Mtoto aliyekataliwa na baba yake

Mtoto aliyekataliwa na baba yake

We Nikas na Nivea hamjawahi kuishi kwa watu? kuishi na watu kwa muda kwa nia ya kuwasaidia wafikie malengo yao, si vibaya.mmoja kufanya makosa msiwapunish wengine wote. mkifa kabla ya siku watoto wenu wataenda kuishi kwa wakina nani?

Muda gani huo? Unawasaidia nini? Kwa nini msaada uzid uwezo? Huruma huzaa dhambi.

HALAFU kufa kabla ya siku ndo nini? Siku gani maalumu kufa? Siku nitakayokufa ndo siku ambayo Mungu amepanga nife.
 
huo ubabe wa kaka yako ndo unafanya ajione yeye Mungu mtu, na vile tena anaona ndugu wanamuogopa, basi ndo kuona yeye ni kila kitu...
usijali dada msaidie huyo bint (assume hata ni Sadaka kwa Mungu), mambo ya wewe sio ndugu yake sijui na nini, ni utoto tu wamsumbua huyo kaka yako, akikua ataacha... nan alimwambia undugu unaondoshwa na maneno?kama ndo hivo watu si wangehama hata makabila.
 
Hapo ndipo wanaponiacha hoi mababa wa dunia hii. Hakika dada wewe umefanya jambo kubwa sana ambalo wengi linawashinda. Kuna rafiki yangu mmoja kazaa na jamaa, mtoto copy ya jamaa, ukimuona huulizi, jamaa kanogowa penzi jipya jingine "hamtaki mtoto". Ikatokea mpaka madada wa huyo bwana wanamjua mtoto na wanaona aibu kwa jinsi kaka yao anavyoikataa damu yake. Cha ajabu hata wao hawataki hata kumsalimia mtoto kisa wanaogopa kaka yao akijua itakuwa tatizo na pia wanaogopa mke mpya wa kaka yao asijue kama wao wanamjua mtoto asietakiwa na kaka yao. Na huyo rafiki yangu si kwamba ana shida saana labda ya kusomeshewa au kutunziwa mtoto kwa namna yoyote.

Mungu atakulipa wewe na mume wako kwa mema yenu. Laana haitasogea katika maisha yenu. Na huyo baba ni aibu tu inamsumbua, tatizo la wanaume wengine wajinga hawataki kujishusha na kukubali kosa. Kaza buti asikutishe na ukali wake , lea dada
 
Nikas hujajibu swali. ukifa wanao wadogo wataishi na nani? maana we hupendi watu waishi kwako, so we wako wataenda kuishi orphanage?
Muda gani huo? Unawasaidia nini? Kwa nini msaada uzid uwezo? Huruma huzaa dhambi.

HALAFU kufa kabla ya siku ndo nini? Siku gani maalumu kufa? Siku nitakayokufa ndo siku ambayo Mungu amepanga nife.
 
ale kona zake, yeye anajua kuzaa tu na kutelekeza? we umefanya jambo jema, mlee huyo mtoto kama nafsi yako inavyokutuma, achana na vitisho vya huyo kaka yako nafsi yake inamsuta na anaona haya tu kukubali kwamba alifanya makosa enzi hizo!!1
Tena anaona haya sana, na anafikiri hao watoto alio nao huko ndiyo wwatakuja msaidia, maana anamkataba na Mungu, mm nakushauri Walimweusi kuwa wewe kaza buti, na usisikilize ya huyo Bro wako, wewe fanya kama unatoa sadaka Mungu atakulipa Mema,. Na kwa kuwa Bro hamtaki huyo mtoto usimwambie baba yake ni nani, Nyamaza kimya. Ila iko siku isiyojulikana kwa uwezo wa Mungu atakuja kukupigia magoti akiomba msamaa. Tumewaona wengi wa hivyo.
 
kwanza hongera kwa uamuzi
ulifanya wa kumchukua mtt
huyo ni wa kwako,huyo kaka ako
apeleke laana zake huko kwa mke wake!
si alimkataa sasa inamuuma nini wewe kumlea mtt!
mungu akubariki wala huyo kaka asikutishe ila
angalia usalama wa mtt,asijemuua bure coz
chuki juu ya mtoto inaonekana dhahiri!shame on him!!!

