mbogela, ni muda mfupi tu uliopita nimepita mahali nakuta mama anamshambulia mtoto wake wa kama miaka 6-7 hivi kwa matusi ikabidi niulize ni mtoto wake au wa jirani wenyeji wakasema wake mwenye....Mtoto anaambiwa " we mbwa ukichelewa kurudi nitakupasua kichwa chako muone kwanza miguu kama umefufuka leo".....Nina imani mtoto wa aina hii ukimuongezea na tabi aya uongo kama huo kuwa mtoto ananunuliwa au anamezwa yumkini atakuwa na akili hiyo kuwa uongo ni sehemu ya maisha yetu....Nadhani ni afadhali kuwajibu kwa polite language angalau kuwa mama anapewa mtoto na mungu....inatosha sana kwani ukweli unabaki pale pale hata ukiweka darasa na kumueleza the whole process still na kudra za mwenyezi mungu zinaingia katika kupatika mtoto!!!Hapo tunajidanganya wenyewe! Leo tunalalamika na mafisadi kuwa wametoka wapi na wanasiasa kuwa ni waongo tunasahau kuwa malezi kam haya ya kuwambia watoto uongo ndiyo yanazaa jamii ya watu tulionao leo,
mwambie mtoto Ukweli, unajua ukimwambia mtoto kwa mfano ukipata maswali yote leo shuleni nitakununulia kigari tulichokiona dukania au kama cha Juma basi akipata nunua, usiseme kitu ambachon huwezi, km ukimwaga hicho chakula nitakuua. Akimwaga utamuua kweli? usipomuua atajua kumbe unaweza kusema jambo usifanye, hakuna shida anakuwa hivyo hivyo. Tusiwaambie watoto wetu malaya Mkubwa eweee kwa kosa la kubamiza mlango tu! Watanzania Bwana.
Hakuna cha mila ya Kitanzania wala ya kizungu chukueni yaliyomazuri ya kweli tufanye bila kisingizio cha mila. Watoto wanastahili ukweli kwa lugha inayoweza kueleweka kwao.