 
Mpuuze huyo kaka yako. We mlee huyo mtoto kama ambavyo ungeweza mlea mtoto mwingine ambae si ndugu yako. Kama alikataa kama mtoto sio wake alifuata nini kwako? nawewe usijipendekeze kwake kujionyesha unamlea mwanae. we komaa kivyako na akikuuliza tena mwambie huyo mtoto hamhusu.

Kiukweli mimi nilipomkuta kwangu sikumjibisha, alibwabwaja na akaondoka bila kuniaga, na mimi sijamuuliza wala kumcall kwa vile contibution yake in my life ni 0!
 
kwanza hongera kwa uamuzi
ulifanya wa kumchukua mtt
huyo ni wa kwako,huyo kaka ako
apeleke laana zake huko kwa mke wake!
si alimkataa sasa inamuuma nini wewe kumlea mtt!
mungu akubariki wala huyo kaka asikutishe ila
angalia usalama wa mtt,asijemuua bure coz
chuki juu ya mtoto inaonekana dhahiri!shame on him!!!


Hilo nalo neno, ila my kids wanalindwa na Damu ya Yesu so I believe hatomuweza kwa njia yeyote ille!!
 
Tena anaona haya sana, na anafikiri hao watoto alio nao huko ndiyo wwatakuja msaidia, maana anamkataba na Mungu, mm nakushauri Walimweusi kuwa wewe kaza buti, na usisikilize ya huyo Bro wako, wewe fanya kama unatoa sadaka Mungu atakulipa Mema,. Na kwa kuwa Bro hamtaki huyo mtoto usimwambie baba yake ni nani, Nyamaza kimya. Ila iko siku isiyojulikana kwa uwezo wa Mungu atakuja kukupigia magoti akiomba msamaa. Tumewaona wengi wa hivyo.

Mama yake mzazi alishamwambia story yote, kwanza kwa jinsi ambavyo now anaridhika na maisha ya sasa hana hata habari na mtu anayeitwa baba, after all baba yupo anaemjali kama mtoto wake so my brother means nothing to the girl.
 
Hilo nalo neno, ila my kids wanalindwa na Damu ya Yesu so I believe hatomuweza kwa njia yeyote ille!!

Ni kweli Bwana atawalinda tu hao watoto na wewe mwenyewe...Bwana" atakulinda na mabaya uingiapo na utokapo tangu sasa na hata milele"......"Bwana atakuagizia malaika wake wakulinde katika njia zako zote mguu wako usijikwae katika jiwe"
 
Blaza nae ana mambo? Kwani alimuona wapi huyo mtoto mpaka aje kukutunishia msuli? Nani kamuambia wake? Au mkewe kaenda kuliungurumisha soo kuwa yule mtoto wa shemeji yenu anayekaa kwa wifi ama mmelendana!

Kama umeguswa kumlea huyo mtoto endelea kumlea tu, na ukubali kuwa huo mzigo wako till further notice....
 
utabarikiwa sana na utapata mengi na faida nyingi kwa kupitia huyo mtoto. Fumba macho na ziba masikio juu ya chochote kibaya utakacho ambiwa juu ya huyo mtoto...hakika mfanye huyo mtoto awe mwanao atakuja kukusaidia

hilo lisiwe lengo, kama amua kumsaidia huyo mtoto amsaidie tu, kwa roho safi, asimuasili.Na kuhusu huyo mtoto kumrudishia fadhila ni majaliwa ya Mungu.
 
Huwa nashangaa mzazi wa namna hii??? Walimweusi mie nakushauri tu hebu jitahidi kwa vihela vyetu hivi hivi vidogo umsomeshe hadi panapo uhai wa Mola. Maana hujui kesho yako!. Hivi huyu baba nafsi mwake anasubiri kusikia mtoto wake kapata mafanikio ndio aje aseme mimi ni baba yako?? Usiogope vitisho kaza roho!
Kwanza Mungu akubariki sana kwa roho yako ya utu. Huyo mtoto hata asingekuwa wa bro, bado ulichofanya ni thawabu kubwa san mbele za MUNGU. Huwezi jua atakuwa nani kesho, na huwezi jua nani atalea wanao yatakapo kufika. Lakini zaidi kwa kufanya hivyo unafungua milango ya baraka, kwani huyo mtoto hakuchagua azliwe katika mazingira yenye utata kiasi hicho. God bless you.
 
umefanya vyema sana tena sana i wil pray that you will be blessed that you can save the baby ungali hai na nguvu
 
Dadangu walimweusi naomba usimame hapohapo kwa hilo. yaani hata sijui nikwambie nini kwa jinsi nilivyofarijika kwa ushupavu wako wa kufanya maamzi magumu kama hayo. huyu kaka yako asikutishe wala kukuonea gele, bali endelea kumtunza kwani watu kama hao Mungu huwa anawajaalia kiasi kwamba akili zao huchaji usiku na mchana. kama vile ambavyo hukupenda kumshirikisha wakati wa kumchukua, vivyo hivyo usimshirikishe kwa lolote juu ya maisha ya mtoto huyo bali chukulia kuwa huo ni msalaba wako tu.

Nakuombea mungu akuzidishie kwa hilo.
 
sikuwahi kudhani WALIMWEUSI ni mwanamke, sijui kwa nini..... unisamehe kwa hilo rafiki.....
Mi naona umefanya jambo zuri sana..... hutakuja kujuta kwa hili, na nina uhakika kuna siku kaka yako atakushukuru kwa hili.
Kama upo close na wifi yako, mimi nakushauri unaweza kumwambia, ila umwambie in such a way that asione mumewe ana kosa (sijui itawezekanaje hapa! ila unaweza kumwambia kulikuwa na hii story lakini kaka kakataa, na kwamba unamsaidia yule dada huyo mtoto sababu ulikuwa unamchukulia mamake kama mdogo wako wakati mnakaa naye. uliona maisha yamekuwa magumu so unamsaidia yule dada, hata kama mtoto siyo wa kakako), ukizingatia mtoto alipatikana kabla yeye hajaolewa....
unajua kwa nini nakushauri wifi ajue? huyo ni mtoto ambaye karibia watu wengi wa familia wanalijua....
maneno yanatembea, amini usiamini, siku wifi yako atakuja tu kujua kuwa huyo ni mtoto wa kaka yako.
wifi atakuchanganya na wewe kuwa ndo wale wale, mnamchekea machoni lakini hamna lolote.
kama kakako angekuwa kakubaliana na hiyo ningekushauri umwambie kakako amwambie mkewe.
Hii ni ngumu sana, wewe ndo unamfahamu wifi yako, na huwezi kujua, wifi anaweza akalipokea positively.... siyo wamama wote hawapendi watoto wa waume zao wa kabla ya ndoa
 
Last edited by a moderator:
na usimwogope uyo kenge maji (kaka yako):nono::nono:,wala usimrudisha uyo mtoto mana ulimchukua kwako na wewe ndo unamlea na hukumwambia so mwambie uyo baradhuli akukome km undugu ufe tu!mana wewe ndie Mungu atakulipa maradufu kwa wema huo ulifanya uyo mtoto atakulea/atakua msaada kwako ktk uzee wako na wanako atawatunza pia.
wewe mwambie uyu mtoto hakuhusu ni wako na kama vipi akileta za kuleta nenda kamu-adopt kabisa tena sema nilimtoa kijijini na mama yake mtoto aridhie kukupa.FULL STOP
WALIMWEUSI nimekupenda bure kwa moyo wako wa maamuzi magumu,safi sana!

walahi nachukia wanaume wanaokataa uzinzi wao na kuwasusa damu zao!
 
Last edited by a moderator:
Nikas hujajibu swali. ukifa wanao wadogo wataishi na nani? maana we hupendi watu waishi kwako, so we wako wataenda kuishi orphanage?

Sijakataa watoto[under 15]. Nimesema kaka/dada/wakwe/Mashemeji zangu ndo sitoish nao. Usinilishe maneno.
 
Umefanya jambo la busara nahata dini zetu zinatusisitiza kutenda mema! wewe usijali lolote kama ni mtoto wa kaka au si mtoto wake! madamu unalofanya ni la heri na Mungu atakuzidishia na wala katika maisha yetu hatujui linalokuja mbele yetu! mwacha hao anaoona ndio watoto wake atakuja juta tuombe Mungu atupe uzima utakuja ona mwenyewe Mungu wetu ni mwema na malipo mara nyingi ni hapa duniani mwombee maisha bro wake aje akitambaa nyumbani kwako kwa kuomba msaada wa mtoto huyo unaelea leo!
 
lea huyo mtoto!
huyo kakako atakuja kukushukuru(kwanza anakushukuru kimoyomoyo)anaogopa tu kumeza alichoapa!
huyo mtoto ni blessings!
hana kosa huna kosa!
 
Back
Top Bottom